Friday, August 20, 2010

Ulafi Wa Ruzuku Wadhihirishwa Na ‘Vyama Vya Mifukoni’


· Vingi havina hata ofisi za taifa, achilia mbali za mikoa
· Badala ya kukimbilia Ikulu, vijipange kusukuma maendeleo

Na Daniel Mbega

KIPENGA cha kampeni za uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani kinapulizwa rasmi Ijumaa hii huku kukiwa na mambo mengi ambayo bado yanaonyesha kambi ya upinzani ina kazi ngumu ya kuingia Ikulu.
Kuanguka kwa vigogo CCM dalili za wananchi kuchoshwa na propaganda

* Watanzania wadhihirisha kweli hawadanganyiki, wanataka maendeleo

Na Daniel Mbega

KURA za maoni za Ubunge na Udiwani kwa wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM) zimemalizika na kushuhudia vigogo wengi, wakiwemo mawaziri na naibu mawaziri wakiangukia pua.

Walioanguka, wakiwemo vigogo na makada wakongwe wa CCM sasa wanasubiri kudura za Kamati za Siasa na Halmashauri Kuu (NEC) ya chama hicho itakayoamua na hatimaye kutangaza ‘wateule’ watakaopeperusha bendera ya chama hicho katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 31, mwaka huu.

Wapo ambao wanasubiria kwa hamu kuona kama ahadi ya CCM ya kuwatosa wanachama waliokumbwa na kashfa ya kushiriki vitendo vya rushwa inatimizwa hasa baada ya wengi wao kukamatwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) katika mchakato wa kura za maoni.

Lakini ni nani hata miongoni mwa wale walioshindwa na kulalamikia matokeo ambaye anaweza kusimama hadharani na kusema hakutoa rushwa? Katika Tanzania ya leo, kuna yeyote anayeweza kudanganya kwamba hakutumia ‘zawadi’ kuwashawishi wanachama wa CCM wamchague?

Binafsi nasema kwamba, hakuna miongoni mwao aliye msafi, wote wameoza na wananuka rushwa na uvundo wa ufisadi na kilichotokea ni kwamba, walitoa rushwa, wakazidiana kete.

Kikubwa zaidi ambacho hawakifahamu wale walioshinda na hata walioshindwa ni kwamba, wananchi wameamua kufanya mabadiliko. Walioshinda wasijisifu kwa ushindi wao wakadhani kwamba fedha walizowapa wapigakura ndizo zilizowafanya wakachaguliwa, kwani yawezekana walitoa fedha kidogo kuliko wale walioshindwa! Ndiyo. Siri yote wanayo wananchi wenyewe.

Kwa wale walishindwa, nao wasije wakadhani kwamba walitoa fedha kidogo ndiyo maana wakaangushwa, la hasha. Yawezekana walitoa fedha nyingi kuliko washindi, lakini wananchi walikuwa wanataka kuleta mabadiliko ya kweli ya maendeleo.

Ni mabadiliko hayo ambayo yamewafanya vigogo wengi kuangushwa, na kwa hakika mabadiliko ya mwaka huu yamewashangaza wengi wakiwemo hata wa vyama vya upinzani ambao hawakuyatarajia.

Kuangushwa kwa wanasiasa wakongwe safari hii kunaonyesha dhahiri kwamba wananchi wamedhamiria kuleta mapinduzi na hii ni dalili tosha kwamba wamechoshwa na propaganda za muda mrefu ambazo haziwaletei maendeleo Watanzania.

Kwamba, huwaona wawakilishi wao siku za kampeni wanapoomba kura, lakini mara wanapochaguliwa hupotea mpaka baada ya miaka mitano ndipo hurejea na ngonjera nyingi zilizopangiliwa vina na mizani mwanana, wakitaka wapewe tena wasaa mwingine ili wawatumikie, bila kutambua kwamba walipokuwa wakati uliopita waliahidi mambo mengi ya maendeleo ambayo hawakutekeleza hata mojawapo.

Mbaya zaidi wanapokuwa madarakani huwasahau waajiri wao, ambao ni wananchi waliowachagua, hata kuwapigania haki zao, zaidi wanapokuwa Bungeni ama kwenye Mabaraza ya Madiwani hupigia kelele nyongeza ya posho za vikao, mishahara na marupurupu mengi. Wanafikiria zaidi matumbo yao kuliko umma wa Watanzania!

Propaganda hizi ndizo zilizowafanya wananchi waamue kufanya kile ambacho hakikutarajiwa na wengi; kuwapiga chini wabunge na madiwani wote ambao ama wamefanya nyadhifa hizo kama za kuzaliwa nazo au wameshindwa kuleta maendeleo katika sehemu zao za utumishi.

Haikuwa ajabu kushuhudia wakongwe wa siasa, makada wa CCM – wakiwemo mawaziri wa serikali zilizotangulia na serikali ya sasa inayomaliza awamu ya kwanza ya miaka mitano, kuangushwa kwenye kura za maoni.

Waziri Mkuu mstaafu na Balozi wa zamani wa Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa, Cigwiyemisi John Samuel Malecela, ni miongoni mwa wanasiasa wakongwe walioangukia pua kwenye kura za maoni, akishindwa kwa tofauti ya kura 351 na ‘mwanawe’ Livingstone Job Lusinde katika Jimbo la Mtera.

Mkongwe huyo wa siasa, almaarufu Tingatinga, kutokana na kutumika katika harakati nyingi za chaguzi ndogo, sasa anasubiri miujiza kutoka NEC, vinginevyo asubiri tu ‘huruma’ ya Rais Kikwete (endapo naye atashinda urais mwaka huu) ili amteue kupitia kwenye ‘kapu’.

Ukiacha Malecela aliyezaliwa Aprili 20, 1934, Buigiri, Dodoma, wengine walioshindwa ni wakongwe Joseph James Mungai (67), Profesa Raphael Benedict Mwalyosi (64), Jackson Muvangila Makweta (67), Monica Ngezi Mbega (54), Profesa Philemon Mikol Sarungi (74), Dk. James Mnanka Wanyancha (58), Pascal Constantine Degera (77), George Malima Lubeleje (60), Zabein Muhaji Mhita (60), na wengineo.

Mawaziri kadhaa wa sasa na waliopata kushika nyadhifa za uwaziri miaka ya nyuma wameambulia patupu. Hao ni Bujiku Sakila, Mudhihir Mohammed Mudhihir, Tatu Mussa Ntimizi, Joel Nkaya Bendera, Dk. Charles Mlingwa, Dk. Juma Ngasongwa, Dk. Ibrahim Msabaha, Nazir Mustafa Karamagi, Ludovick Mwananzila, Harith Bakari Mwapachu, Dk. Diodorus Kamala, Wilson Mutagaywa Masilingi, Shamsa Selengia Mwangunga, na Mwantumu Bakari Mahiza.

Ukitazama mchakato ulivyokuwa mkoa kwa mkoa, hakika utaona ni kwa namna gani wananchi wamedhamiria kuleta mabadiliko ya uongozi, kwani ipo mikoa ambayo imewatosa hadi wabunge sita na hivyo kufanya wabunge walionyimwa ridhaa ya kurejea majimboni kufikia 68 ndani ya CCM pekee, wakati kwenye Chama cha Wananchi (CUF) wabunge 12 wametemwa na mmoja wa Chadema.

Iringa, Tanga, Morogoro na Mwanza ndiyo mikoa iliyoongoza kwa kuwatema wabunge wake kwa sababu mbalimbali, zikiwemo za ukongwe na kukosekana kwa maendeleo. Mikoa hiyo imewatema wabunge sita wa majimbo kila mmoja ambapo wa Iringa ni Joseph Mungai (Mufindi Kaskazini), Profesa Raphael Mwalyosi (Ludewa), Jackson Makwetta (Njombe Kaskazini), Monica Mbega (Iringa Mjini), Yono Kevela (Njombe Magharibi) na Benito Malangalila (Mufindi Kusini).

Aidha, Tanga imewatema Joel Bendera (Korogwe Mjini), Balozi Abdi Mshangama (Lushoto), William Shelukindo (Bumbuli), Laus Mhina (Korogwe Vijijini), Bakari Mwapachu (Tanga Mjini) na Abdallah Rished (Pangani).

Waliotemwa Morogoro ni Hamza Mwenegoha (Morogoro Kusini), Castor Ligalama (Kilombero), Dk. Juma Ngasongwa (Ulanga Magharibi), Suleiman Sadiq Murad (Mvomero), Clemence Lyamba (Mikumi) na Omar Mzeru (Morogoro Mjini).

Mkoani ni Mwanza waliotemwa ni Samuel Chitalilo (Buchosa), James Musalika (Nyang'hwale), Ernest Mabina (Geita), Jacob Shibiliti (Misungwi), Bujiku Sakila (Kwimba) na Raphael Chegeni (Busega).

Mikoa ya Kagera na Tabora imewatema wabunge watano wa zamani kila mmoja. Waliotemwa Kagera ni Nazir Karamagi (Bukoba Vijijini), Diodorus Kamala (Nkenge), Wilson Masilingi (Muleba Kusini), Profesa Feetham Banyikwa (Ngara) na Ruth Blasio Msafiri (Muleba Kaskazini).

Wabunge wa Tabora waliokumbwa na fagio la chuma ndani ya CCM ni Tatu Ntimizi (Igalula), Said Nkumba (Sikonge), Siraju Kaboyonga (Tabora Mjini), James Nsekela (Tabora Kaskazini) na Lucas Selelii (Nzega).

Mikoa ya Dodoma, Mara, Mtwara na Pwani imewaacha wabunge wanne kila moja. Waliotemwa mkoani Dodoma John Malecela (Mtera), Pascal Degera (Kondoa Kusini), George Lubeleje (Mpwapwa) na Ephraim Madeje (Dodoma Mjini), wakati waliotemwa Mara ni Profesa Philemon Sarungi (Rorya), Dk. James Wanyancha (Serengeti), Charles Kajege (Mwibara) na Charles Mwera wa Tarime aliyetokana na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Mkoani Pwani waliotemwa ni Dk. Zainab Gama (Kibaha Mjini), Profesa Idriss Mtulia (Kibiti), Ramadhan Maneno (Chalinze) na Dk. Ibrahim Msabaha (Kibaha Vijijini), wakati huko Mtwara ni Mohamed Sinani (Mtwara Vijijini), Raynald Mrope (Masasi), Suleiman Kumchaya (Lulindi) na Dunstan Mkapa (Nanyumbu).

Huko Kigoma wabunge watatu wa majimbo wametemwa ambao ni Kilontsi Mporogomyi (Kasulu Magharibi), Manju Salumu Msambya (Kigoma Kusini) na Felix Ntibenda Kijiko (Muhambwe).

Waliotemwa Shinyanga ni John Shibuda (Maswa) na Charles Mlingwa (Shinyanga Mjini), wakati walioshindwa Rukwa ni Ponsian Damiano Nyami (Nkasi) na Ludovick Mwananzila (Kalambo).

Huko Arusha Felix Mrema (Arusha Mjini) na Elisa Mollel (Arumeru Magharibi), wameshindwa, wakati walioshindwa Mbeya ni Esterina Kilasi (Mbarali) na Guido Sigonda (Songwe). Walioshindwa Singida ni Mgana Izumbe Msindai (Iramba Mashariki) na Juma Kilimbah (Iramba Mashariki), wakati huko Manyara ni Damas Paschal Nakei (Babati Vijijni) na Omar Shaaban Kwaangw' (Babati Mjini).

Wengine waliotemwa ni Mwinchoum Abdulrahman Msomi (Kigamboni, Dar), Mudhihir Mudhihir (Mchinga, Lindi), na Aloyce Kimaro (Vunjo, Kilimanjaro).

Hizi ni mvua za vuli tu, sasa tusubiri masika itakapoanza hapo Agosti 20, mwaka huu wakati kampeni za vyama vyote zitakapoanza rasmi. Ni imani yetu kwamba wananchi wanaweza kuleta mabadiliko makubwa, na kwa hakika jambo hili litakuwa fundisho kwa viongozi ambao wakichaguliwa huamua kufikiria zaidi matumbo yao huku Watanzania walio wengi wakitopea kwenye umaskini mkubwa kwa kushindwa kupatiwa hata huduma muhimu kama afya, elimu na barabara.

SOURCE: DIRA YA MTANZANIA.
Sheria ya Gharama za Uchaguzi yadhihirisha ufisadi wa CCM

Kudakwa wa wagombea na Takukuru ni dalili za kushindwa kupambana na rushwa
Mikoani wakamatwa, Dar wagawa fedha kama njugu usiku wa manane

Na Daniel Mbega

MATOKEO tumeyaona. Ndiyo. Ya makali ya Sheria ya Gharama za Uchaguzi 2010 ambayo imefanikiwa kufichua vitendo vingi, kama si vyote, vya madudu yanayofanywa na watu wanaoomba ridhaa ya wananchi kushika madaraka ya kuongoza Serikali.

Kura za maoni za Chama cha Mapinduzi (CCM) mwaka huu zimefichua maovu mengi ambayo yamekuwa yakifanywa na wale ambao tumekuwa tukiwaamini na kuwapa dhamana ya kuongoza Dola. Wale ambao daima wamekuwa wakisimama majukwaani na kuhubiri kwa HERUFI KUBWA kwamba wanaichukia rushwa kwani ni ‘Adui wa Haki’.

Lakini yaliyoshuhudiwa safari hii ni kinyume cha yale wanayoyahubiri kila siku, na kwa hakika Sheria hii mpya imeanza kukivua nguo hadharani Chama cha Mapinduzi ambacho kimekuwa kikijinasibu katika machapisho yake kwamba kinalaani rushwa na ufisadi.

Hawa hawa ambao safari hii tumeshuhudia wakikamatwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) ndio ambao tunawapa dhamana ya kusaini mikataba mikubwa ya Kimataifa kwa niaba ya Serikali, lakini kwa sura tuliyoishuhudia ni dhahiri kwamba wamekuwa wakiitumia mikataba hiyo kwa maslahi yao kurejesha gharama zao walizotumia kuchaguliwa.

Tunawezaje baadaye kusimama na kusema kwamba mikataba mingi inayosainiwa na watu hawa ina maslahi ya kweli kwa Watanzania wakati wao wenyewe wameingia madarakani baada ya kuwapatia wananchi shilingi 2,000, fulana na pombe.

Kwa kiasi kikubwa hatuna budi kuishukuru Takukuru ambayo tangu siku ya kwanza ya uchukuaji fomu za CCM kwa wanachama wake wanaowania ubunge na udiwani ilitumia mbinu mbalimbali za kudhibiti utoaji rushwa, ingawa kwa namna nyingi baadhi ya maofisa wasio waaminifu wa taasisi hiyo nyeti wamezitumia kura za maoni kutunisha mifuko yao!

Ndiyo. Maofisa kadhaa wasio wazalendo wa Takukuru walitumia mwanya huo kukusanya fedha kwa wagombea ‘wenye hadhi zao’ ambao hawakutaka kufichuliwa vitendo vyao vya ufisadi ili taarifa zao zisitangazwe ama kuvujisha siri na kuwakamata wagombea wengine, yaani washindani na wale waliovujisha siri hizo.

Hili linaweza kukanushwa na wahusika, lakini wale waliojihusisha na vitendo hivyo nafsi zao zinawasuta huko waliko, na kwa hakika mamlaka husika zinapaswa kuwashughulikia ipasavyo kwa maana hawafai kupewa dhamana ya kusimamia utawala bora.

…KWA NINI UFISADI HUU?
Kwa muda mrefu imekuwa ikiripotiwa kwamba, CCM inalea mafisadi na wala rushwa na kwamba hata chaguzi zake nyingi zimekuwa zikigubikwa na vitendo vya rushwa, ingawa viongozi wa chama hicho tawala wamekuwa wakisimama majukwaani na kukanusha huku mishipa ya shingo ikiwatoka kwamba hakuna kitu kama hicho.

Imeshuhudiwa hata ndani ya chaguzi zake nyingi na itakumbukwa kwamba mwaka 2007 katika uchaguzi wa chama hicho Wabunge wawili mkoani Arusha walitakwa na Takukuru kwa tuhuma za kutoa rushwa kwenye mchakato huo.

Ingawa walishinda kesi ya tuhuma hizo, lakini tayari ujumbe ulikuwa umewafikia Wananchi na kuamini hali halisi ilivyo ndani ya chama hicho.

Mwishoni mwa mwaka 2009 wakati wa uchaguzi wa viongozi wa Chipukizi wa CCM mjini Morogoro iliripotiwa kwamba kulikuwepo na vitendo vya rushwa, hali ambayo inatishia usalama wa nchi ikiwa rushwa inaanzia ngazi ya chini kama hii.

Habari kutoka katika mkutano huo uliofanyika katika Chuo cha Ualimu Kigurunyembe Desemba 29, 2009 zinaeleza kwamba kulikuwepo na mazingira ya rushwa na kushinikiza watoto wa vigogo wachaguliwe, ambapo ilifikia mahali makamanda wa chipukizi waliishia kugoma siku moja kabla ya uchaguzi kwa madai kwamba posho waliyopewa ilikuwa ndogo, hivyo wasingekuwa tayari kuwachagua watoto hao wa vigogo. Ikabidi waongezewe shilingi 30,000 kila mmoja.

Hii ilikuwa ni aibu kubwa na ishara mbaya kwa CCM kwa vile sasa hata watoto wadogo wa miaka 10, wanafundishwa kutoa na kupokea rushwa. Wajumbe wa mkutano huo ni wenyeviti wote wa Chipukizi wilaya ambao ni watoto wa miaka 10 hadi 13, na makatibu wa Chipukizi na uhamasishaji wa wilaya ambao huwa ni vijana wakubwa.

Matokeo ya vitendo hivyo vya rushwa yalishuhudia watoto wa vigogo wa CCM - Gabriel Makala ambaye ni mtoto wa Katibu wa Fedha na Uchumi wa CCM Taifa, Amos Makala aliyechaguliwa kuwa Mwenyekiti mpya wa chipukizi taifa baada ya kupata kura 300 kati ya kura 357 zilizopigwa na hivyo kuwashinda wagombea wenzake saba waliojitokeza kuwania nafasi hiyo.

Mbali na Makala pia mtoto wa Rais Jakaya Kikwete, Halfan Kikwete alichaguliwa kuwa mjumbe wa baraza kuu kutoka Tanzania Bara kwa kura 301 bila kuwako ukumbini hali ambayo iliwashangaza wafuatiliaji wengi wa uchaguzi huo.

Uchaguzi huo ulihudhuriwa na Naibu Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Emanuel Nchimbi, mshauri wa rais January Makamba, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, John Guninita, Katibu wa Fedha na Uchumi wa CCM taifa, Amos Makala pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Issa Machibya.

Safari hii katika kura za maoni za ubunge na udiwani tumeshuhudia vigogo wengi, wakiwemo mawaziri na waliopata kushika nyadhifa mbalimbali serikalini – wakiwemo wanasiasa na wabunge wakongwe, wakinaswa na Takukuru kwa vitendo vya rushwa.

Kwa hali iliyojitokeza, napenda kuungana na Waziri Mkuu Mstaafu, Jaji Joseph Sinde Warioba ambaye alikaririwa hivi karibuni akisema CCM bado haijapata dawa halisi ya kupambana na rushwa kuanzia ngazi ya kijiji hadi taifa.

