Wednesday, December 5, 2007

YANGA BWANGA AVUNJA PAMBANO SIMBA IKIINYUKA YANGA 2-1

DANIEL MBEGA

SIMBA SC Jumapili ya Novemba 27, 1977 kwa mara nyingine iliifunga tena Yanga kwa mabao 2-1 katika pambano ambalo lilivunjika dakika 12 kabla ya wakati wake kutokana na mchezaji Yanga Bwanga wa Yanga kukataa kutoka nje baada ya kuamuliwa na mwamuzi kufanya hivyo.

Bwanga, kwa makusudi kabisa, alimpiga daluga Nicodemus Njohole wa Simba kifuani ikiwa ni kulipiza kisasi kwa mchezaji huyo ambaye alikuwa amemtegea wakati wakiwania mpira. Bwanga alikuwa ameonywa mara ya kwanza kwa kadi ya njano katika dakika ya 16 alipomfanyia rafu Nicodemus tena na hivyo baada ya rafu mbaya kwa mara ya pili ikalazimika atolewe nje.

Lakini mchezaji huyo hakushtuka kwa amri hiyo badala yake akaendelea kurukaruka uwanjani akifanya mazoezi mepesi. Mwamuzi Stephen Lutayangirwa baada ya kusubiri kwa dakika 10 alipuliza kipenga cha kumaliza mchezo.

Mchezo wenyewe ulikuwa wa kwanza wa kuwania Kombe la Jitegemee, ambapo uliharibiwa kabisa kutokana na uchezaji mbaya wa wachezaji wa timu zote ambao walikuwa wakitembezeana madaruga na kuonyeshana ubabe wa dhahiri.

Kulikuwa na vipindi vichache sana vyenye msisimko na mara nyingi kulikuwa na rafu na mchezo wa hasira. Mwamuzi naye alistahili lawama kwa kufanya mchezo kuharibika zaidi. Hakuwa mkali inavyopasa kila wachezaji walipokuwa wakifanya makosa uwanjani.

Ukali pekee aliouonyesha wenye busara ni alipomtoa nje ya uwanja Daudi Salum 'Bruce Lee' wa Simba na Ayubu Shaaban wa Yanga walipokingiana ngumi. Kabla ya hapo alikuwa amewaonyesha kadi za njano Omar Mahadh na Daudi Salum wa Simba, na Yanga Bwanga wa Yanga.

Mameneja wa timu hizo Mohammed Viran wa Yanga na Abdulrahman Khamis Muchacho wa Simba ndio walioonyesha urafiki baada ya kuvunjika kwa mchezo huo kwani walitoka nje wakiwa wameshikana mikono huku wapenzi wa timu hizo mbili wakilaumiana kwa mchezo mbovu wa timu zao.

Simba iliwazidi kimchezo wapinzani wao katika dakika za mwanzo hadi walipojipatia bao lao la kwanza katika dakika ya 18. Mpira uliotoka kwa Abdallah Kibadeni aliyeupeleka mbele ulimkuta Jumanne Hassan Masimenti ambaye naye alitoa pasi ya kichwa kwa George Kulagwa ambaye aliachia mkwaju mkali ambao kipa wa Yanga Isega Isindani alishindwa kuukumbatia. Rahim Lumelezi aliyekuwa karibu akauwahi na kuutumbukiza wavuni.

Kuanzia hapo hadi mapumziko mchezo ulipooza sana ingawa Yanga ilikuwa ikicheza kwa ufundi zaidi ambao ungewaletea goli la kusawazisha kunako dakika ya 22 kwa kiki ya nguvu iliyopigwa na Karabi Mrisho lakini ikapaa juu ya goli.

Yanga iliwaingiza Ramadhan Mwinda na Danny Mwalusamba badala ya Karabi Mrisho na Burhani Hemed kipindi cha pili kilipoanza, lakini mabadiliko hayo hayakuleta tofauti sana.

Katika mojawapo ya hatari langoni mwa Simba, Filbert Rubibira aliunawa mpira na mwamuzi akaamuru penalty ipigwe. Wachezaji wa Yanga walitegeana kupiga mpaka Charles Mwanga alipojitolea lakini alipopiga mpira ukaota mbawa kwa kupaa juu ya goli.