Tumewashuhudia mamluki wengi katika kura za maoni, wenye uwezo wa fedha, wanaoimba nyimbo nzuri na tamu zinazopendeza masikioni, wakitoa ahadi za kufanya hiki na kile, lakini Watanzania tuna mashaka kwamba tunaweza siku tukawakabidhi fisi kuuza nyama buchani, ama mbu akapewa jukumu la kutibu malaria!

Wengi walianza hata kabla ya mchakato wa kura za maoni, wakigawa pikipiki, baiskeli na zawadi kedekede, na wengine wakaanza kuitwa ‘mheshimiwa’ hata kabla ya kuchaguliwa kwa sababu tu wanatumia fedha nyingi ambazo zinaweza kuwa zaidi ya shilingi milioni 200.

Nakumbuka maneno ya Mwalimu Julius Nyerere aliyoyasema kule Mbeya wakati wa Sherehe za Mei Mosi mwaka 1995, alipohoji kwamba wanaotafuta madaraka kwa fedha, tuwaulize wamezipata wapi na watazirejeshaje baadaye?! Isije kuwa fedha za bangi ndizo zinazonunua uhuru wa kidemokrasia wa wananchi na kuwaweka mbwa mwitu wachunge kondoo!

Kama kweli CCM inataka kujisafisha, hebu tuone sasa kwamba wale wote waliokamatwa kwa vitendo vya rushwa, watakapothibitishwa bila shaka na Takukuru, wanaenguliwa katika kinyang’anyiro hicho hata kama watakuwa wameshinda kwenye kura za maoni.

Kinyume cha hapo CCM itambue kwamba kufikia hapa ilipo tayari iko uchi kwa sababu ile ahadi yake iliyoirithi kutoka TANU ya ‘Rushwa ni Adui wa Haki, Sitapokea wala kutoa rushwa’ imevunjwa na wateule wake mchana kweupe.

VURUGU HIZI NI HATARI…
Kwa namna hali ilivyojionyesha kwenye kura za maoni, ni dhahiri kwamba kuna hatari kubwa tunapoelekea kwenye uchaguzi mkuu Oktoba 31, mwaka huu, kwani inaonyesha vitendo cha rushwa vinaweza kuwa maradufu ya hapa.

Tunafahamu kwamba, kampeni kubwa zitakapoanza zikihusisha vyama vyote vya siasa, watakuwepo wanasiasa wa kweli na bandia, ambao – kama tulivyoshuhudia ndani ya CCM – watakuwa tayari kujinadi, kujipendekeza, wakidanganya kwa ngonjera zilizopangiliwa vina vizuri na mizani, wakifanyiana fitina na wengine wakiloga ili tu wapate kuingia madarakani.

Kama tumeshuhudia hata maofisa wa serikali wenye dhamana ya utawala bora wakitoa fedha ili wachaguliwe kwenye kura za maoni, nadhani safari hii itakuwa zaidi kwa sababu hiki kitakuwa kihunzi cha mwisho cha neema.

Hili ndilo linalowafanya Watanzania wengi wahisi hatari iliyopo mbele yao, hasa kwa kuzingatia kwamba fedha inawatia wengi wehu na kuwasahaulisha msimamo waliokuwa nao awali wa kuleta mabadiliko.

Kama chama kinachotawala kina watu wabovu, waliooza kwa rushwa na ufisadi kama tulivyoshuhudia, wananchi watakuwaje na imani tena hapo baadaye?

Watanzania tuna kila sababu ya kuleta mabadiliko ya kweli, kwa kukemea, kukosoa na kutoa mapendekezo ya kizalendo ambayo yataendelea kuifanya nchi hii kuwa kisiwa cha amani, utulivu na mshikamano. Hatupaswi kuwa wanafiki kwa sababu kuwalinda watu fulani, kwa sababu kufanya hivyo tutakuwa tunaweka msingi mbovu ambao utakiharibu kizazi cha sasa na kijacho.

SOURCE: DIRA YA MTANZANIA.
Watanzania ‘wana imani’ na Dk. Slaa
*Anauzika, anachagulika na mzalendo wa kweli
Na Clement Magembe
DK.WILLIBROD Peter Slaa ,Katibu Mkuu wa CHADEMA ambaye amependekezwa na chama hicho kuwania nafasi ya urais anatajwa kuwa ni mwiba mkali kwa mgombea wa nafasi hiyo kwa tiketi ya CCM, Rais Jakaya Kikwete.
Dk. Slaa ni jina ambalo limekuwa likisikika sana katika jamii ya Watanzania kutokana na kuonekana kama shujaa aliyekuwa na utayari wa kuthubutu kupigana vita dhidi ya “wakoloni wazawa” au mafisadi kama wanavyofahamika sasa, waliojitokeza kwa ajili ya kudhulumu rasilimali zilizopo nchini kwa maslahi yao binafsi na watu wanaoingizwa nchini kwa kivuli cha uwekezaji.
Watanzania wengi wanathibitisha kuwa ni kiongozi safi na bora, shujaa, mkakamavu na mkemea hila na mienendo mibaya ya watu walioko madarakani waliozoea kuwayumbisha Wananchi tangu kupatikana kwa uhuru wa taifa hili na pia kufanikiwa kwa kiasi kikubwa kuigawa jamii baina ya matajiri na masikini ambao ndio wengi wanaopoteza maisha baada ya kupokea ahadi hewa kutoka kwa wagombea urais, ubunge na udiwani.
Jina la Dk.Slaa sio geni miongoni mwa Watanzania wengi kutokana na mchango wake kufichua “ufisadi” uliofanyika Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na maeneo mengine na kuithibitishia jamii ya Watanzania kuwa wafanyabiashara walioamua kufanyabiashara na chama tawala na baadhi ya viongozi waliokosa uaminifu kwa kulitumikia taifa kwa mujibu wa ‘mashairi’ ya ilani zao walizozinadi wakati wa kuomba ajira kwa wapiga kura.
Sakata la wizi wa fedha za EPA ndani ya BoT hili ndilo limefanya jina lake liwe miongoni mwa majina maarufu sio tu kutoka kambi ya upinzani bali katika anga za wanasiasa nchini Tanzania.
Dk.Slaa alizaliwa katika kijiji cha Kwermusl, Wilaya ya Mbulu Oktoba 10, mwaka 1948 na kupata taaluma ndani na nje ya Nchi hadi kufikia hadhi ya Udaktari wa Falsafa na kuamua kuingia katika uwanja wa siasa mwaka 1995.
Awali alishiriki shughuli mbalimbali za uongozi akiwa katibu wa TANU Youth League Seminari ya Kipalapala na kufungua matawi mengi ya TANU wakati huo, Katibu wa Shina la CCM, Tawi la Mambo ya Nje, Rome mwaka 1980.
Aliamua kugombea ubunge baada ya Wazee wa Karatu kumfuata akiwa jijini Dar es Salaam wakati wa uchaguzi mkuu uliovirikisha vyama vingi vya siasa wa vyama huku vilivyokuwa na nguvu kubwa ikiwa ni pamoja na CCM, Chadema, NCCR-Mageuzi na CUF.
DK.Slaa aliingia kwenye uwanja wa kisiasa kupitia CCM ambacho alikichagua kutoka awali na kushinda kura za maoni lakini jina lake liliondolewa kwa mizengwe kwa sababu yeye “hakuwa mwenzao” na kwamba alifahamu baadae kuwa alipotea njia kutokana na hali ya ufisadi iliyojitokeza.
Pamoja na hayo anaeleza kuwa hakujutia kabisa hali hiyo na kuamua kujiunga na Chadema na kufanikiwa kupata nafasi hiyo na kuwatumikia Wananchi wa Karatu kama alivyowaahidi.
Slaa alikuwa Padre wa Kanisa Katoliki na kushika nafasi za juu za uongozi ndani ya Kanisa hilo kuanzia jimboni kwake akiwa Makamu wa Askofu, Mkurugenzi wa Maendeleo na Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu (TEC) 1985 hadi 1991 na kuamua kuachana na Upadre bila kushinikizwa na yeyote, wala kufukuzwa, wala hata kupewa onyo, wala kuwa na ugomvi wa aina yeyote na Kanisa Katoliki na mshiriki wa shughuli mbalimbali za Kanisa.
Achilia mbali historia aliyojingea kwa kipindi chote alichokuwa akishikilia nafasi ya ubunge huku akiiadhibu serikali ya CCM kwa kufichua kila namna uovu uliokuwa umesitirika kwa kipindi kirefu huku chama hicho kikigeuzwa kama pango la wanyang’anyi wasiojali wala kuthamini haki za Wananchi wa kawaida.
Dk. Slaa ambaye anakuwa silaha kali ya kanisa Katoliki lenye idadi kubwa ya wafuasi nchini anaelezwa kuwa ni chaguo la kanisa hilo ambalo hivi karibuni kwa nyakati tofauti litoa waraka wake unaotaka kuchaguliwa kwa viongozi wa nchi walio chini ya dhehebu hilo watakaotekeleza wajibu wao wa kuitumikia jamii baada ya umaarufu wa CCM kuonekana kuyumba kutokana na baadhi ya wanachama na wafadhili wake kuonekana ni watu ovyo na watuhumiwa wa ufisadi.
Kuteuliwa kwa Dk.Slaa kuwania nafasi ya urais kwa tiketi ya Chadema hakuungwi mkono na kanisa Katoliki tu bali wananchi wa kada mbalimbali wapenda mabadiliko na wengi wao wanatajwa kuwa Wafanyakazi wa serikali ambao rais Kikwete aliwaeleza kuwa hazihitaji kura zao baada ya kutishia mgomo ili kushinikiza nyongeza ya mishahara yao na kuwakataa viongozi wa serikali kuwa wageni rasmi katika maadhimisho ya Siku kuu ya Wafanyakazi (Mei Mosi) mwaka huu.
Wachunguzi wa masuala ya kisiasa wanaeleza kuwa wanachotazamia ni mabadiliko makubwa ya kiutawala nap engine kuutokomeza utawala dhaifu ambao umekuwa chanzo cha umasikini kwa Watanzania baada kuingiliwa na kundi la wafanyabiashara matapeli waliojiingiza kufanya biashara na Serikali kwa mgongo wa ufadhili wa CCM.
Kutokana na hali ilivyo sasa huku migogoro baina ya Wastaafu wa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki, Waislamu wanaodai ahadi ya Mahakama ya Kadhi na OIC na mengine ushindani mkubwa utaibuka katika uchaguzi mkuu ikiwa tofauti kabisa na chaguzi zilizopita.
Hakuna mtetezi tena kwa CCM aliye na sauti ya kuonya ili kukinusuru chama hicho ama kutuliza hasira za Wananchi wanaoishi maisha bora ya kufikirika sambamba na kejeri za mafanikio ya misongamano ya magari katika barabara za Jiji la Dar es Salaam.
Ufisadi, rushwa na madudu mengine yanayoonyeshwa na waliojitokeza kuwania nafasi za ubunge na udiwani kwa tiketi ya CCM ni fimbo nyingine ya wananchi kutaka mabadiliko ya Uongozi, Katiba, Tume Huru ya Uchaguzi baada ya kwa kuichagua kambi ya upinzani na lengo kubwa likiwa ni kunufaika na rasilimali za taifa hili ambazo zinawanufaisha watu wachache na wageni huku maelfu wakipoteza maisha kwa kukosa huduma za afya.
Lakini jambo jingine ambalo linakuwa ni mwiba kwa CCM na kikomo cha utawala wake ni kile kinachoelezwa kuwa ni kukorofishana na Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF), Zachary Kakobe, ambaye alikuwa mtetezi mkubwa wa serikali ya awamu ya nne baada ya Maaskofu wa Katoliki na Waumini wa dini ya Kiislamu kuitisha serikali kwa nyaraka nzito zilizoonesha kuuchukia utawala wake.
“Sasa hawana mtetezi kabisa na kila mmoja anafanya jitihada zake mwenyewe ili kuingia madarakani au kuanguka, utawala wa CCM umefitinika na hakuna unafuu mamilioni ya Wananchi wanyonge watamuunga mkono Dk. Slaa ili kuliletea maendeleo ya kweli taifa hili”, alieleza Richard Conrad aliyejitambulisha kuwa ni mwanachama wa CCM mpenda mabadiliko na mkazi wa Kimara Bucha Jijini Dar es Salaam.
Anasema kuwa CCM haina mtetezi kwa kuwa watu wamechoka na ufisadi huku watuhumiwa wakikingiwa kifua kwa kufunguliwa kesi zinazoendeshwa kwa mfumo wa filamu na michezo ya mazingaombwe.
Anasema kuwa uongozi wa kununua kwa sasa utafikia kikomo baada ya wanyonge kutafuta ukombozi baada ya kilio cha muda mrefu na uziwi wa viongozi wa serikali ambao hawataki kusikia wala kuelezwa lolote lile licha ya kutoa ahadi za kilaghai.
Chadema inajulikana wazi kwa misimamo yake katika maswali mbalimbali ikiwemo kushindwa kwa CCM kupiga vita rushwa, taifa kupoteza mwelekeo katika mambo mbalimbali huku Serikali ikigeuka kiziwi na kujipongeza na miradi ya MMEM na MMES, ambayo kimsingi si sera yao ikiwa imetokana na maamuzi ya Kimataifa yaliyofanyika Jomtien, Thailand, mwaka 1990.
Uchafu ulioambatana na kuchota fedha BoT, Tangold, Meremeta kupitia DEEP GREEN,kuingiza serikali katika mkataba wa kitapeli wa kampuni ya kufua umeme ya RICHMOND na tuhuma zingine zilizoibuliwa na kambi ya upinzania umekitia kiwewe chama hicho ambacho sasa kimebakiwa na propaganda za kisiasa zikiambatana na ilani zisizotekelezeka jambo linaloacha maswali juu ya usalama wa rasilimali za umma.
SOURCE: DIRA YA MTANZANIA.
Shigongo kiungo sahihi maendeleo ya Buchosa
Na Mwandishi Wetu
ILIMCHUKUA muda mrefu kuamua kukubali ombi la wananchi wa Buchosa. Kwa kitambo kirefu walimtaka awe mbunge wa jimbo lao. Waliamini katika maono yake, nidhamu aliyonayo, sifa aliyojaaliwa ya uchapakazi, moyo wa kujitolea kwa wengine na upendo kwa watu wote.
Mwalimu wa Kimataifa wa somo la ujasiriamali, Eric James Shigongo ameamua kusikia la wakuu. Tofauti na vipindi vilivyopita, awamu hii ameona si vema kuendelea kuchelewa kutii ombi la wazee wa Buchosa na wananchi wengine wanaomuamini na kumpenda. Amechukua fomu ya kugombea ubunge, na sasa yupo uwanja wa mapambano.
Shigongo ambaye ni kada wa siku nyingi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) aliye pia Mwenyekiti Mstaafu wa Kamati ya Ukimwi katika Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), anapoamua kugombea Buchosa, anageuza tafsiri ya “mti ukirefuka sana, hutoa faida kwa jirani kuliko kwa mmiliki.”
Umepanda mti unarefuka mno. Matokeo yake kivuli kinakwenda nyumba ya jirani. Shigongo anaona hilo siyo sawa. Kwa umaarufu wake na jinsi alivyojitawanya kitaifa angeweza kugombea majimbo mengine na kushinda lakini kwa kutambua alipotoka, anarudi Buchosa alikozaliwa.
Je, unadhani Shigongo anahitaji ubunge tu? Kama unafikiria hivyo, hapo utakuwa umekosea. Tena upo mbali mno na ukweli! Kilichompeleka kugombea Buchosa ni kurejesha kivuli nyumbani. Ana wito wa shida walizonazo wananchi.
Alizaliwa hapo, anajua matatizo ya ndugu zake. Alishiriki miradi mingi ya kusaidia jimbo lake, lakini anaamini akiwa mwakilishi wa jimbo hilo ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, atasaidia kuharakisha maendeleo. Atakuwa msaada wa Mwenyekiti wa CCM Taifa, Jakaya Kikwete katika kutekeleza ilani ya chama.
“Sigombei ubunge kutaka gari, umaarufu au uwaziri. Nimevutwa na shida walizonazo wananchi wa Buchosa. Nina nia ya dhati ya kushirikiana na Rais Kikwete katika kuwaletea maendeleo ya kweli wananchi wa Buchosa,” anasema Shigongo anapowasha taa kuomba njia ya kupita kuelekea bungeni, Dodoma.
Anasema: “Nimezaliwa Buchosa na kukulia hapo. Nawajua ndugu zangu wa Buchosa, nazitambua shida zao. Wanahitaji mtu makini ambaye anaweza kuwaongoza. Ambaye atarudisha umoja wao ambao kwa muda mrefu umetoweka. Kuna makundi kwa sababu za kisiasa, mimi nataka nizimalize tofauti zote halafu tushirikiane kuleta maendeleo.
“Sitaki kusema uongo, niwadanganye wananchi kwamba mimi ni msomi mkubwa au nina degree (shahada ya chuo kikuu). Siwezi kujivika sifa ambazo sina, ila nina uwezo wa kusimamia kitu kutoka sifuri hadi kupanda juu kabisa kama ambavyo maisha yangu ya kijamii na kibiashara yanavyojifafanua.”
Hata hivyo, Shigongo anatoa mwanga kwa wana Buchosa kuchagua kilicho bora kulingana na upeo wao. Anasema: “Siingii kwenye kinyang’anyiro cha ubunge Buchosa kufanya siasa za chuki. Hata siku moja sitozua kitu kumchafua mtu, wala sitothubutu kutukana mtu.
“Nitaeleza dhamira yangu ya kuleta maendeleo na umoja kwa ndugu zangu. Kila mara natembelea nyumbani kwetu na kuona watu wanavyotaabika. Kwa miaka yote, Buchosa hatuna hata high school (shule ya juu) hata moja. Vijana wa kike wanashindwa kuendelea na masomo, matokeo yake wanakwenda kutafuta unafuu visiwani.
“Huko nako siyo pazuri. Wengi wanaambukizwa virusi vya ukimwi na kugeuka mzigo kwa familia zao. Tiba ya hilo ni kujenga shule za juu na za ufundi. Vijana wasome na kujifunza kujitegemea. Kama wana Buchosa watanipitisha, nitashirikiana nao kupata ufumbuzi wa kudumu wa matatizo hayo.”
Kwanini Buchosa? Shigongo analijibu hilo: “Nikiwa Dar es Salaam, naishi Mbezi, kwahiyo ningeweza kugombea Kawe. Mwanza mjini, nyumbani kwangu ni Capripoint, kwahiyo ningeweza kusimama na kugombea Nyamagana. Wazazi wangu wanaishi Nyakato, ningeweza kugombea Ilemela.
“Kote huko naishi vizuri na watu, wananipenda na wao wananipenda. Sina kawaida ya kuwa na matatizo na watu, lakini akili yangu haipo kwenye jimbo lolote zaidi ya Buchosa. Mimi ni mtu wa Buchosa. Hata nikiwa naishi Marekani, nikifa maiti yangu itarudishwa Buchosa.
“Ninavyoishi na familia yangu kila siku, nawafundisha watoto wangu watambue kuwa wao nyumbani kwao ni Buchosa. Hii ndiyo sababu iliyonifanya nisichague jimbo lolote, badala yake nirudi nyumbani kwetu, na kama ni mafanikio basi niyajenge kwenye ardhi niliyozaliwa.
“Na kwa sababu Buchosa ni nyumbani, sitokubali siasa za chuki zichukue nafasi na kuongeza uadui ambao umekuwepo kwa muda mrefu. Makundi ya mwanasiasa huyu na yule, mimi nataka kumaliza matabaka, lakini nawataka watu wa Buchosa kufanya uchaguzi wa sahihi.
“Wamchague mtu ambaye anaweza kumaliza uadui uliopo kwa muda mrefu. Hata kama siyo mimi, basi watupe kiongozi ambaye hatotufanya tujute kwa miaka mitano ijayo. Mimi najiamini kwa sababu nina dhamira ya dhati. Uongozi ni uwezo, moyo na hekima kutoka kwa Mungu.”
Shigongo anasema kuwa wananchi wa Buchosa wana kila sababu ya kumuamini kwa sababu amejaliwa karama na Muumba ya kuongoza na kusimamia vitu. Anaeleza kwamba nguvu iliyomhamisha kutoka katika maisha duni kwenye kijiji cha Bupandwa, Buchosa wilayani Sengerema ni hoja kuu ya kukubali maono yake.
Kada huyo wa CCM ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Global Publishers & General Enterprises Ltd, inayochapisha magazeti mbambali maarufu nchini, anasema kuwa kutanuka kibiashara kwa kampuni yake mpaka Los Angeles, California, Marekani ni ishara ya wazi kwamba anaweza kuongoza.
Anasema kuwa ndoto zake ni kuona vijana wengi zaidi wa Buchosa wanapata muamko wa kusaka maendeleo yao. Anaeleza kwamba hilo halitowezekana endapo hawatopata mtu anayewapenda, atakayewatetea, kuwapigania na kuwapa muongozo ambao ni taa ya mafanikio.
Shigongo anaeleza kwamba atakapokuwa mbunge wa Buchosa, atakuwa taa ya vijana kuwa wajasiriamali. Atahakikisha anautumia uzoefu wake kama tiba kwa wengine. Anasisitiza: “Nimezunguka sehemu mbalimbali nafundisha watu kuwa wajasiriamali.
“Nimetoa semina nyingi nchini. Naandika makala ya Waraka wa Shigongo kwenye gazeti la Ijumaa Wikienda ili kuwasaidia watu kujikwamua kiuchumi. Hivi karibuni nilikuwa Minnesota, Marekani ambako nilizungumza na Watanzania wanaoishi nchini humo na kuwaambia umuhimu wa kuja nchini tujenge nchi.
“Uzoefu wangu huo wa kibiashara na kufundisha ujasiriamali, naamini ni lulu itakayorahisisha maendeleo ya mtu mmoja mmoja kwa wakazi wa Buchosa na jimbo letu kwa jumla. Naomba waniamini ili tutumie fursa tulizonazo ili kusaidia kizazi cha sasa na kijacho jimboni kwetu.
“Buchosa tuna msitu mkubwa. Tuna ziwa na ardhi yenye rutuba kuliko sehemu yotote ya mkoa wa Mwanza. Endapo wana Buchosa wataniamini na kuniteua kuwa mgombea kwenye chama changu na baadaye kunichagua kuwa mbunge, naamini tunaweza kuifanya Buchosa kuwa kitovu cha uchumi Mwanza.”
Shigongo ambaye alijipatia umaarufu mkubwa nchini kutokana na umahiri wake wa kuandika riwaya zinazochapishwa na magazeti pendwa nchini na kuvutia wasomaji wengi, anawaonya wakazi wa Buchosa kutomhukumu kwa sababu hana shahada ya chuo kikuu.
Mwandishi huyo wa vitabu vya Machozi na Damu, Siku za Mwisho za Uhai Wangu na Rais Anampenda Mke Wangu, anawakumbusha kauli ya mzee mmoja anayeitwa Matahekumi ambaye alisema akiwa kwenye kijiji cha Nyakalilo, Buchosa kuwa Chama cha Ushirika cha Nyanza kilikufa kwa sababu ya kuwaamini wasomi.
Shigongo anasema kwa kumnukuu Matahekumi: “Nyanza ililelewa na wazee ambao hawakuwa na elimu ya darasani, lakini kwa sababu walikuwa na nidhamu ya kuongoza, chama kilikua mpaka kikafikia hatua ya kutaka kununua ndege.
“Lakini chama kilipokabidhiwa kwa wasomi kilikufa hapo hapo.” Baada ya mfano huo, Shigongo anasema: “Ni vizuri wana Buchosa wakaniamini. Elimu ya kuwaongoza ninayo, tena kubwa mno ambayo inaweza kuwasaidia. Kuhusu shahada ya Chuo Kikuu, wachukue kauli ya kizalendo ya mzee Matahekumi.”
Shigongo mbali na ujasiriamali, pia alipata umaarufu mkubwa pale alipoanzisha na kusimamia kampeni mbalimbali za kusaidia jamii ya watu wenye matatizo, wakiwemo wagonjwa waliokata tamaa na kuwawezesha kupata tiba bora nje ya nchi, hasa India na kupona kabisa.
Akiwa Mwenyekiti wa Kamati ya Ukimwi katika UVCCM, Shigongo aliendesha kampendi maalum ya kupiga vita ugonjwa huo. Alihakikisha kila mwaka anaandaa kauli mbiu na maonesho maalum katika mikoa mbalimbali nchini, yenye sura ya kupambana na VVU kila Desemba Mosi ambayo kwa kawaida ni kilele cha Siku ya Ukimwi Duniani.
Mwaka 2005, wazee na wananchi wengine wa Buchosa walimtaka agombee, lakini kutokana na kukabiliwa na matatizo ya kifamilia, aliamua kumpa ushirikiano mbunge anayemaliza muda wake, Samuel Chitalilo.
Hata hivyo, uamuzi huo uliibua hasira kwa wazee, wazazi pamoja na wakazi wengine wa jimbo hilo ambapo mwaka 2006, Shigongo alilazimika kutoa waraka maalumu uliojaa ukurasa mzima kwenye gazeti la Uwazi, akiomba radhi na kuahidi kutowaangusha kwenye Uchaguzi Mkuu 2010.
Shigongo, alizaliwa miaka 40 iliyopita kwenye kijiji cha Mwangika, Buchosa wilayani Sengerema Mwanza. Ni baba wa familia yenye mke mmoja, Veneranda na watoto watatu, Andrew, Samuel na Baraka. Ni mkulima pia, anamiliki shamba la ekari 250 Kiwangwa Bagamoyo na anayo kampuni ya matrekta.
Mwenye kisu kikali ndiye atakula nyama Songea Mjini 2010

* Dk. Nchimbi atamba amefanya mengi, ahukumiwe kwa mafanikio
* Asema ni haki kwa yeyote kugombea, lakini Mbunge ni mmoja tu

Na Mwandishi Maalum, Songea

“Usimpe maskini samaki, mfundishe jinsi ya kuvua!” Huu ni msemo wa Wahenga ambao kwa hakika una mantiki kubwa katika maisha yetu ya kila siku. Ukimpa samaki atakula, atashiba, lakini kesho njaa itamuuma tena, atakufuata, hivyo bora umfundishe uvuvi ili njaa ikimuuma hatavua wa kula pekee bali na wa akiba.
Tafsiri hii ndiyo inayoonekana kutumika kwa Mbunge wa Songea Mjini (CCM) Dk. Emmanuel John Nchimbi, baada ya kufanikisha ujenzi wa Shule ya Sekondari Mkuzo ambayo itakuwa inachukua wanafunzi wa kidato cha tano na sita.
Shule hiyo iliyojengwa katika eneo la Msamara, Kata ya Bombambili katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea Mjini, tayari imekwishakabidhiwa serikalini tangu mwezi Mei 2010 ili kusaidia kupunguza tatizo la wanafunzi kukosa nafasi za kujiunga na masomo ya kidato cha tano, hivyo kuwakomboa kielimu wananchi wa Songea.
Shule hiyo imejengwa kwa gharama ya shilingi milioni 112 bila ya michango ya wananchi na ina madarasa 10 na jengo la utawala ambapo kwa sasa ina uwezo wa kuchukua wanafunzi 400 kwa wakati mmoja na itakapokamilika itakuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi 800 kwa wakati mmoja.
Dk. Nchimbi anasema ameijenga shule hiyo kutokana na misaada aliyoipata kutoka kwa ndugu, marafiki zake na mshahara wake wa unaibu waziri wa miaka minne iliyopita.
Mbali ya kujenga mwenyewe shule hiyo, lakini pia maeneo mengine ambayo amechangia katika sekta ya elimu kuwa ni msaada wa fedha za ujenzi wa sekondari za kata zote 13 za Manispaa ya Songea vikiwa na thamani ya shilingi 141,398,000, kununua vitabu kwa ajili ya shule za sekondari binafsi na serikali vilivyogharimu shilingi milioni 30, na pia anawalipia ada wanafunzi 28 wa sekondari, wanafunzi 10 wa vyuo vya kawaida, na wanafunzi sita wa chuo kikuu, ambapo gharama zake ni jumla ya shilingi 11,900,200.
"Wananchi wenzangu leo nawakabidhi majengo mazuri ya sekondari hapa Mkuzo niliyoyajenga kwa zaidi ya milioni 112/=. Kwa fedha hizi ningeweza kujenga hoteli nzuri ya kisasa kwenye uwanda mzuri wa Matogoro na kuzifungua kifahari, lakini ingekuwa kwa maslahi yangu na familia yangu, lakini kwa kuwa nawapenda nimeamua kuwekeza kwenye elimu ya watoto wetu wote wa Songea," alisema Nchimbi siku ya kukabidhi shule hiyo.
"Leo ni siku muhimu katika manispaa yetu mtakumbuka miaka minne iliyopita CCM iliahidi kuwa tuitajenga sekondari kila kata ni faraja kubwa jambo hilo tumelikamilisha, matokeo ya kujenga shule yapo wazi kwani uwekezaji wa elimu ni muhimu kuliko yote," anasema Dk. Nchimbi na kuthibitisha kwamba elimu bora ni sawa na kumfundisha mtu uvuvi badala ya kumpatia samaki kwa njaa ya siku moja.
Dk. Nchimbi anasema pamoja na mafanikio hayo lakini bado kuna changamoto nyingi katika sekta hiyo ya elimu jimboni kwake ambapo alizitaja changamoto hizo kuwa ni upungufu wa walimu, vifaa, kuboresha majengo na miundombinu ya shule za msingi, walimu kulipwa haki zao kwa wakati na kujenga chuo kikuu mjini Songea ambacho kitasaidia wananchi wa mkoa wa Ruvuma kujiendeleza zaidi kielimu.
Anasema iwapo wananchi wataendelea kumpatia ushirikiano atasaidiana nao kujenga chuo kikuu katika Manispaa hiyo kwani kwa sasa ndoto yake kubwa ni kuhakikisha kuwa watoto wote wenye uwezo wa kusoma wanaenda shule ili kuongeza idadi ya wasomi katika mkoa wa Ruvuma, ahadi ambayo ilipokelewa kwa shangwe na wazazi pamoja na wanafunzi.
Wananchi wa Jimbo hilo bado wanalalamikia kero mbalimbali zinazowakabili na wamemtaka mbunge wao aongeze juhudi za kutatua kero hizo katika sekta ya maji, umeme, afya, elimu na barabara.
Lakini Dk. Nchimbi anasema kwa kipindi cha miaka minne na nusu ya uwakilishaji wake amejitahidi kutekekeza ahadi zake muhimu alizoziahidi, ambazo anasema zilikuwa kikwazo kwa maendeleo ya wapiga kura wake katika sekta ya elimu, afya na barabara, ingawa amewaomba wapiga kura wake wawe na subira kwani kero zao anazitambua na ameanza kuzitatua ingawa anakiri kuchelewa kuzitatua.
Ujenzi wa shule za sekondari za kata uligharimu fedha nyingi, ambapo wananchi walichanga jumla ya shilingi milioni 60 na Manispaa ikachangia shilingi milioni 70, hivyo kufanya kata zote kuwa na shule.
Jimbo hili la Songea Mjini lina jumla ya Kata 13 ambazo ni Matogoro, Mletele, Bombambili, Mshangano, Ruhuwiko, Subira, Ruvuma, Lizaboni, Majengo, Matarawe, Misufini na Mjini.
Katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu, wapo watu ambao wamekuwa wakisema kwamba huenda hizi ni mojawapo ya kampeni, jambo ambalo Dk. Nchimbi analikanusha na kusema kwamba ujenzi huwa hauchukui siku moja, bali ni mipango ya muda mrefu, hivyo lilikuwa mojawapo ya ahadi zake kwa wananchi na amelitekeleza.
Kauli hizi zimekuwa zikitolewa katika kipindi hiki ambacho vuguvugu la uchaguzi limepamba moto ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM), ambapo katika jimbo hilo mbali ya Dk. Nchimbi anayetaka kulitetea, wamejitokeza watoto wa wanasiasa wakongwe nchini, Balozi Paulo Mhaiki na Nassor Hassan Moyo, ambao ni Oliver Mhaiki na Said Nassor Moyo.
Mhaiki, Katibu Mkuu wa Wizara ya Sheria na Katiba, anajivunia uzawa na ukazi mjini Songea, huku baadhi ya watu wakisema kwamba Dk. Nchimbi hakuzaliwa Songea na kwamba amejenga Mbeya.
Lakini hoja za aina hii ni za ubaguzi ambazo hazistahili kupewa nafasi, kwani Tanzania ni moja na masuala ya ukabila, udini hayastahili kupewa nafasi kwa sababu mwishowe zitakuja kuzuka hoja za “Huyu ni mtoto wa ukoo gani?” na mambo kama hayo.
Dk. Nchimbi anabainisha kwamba, ni haki kwa mwananchi yeyote mwenye sifa kugombea, kwani hata Katiba ya nchi inaeleza hivyo, lakini anaamini kwamba wananchi watamhukumu kwa mafanikio yake.
“Nimejitahidi kwa kadiri ya uwezo wangu, pamoja na majukumu mengi ya kiserikali niliyo nayo, hata hivyo huwezi kumridhisha kila mtu, na daima kero zote haziwezi kutatuliwa mara moja. Naamini nimefanya mengi na wananchi watakuwa mashuhuda.
“Wacha wajitokeze wengi kwa sababu ndiyo demokrasia, lakini naamini mwisho wa siku Mbunge atakuwa mmoja! Hili halina ubishi,” anabainisha Dk. Nchimbi ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.
Wachunguzi wa masuala ya siasa wanaona kwamba, nguzo pekee ya kuegemea ni kama kiongozi aliyechaguliwa na wananchi anawaletea maendeleo ama la, bila kujali anatoka mahali gani.
Ni wazi kwamba joto la uchaguzi jimboni humo limepanda kwa nyuzi nyingi, lakini wananchi ndio watakaopima mafanikio na kuamua kwa busara nani anayestahili kuwaongoza badala ya kuanzisha hoja zisizo na msingi.
Kwa sasa siasa chafu ndizo zinazotawala ndani ya jimbo la Songea Mjini, ambapo kuna kundi la mgombea mmoja lililodhamiria kumchafua mgombea mwenzake kwa kila hali na kuhakikisha anashindwa katika kura za maoni.
Kitendo cha kutumia mbinu za aina hiyo hakipaswi kufumbiwa macho, kwa sababu hakilengi kutumia demokrasia ya kweli bali hila za wazi, ambazo mwelekeo wake hautakuwa na matunda mazuri hata kama anayetumia mbinu hizo chafu ataingia madarakani.
Kwa upande wao baadhi ya wananchi wamesema kuwa kitendo cha Mbunge wao kuwajengea shule ni cha kuungwa mkono na wananchi wote wa manispaa hiyo kwani shule hiyo itawasaidia wananchi wote bila kujali itikadi za dini na siasa kupata elimu na wamewataka wenzao kuunga mkono jitihada za mbunge huyo.
Jacob Chidumule, mkazi wa Kata ya Matarawe, anasema kipindi cha uchaguzi kina mambo mengi, lakini lazima wananchi watumie busara wanapotaka mabadiliko ya maendeleo na siyo kufanya mabadiliko kwa shinikizo la watu wachache.
“Tunahitaji maendeleo, lakini siyo kukurupuka na kusema tunataka mabadiliko bila kutathmini mafanikio yaliyopatikana kwa yule tuliyemchagua. Binafsi naamini Nchimbi bado anastahili kutuwakilisha. Maendeleo yanaletwa kwa ushirikiano wa wote, viongozi na wananchi, na tusiwaachie viongozi pekee,” anafafanua Chidumule.
Naye Hassan Komba, mkazi wa Kata ya Bombambili, anasema kwamba CCM itafanya makosa ikiwa italeta mabadiliko ya lazima kwa mwakilishi, kwani wananchi bado wana imani na Mbunge wa sasa.
“Wakifanya mabadiliko ya ghafla, hakika wanaweza kujikuta wakilipoteza Jimbo kwa wapinzani. Tunaamini Mbunge wa sasa bado ana uwezo wa kuleta maendeleo. Hizi hoja za kazaliwa wapi anaishi wapi zisilete matabaka na hazijengi. Sote ni Watanzania na tunapaswa kuthaminiana kwa Utanzania wetu, tusije tukafikia mahali tukaanza kuulizana huyu ni mtoto wa nani?” anaonya Komba.
Felister Herman Haule, mkazi wa Kata ya Ruhuwiko, mewataka wananchi wenzake wa Manispaa ya Songea kumuunga mkono Mbunge wao kwa kushirikiana naye kwa vitendo ili kulipa shukrani kwa kuwakomboa kielimu kwani kitendo chake cha kujenga shule kitasaidia wananchi wengi kupata elimu na hivyo kuwa na wasomi ambao watasaidia kuleta maendeleo.
"Elimu ni msingi wa maendeleo yetu, Dk. Nchimbi amesababisha watoto wetu waende shule, ametoa fedha zake ili wananchi wake wajikomboe na tatizo la ujinga na umaskini hivyo wananchi tuache kubabaishwa na majambazi wa siasa tuchague viongozi ambao watatusaidia kujikomboa kielimu, kiuchumi na kulisaidia taifa letu katika nyanja mbali mbali za maendeleo,” anasema.
Fomu za kuwania Ubunge kwa upande wa Chama cha Mapinduzi (CCM) zinatarajiwa kuanza kutolewa Julai 19, mwaka huu, na kampeni ndani ya chama hicho zitaanza mapema mwezi Agosti.
Tusubiri tuone matokeo, lakini hakika mwenye kisu kikali ndiye atakayekula nyama Songea Mjini mwaka 2010!
SOURCE: DIRA YA MTANZANIA.
Mwenye kisu kikali ndiye atakula nyama Songea Mjini 2010

* Dk. Nchimbi atamba amefanya mengi, ahukumiwe kwa mafanikio
* Asema ni haki kwa yeyote kugombea, lakini Mbunge ni mmoja tu

Na Mwandishi Maalum, Songea

“Usimpe maskini samaki, mfundishe jinsi ya kuvua!” Huu ni msemo wa Wahenga ambao kwa hakika una mantiki kubwa katika maisha yetu ya kila siku. Ukimpa samaki atakula, atashiba, lakini kesho njaa itamuuma tena, atakufuata, hivyo bora umfundishe uvuvi ili njaa ikimuuma hatavua wa kula pekee bali na wa akiba.
Tafsiri hii ndiyo inayoonekana kutumika kwa Mbunge wa Songea Mjini (CCM) Dk. Emmanuel John Nchimbi, baada ya kufanikisha ujenzi wa Shule ya Sekondari Mkuzo ambayo itakuwa inachukua wanafunzi wa kidato cha tano na sita.
Shule hiyo iliyojengwa katika eneo la Msamara, Kata ya Bombambili katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea Mjini, tayari imekwishakabidhiwa serikalini tangu mwezi Mei 2010 ili kusaidia kupunguza tatizo la wanafunzi kukosa nafasi za kujiunga na masomo ya kidato cha tano, hivyo kuwakomboa kielimu wananchi wa Songea.
Shule hiyo imejengwa kwa gharama ya shilingi milioni 112 bila ya michango ya wananchi na ina madarasa 10 na jengo la utawala ambapo kwa sasa ina uwezo wa kuchukua wanafunzi 400 kwa wakati mmoja na itakapokamilika itakuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi 800 kwa wakati mmoja.
Dk. Nchimbi anasema ameijenga shule hiyo kutokana na misaada aliyoipata kutoka kwa ndugu, marafiki zake na mshahara wake wa unaibu waziri wa miaka minne iliyopita.
Mbali ya kujenga mwenyewe shule hiyo, lakini pia maeneo mengine ambayo amechangia katika sekta ya elimu kuwa ni msaada wa fedha za ujenzi wa sekondari za kata zote 13 za Manispaa ya Songea vikiwa na thamani ya shilingi 141,398,000, kununua vitabu kwa ajili ya shule za sekondari binafsi na serikali vilivyogharimu shilingi milioni 30, na pia anawalipia ada wanafunzi 28 wa sekondari, wanafunzi 10 wa vyuo vya kawaida, na wanafunzi sita wa chuo kikuu, ambapo gharama zake ni jumla ya shilingi 11,900,200.
"Wananchi wenzangu leo nawakabidhi majengo mazuri ya sekondari hapa Mkuzo niliyoyajenga kwa zaidi ya milioni 112/=. Kwa fedha hizi ningeweza kujenga hoteli nzuri ya kisasa kwenye uwanda mzuri wa Matogoro na kuzifungua kifahari, lakini ingekuwa kwa maslahi yangu na familia yangu, lakini kwa kuwa nawapenda nimeamua kuwekeza kwenye elimu ya watoto wetu wote wa Songea," alisema Nchimbi siku ya kukabidhi shule hiyo.
"Leo ni siku muhimu katika manispaa yetu mtakumbuka miaka minne iliyopita CCM iliahidi kuwa tuitajenga sekondari kila kata ni faraja kubwa jambo hilo tumelikamilisha, matokeo ya kujenga shule yapo wazi kwani uwekezaji wa elimu ni muhimu kuliko yote," anasema Dk. Nchimbi na kuthibitisha kwamba elimu bora ni sawa na kumfundisha mtu uvuvi badala ya kumpatia samaki kwa njaa ya siku moja.
Dk. Nchimbi anasema pamoja na mafanikio hayo lakini bado kuna changamoto nyingi katika sekta hiyo ya elimu jimboni kwake ambapo alizitaja changamoto hizo kuwa ni upungufu wa walimu, vifaa, kuboresha majengo na miundombinu ya shule za msingi, walimu kulipwa haki zao kwa wakati na kujenga chuo kikuu mjini Songea ambacho kitasaidia wananchi wa mkoa wa Ruvuma kujiendeleza zaidi kielimu.
Anasema iwapo wananchi wataendelea kumpatia ushirikiano atasaidiana nao kujenga chuo kikuu katika Manispaa hiyo kwani kwa sasa ndoto yake kubwa ni kuhakikisha kuwa watoto wote wenye uwezo wa kusoma wanaenda shule ili kuongeza idadi ya wasomi katika mkoa wa Ruvuma, ahadi ambayo ilipokelewa kwa shangwe na wazazi pamoja na wanafunzi.
Wananchi wa Jimbo hilo bado wanalalamikia kero mbalimbali zinazowakabili na wamemtaka mbunge wao aongeze juhudi za kutatua kero hizo katika sekta ya maji, umeme, afya, elimu na barabara.
Lakini Dk. Nchimbi anasema kwa kipindi cha miaka minne na nusu ya uwakilishaji wake amejitahidi kutekekeza ahadi zake muhimu alizoziahidi, ambazo anasema zilikuwa kikwazo kwa maendeleo ya wapiga kura wake katika sekta ya elimu, afya na barabara, ingawa amewaomba wapiga kura wake wawe na subira kwani kero zao anazitambua na ameanza kuzitatua ingawa anakiri kuchelewa kuzitatua.
Ujenzi wa shule za sekondari za kata uligharimu fedha nyingi, ambapo wananchi walichanga jumla ya shilingi milioni 60 na Manispaa ikachangia shilingi milioni 70, hivyo kufanya kata zote kuwa na shule.
Jimbo hili la Songea Mjini lina jumla ya Kata 13 ambazo ni Matogoro, Mletele, Bombambili, Mshangano, Ruhuwiko, Subira, Ruvuma, Lizaboni, Majengo, Matarawe, Misufini na Mjini.
Katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu, wapo watu ambao wamekuwa wakisema kwamba huenda hizi ni mojawapo ya kampeni, jambo ambalo Dk. Nchimbi analikanusha na kusema kwamba ujenzi huwa hauchukui siku moja, bali ni mipango ya muda mrefu, hivyo lilikuwa mojawapo ya ahadi zake kwa wananchi na amelitekeleza.
Kauli hizi zimekuwa zikitolewa katika kipindi hiki ambacho vuguvugu la uchaguzi limepamba moto ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM), ambapo katika jimbo hilo mbali ya Dk. Nchimbi anayetaka kulitetea, wamejitokeza watoto wa wanasiasa wakongwe nchini, Balozi Paulo Mhaiki na Nassor Hassan Moyo, ambao ni Oliver Mhaiki na Said Nassor Moyo.
Mhaiki, Katibu Mkuu wa Wizara ya Sheria na Katiba, anajivunia uzawa na ukazi mjini Songea, huku baadhi ya watu wakisema kwamba Dk. Nchimbi hakuzaliwa Songea na kwamba amejenga Mbeya.
Lakini hoja za aina hii ni za ubaguzi ambazo hazistahili kupewa nafasi, kwani Tanzania ni moja na masuala ya ukabila, udini hayastahili kupewa nafasi kwa sababu mwishowe zitakuja kuzuka hoja za “Huyu ni mtoto wa ukoo gani?” na mambo kama hayo.
Dk. Nchimbi anabainisha kwamba, ni haki kwa mwananchi yeyote mwenye sifa kugombea, kwani hata Katiba ya nchi inaeleza hivyo, lakini anaamini kwamba wananchi watamhukumu kwa mafanikio yake.
“Nimejitahidi kwa kadiri ya uwezo wangu, pamoja na majukumu mengi ya kiserikali niliyo nayo, hata hivyo huwezi kumridhisha kila mtu, na daima kero zote haziwezi kutatuliwa mara moja. Naamini nimefanya mengi na wananchi watakuwa mashuhuda.
“Wacha wajitokeze wengi kwa sababu ndiyo demokrasia, lakini naamini mwisho wa siku Mbunge atakuwa mmoja! Hili halina ubishi,” anabainisha Dk. Nchimbi ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.
Wachunguzi wa masuala ya siasa wanaona kwamba, nguzo pekee ya kuegemea ni kama kiongozi aliyechaguliwa na wananchi anawaletea maendeleo ama la, bila kujali anatoka mahali gani.
Ni wazi kwamba joto la uchaguzi jimboni humo limepanda kwa nyuzi nyingi, lakini wananchi ndio watakaopima mafanikio na kuamua kwa busara nani anayestahili kuwaongoza badala ya kuanzisha hoja zisizo na msingi.
Kwa sasa siasa chafu ndizo zinazotawala ndani ya jimbo la Songea Mjini, ambapo kuna kundi la mgombea mmoja lililodhamiria kumchafua mgombea mwenzake kwa kila hali na kuhakikisha anashindwa katika kura za maoni.
Kitendo cha kutumia mbinu za aina hiyo hakipaswi kufumbiwa macho, kwa sababu hakilengi kutumia demokrasia ya kweli bali hila za wazi, ambazo mwelekeo wake hautakuwa na matunda mazuri hata kama anayetumia mbinu hizo chafu ataingia madarakani.
Kwa upande wao baadhi ya wananchi wamesema kuwa kitendo cha Mbunge wao kuwajengea shule ni cha kuungwa mkono na wananchi wote wa manispaa hiyo kwani shule hiyo itawasaidia wananchi wote bila kujali itikadi za dini na siasa kupata elimu na wamewataka wenzao kuunga mkono jitihada za mbunge huyo.
Jacob Chidumule, mkazi wa Kata ya Matarawe, anasema kipindi cha uchaguzi kina mambo mengi, lakini lazima wananchi watumie busara wanapotaka mabadiliko ya maendeleo na siyo kufanya mabadiliko kwa shinikizo la watu wachache.
“Tunahitaji maendeleo, lakini siyo kukurupuka na kusema tunataka mabadiliko bila kutathmini mafanikio yaliyopatikana kwa yule tuliyemchagua. Binafsi naamini Nchimbi bado anastahili kutuwakilisha. Maendeleo yanaletwa kwa ushirikiano wa wote, viongozi na wananchi, na tusiwaachie viongozi pekee,” anafafanua Chidumule.
Naye Hassan Komba, mkazi wa Kata ya Bombambili, anasema kwamba CCM itafanya makosa ikiwa italeta mabadiliko ya lazima kwa mwakilishi, kwani wananchi bado wana imani na Mbunge wa sasa.
“Wakifanya mabadiliko ya ghafla, hakika wanaweza kujikuta wakilipoteza Jimbo kwa wapinzani. Tunaamini Mbunge wa sasa bado ana uwezo wa kuleta maendeleo. Hizi hoja za kazaliwa wapi anaishi wapi zisilete matabaka na hazijengi. Sote ni Watanzania na tunapaswa kuthaminiana kwa Utanzania wetu, tusije tukafikia mahali tukaanza kuulizana huyu ni mtoto wa nani?” anaonya Komba.
Felister Herman Haule, mkazi wa Kata ya Ruhuwiko, mewataka wananchi wenzake wa Manispaa ya Songea kumuunga mkono Mbunge wao kwa kushirikiana naye kwa vitendo ili kulipa shukrani kwa kuwakomboa kielimu kwani kitendo chake cha kujenga shule kitasaidia wananchi wengi kupata elimu na hivyo kuwa na wasomi ambao watasaidia kuleta maendeleo.
"Elimu ni msingi wa maendeleo yetu, Dk. Nchimbi amesababisha watoto wetu waende shule, ametoa fedha zake ili wananchi wake wajikomboe na tatizo la ujinga na umaskini hivyo wananchi tuache kubabaishwa na majambazi wa siasa tuchague viongozi ambao watatusaidia kujikomboa kielimu, kiuchumi na kulisaidia taifa letu katika nyanja mbali mbali za maendeleo,” anasema.
Fomu za kuwania Ubunge kwa upande wa Chama cha Mapinduzi (CCM) zinatarajiwa kuanza kutolewa Julai 19, mwaka huu, na kampeni ndani ya chama hicho zitaanza mapema mwezi Agosti.
Tusubiri tuone matokeo, lakini hakika mwenye kisu kikali ndiye atakayekula nyama Songea Mjini mwaka 2010!

SOURCE: DIRA YA MTANZANIA.
Tuwapime, tuwachambue kama wanafaa kupewa dhamana ya uongozi

* Tujiulize, ni nani aliyewapa hatimiliki ya majimbo

Na Daniel Mbega

PEPO za Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 zimezidi kuvuma kila kona ya nchi hivi sasa huku tukishuhudia vikumbo na tambo mbalimbali miongoni mwa wale wanaotaka kuomba ridhaa yetu ili tuwaongoze.
Wapo ambao tayari wako madarakani, wakifanya kila linalowezekana kuendelea kubaki kwa gharama yoyote ile ili waendelee kufaidi keki ambayo wananchi wa kawaida tunaendelea kuambulia harufu tu. Lakini pia wapo ambao wanataka kuomba ridhaa kwa mara ya kwanza, ili nao wakafaidi hayo ambayo wenzao wanayapata sasa.
Katika mchakato huo, wapo pia waliopata kushika nyadhifa mbalimbali, hasa za Ubunge na Udiwani, ambao kwa sababu mbalimbali walipigwa kumbo na hawa waliopo madarakani kwa sasa, na katika kipindi ambacho wamekuwa nje wamejaribu kutafakari makosa yao na kuwasoma wapinzani wao ili wakiingia tena wasifanye makosa.
Chama cha Mapinduzi (CCM) ndicho kinachoonekana kuwa na ushindani mkubwa, kutokana na ukweli kwamba ndicho chama tawala na kina wabunge wengi kwa sasa, na ndani yake wapo wanachama wanaotaka kuwanyang’anya wenzao nafasi ya uongozi wa wananchi.
Kura za maoni ndani ya CCM zitaanza kupigwa kuanzia Agosti 10, 2010, lakini inaonyesha bayana kwamba upinzani mkali unatarajiwa kuwepo, hasa ikizingatiwa kwamba dalili zilikwishajionyesha Novemba 6, 2007 baada ya mawaziri kadhaa na wabunge kupigwa mwereka katika nafasi za uwakilishi wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya chama hicho.
Manaibu waziri watano ni miongoni mwa waliokosa nafasi katika uwakilishi wa Viti 20 NEC nao ni pamoja na Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Dk. David Mathayo, Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mshariki Dk. Diodorus Kamala na Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja.
Wengine ni Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Mwantumu Mahiza na aliyekuwa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Ritha Mlaki aliyegombea nafasi hiyo kupitia kundi la Wanawake.
Pia wapo manaibu waziri watatu wa SMZ waliotupwa chini ambao ni Jabir Makame Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali, Khatib Suleiman ambaye ni Naibu Waziri Kilimo, Mifugo na Mazingira na Dk. Mwinyi Haji Makame, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais.
Katika nafasi za kundi la Wanawake Tanzania Bara kuna Mbunge wa zamani wa Afrika Mashariki na sasa Mbunge Beatrice Shelukindo. Pia yupo Mbunge Tatu Ntimizi na Katibu Mkuu mstaafu wa UWT Halima Mamuya.
Katika kundi la Wazazi Tanzania Bara, hapa kulikuwa na wagombea wengi ambao ni wabunge. Katika kundi hili kuna jina moja tu la aliyeshinda ambaye si mbunge, Nondo Mohamed. Lakini pia Danhi Makanga, Ruth Msafiri, Thomas Ngawaiya na Tambwe Hiza walipoteza katika kundi hili. Ngawaiya na Hiza walitoka upinzani na walitarajiwa kupewa ‘kura za huruma’ jambo ambalo halikufanyika.
Wengine ni pamoja na wabunge Margareth Agness Mkanga, Zuhura Mikidadi na mhamasishaji wa tenzi wa CCM, Salim Shomvi Tambalizeni, Naibu Meya wa Ilala Mustafa Yakub, Mkuu wa Mkoa wa Mara (sasa yuko Arusha) Isidore Shirima na Mkuu wa Wilaya Frank Uhahula walikosa nafasi hizo.
Wanasiasa wengine maarufu waliokosa nafasi baada ya kupata kura chache ni Wilson Masilingi, Brigedia Jenerali mstaafu Hassan Ngwilizi, Tarimba Abbas, Filbert Bayi, Enock Chambiri, Christopher Gachuma, Charles Kagonji, Lucas Kisasa, Pascal Mabiti, Dk. James Msekela, Profesa Idrisa Mtulia, Abeid Mwinyimsa na Job Ndugai. Wengine ni waandishi wa habari Jacqueline Liana, Jane Mihanji, Novatus Makunga na Shyrose Banji.
Kwa hiyo utaona kuwa kutokana na yaliyojitokeza mwaka 2007, wale walioko madarakani wanahofia yasije yakatokea tena kwenye Ubunge, hatua ambayo inawafanya wale walio madarakani wafanye kila liwezekanalo kutetea vitumbua vyao visiingie mchanga. Lakini hiyo ndiyo siasa.

Umiliki wa majimbo…
“Kuna watu wanataka kuninyang’anya jimbo langu!” “Atakayetia mguu jimboni kwangu atakiona!” “Nimefanya mambo mengi, sasa waniachie jimbo langu niliendeleze!” hizi ni kauli nyingi zilizozoeleka kuonekana kwenye vyombo vya habari, hasa katika siku za karibuni.
Kauli hizi zimekuwa zikitolewa na wale walioko madarakani kwa sasa ambao wanahisi kwamba wanaoonyesha nia ya kutaka kugombea wanawanyang’anya ‘majimbo yao’.
Kwamba inakuwaje mbunge alalamike ati kuna watu wananyemelea jimbo lake, ndilo swali ambalo limekuwa likiwatatiza wachambuzi wengi wa masuala ya siasa na demokrasia! Tangu lili jimbo likawa chini ya hatimiliki ya mtu mmoja?
Kwa mujibu wa taratibu, kanuni na sheria za uchaguzi mtu anapopata ubunge huwa anadumu kwa miaka mitano kisha uchaguzi unapowadia wananchi watapima na kuamua wamrudishe au wamuondoshe ili waweke mtu mwingine atakayewahudumia vema katika suala zima la maendeleo. Wananchi wenyewe ndio wenye mamlaka ya kumchagua ama kumkataa mgombea, lakini sasa watamchagua vipi mtu ikiwa mbunge wa sasa anang'ang'ania na kukataa ushindani?
Kwa zaidi ya mwaka sasa wabunge kadhaa, wakiwemo Dk. Harrison Mwakyembe (Kyela – CCM), Aloyce Kimaro (Vunjo – CCM), Christopher Olonyoike ole-Sendeka (Simanjiro), James Lembeli (Kahama - CCM), Anne Kilango Malecela (Same Mashariki), Dk. Zainab Gama (Kibaha Mjini), Kapteni mstaafu John Chiligati (Manyoni Mashariki), Wilson Masilingi (Muleba Kusini), na wengineo wamekuwa wakilalamika ‘kuhujumiwa’ na wale wanaopita kutangaza nia.
“Wapo watu wanaojipitisha pitisha kule jimboni kwangu, nawaonya kabisa waache, maana nitawapiga mwereka wa hali ya juu,” alipata kukaririwa akisema Mbunge wa Mtera, John Samuel Malecela, akiwaonya watu walioonyesha nia ya kugombea jimboni humo.
Ukiacha Mzee Malecela, wabunge wengine kama mkewe Anne Kilango, Dk. Mwakyembe, James Lembeli, Aloyce Kimaro, Lucas Selelii, Ole Sendeka na wenzao wamekuwa wakipiga kelele kwamba kuna watu wametumwa ama kupandikizwa na watuhumiwa wa ufisadi kuwachafua majimboni kwao ili wapoteze ubunge.
‘Majeruhi’ hao wanasema kwamba, kundi la mafisadi limemwaga fedha nyingi kwenye majimbo yao kuhakikisha kwamba wanaanguka katika kinyang’anyiro cha uchaguzi wa mwaka huu.
Wanaotajwa kuhusika na njama hizo ni Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa na Mbunge wa Igunga Rostam Aziz, ambao wanadaiwa kwamba wamewaweka watu wao washindane na wale wabunge waliokuwa mstari wa mbele kuzungumzia sakata la kampuni ya Richmond Development LLC.
Kilio hicho cha wabunge hao kimevuka mpaka kwa sasa, ambapo yeyote anayejitokeza kutaka kugombea anatajwa kuwa katumwa na ama Lowassa au Rostam kumnyang’anya ‘jimbo lake’.Inafahamika vyema kwamba siasa inatumia hila nyingi, na hili wanasiasa wanalitambua fika.
Lakini kinachotia shaka ni kwamba, kwa nini kila anayejitokeza hata kwa dhamira yake binafsi awe katumwa? Hivi ni lini basi ambapo Lowassa na Rostam watachagua watu wa kuwaunga mkono badala ya kutuma?
Wapembuzi wa masuala ya siasa wanahisi kwamba, hii inaweza kuwa ni mbinu nyingine ya wanasiasa hawa wapambanaji wa ufisadi kutaka ‘huruma’ ya wapiga kura wawachague kwa kisingizio wanaonewa ili wasirudi Bungeni.
Jambo moja wanalolisahau ni kwamba, yawezekana wao wamejisahau kutekeleza ahadi zao kwa wananchi na sasa wamegeuziwa kisogo, hivyo wanakimbia vivuli vyao. Wachambuzi wa masuala ya siasa wanasema, kosa kubwa ambalo wapiganaji hao wa ufisadi walilifanya ni kukubali kuachia hoja ya Richmond ifungwe Bungeni wakati tayari walikuwa wamejiweka katika nafasi nzuri.
Aidha, woga wao wa kuhofia kufukuzwa kwenye chama umewaponza wengi, lakini kama wangethubutu pengine wangeondoka kama mashujaa na ushindi juu na leo hii wangesimama mbele ya Watanzania na kujipambanua kwamba ni wapinga ufisadi, hivyo wangeungwa mkono na wapiga kura wengi.
Wapambanaji hawa wanashindwa pia kuelewa kwamba, wamejimaliza wenyewe kwa kuwa wanafiki, kwa sababu kipindi chote cha kuanzia Septemba 2007 hadi leo hii wameonyesha juhudi tu za kufichua ufisadi lakini hawajaonyesha njia za kupambana ama kukomesha ufisadi huo.
Inaelezwa pia kwamba, kitendo cha ‘kumtoa kafara’ mpambanaji mwenzao, Fred Mpendazoe Tungu, waliyemtanguliza kwenye Chama cha Jamii kinachodaiwa kuanzishwa kwa ushirikisho wa baadhi ya wapambanaji hao, nacho kimewapunguzia nguvu kwa wananchi kwani wameshindwa ‘kumfuata’ huko alikokwenda.
Wananchi wengi wanasema wapambanaji hao waliitumia hoja ya Richmond kujipatia umaarufu badala ya ukombozi wa Taifa.
Naamini wanacholilia ni mbinu chafu zinazofanywa dhidi yao za kuwanyima wananchi fursa ya kuwachagua tena, mbinu ambazo wakati mwingine kwa maoni yao zinapakana na vitendo vya uhalifu na ndio maana wanataka vyombo vya sheria vifuatilie.
Lakini hapa pia wanashindwa kutambua kwamba, mbinu walizoingilia wao madarakani ndizo hizo hizo ambazo zinatumiwa na wale wanaotangaza dhamira ya kugombea majimbo hayo. Sijajua kwa nini hawa wabunge walio madarakani wanalia ovyo utadhani majimbo ni 'mali yao'. Tatizo wanataka kuziba njia ambazo wao walipitia, ili wanaokuja wasipite hizo, wakati njia hizo ndizo za mkato za kuelekea kwenye unono.
Kama kuna mbunge yeyote anayeweza kujigamba kuwa hakutumia mbinu chafu kuwalainisha wapiga kura na aseme sasa. Kila mbunge ama katoa chakula, au katoa chochote japo hata "kitochi" ili akumbukwe kwenye kura. Bila shaka wanaowania nao wanatumia mbinu hizi ili waonekane kwa mpiga kura. Takrima ilishapigwa marufu kisheria lakini bado kuna vijitarima vinaendelea pamoja na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kutoa onyo.
CCM inajinasibu kwamba ina uhakika wa kutwaa majimbo mengi mwaka huu, lakini zipo taarifa kwamba kuna wabunge zaidi ya 100, wakiwemo nusu ya mawaziri wa sasa, hawauziki na CCM inapaswa kuwa makini kutoyarudisha majina ya wabunge hao (wenyewe wanawajua) ili kukiepusha chama na kushindwa katika majimbo yao. Kimsingi CCM inapaswa kusimamisha wagombea wanaokubalika kama kweli inataka kushinda.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM taifa (NEC), Bw. Salum Msabah, alipata kukaririwa Februari 26, 2008 mkoani Mara wakati akizungumza na viongozi wa chama hicho, kwenye mikutano ya ndani, katika kata ya Kibara na Nansimo wilayani Bunda, kwamba tayari makao makuu ya chama hicho wamekwishabaini wabunge hao kuwa wakirudi utakuwa mzigo kwa chama hicho na iwapo watagombea tena katika uchaguzi wa mwaka 2010 majina yao hayatapendekezwa na uongozi wa juu wa chama hicho. Kwa muda mrefu baadhi ya wabunge hao wamekwisha kuwa kero kwa wananchi kwa kuwa wakichaguliwa hawarudi tena kwenye majimbo yao na badala yake wanakuwa watu wa mijini tu.
Utafiti uliofanywa na asasi isiyo ya kiserikali ya Nyota, umeonyesha kwamba zaidi ya nusu ya mawaziri waliotajwa kuwa makamanda katika Serikali ya Awamu ya Nne wanaweza kupoteza nafasi zao za ubunge na hali ni tete katika majimbo ya mawaziri hao kutokana na wananchi wengi wa majimbo hayo kukosa imani nao.
Taarifa ya awali iliyotolewa na Mratibu wa asasi hiyo, Vincent Kornald Mkisi, ilisema kuwa mazingira ya mawaziri na manaibu hao kupoteza nafasi zao yalianza kuonekana tangu Januari 2010 na mawaziri walio katika hali mbaya kurudi bungeni ni pamoja na Profesa Peter Msolla ambaye anakabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa aliyewahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Kilolo, Venance Mwamoto ‘Motto’.
Duru za kisiasa zinasema kuwa Profesa Msolla alitarajia kudra za Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuligawa Jimbo la Kilolo na kuwa mawili, hivyo alijipanga kuwania ubunge katika eneo la Ilula ambako anakubalika zaidi kuliko maeneo mengine.
Waziri mwingine anayetajwa kuwa katika kaa la moto kwa mujibu wa utafiti huo, ni Profesa Jumanne Maghembe, anayekabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa mwanasheria wa kujitegemea, Joseph Tadayo. Inaelezwa kuwa baada ya Tadayo kuweka bayana nia ya kuwania ubunge katika Jimbo la Mwanga, waziri huyo alianza mkakati wa kutumia nguvu kulazimisha kukutana na wazee kwa nia ya kuwaweka sawa na kujihakikishia kuilinda nafasi yake ya ubunge.
Hata hivyo, Profesa Maghembe anapaswa kujilaumu mwenyewe kutokana na kile ambacho wananchi wa Mwanga wamekuwa wakikitaja kuwa ni ubabe na kujiona ana haki ya kifalme ya kuliwakilisha jimbo hilo. Watafiti wanasema ameshindwa kuwaunganisha wananchi wa Mwanga, na kwamba hata waziri mkuu mstaafu ambaye pia alikuwa mbunge wa jimbo hilo, Cleopa David Msuya, hakubaliani naye.
Nyota imeonyesha kuwa pamoja na kuwa sura za vijana katika Baraza la Mawaziri ilionekana kuwa nuru mpya kwa wananchi na kuwafanya kuwa na imani na Serikali ya Rais Jakaya Kikwete, mawaziri wake wawili vijana, William Ngeleja wa Nishati na Madini na Dk. Lawrence Masha wa Mambo ya Ndani wako juu ya kaa la moto.
Ngeleja anakabiliwa na mchumi mwandamizi na mwanamageuzi wa kilimo anayeendana na falsafa mpya ya ‘Kilimo Kwanza’, Francisco Kimasa Shejamabu, ambaye pia ni meneja na mmiliki mwandamizi wa Kampuni ya Tanwat ya jijini Mwanza.
Habari zinasema kuwa Ngeleja alikuwa akiandaa mkakati wa kutaka matawi na kata za CCM katika Jimbo la Sengerema kutoa tamko la kumtangaza kuwa mgombee pekee ili aweze kupitishwa bila kupingwa. Hata hivyo, inaelezwa kuwa mpango wake huo umekwama kutokana na kuwapo kwa kundi kubwa la wanachama wa CCM walioamua kupingana na dhana hiyo na kutaka kuwapo demokrasia ndani ya chama chao.
Mwingine anayekabiliwa na hali mbaya ni Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo, Kapteni George Huruma Mkuchika (Newala), Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Diodoros Kamara (Nkenge), Waziri wa Sheria na Katiba, Mathiasi Chikawe (Nachingwea), Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkullo (Kilosa Kati), Waziri wa Kilimo na Chakula, Stephen Wassira (Bunda) na Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk. Mary Nagu (Hanang).
CCM inapaswa kusikiliza kilio cha wananchi kuhusu suala la wabunge kung’ang’ania madaraka kwa ajili tu ya kujipatia mishahara mikubwa, posho na mafao lukuki bila kutambua kwamba wanapaswa kuwatumikia wananchi. Hili limekuwa siyo siri tena, hasa katika kipindi hiki ambacho wananchi wanaelewa hata mambo yanayoendelea sirini. Wabunge wazee na wale walioshindwa kutekeleza majukumu yao ya uwakilishi wa wananchi wanatakiwa wasipate ridhaa ya wananchi tena hata kama watapitishwa na vyama vyao, huo ndio uwe msimamo wa Watanzania kama kweli wanataka kujiletea maendeleo.

SOURCE: DIRA YA MTANZANIA.

Friday, May 14, 2010






SANA: Asasi yenye mwarobaini wa kutokomeza uharibifu wa mazingira






















· Badala ya kukata miti, yawafundisha wananchi kutengeneza mkaa wa mabua




Na Daniel Mbega

SUALA la kuhifadhi mazingira limekuwa moja ya ajenda zinazopewa kipaumbele katika mikutano na makongamano mengi kote ulimwenguni kwa sasa kutokana na ukweli kwamba mazingira yanaharibiwa kila siku na binadamu hao hao wanaoyahitaji kwa ustawi wa maisha yao.
Uharibifu wa mazingira umezikumba nchi nyingi duniani, lakini umekuwa na athari kubwa sana hasa kwa nchi za dunia ya tatu au zinazoendelea, Tanzania ikiwa miongoni mwazo.

Inaelezwa kwamba tabaka la anga, maarufu kama Ozone Layer, limeharibika vibaya kutokana na kemikali nyingi zinazozalishwa katika nchi zilizoendelea na zenye viwanda vingi, kiasi kwamba kwa miaka ya karibuni hata hali ya hewa imebadilika ambapo mvua hazinyeshi kwa kiwango kinachotakiwa na joto limezidi sana duniani.

Lakini, pamoja na viwanda hivyo kuharibu mazingira, pia ukataji wa miti umekuwa chanzo kikubwa cha nchi nyingi kugeuka jangwa huku vyanzo vya maji navyo vikiathirika kwa kiwango kikubwa, kwani hata baadhi ya chemchem zilizokuwepo tangu zama zimeshakauka.

Milima mingi nayo imebaki na vipara vya hapa na pale huku misitu, hasa ile ya asili, ikiondolewa kwenye uso wa dunia kutokana na kukatwa miti kunakofanywa na binadamu.

Aidha, ukataji huo wa miti na uharibifu wa mazingira kwa ujumla – ya nchi kavu na hata majini – umesababisha viumbe hai wengi wakiwemo samaki, ndege na wanyama wa porini kutoweka katika ramani ya ulimwengu.

Tanzania imejaaliwa kuwa na rasilimali nyingi za asili – ardhi yenye rutuba, misitu na wanyama – lakini ukizunguka kwa sasa unaweza kushangaa kuona maeneo yale yaliyokuwa na misitu takriban miaka 10 iliyopita yamegeuka kuwa nusu jangwa kutokana na kutokuwepo na hata mti mmoja wa asili, achilia mbali miti ya kupandwa.

Hii inatokana na ukweli kwamba, binadamu ameyaharibu mazingira mengi yanayomzunguka na kama juhudi za makusudi hazitafanyika, Tanzania itakuwa jangwa katika miaka michache ijayo.

Sababu kubwa zinazochangia ukataji wa miti ni za kiuchumi na kijamii. Ukizunguka katika sehemu kubwa ya kaskazini mwa Wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma, na kusini mwa Wilaya ya Kiteto mkoani Manyara, utakuta eneo kubwa la misitu limefyekwa kwa sababu za kiuchumi. Wanaofanya hivyo, wengi wanataka maeneo ya kilimo.

Ukiacha shughuli hizo za kilimo, sehemu nyingine miti inakatwa kwa ajili ya matumizi ya kijamii, hususan nishati ya kuni na mkaa. Ni shughuli za kijamii, lakini zinazoambatana na kiuchumi, kwani kuni na mkaa huo unauzwa na wahusika ili kujipatia fedha za kuendesha maisha yao.

Lakini je, hivi hakuna njia mbadala ya kujipatia fedha kuliko kukata miti hii ambayo ni chanzo kikubwa cha mvua? Hili ndilo swali linalojibiwa na Angela Damas, Miss Tanzania wa mwaka 2002, ambaye kwa sasa ni Meneja Miradi wa taasisi isiyo ya kiserikali ya Saving Africa’s Nature (SANA).

Angela anasema inawezekana kabisa kupata njia nyingine mbadala ya kuwawezesha Watanzania kupata nishati na kipato pia, ndiyo maana wao SANA wameamua kuja na mradi wa Mkaa kwa Njia Endelevu (Sustainable Charcoal Project) ambao siyo tu unajali, kutunza na kuyaendeleza mazingira, lakini pia unawawezesha wananchi wenyewe kuyapenda na kuyahifadhi zaidi kwa manufaa yao wenyewe na vizazi vijavyo.

“Mradi huu hauhitaji kukata mti hata mmoja, zaidi tunahimiza upandaji wa miti na pia kuitunza ile iliyopo kwa faida yao na vizazi vijavyo,” anasema Angela ambaye taasi yake imesajiliwa rasmi Novemba 2008.

Anasema kwa kupitia progamu hiyo, wanahimiza wananchi kutotumia miti kupata nishati ya mkaa, badala yake wanatumia taka shamba – mabua na taka nyingine laini – ambazo huzichoma kwenye kinu maalum na kisha kusindika majivu yake ambayo matokeo yake yanatoa mkaa ulio bora kuliko hata ule unaotokana na kuchoma miti.


“Mabua yanakusanywa na kushindiliwa kwenye mapipa ya kawaida yaliyo wazi, halafu mapipa haya yanaingizwa kwenye pipa maalum ambapo yanachomwa. Baada ya hapo majivu yanayopatikana yanachanganywa na kusindikwa kwa kutumia kinu kidogo kutoa mabonge ya mkaa tayari kwa matumizi,” anasema Angela.

Angela anasema kwamba, tayari teknolojia hii mpya wameianzisha katika kijiji cha Mkange wilayani Bagamoyo, Pwani ambacho kwa kiasi kikubwa kimeathirika kutokana na ukataji miti kwa nia ya kuchoma mkaa.

“Kijiji cha Mkange biashara yake kubwa ni mkaa, hivyo kimeathirika mno kutokana na misitu mingi kukatwa kwa lengo la uchomaji wa mkaa. Awali tulipoingia na wazo hili ilionekana kama elimu ngeni na wengi waliipuuza, lakini kwa sasa tunashukuru kwamba tumeshaokoa miti mingi na tayari wananchi wanaichangamkia teknolojia hii kwa kuchoma mkaa huu.

“Wanajipatia pesa, lakini pia inawasaidia kusafisha mashamba yao kwa njia ya faida. Kama zamani walikuwa wakikusanya taka za shamba na kuzichoma moto ovyo, leo hii hawataki mtu mwingine aingie mashambani mwao kukusanya mabua, wanayakusanya wenyewe na kuyachoma kisha kutengeneza mkaa ambao wanauza na kujipatia kipato,” anasema kwa tabasamu.

Aidha, anasema taasisi yao ambayo siyo ya kibiashara, inakabiliwa na changamoto kubwa ya ukosefu wa fedha ili kuifikisha elimu hiyo katika sehemu kubwa ya Tanzania, kwani zaidi wanategemea wahisani ili kufanikisha azma hiyo.

“Kwa kupeleka elimu katika eneo moja tunahitaji Dola za Marekani 650 ambazo tunazitumia kwa ajili ya kununulia kitu maalum cha kusindika mkaa pamoja na gharama za mafunzo. Elimu hii tunayo na tunataka imfikie kila mwananchi kwa lengo la kumsaidia kupata fedha na kuokoa mazingira yasiharibiwe huku tukiwahimiza wapande miti kwa wingi,” anaongeza.

Wazo hili lilitoka wapi? Angela anasema wazo la kuanzisha miradi kama hiyo lilitoka kwa Costas Coucolis, Mkurugenzi Mkuu wa Saadani Lodge ambaye aliona teknolojia hiyo katika nchi nyingi zilizoendelea.

Awali walianza kutoa misaada tu kwa jamii, lakini baadaye wakaamua kujisajili rasmi ili watambulike hata kimataifa kwa lengo la kuhimiza utunzaji wa mazingira. Mkurugenzi wake ni Marianna Balampama, ambaye anaonekana kuwa mwenye uchungu na jinsi mazingira yanavyoharibiwa ulimwenguni.

Malengo yao makubwa ni kuhimiza na kuendesha programu zinazoweza kuwa njia mbadala ya nishati kwa jamii, kuendesha shughuli za uzalishaji mali zinazoweza kuwafaa wanajamii katika sekta za elimu, afya na maendeleo kwa ujumla, kuimarisha uelewa wa jamii kwa kuyatambua mazingira yao na viumbe vilivyomo, kuwajengea uwezo wanajamii kukabiliana na kupambana na umaskini kwa kuzingatia miongozo ya Mpango wa Kukuza Uchumi na Kutokomeza Umaskini (Mkukuta) na mipango na sera zingine.

Kwa sasa SANA inaendesha programu zake katika vijiji kadhaa; Saadani, Mkange, Kijiji cha Maasai huko Miono, na Gongo – Matipwili, vyote vikiwa katika wilayani ya Bagamoyo mkoani Pwani, lakini malengo yake makubwa yakiwa kusambaza teknolojia na elimu ya uanzishaji wa miradi mbalimbali nchini kote.

“Ni taasisi ya kujitolea, hivyo kila mmoja wetu anajitahidi kutimiza wajibu wake katika miradi ambayo tayari tunaisimamia kama elimu, afya na teknolojia. Tayari SANA inafadhili wanafunzi 10 kutoka Saadani wanaosoma sekondari na mmoja anayesoma Shule ya Sekondari Matipwili,” anasema mratibu wa SANA, Ally Abdallah.

Anaongeza: “Tunatarajia kujenga zahanati katika Kijiji cha Gongo ambayo itakuwa na wodi ya wazazi ili kuwaokoa wanawake kutokana na vifo vinavyotokana na uzazi, kuanzisha ushirika katika Kijiji cha Maasai cha Msete, na tutajenga kituo vya kujipatia fedha katika Kijiji cha Mseni ambayo itamilikiwa na wananchi wenyewe.”

Lakini, mbali ya hayo, Angela kwa upande wake anasema wanawake wanapewa msukumo kwenye programu zao ambapo tayari wamefunzwa na kuwezeshwa kuanzisha miradi mbalimbali, hususan wa bustani ili kujipatia kipato.

“Iko mipango mingi inayohitaji uwezeshwaji. Tuna mradi wa matumizi ya gesi asilia (Bio gas), ambapo tayari Saadani Lodge na Shule ya Sekondari ya Azania, Dar es Salaam wanatumia…

…Tuna mpango wa kuhamasisha na kuelimisha kuhusu teknolojia ya umeme-jua, yote hii inahitaji uwezeshwaji, ingawa sisi kama watendaji tuko tayari. Yeyote mwenye nia thabiti ya kuokoa mazingira yetu tunaomba atuunge mkono kwa kutoa mchango wake ili kutuwezesha tutende kazi,” anaongeza Angela.

Lakini, kila kitu kinawezekana ikiwa Watanzania wataamua kuwaunga mkono SANA na taasisi zingine ambazo zimekuwa mstari wa mbele kuyatunza mazingira yasiharibiwe kwa kiasi kikubwa kwa kisingizio cha kutafuta mapato.

Idadi kubwa ya wananchi, hasa wale wa vijijini wakipata elimu ya kutunza mazingira na hasa kuwaelimisha njia mbadala ya kuacha kukata miti kwa ajili ya mkaa au kuni kwa kuwapa elimu kama inayotolewa na SANA.

Nishati mbadala ni ngao muhimu kwa kutunza miti na hatimaye mazingira yote kwa neema ya vizazi vya sasa na baadaye.

Elimu ya kutengeneza mkaa kwa taka za shamba ni mwokozi wa mazingira yetu, hivyo kila mmoja awajibike. Inawezekana


Ends
Kilimo hai ni mkombozi pekee wa mkulima wa Tanzania
*Serikali yatakiwa kuhamasisha mboji badala ya chumvichumvi
*Bidhaa za kilimo hai zinaongoza soko duniani, hazina madhara

Na Mwandishi Wetu,
Dar es Salaam

Kilimo ndio msingi wa maisha ya binadamu, na kwa Mtanzania, tunaambiwa daima kwamba kilimo ndio uti wa mgongo wa uchumi, kikiwa kinachangia asilimia kubwa ya pato la taifa, na pia kilimo ndiye mwajiri wa takriban asilimia 80 ya Watanzania.

Kama viongozi wetu walivyopata kutueleza, ili tuweze kupata maendeleo, ni lazima kuwepo na vitu vitatu: Ardhi, Uongozi Bora na Siasa Safi. Tayari vitu hivi vipo kwa sababu taifa letu linaendeshwa kwa misingi ya demokrasia, na ardhi ipo ya kutosha.

Hata hivyo, ni lazima kutambua kwamba, ardhi ama udongo ndiyo rasilimali mama ulimwenguni. Madini ya thamani yanapatikana ardhini, miti ya mbao inapatikana ardhini pamoja na mimea ya kila aina, bila kusahau kwamba viumbe hai wengine, binadamu na hayawani wa mwituni, nao pia wanaitegemea ardhi kwa ajili ya ustawi wao, kwani udongo huu unatumika kuzalisha kitu chochote ambacho kinahitajika kwa matumizi ya binadamu na wanyama.

Tumeirithi ardhi kutoka kwa vizazi vilivyotangulia ikiwa na ubora wa asili, lakini kutokana na matumizi ya muda mrefu, ardhi hii huzeeka na kushindwa kutoa mazao bora juu yake, hivyo kumfanya binadamu kutafuta namna nyingine ya kuifanya ardhi hiyo itoe mazao bora.

Katika sehemu kubwa ya nchi yetu, ardhi imekuwa chanzo cha migogoro ya mara kwa mara kutokana na matumizi yake, ambapo jamii za wakulima na wafugaji zimekuwa zikigombana – na hata wakati mwingine kusababisha maafa – kila moja ikisema inastahili kutumia ardhi hii.

Hii ni kwa sababu mkulima, baada ya kuona ardhi yake imechoka huamua kutafuta maeneo mengine yaliyo bora na kuanza kuyatumia. Wakati mwingine hulazimika kufyeka misitu ili kupata mashamba mapya, hali ambayo siyo tu inaharibu mazingira, lakini pia inaweza kututia umaskini wa milele kwa sababu ardhi iliyoachwa awali huwa haitafutiwi njia muafaka ya kuifanya irejee kwenye ubora wake.

Katika baadhi ya maeneo, wakulima wengine hutafuta mbolea, hasa za chumvi chumvi, na kuzitumia katika ardhi ile inayoonekana kuzeeka. Lakini matatizo mengi huibuka kutokana na matumizi ya mbolea pamoja na madawa ya kemikali kwenye kilimo. Hii ni kwa sababu mbolea hizi zina kemikali na yale madawa ya kuua wadudu yana madhara yake kwani yana sumu isiyoonekana. Hii sumu tunakula au tunakunywa na ndizo zinazoleta madhara kwa binadamu na udongo.

Aidha, mazao yatokanayo na kilimo cha mbolea hizi za kemikali yanaleta athari kubwa zisizoonekana kwa binadamu na hata wanyama. Lakini jambo la kuzingatia kwa sasa, kila mtu anatakiwa kuvuta kumbukumbu zake kulingana na umri alioishi na kuangalia yafuatayo: Hali ya udongo enzi zile na sasa ikoje? Kiwango cha maradhi wakati ule na sasa kikoje? Uwezo wa udongo kuzalisha mazao umepungua au unazidi mwaka hadi mwaka?

Wengi wetu tumegundua kwamba mbolea za chumvichumvi zimechakaza udongo na hivyo kufanya uzalishaji upungue. Hata mazao yatokanayo na matumizi ya mbolea hizo yamekosa ubora wa asili unaotakiwa. Hii inatia shaka kama umaskini wa mkulima utakwisha ikiwa hatabadili aina ya pembejeo kuokoa ardhi yake isizidi kuchakaa, na wakati huo huo kupunguza sumu isiyoonekana kwenye udongo na vyanzo vya maji.

Katika mataifa mengi ya ulimwengu wa kwanza, mbolea za chumvi chumvi zinatumika kupandia na kukuzia miti, hasa ya mbao. Vile vile inatumika kutengenezea mazingira kwa maeneo ambayo hayatumiki kuzalisha mazao ya chakula cha binadamu. Wao wamekuwa wakipiga sana vita vyakula vilivyolimwa kwa kutumia mbolea za chumvi chumvi, na ndiyo maana hivi sasa katika soko la dunia, bidhaa zilizozalishwa kwa kutumia mbolea hizi za chumvi chumvi zimekuwa zikiuzwa kwa bei ya chini kuliko zile zinazolimwa kwa kutumia kilimo hai. Sasa tujiulize, kwa nini sisi tunaendelea kutumia mbolea hizi zinazoua udongo wetu na kuweka sumu? Hivi hakuna mbolea nyingine mbadala? Jibu ni kwamba, mbolea mbadala zipo.

Mbolea mbadala ni zile zinazotokana na uozo wa asili. Uozo wa asili unaotokana na majani mbalimbali, samadi ya mifugo asili; mabaki ya nafaka au mazao mbalimbali (kama maganda ya karanga, mabua ya mahindi, n.k.).

Mbolea hizi zinaweza kupatikana au kutengenezwa katika mazao tunayolima, kwenye mazingira tunayoishi. Mbolea hizi zinasaidia kurudisha udongo katika hali ya rutuba na asili yake na gharama za mbolea hizi ni nafuu kabisa na zinadumu ardhini kwa muda mrefu.

Jambo la kuzingatia ni kwamba, udongo ni mali pekee yenye thamani kubwa ambayo tumepewa na Mwenyezi Mungu. Hivi sasa kuna migogoro mingi vijijini kutokana na watu kukimbilia mashamba mapya kwa ajili ya kutafuta rutuba baada ya mashamba yao ya zamani kufa kutokana na matumizi ya mbolea zenye kemikali.

Ni ukweli usiopingika kwamba, mbolea za chumvi chumvi zikiisha muda wake hugeuka sumu na baadaye mkulima analazimika kutumia gharama kubwa kuweka mbolea za mboji ili kurudisha udongo katika hali nzuri. Sumu hii isiyoonekana inaharibu udongo, vyanzo vya maji na hata mwili wako mwenyewe.

Mkulima anahitaji kupata mazao bora na ya kutosha ili yamsaidie kwa chakula, na ziada inayopatikana auze kwa ajili ya matumizi mbalimbali ya familia, lengo ambalo linaonekana kuwa gumu kufikiwa katika nyakati za sasa ambapo pembejeo za kilimo zimekuwa ghali na zaidi matumizi ya mbolea za kemikali yanazidi kuua ardhi, hivyo kupunguza uzalishaji wenyewe.

Aidha, hata mazao yatokanayo na kilimo cha mbolea za kemikali nayo hayana bei kubwa katika soko la dunia ikilinganishwa na mazao yatokanayo na kilimo hai, ambacho kwa sasa ndicho kinachohamasishwa ulimwenguni kwa sababu kinatumia viuatilifu asilia ambavyo siyo tu vinaongeza tija ya mazao, lakini pia ni rafiki wa mazingira, kama ilivyo kwa mbolea ya Erth Food inayoonekana kutelekezwa kwa sasa.

Kwa mfano, katika mwaka 2003/2004 wastani wa bei za mazao ya kilimo hai ilikuwa takriban asilimia 20 hadi 50 juu ya bei za mazao yasiyo ya kilimo hai katika Soko la Jumuiya ya Ulaya na Marekani. Kwa mwaka 2005/2006 kahawa iliyozalishwa kwa kilimo hai (organic coffee) iliuzwa kwa Dola za Kimarekani (USD) 65.7 kwa kilo 50 ikilinganishwa na USD 50.0 kwa kilo 50 za kahawa iliyozalishwa kwa kutumia kemikali za kilimo (agro-chemicals). Aidha, vanilla iliyouzwa nchi za Jumuiya ya Ulaya ilipata premium ya asilimia 20 hadi 300.

Kilimo hai au organic farming ni aina ya kilimo kinachozingatia matumizi endelevu ya rasilimali za uzalishaji wa mazao ya kilimo na mifugo. Kilimo hicho kinatumia mbolea na madawa yasiyotengenezwa viwandani na kinazingatia utunzaji wa mazingira kwa ajili ya manufaa kwa jamii, kiuchumi na kiafya.

Ili bidhaa zikubalike katika Soko la Kimataifa kuwa zimezalishwa kwa kutumia mbinu za kilimo hai, zinapaswa kwanza kupitishwa na Taasisi zinazosimamia ubora wa bidhaa hizo. Taasisi hizo ni International Federation of Organic Agriculture Movement (IFOAM) na Shirika la Ubora wa Viwango vya Vyakula la Umoja wa Mataifa (Codeaux Alimentarius Commission). Soko la mazao ya kilimo hai hutegemea walaji wa mazao hayo ambao wapo tayari kulipa bei kubwa kwa mazao ambayo yamezalishwa bila ya kutumia viatilifu na mbolea za viwandani.
Kilimo hai nchini kilianza kupata umaarufu katika miaka ya 1990 baada ya Serikali kuruhusu Taasisi kadhaa zisizo za Kiserikali (NGO) zikiwemo EGAJ, INADESTZ, PELUM, Meatu Cotton Projects, Babati LAMP na nyinginezo zilizojitokeza kueneza elimu na teknolojia za kilimo hai.

Aidha, Serikali kwa kutambua umuhimu wa kilimo hai na nia ya kuwasaidia wakulima kuendeleza kilimo hicho imeweka vipengele muhimu kwenye sera yake ya kilimo ikiwa ni pamoja na kuruhusu Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kusimamia biashara na bidhaa zake ambapo mwaka 2005 iliruhusu kuundwa kwa Tanzania Organic Agriculture Movement (TOAM) yenye lengo la kuwaunganisha wadau wa kilimo hai na kuwajengea uwezo.

Kutokana na juhudi hizo hivi sasa kilimo hai kinalimwa katika Mikoa ya Kilimanjaro, Tanga, Kigoma, Iringa, Pwani, Kagera, Mbeya, Morogoro, Shinyanga na Arusha. Mazao yanayozalishwa kwa njia ya mkataba ni pamoja na kahawa, chai, korosho, cocoa na pamba. Mazao mengine ni matunda na viungo hususan mananasi, tangawizi, tumeric, vanilla, pilipili na vitunguu. Sehemu kubwa ya bidhaa wanazozalisha zinauzwa moja kwa moja katika Soko la Jumuiya ya Ulaya na kiasi kidogo katika Soko la Marekani.

Hata hivyo, masharti yanayoambatana na kilimo hai yanakuwa magumu kwa baadhi ya wakulima na hivyo wakulima wengi kushindwa kuzalisha mazao hayo pamoja na kuwa yana bei kubwa. Wizara yangu itaendelea kushirikiana kwa karibu na Taasisi zinazoendeleza kilimo hai nchini ili kuhakikisha kwamba ubora wa mazao yanayozalishwa ni wa juu kulingana na viwango vya Kimataifa.
Utafiti wa kina unafanywa na Mashirika ya Nchi za Afrika Mashariki ambayo ni (Kenya Organic Agricultural Network (KOAN), National Organic Agricultural Movement of Uganda (NGAMU) na Tanzania Organic Agricultural Movement (TOAM) ili kuboresha uzalishaji na fursa za biashara ya bidhaa za kilimo hai katika nchi za Afrika Mashariki. Matokeo yatatolewa baada ya utafiti kukamilika.
Kilimo hai ni muhimu sana nchini Tanzania na mkombozi wa mkulima kwa kuwa kitamfanya kudumu mahali pamoja kwa muda mrefu na kuweza kujipanga vyema namna ya kujikwamua kimaisha. Pia kilimo hai kitainusuru nchi isigeuke jangwa kutokana na watu wanaokimbilia kufyeka misitu kwa minajiri ya kutafuta ardhi yenye rutuba, na zaidi kitasaidia kupunguza migogoro baina ya wakulima na wafugaji ambayo inatokea sasa.

Mikakati ya kuhamaisha kilimo hai ni elimu ya uhamasishaji ambayo inatakiwa ianzie ngazi ya chini, kwa mkulima mmoja mmoja, kwa vikundi tukitumia viongozi wa vijiji, kata, wilaya, mikoa na taifa ili kila mtu afahamu faida zake kwa ukamilifu.

Uwepo wa pembejeo za mboji nchini utamkwe kwa wananchi na serikali yenyewe. Hii itasaidia wakulima waelewe haraka na itasaidia kuharakisha watu wanaotaka kuweka miradi ya kutengeneza pembejeo hizo hapa nchini wapate mwelekeo mzuri.

Pembejeo za mboji pia zinapaswa kutambuliwa na kuingizwa kwenye ruzuku kama pembejeo zingine ili mkulima apate unafuu na serikali haipaswi kupendelea zaidi mbolea za kemikali.

Taasisi ya TIGI International (T) Limited, ambayo ni mwagizaji na msambazaji mkubwa wa mbolea ya mboji asilia aina ya Erth Food kutoka Marekani, inasema mbolea hiyo ndiyo mkombozi wa mkulima wa Tanzania kwa kuwa inatengenezwa kwa kutumia taka za shamba zisizo na kemikali ambapo inasaidia kurudisha udongo uliochoka kurudi katika hali yake ya asili; inatumika kwa mazao ya aina zote hata maua, miti na nyasi; inakaa na unyevunyevu muda mrefu; ni rafiki mkubwa wa mazingira; hutakiwi kuchanganya mbolea hii na mbolea nyingine za kemikali; mazao unayolima kutumia mbolea za asili ni bora sana na huchukua muda mfupi kukomaa; na zaidi, ukitumia mboji hutakuwa na haja ya kuhama shamba kwa sababu ardhi itakuwa na rutuba yake ya asili.

Hata hivyo, Tanzania bado haijafikia lengo la kuuza bidhaa za kilimo hai katika masoko ya Ulaya, Marekani na Japan kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ya wakulima kukosa elimu ya kilimo hicho kama alivyopata kusema Mkurugenzi wa kampuni ya Tanzania Zanzibar Organic Producers Limited (TAZOP), Bw. Khamis Issa Mohamed, wakati wa kongamano la wadau wa mazao ya kilimo hai nchini lililofanyika mwaka 2006 katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha kilimo (SUA).
Alisema wakulima wengi nchini hawana elimu ya kutosha kuhusu kilimo hicho pamoja na mtaji wa kuwawezesha kulima kilimo hai jambo linalokwamisha Tanzania kuuza bidhaa nyingi katika masoko ya Ulaya na Marekani.
Akatoa mfano wa kampuni yake ambayo mwaka 2005 ilikuwa na zabuni ya tani 200 za viungo mbalimbali kama hiliki, tangawizi, mdalasini, bizari, maganda ya machungwa na limao kupeleka nchini Ujerumani lakini ilishindwa kufikia lengo na badala yake iliuza tani 71 tu kwa kipindi hicho na kuingiza jumla ya dola za Kimarekani 192,000.

Hata hivyo, serikali inatakiwa kuongeza juhudi zaidi katika kuhamasisha wananchi waendeleze kilimo hai, ambacho ni endelevu na rafiki wa mazingira, ili kiwanufaishe zaidi kwani mazao yatokanayo na kilimo hicho yana uhakika wa soko ulimwenguni tofauti nay ale yanayotumia mbolea za kemikali.

Kukaa kimya kwa serikali kunamaanisha kwamba hata wadau wanaojitokeza kushabikia kilimo hai nchini watakata tamaa, kwani hata mbolea asilia wanazoziagiza kutoka nje ama kuzitengeneza zinakosa soko kutokana na wakulima kutokuwa na elimu na maafisa kilimo kugoma kuhamasisha utumiaji wa mbolea hizo kwa maelezo kwamba hawajapewa maagizo kutoka wizarani.

Kama kweli tunataka kujikomboa kupitia kilimo, kwa kweli hatuna budi kutumia zaidi kilimo hai ambacho pia kinaweza kutuepusha na migogoro ya ardhi kama inayojitokeza sasa baina ya wakulima na wafugaji.

Mwisho.
Miaka 46 ya Muungano uliokumbwa na migogoro lukuki

* Zanzibar ilipojiunga OIC, G55 wakaitaka serikali ya Tanganyika
* Wazanzibari sasa wataka Utaifa wao, mafuta yawapa kiburi

DANIEL MBEGA
Dar es Salaam
ILIKUWA Jumapili, Aprili 26, 1964, saa 4.00 asubuhi wakati Mwenyekiti wa TANU Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Mwenyekiti wa Afro-Shiraz Party (ASP) Sheikh Abeid Amani Karume walipokutana mjini Dar es Salaam na kusaini hati ya makubaliano ya kuziunganisha nchi zao.

Muungano huu ulifikiriwa kwa takribani miezi mitatu na siku 24 tu tangu yalipofanyika mapinduzi ya kuung'oa utawala dhalimu wa Kisultani visiwani Zanzibar hapo Januari 12, 1964. Kabla ya kutiwa saini, wakuu hao wa nchi mbili walikuwa wamefanya mazungumzo mara kadhaa mjini Dar es Salaam na Unguja na ndipo wakafikia mwafaka wa kuziunganisha nchi hizo.

Wapo walioupinga (na wanaendelea kuupinga) kwamba haukufuata misingi inayotakiwa katika muungano halisi, lakini pia wapo walioufurahia na wanaendelea kuufurahia kwa kuwa umeleta udugu na kujenga umoja na mshikamano.

Kwa miaka 46 Muungano huo umewaunganisha vyema Watanganyika na Wazanzibari na hivyo kuijenga Tanzania yenye nia, umoja, amani, upendo na mshikamano.

Hata hivyo, Muungano huo umepitia katika vipindi vigumu mno na kuna nyakati ambapo umetiwa msukosuko kiasi cha kutishia hatma yake. Hilo, kwa kiasi kikubwa, limetokana na baadhi ya watu kutoa mapendekezo anuai yanayoashiria muungano huo ama unaweza kuendelea kudumu au kuvunjika kabisa.

Hali hiyo imezidi kuwaweka njiapanda Watanzania, na viongozi wa serikali ya Muungano na ile ya Mapinduzi, na sasa wameazimia kuulinda kwa hali na mali ili kuwaenzi waasisi wake. Katika hotuba yake ya kwanza aliyoitoa mjini Dodoma baada ya kuapishwa, Rais Jakaya Mrisho Kikwete aliweka bayana kwamba suala la muungano litashughulikiwa kikamilifu ili kuunusuru, na kwa kuthibitisha hilo akaunda wizara mpya inayoshughulikia masuala ya Muungano.

Kuundwa kwa wizara hiyo nyeti hakumaanishi kwamba ubabe utatumika kuulinda muungano, bali busara ndizo zinazotumika, kwani miongoni mwa majukumu yake ni kukusanya kero za Muungano na kuzitatua, na pia kuweka misingi imara inayoweza kuudumisha kwa maslahi na ustawi wa taifa hili.

Wananchi wa Tanzania wanazijua faida na hasara za muungano huo kwa kipindi chote hicho na ni wazi kwamba wako katika nafasi nzuri ya kuchangia na kurekebisha kasoro zilizojitokeza ama mapungufu yaliyopo ili kuuimarisha zaidi.

Hoja ya Mwalimu Nyerere na Sheikh Karume ya kuanzisha Muungano haikuwa mbaya asilani, lakini katika kipindi cha karibuni kila upande wa Muungano umekuwa ukiona kama unakandamizwa na upande mwingine.

Wakati Wazanzibari wanasema Muungano umeumeza utaifa wao, baadhi ya Watanganyika nao wamekuwa wakisema rasilimali nyingi za Tanzania Bara zimekuwa zikitoweka kuwanufaisha Wazanzibari katika kile kinachoonekana kama kujipendekeza kwa serikali ya CCM kulinda kwa nguvu zote ili usivunjike.

Wazanzibari, kwa upande wao wanaendelea kusema kwamba kwa kipindi chote hicho wameshindwa kufanya jambo lolote kwa maendeleo yao kutokana na kivuli cha muungano na kwamba kila wanalotaka kulifanya lazima serikali ya Muungano ihoji.

SUALA LA UTAIFA...
Yapo mengi ambayo Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imekuwa ikitaka kufanya bila kupitia kwenye Muungano na mojawapo ni uamuzi wake wa kutaka kujiunga na Shirikisho la Nchi za Kiislamu Duniani (Organisation of Islamic Conference - OIC) mwaka 1992. Hapo ndipo hasa 'chunusi' wa Muungano alipoingia.

Lengo kubwa la SMZ kwa wakati ule, chini ya Dk. Salmin Amour Juma, lilikuwa kuifanya Zanzibar kuwa nchi au taifa la Kiislamu, wakati inafahamu fika suala kama hilo lilipaswa kujadiliwa kabla ya kuchukua maamuzi mazito kama aliyokuwa amechukua Dk. Salmin.

Uamuzi huo ukazua mjadala mrefu sana ndani ya Chama cha Mapinduzi (wakati huo serikali ilikuwa bado ya chama kimoja) na hata bungeni, ambako wabunge na wana-CCM wa Bara waliona wamesalitiwa na kiongozi huyo wa Zanzibar ambaye pia kikatiba, ndiye Makamu Mwenyekiti wa CCM upande wa Zanzibar na pia wakati huo alikuwa ndiye Makamu wa Kwanza wa Rais wa Muungano!

Lakini Zanzibar haikujiondoa OIC kama tulivyoelezwa na viongozi wetu, bali kilichotokea ni kwamba, OIC ilichunguza na kukuta Zanzibar siyo Taifa linalojitegemea, yaani Sovereignty State, na kwa mujibu wa masharti yao, haikustahili kuwa mwanachama, hivyo wakaiondoa, siyo kwamba yenyewe ilijitoa baada ya shinikizo.

Pamoja na kuondolewa huko, Zanzibar iliendelea kulalamika kwa kuingiliwa katika mambo yake ya ndani kwa kisingizio cha muungano, ambao kwa kizazi cha sasa wanaiona hali hiyo kana kwamba imewadumaza.

Kujiunga kwa Zanzibar katika OIC kuliwazindua wabunge wa Tanzania Bara, ambao waliona kuwepo kwa serikali mbili ndani ya Muungano kulikuwa ni kama kuwapa kiburi Wazanzibari, kiasi cha kufanya lolote wanalotaka bila kusubiri baraka za upande mwingine.

Ndipo katika kikao cha Bunge la Bajeti cha mwaka 1993, aliyekuwa Mbunge wa Chunya, Mheshimiwa Njelu Edward Mulugale Kasaka akawasilisha hoja binafsi bungeni na kudai Serikali ya Tanganyika ndani ya Muungano ili kutoa uwiano sawa.

Kwa bahati nzuri hoja hiyo ilipata baraka za Waziri Mkuu wa wakati huo, John Samwel Malecela 'Cigwiyemisi' na kupitishwa na Spika wa Bunge wa wakati huo, marehemu Chifu Adam Sapi Mkwawa ili ijadiliwe ingawa alizuia mjadala usiwe mrefu sana. Hata katika Bajeti ya Wizara ya Sheria na Katiba iliyokuwa chini ya Spika wa sasa Samuel Sitta, waliainisha kwamba kulikuwa na ‘Waraka wa Kutaka Maoni ya Wananchi kuhusu Hoja ya Tanganyika (White Paper)’.

Ni katika mjadala huo ambapo kulionekana kuna mchanganyiko; wengine wakiunga mkono na wengine wakipinga mabadiliko ya Katiba ya Muungano kufanya ziwepo serikali tatu.

Wabunge 55 waliofahamika kama G55, wakiongozwa na mtoa hoja, Njelu Kasaka, waliiunga mkono hoja hiyo. Baadaye wakaongezeka wengine kumi na kuifanya idadi yao kuwa 65 hadi kufikia Julai 22, 1994. Wabunge waliounga mkono na majimbo yao ya wakati huo yakiwa kwenye mabano ni; Mateo Tluway Qaresi (Babati), Jenerali Twaha Khalfani Ulimwengu (Taifa/Jumuiya ya Vijana), Mbwete Polile Hombee (Mbeya Vijijini), John Byeitima (Karagwe), Chediel Yohane Mgonja (same), Japhet Sichona (Mbozi), Benedict Losurutia (Kiteto), Dk. Mganga Kipuyo (Arumeru Magharibi), Stanley Kinuno (Nyang'hwale), Dk. Aaron Chiduo (Gairo), Edward Oyombe Ayila (Rorya) na Shashu Lugeye (Solwa).

Wengine walikuwa John Mwanga (Moshi Mjini), Dk. Deogratius Mwita (Serengeti), Abel Mwanga (Musoma Mjini), Juma Jamaldin Akukweti (Tunduru), Patrick Silvanus Qorro (Karatu), Steven Mwaduma (Iringa Mashariki), Dk. Ndembwela Ngunangwa (Njombe Kusini), Richard Koillah (Ngorongoro), Ahmed A. Mpakani (Iringa Magharibi), Paschal K. Mabiti (Mwanza), Luteni Lepilal Ole Moloimet (Monduli), Lumuli Alipipi Kasyupa (Kyela), Profesa Aaron Masawe (Hai) na Arcado Ntagazwa (Kibondo).

Walikuwemo pia Phineas Nnko (Arumeru Mashariki), Paschal Degera (Kondoa Kusini), Mussa Nkhangaa (Singida Mjini), Halimenshi Kahema Mayonga (Kigoma Kaskazini), Said Abdallah Nakuwa (Lindi Mjini), na Mosi Tambwe (Taifa/Wanawake).

Wengine ni Luteni Kanali John Mhina (Muheza), Charles Kagonji (Mlalo), Kisyeri Werema Chambiri (Tarime), Tobi Tajiri Mweri (Pangani), William H. Mpiluka (Mufindi), Aidan Livigha (Ruangwa), Philip Sanka Marmo (Mbulu), Erasto K. Lossioki (Simanjiro), Shamim Khan (Morogoro Mjini), Raphael Shempemba (Lushoto), Phares Kabuye (Biharamulo), Evarist Mwanansao (Nkasi), Mussa Masomo (Handeni), Jared Ghachocha (Ngara), na Mariam Kamm (Taifa/Wanawake).

MAMBO WALIYOYATAKA...
Walitaka Muungano wa Tanzania, uliozaliwa bila kupata baraka za wananchi wengine na hivyo kuwa na mapungufu, utazamwe upya. Walifikiria kwamba kwa wakati huo ulizaliwa kwa makubaliano tu kati ya TANU na Afro-Shiraz Party (ASP), lakini bila ridhaa ya wananchi.

Wakaeleza kwamba kwa wakati huo ilikuwa lazima Muungano huo ufanywe haraka ili kulinda mapinduzi ya kumwaga damu ya ndugu zatu wa Zanzibar; Unguja na Pemba, ambavyo ni visiwa vidogo sana, kwa hiyo Sultan Jamshid angeweza kurejea tena kwa msaada kutoka kokote kule duniani na inasemekana tayari alikuwa ameandaa majeshi ili arudi kuivamia Zanzibar.

Lakini baada ya kusikia Zanzibar na Tanganyika zimeungana hata yeye kule alikokimbilia na wafadhili wake walikata tamaa kurejesha tena utawala wa kibwanyenye (Usultani) visiwani humo.

Kwa maana nyingine, tunaweza kusema nchi hizo ziliungana kwa sababu za ki-ulinzi au kiudugu zaidi na kwa uzalendo wa Kiafrika, Muungano ambao haukupata baraka za wananchi kama walivyokuwa wakipigania uhuru wao. Lakini sasa baada ya miaka 43 hakuna tena tishio kama hilo (dhidi ya ndugu zetu wa Visiwani).

Kwanza, hata wale ambao wangefanya hivyo, sasa nao wamekata tamaa kabisa. Pili, kikubwa zaidi ni kwamba hata serikali yenyewe ya Mapinduzi Zanzibar sasa ina uhusiano mzuri tu hata na watawala wake wa zamani.

Ni suala la u-taifa tu kwa sababu chini ya mwavuli wa Muungano, Mtanganyika amepoteza kabisa utaifa wake (National Identity). Hakuna popote katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano panapotaja kitu kinachoitwa 'Tanganyika' au u-Tanganyika. Badala yake sehemu kama hiyo imemezwa na neno Tanzania. Lakini Zanzibar ina serikali yake yenyewe, SMZ.

Ndiyo maana hata serikali ya CCM ilipoagiza hoja hiyo iondolewe Bungeni mwaka 1994 na kuamua kuendelea na mfumo wa serikali mbili ndani ya Muungano huku ikifanya mikakati kuunda serikali moja, Wazanzibari waligoma kabisa kuafiki muundo huo wa serikali moja.

Wazanziibari, wakiongozwa na Rais wao wa wakati ule Dk. Salmin Amour Juma, walisema katu SMZ haiwezi kufa na kwamba hawaafiki serikali moja. Wengine wakaendelea kusema kwamba Muungano haujainufaisha Zanzibar kwa lolote, hivyo kumaanisha kwamba hawana haja nao.

CCM iliamua kuendesha kura za maoni kwa wanachama wake na wananchi kwa ujumla ili kuona walikuwa na mtazamo gani kuhusu suala la Muungano. Waliokuwa wakitetea Muungano ilionekana waliutetea kwa lugha kali ya hasira, ghadhabu na hata vitisho vya kuwafukuza wenzao kwenye Chama. Waliodai Utanganyika nao walidai kwa lugha hiyo hiyo ya ukali, wakijibu mapigo.

Kitu kilichopaswa ama kinachopaswa kutazamwa hapa ni mambo machache kama yafuatayo; Kwanza kabisa, kudai Utanganyika siyo kosa la uhaini wala la jinai. Pili, Chama cha Mapinduzi siyo wananchi kwa sababu wananchi wako milioni 35, lakini wanachama wa CCM hadi kufikia mwaka 1994 walikuwa 3,506,355 tu. Pengine kutokana na kuwepo kwa vyama vingi vya siasa idadi hiyo imepungua kwa sasa.

Tatu, walioulizwa maoni hayo kuhusu Muungano mwaka 1994 ni wanachama wa CCM peke yao, tena wapatao 1,349,501. Hesabu hiyo ilikuwa sawa na asilimia 33.49 tu ya wanachama wote nchi nzima. Asilimia 61.75 ya asilimia 33.49 walipendekea serikali mbili, asilimia 29.21 walipendekeza serikali moja, na asilimia 8.27 walitaka serikali ya Tanganyika ndani ya Muungano. Kura za maoni zilizoharibika zilikuwa asilimia 0.67.

Jambo la kujiuliza, kura hizo zilihesabiwa na nani? Waliopiga kura ni wana-CCM na waliozihesabu ni hao hao wanachama wa CCM pamoja na viongozi wao, ambao walikuwa wakipinga hoja hiyo. Unategemea wangetoa majibu gani? Walichosahau ni kwamba, suala hili ni nyeti na linawagusa wote, wananchi wa Tanzania kwa ujumla wao, bila kujali itikadi zao za siasa.

Nakumbuka Mkuu wa Mkoa wa Mara wa wakati huo, Bwana Joseph Butiku, alitoa kauli kali kwamba msimamo uliokuwa umefikiwa na CCM ni kuwa na serikali mbili katika Muungano kuelekea serikali moja na kwamba kama Rais wa Zanzibar, Dk. Salmin Amour Juma, alikuwa anapinga shauri yake.

Bwana Butiku aliyasema hayo Jumanne, Agosti 23, 1994 kwenye ukumbi wa Karimjee, Dar es Salaam wakati akishiriki mjadala wa hoja ya serikali ya kufuta Azimio la Bunge la mwaka 1993 la kuanzishwa kwa serikali ya Tanganyika ndani ya Muungano. Nanukuu maneno yake: "Wananiuliza, umemsikia Rais wa Zanzibar? Aah mimi nasema Rais wa Zanzibar ni kiongozi wetu... tunamheshimu ... lakini kakosea ... Huu ndio msimamo wa Chama; serikali mbili kuelekea serikali moja na kama Waziri Mkuu hataki, shauri yake, kama Rais wa Zanzibar hataki, shauri yake, maana Chama cha Mapinduzi kina utaratibu wa kuliongoza taifa hili..." mwisho wa kunukuu.

Mwasisi wa Muungano huo, Hayati Nyerere, aliamua kuingilia kati hoja ya Tanganyika na kusema kwamba, kuundwa kwa serikali hiyo kungemaanisha kifo cha Muungano. Hivyo, akasema asingekuwa tayari kuona Muungano unakufa hali yeye akiwa hai!

Ndipo akaamua kutunga kitabu cha 'Uongozi wetu na hatma ya Tanzania' kilichokuwa kinaponda utaratibu uliotumiwa na viongozi wa Muungano wakati huo kuipitisha hoja ya Tanganyika ijadiliwe bungeni bila kupata baraka za CCM.

Pengine kwa kuwa sasa amekufa ndiyo maana baadhi ya watu wanatumia mwanya huo kutaka kuua Muungano kama walivyoshiriki kuua 'mtoto mwingine' wa Mwalimu, Azimio la Arusha lililosisitiza Ujamaa na Kujitegemea.

Jambo la kusikitisha zaidi ni kwamba, wale wabunge walioonekana kuipigia kelele sana hoja hiyo walipewa vyeo enzi zile za Rais Ally Hassan Mwinyi; wengine walikuwa mawaziri, na wengine manaibu mawaziri, wakuu wa mikoa na nyadhifa nyingine. Sisi akina yakhe ambao tulitegemea kwamba tungeona mabadiliko, tulitafsiri kitendo hicho kama kuwaziba midomo wabunge hao, maana baada ya kupata vyeo hivyo wakakaa kimya, wengine mpaka sasa hawataki kabisa kuisikia hiyo. Ya nini? Mbona wanakula na kusaza?

SERIKALI ILIKUWEPO...
Wazanzibari wanaendelea kupinga muundo wa muungano wa serikali moja, pengine ndiyo maana mpaka sasa - miaka 14 baadaye - CCM haijasema lolote kuhusu muundo wa serikali kwenye muungano, iwe ni serikali mbili kama ilivyo sasa, moja au tatu.

Sababu kubwa inayowafanya Wazanzibari wakatae muundo huo ni kwamba wanadai Zanzibar ilikuwa na serikali yake kamili wakati Muungano ulipofanyika Aprili 26, 1964! Ni kweli kabisa, tangu Januari hadi Aprili 1964 Zanzibar ilikuwa nchi huru (Sovereign State) ikiitwa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar. Mnamo Aprili 6, 1964 Zanzibar ilikuwa imefungua Balozi tatu; London, Uingereza alikuwepo Othman Shariff; Cairo, Misri alikuwepo Salim Ahmed Salim, na New York, Marekani alikuwepo Hasnu Makame. Waziri wa Mambo ya Nje alikuwa Profesa Abdulrahman Mohammed Babu.

Pia nchi 17 zilikwishaitambua Zanzibar hadi kufikia Aprili 26, 1964. Nchi hizo ni Ghana (28/1/1964), Cameroon (30/1/1964), German Democratic Republic - GDR (30/1/1964), Poland (30/1/1964), Israel (1/2/1964), Misri (4/2/1964), Urusi (4/2/1964), China (6/2/1964), Czechoslovakia (18/2/1964), Algeria (18/2/1964), India (22/2/1964), Uingereza (24/2/1964), Marekani (24/2/1964), Mali (26/2/1964), Congo-Brazzaville (26/2/1964), Ceylon (26/2/1964) na Liberia (29/2/1964).

Aidha, nchi tisa zilikwishafungua Balozi zao huko Zanzibar kabla ya Muungano. Nchi hizo ni Ghana, GDR, Israel, Urusi, China, Uingereza, Vietnam, Marekani na Ufaransa.

Zanzibar pia tayari ilikuwa mjumbe katika Umoja wa Nchi Huru za Afrika (OAU), Jumuiya ya Madola na Umoja wa Mataifa (UN), mnamo Aprili 6, 1964, na ilikuwa inashirikishwa UNESCO, ADB na mashirika mengine ya kimataifa.

Hata hivyo, hiyo siyo hoja ya msingi kwao kukataa serikali moja eti kwa vile wakati huo ilikuwa na serikali yake. Ikumbukwe pia kwamba Tanganyika nayo ilikuwa na serikali yake kamili kabla ya Muungano.

Cha msingi kuzungumzia ili kuunusuru Muungano ni kuangalia maeneo gani muhimu yanayotakiwa kurekebishwa na muundo gani wa serikali unaoweza kuwa muafaka, maana pamoja na hoja hiyo kuzimwa miaka 16 iliyopita, hivi sasa imeibuka tena na inazidi kufukuta kama moto wa volvano, matokeo yake yatakuwa mabaya zaidi hasa katika kipindi hiki cha siasa ya vyama vingi.

Wazanzibari wameibuka upya wakitaka utaifa wao, hoja ambayo imekuwa ikizusha hata mijadala Bungeni. Hoja hii inonekana kama imezuka mara tu baada ya kuibuka kwa tetesi kwamba Zanzbar kunaweza kuwepo na hazina ya mafuta ya petroli. Je, wenzetu hawa hawataki kushirikiana nasi kula keki hiyo? Mbona mapato yetu ya madini, utalii na raslimali nyingine wanatumia?

Katiba ya Tanzania siyo Msahafu, yaani siyo Biblia wala Qur'an, ambayo haiwezi kukosolewa. Hii imetungwa na wananchi kwa manufaa yao wenyewe, na wanapoona kwamba kuna ulazima wa kufanya matengenezo (marekebisho) basi wanaweza kwa kufuata taratibu. Lakini ni taratibu gani zilizofanyika mpaka sasa miaka 13 imepita kama siyo hoja hiyo kutupwa kapuni? Jibu wanalo wana-CCM, sisi wengine ni wafuasi tu! Pengine kuundwa kwa Wizara ya Muungano kunaweza kuleta picha kalisi. Sijui! Labda, tutaona!

MWISHO.

JUST ANOTHER THOUGHT

JUST ANOTHER THOUGHT

A person asked God, “What surprises you most about mankind?”

And God answered,
“That they loose their Health to make money and they loose their money to restore their Health.

That by thinking anxiously about the future, they forget the present, such that they live neither for the present nor the future.

That they live as if they will never die and they die as if they had never lived.….”

BECAUSE I'M A MAN...

Because I’m a man, when one of our appliances stops working I will insist on taking it apart, despite evidence that this will just cost me twice as much once the repair person gets here and has to put it back together.

Because I’m a man, I don’t think we’re all that lost, and no, I don’t think we should stop and ask someone. Why would you listen to a complete stranger I mean, how the hell could he know where we’re going?

Because I’m a man, there is no need to ask me what I’m thinking about. The answer is always either sex or football, though I have to make up something else when you ask, so don’t.

Because I’m a man, I do not want to visit your mother, come visit us, or talk to her when she calls, or think about her any more than I have to. Whatever you got her for mother’s day is okay, I don’t need to see it. And don’t forget to pick up something for my mommy, too!

Because I’m a man, I am capable of announcing, “one more beer and I really have to go”, and mean it every single time I say it, even when it gets to the point that the one bar closes and my buddies and I have to go hunt down another. I will find it increasingly hilarious to have my pals call you to tell you I’ll be home soon, and no, I don’t understand why you threw all my clothes into the front yard. Like, what’s the connection?

Because I’m a man, you don’t have to ask me if I liked the movie. Chances are, if you’re crying at the end of it, I didn’t.

Because I’m a man, yes, I have to turn up the radio when Bruce Springsteen or The Doors comes on, and then, yes, I have to tell you every single time about how Bruce had his picture on the cover of Time and Newsweek the same day, or how Jim Morrison is buried in Paris and everyone visits his grave. Please do not behave as if you do not find this fascinating.

Because I’m a man, I think what you’re wearing is fine. I thought what you were wearing five minutes ago was fine, too. Either pair of shoes is fine. With the belt or without it looks fine. Your hair is fine. You look fine. Can we just go now?

Because I’m a man and this is, after all, the 90’s, I will share equally in the housework. You just do the laundry, the cooking, the gardening, the cleaning, and the dishes. I’ll do the rest.

A SIMPLE GUIDE TO LIFE

1. Follow your dream! Unless it’s the one where you’re at work in your underwear during a fire drill.

2. Always take time to stop and smell the roses and sooner or later, you’ll inhale a bee.

3. Do not walk behind me, for I may not lead. Do not walk ahead of me, for I may not follow. Do not walk beside me, either. Just leave me alone.

4. If you don’t like my driving, don’t call anyone. Just take another road. That’s why the highway department made so many of them.

5. If a motorist cuts you off, just turn the other cheek. Nothing gets the message across like a good mooning.

6. When I’m feeling down, I like to whistle. It makes the neighbor’s dog run to the end of his chain and gag himself.

7. It’s always darkest before dawn. So if you’re going to steal the neighbor’s newspaper, that’s the time to do it.

8. A handy telephone tip: Keep a small chalkboard near the phone. That way, when a salesman calls, you can hold the receiver up to it and run your fingernails across it until he hangs up.

9. Each day I try to enjoy something from each of the four groups: the bonbon group, that salty-snack group, the caffeine group and the “What ever-it-is-the-tinfoil-in-the-back-of-the-fridge”.

10. Into every life some rain must fall. Unusually when your car windows are down.

11. Just remember: You gotta break some eggs to make a real mess on the neighbor’s car!

12. When you find yourself getting irritated with someone, try to remember that all men are brothers and just give them a noogie.

13. This morning I woke up to the unmistakable scent of pigs in a blanket. That’s the price you pay for letting the relatives stay over.

14. It’s a small world. So you gotta use your elbows a lot.

15. Keep your nose to the grindstone and your shoulder to the wheel. It’s a lot cheaper than plastic surgery.

16. This land is your land. This land is my land. So stay in your land.

17. Love is like a roller coaster: When it’s good you don’t want to get off, and when it isn’t, you can’t wait to throw up.

DEDICATION TO YOUNG PEOPLE

Youth is a time of hope. Also of uncertainty. But for a person who is young and healthy, uncertainty just means a challenge. It is important to be positive. First of all about yourself. But also about your family and your people. As a unique person and each human being are unique, you have enormous potential. Because you have so much potential, people may sometimes feel negatively challenged by that potential and try to undermine it.

You have to fight for your right to make your place in society. To do that you have to use all the chances given you now to be a positive element in whatever situation you find yourself in, in future. So, it may be necessary to be a ‘rebel in reverse’ as it were. That takes real courage, to set your goal and stick to it. You choose your crowd. You exercise your right to choose.
Don’t lose your freedom for the sake of anyone. Real freedom, freedom to choose the right thing, the best for you.

Always bear a few things in mind while exercising your right to choose.

* Never take a decision when you are in a fit of anger or depression.
* Never take a decision when you are emotionally high.
* Why should fads or the decision of the group tie you down?
* What are you?
* What do you want tomorrow to be for you?

No matter how strong the group decision may be, you must think and make your decision. Many times it is necessary to consult before taking a decision. Go to someone whose life you admire, not necessarily the person you like most, but the person who is whole, who is one person, wherever she or he is and whatever she or he does.

* Remember that there is always tomorrow, and tomorrow is hope. Very few things are ‘written in stone’. Most of the mistakes we make can be rectified. They can be corrected. Problems have a solution, and each new day is a new start, a new chance, a New Hope. Indeed the youth are our hope you are our future.

Also remember that your parents love you unconditionally, you have their support and want the best in life for you ¨

COSTA VICTOR NAMPOKA

Mguu ulivyokatisha ndoto za kucheza soka Ulaya

DANIEL MBEGA
Dar es Salaam

NI majira ya saa 5.20 hivi asubuhi, niko hapa Ukonga-Banana nikiwania kupanda daladala la kwenda kwenye kitongoji cha Kitunda-Kibeberu, moja ya vitongoji vinavyokua kwa kasi hapa jijini Dar es Salaam.
Sijui ni umbali gani kutoka hapa, hivyo namuuliza dereva ambaye nimeketi naye pembeni yake. Ananiambia ni mwendo kama wa dakika 15 tu hivi. Nashusha pumzi kwa kujua kwamba kumbe si mbali sana kama nilivyofikiria.
Nawasili kwenye kitongoji cha Kibeberu, ambako ndiko magari yanakogeuzia, na bila kupoteza muda nampigia simu mwenyeji wangu kwamba tayari nimeshafika. Namhurumia huko aliko kama ataamua kuja kunipokea, lakini nafarijika anaponiambia kwamba nimuulize mtu yeyote hapo kituoni atanileta.
Watoto wawili wanajitolea kunipeleka nyumbani kwa mwenyeji wangu, ambaye namkuta akiwa kajilaza kwenye kochi akizungumza na rafiki zake wawili waliomtembelea. Anapenda kuketi vizuri, lakini hali haimruhusu.
“Poleni jamani kwa safari ndefu!” ndivyo anavyoanza kusema huyu mwenyeji wangu, ambaye si mwingine zaidi ya mlinzi mahiri wa timu ya soka ya Taifa, Taifa Stars, pamoja na klabu ya Simba, Costa Victor Nampoka ‘Nyumba’. Anajaribu kuuweka vyema mguu wake wa kulia ambao bado umefungwa bandeji gumu (POP) baada ya kuvunjia mazoezini takribani mwezi mmoja na nusu uliopita.
“Hakuna shaka, Dar es Salaam ni moja na hakuna sehemu unayoweza kusema ni mbali,” namjibu kumpa matumaini.
“Hapana! Pamoja na ukweli kwamba mkoa kazini, lakini naamini uamua kufunga safari mpaka kuja kuniona ni jambo kubwa sana. Mngeweza hata kuniuliza maendeleo yangu kwa njia ya simu. Sina budi kushukuru kwa kuja kunijulia hali,” anasema.
Mara anaingia dada mmoja mweupe hivi ambaye anaketi pamoja na Costa kwenye kochi moja. Costa mwenyewe anamtambulisha kwamba ndiye mkewe, Dina, ambaye wamebahatika kuzaa naye watoto wawili; Victor Costa mwenye miaka miwili na Rio Costa mwenye mwaka 1.5. Anatukaribisha.
Anapoondoka namwambia ni jambo la kawaida kuwatembelea wagonjwa, na katika suala lake yeye ni mmoja wa watu waliotoa mchango mkubwa katika timu ya taifa ya soka ambayo sasa iko katika nafasi nzuri ya kufuzu kwa fainali za Mataifa ya Afrika mwakani ikiwa tu itashinda mechi yake ya mwisho.
“Nashukuru kusikia hivyo, lakini sura zinazokuja hapa daima ni zile nilizozizowea, yaani marafiki zangu na wachezaji wenzangu wa klabu ya Simba, labda na viongozi wa Simba,” anasema kwa huzuni.
“Una maana kwamba viongozi wa timu ya taifa na hata TFF huwa hawakutembelei?” nauliza.
Anasema tangu alipoumia siku tatu kabla ya Taifa Stars kupambana na Zambia katika mechi ya kirafiki na kupelekwa Muhimbili na daktari wa timu Shecky Mngazija, hajatembelewa wala kujuliwa hali hata kwa simu na kiongozi yeyote yule wa chombo hicho cha juu cha soka nchini.
Anaongeza kwamba, ni wachezaji wenzake wa Simba ndio baadhi yao huwa wanawasiliana naye pamoja na viongozi na marafiki wa klabu ambao wameonekana kumjali vya kutosha kiasi cha kutuma gari kila siku katika mechi zote ambazo Simba ilicheza kwenye hatua ya Sita Bora ya Ligi ya Mpito hadi fainali.
“Kwa kweli viongozi wa klabu yangu wananijali sana na sina budi kuwashukuru,” anasema. Kama vile amekumbuka kitu, anasema anamshukuru pia mtu mmoja wa Benki ya NMB anayeitwa Kajura (Imani Kajura ambaye ni Meneja Masoko).
“Huyu jamaa baada ya kutoa zawadi za shilingi 500,000 kwa kila mchezaji kutokana na timu ya Taifa kushinda kule Burkina Faso, alinipigia simu kuniambia nilitakiwa kwenda kusaini fomu za akaunti. Nikamwambia sina hata pesa ya nauli na kwa jinsi ninavyoumwa nisingeweza kupanda daladala, lakini akaniambia nichukue teksi nay eye angelipa. Namshukuru sana,” anasema.
Hata hivyo, amewaasa wachezaji wengine; wa klabu na hata timu ya taifa, kwamba pindi watakapoumia na kushindwa kujuliwa hali na viongozi wao wasife moyo bali hiyo iwe changamoto kwao kufanya vizuri watakaporejea uwanjani.
“Binafsi sina kinyongo na yeyote. Naomba Mungu nipone nirejee uwanjani, ikibidi niliwakilishe taifa langu, kwa sababu natambua kwamba timu ya Taifa ni ya Watanzania wote wala si ya mtu mmoja. Naamini Watanzania milioni kadhaa wako pamoja na mimi na hata walipojua kwamba nimeumia walinitumia meseji za pole zaidi ya 3,000, hata sijui walikoipata namba yangu,” anasema.

Kuvunjika mguu
Costa anasema kwamba walikuwa kwenye mazoezi kama kawaida kwenye uwanja wa Karume, akauzuia mpira bila kumkwatua ama kukwatuliwa, kisha akaserereka.
“Ghafla nikasikia maumivu makali sana, ikabidi wajaribu kuniganga pale, lakini yalipozidi wakanikimbiza Muhimbili. Huko nikaambiwa kwamba nimevunjika mfupa mdogo wa mguu wa kulia. Sikuwa na jinsi, wakanifunga hogo (bandeji gumu – POP) na kusema kwamba nirudi baada ya wiki sita,” anasema kwa majonzi.
Anasema kwamba, baada ya kutolewa kwa bandeji hilo ndipo atakapojua kama atakuwa nje ya uwanja kwa muda gani, kwani mpaka sasa hajaanza hata kuukanyangia mguu huo.
Akasema kuvunjika mguu kumemnyima nafasi ya kuliwakilisha taifa, na zaidi kumechelewesha kutimia kwa ndoto zake kwani pengine hivi sasa angeweza kuwa Afrika Kusini kujaribu kucheza soka ya kulipwa akiwa njiani kwenda cheza Ulaya.
“Kuna wakala mmoja ambaye kwa muda mrefu sasa amekuwa akinufuatilia, yuko Afrika Kusini, na alikwenda Burkina Faso kunitazama, lakini mimi sikuwepo. Ilikuwa niende Afrika Kusini kufanya majaribio na naamini ningewea kufanikiwa,” anasema mchezaji huyo.
Anasema kwamba, alikuwa na matumaini ya kufuzu kwa sababu soka ya Afrika Kusini haina tofauti na ya huku, tena hakuwa mgeni baada ya kucheza kwa muda nchini humo miaka mitatu iliyopita.
“Wanachotuzidi kule ni promosheni, televisheni zinajitahidi sana kuonyesha mpira hata wa daraja la tatu, na hiyo inamsaidia mchezaji kutazama na kuona wapi alipokosea ili kujirekebisha, ama afanye nini kuongeza jitihada,” anasema.
Anaongeza kwamba alishindwa kuendelea kucheza huko kwa sababu klabu aliyokuwa akiichezea wakati ule ya Marlasburg (Tembas) iliyokuwa daraja la kwanza mwaka 2005 ikiwa chini ya kocha wa zamani wa Simba Trott Moloto, iliinunua klabu moja iliyokuwa ligi kuu. Ikabidi wachezaji wa timu hizo wachekechwe, na majungu ndipo yakaibuka ambapo Moloto, ambaye ndiye aliyemfanyia mpango wa kwenda huko, akamgeuka. Ikabidi afungashe virago kurejea.
Hata hivyo, anasema kwamba ndoto zake bado hazijafutika, kwani anaamini anaweza kucheza Ulaya bila matatizo yoyote, na zaidi anasema angependa siku moja avae ‘uzi’ wa Manchester United akicheza pembeni ya Rio Ferdnand ambaye uchezaji wake unamvutia kiasi cha kumwitia mwanawe mdogo jina hilo kutokana na kumhusudu.
Akizungumzia nafasi ya Taifa Stars kufuzu kwa fainali za Mataifa ya Afrika mwakani, Costa (25) ambaye ni mtoto wa nne katika familia ya watoto watano wa mzee Victor Nampoka – wawili wanawake na watatu wanaume, anasema kwamba nafasi ipo, lakini mechi ya mwisho dhidi ya Msumbiji ni ngumu sana.
“Ile mechi ni kama fainali na inabidi maandalizi ya nguvu yafanyike pengine kuliko mechi zote zilizotangulia. Msumbiji ni wazuri sana kuliko hata Burkina Faso, na ina nafasi ya kufuzu ikiwa itashinda na Senegal wakafungwa, hivyo Watanzania tusibweteke bali tujiandae vizuri,” anasema huku akisikitika kwamba anaweza kuikosa mechi hiyo pia ikiwa ataambiwa apumzike.
Akizungumzia kuhusu maendeleo ya soka, mlinzi huyo anasema kwamba hakuna kitakachoinua zaidi ya soka la vijana, na kuongeza kwamba mashindano ya Copa Coca Cola yawe chachu wa klabu na wadau mbalimbali kuanza kuibua vipaji.
“Kule Brazil tulikokwenda kuna taasisi ya soka ya watoto wadogo. Watoto wanatoka nchi mbalimbali kwenda kufundishwa mpira, na wazazi wao wanalipia wastani wa dola 1,500 kwa mwezi ili watoto wao wajue mpira. Tusione wenzetu wamepiga hatua tukadhani kwamba ni miujiza, wamewekeza.
“Watanzania wanapaswa kuunga mkono juhudi za maendeleo ya soka ya vijana, kuanzia kwa wazazi, ambao wanapaswa kuwapa ‘sapoti’ watoto wao ikiwa ni pamoja na kuwapatia vifaa vya michezo na nauli ya kwenda mazoezini,” anaongeza.
Costa aliyemaliza elimu ya msingi mwaka 1994 Kinondoni Hananasif, jijini Dar es Salaam na kuungana na maelfu ya watoto ambao hawakufanikiwa kuchaguliwa kujiunga na sekondari, amewashauri wachezaji kuachana na anasa na kwamba wawe na malengo kama kweli wanataka kupiga hatua katika mchezo huo.
“Sijafanikiwa sana, lakini niseme ukweli kwamba nimejiepusha na mambo mengi. Sivuti sigara wala bangi, halafu niliacha kitambo kunywa pombe, tena basi nilikuwa nikinywa bia mbili ama tatu tu, lakini sasa sitaki kabisa nahitaji kukazana kwenye mpira ambao pekee ndio mwokozi wangu katika maisha,” anamalizia.

Wasifu:
Jina: Costa Victor Nampoka
Kuzaliwa: Oktoba 11, 1982, Dar es Salaam.
Umri: 25

Klabu za awali:
Five Star Kinondoni, Mkunguni FC Ilala, Eleven FC Buguruni, Saddam FC na International FC za Kinondoni.
Taifa Jang’ombe – Zanzibar (1998 – 1999)
Forodha Zanzibar (2000 – 2001)
Mtibwa Sugar (2002)
Simba (2003 – 2004)
Marlsburg – Afrika Kusini (2005)
Simba (2006 – mpaka sasa).