Simba ilijiongezea bao la pili dakika ya 54. Bao hilo lilianzia na mpira wa kona iliyochongwa na Abdallah Kibadeni na kusababisha kizaazaa langoni, Nico Njohole akatokea na kufunga kirahisi.

Bao pekee la Yanga lilifungwa na Ezekiel Grayson dakika ya 64. Mohammed Kajole ndiye aliyesababisha bao hilo baada ya kuuachia mpira ambao angeweza kuokoa akidhani kipa wake Omar Mahadh atauwahi. Ezekiel akatokea na bila taabu akafumua mkwaju uliotinga wavuni.

Yanga ikaanza kucheza vizuri kuanzia hapo hadi mchezo ulipovunjika, lakini juhudi zao hazikuzaa matunda.

Mbali ya Bwanga kuamuliwa atoke nje, siku hiyo pia wachezaji Ayoub Shaaban wa Yanga, pamoja na Daudi Salum ‘Bruce Lee’ wa Simba, walitolewa nje kwa kadi nyekundu baada ya kuonywa mara mbili kila mmoja kwa mchezo mbaya, wakati Omar Mahadh bin Jabir wa Simba alionywa mara moja.

Yanga: Isega Isindani, Charles Mwanga, Fadhil/Boniface Makomole, Selemani Jongo, Hashim Kambi, Sam Kampambe, Burhani Hemed/Danny Mwalusamba, Ezekiel Grayson, Karabi Mrisho/Ramadhan Mwinda, Yanga Bwanga, Ayoub Shaaban.
Simba: Omar Mahadh, Daudi Salum, Mohammed Kajole, Aloo Mwitu, Filbert Rubibira, Athumani Juma, Rahim Lumelezi, Nico Njohole, Jumanne Hassan, Kibadeni, George Kulagwa.
WEWE MTOTO ROSA HEBU NENDA SHULE!

AHLANI Wasaalani mabibi na mabwana ambao daima siku kama ya leo hupendelea kuperuzi katika kona hii ya Tunazikumbuka, ambamo tunabarizi na kujikumbusha ile mikito ya zamani, miziki ya Bakulutu ambayo mpaka leo bado ni keki kweli inapodundwa.

Kwanza nianze kwa kumshukuru msomaji wangu mmoja kutoka Finland kwa kunipa fagio kuhusu uchambuzi wa nyimbo hizi za zamani. Msishangae, sasa hivi dunia imeshakuwa kama kiganja kutokana na mtandao ulio wazi, au utandawazi. Nimwambie tu kwamba, ombi lake la wimbo wa OSS, siutaji, lakini mwenyewe atauona tu.

Jana wakati nikiwa kwenye daladala, ule usafiri wetu akina siye, nilikumbana na mkasa mmoja ambao hakika ndio uliozaa mada yangu ya leo. Akina mama wawili, mtu na rafikiye, walikuwa wameketi siti moja wakizungumza kwa masikitiko makubwa.

Awali sikuelewa kisa ni nini, lakini baada ya muda mmojawao akapigiwa simu na baada ya kuzungumza na mtu huyo huku akipewa maelekezo, akasema kwamba wako njiani wanakwenda.

Alipokata simu mwenzake akamuuliza ni nani. Yule wa kwanza akasema kwamba wamempata mtu wanayemsaka. Mwenzake akamshauri awaambie waliompigia simu wampeleke huyo mtu polisi, lakini wakakubaliana kwamba haina haja kwa sababu walikuwa wamekaribia kufika. Wakateremka pale Keko Maflati karibu na uwanja wa taifa.

Hata hivyo, baada ya simu hiyo mmoja wao alikuwa akilaumu kwamba mtoto huyo wa kike amekuwa msumbufu sana. Ametafutiwa shule lakini badala ya kwenda huko akaamua kuzamia moja kwa moja anakokujua yeye.

“Akipelekwa polisi atasema tu alikokuwa na hao aliokuwa nao siku zote hizi. Yaani ni balaa kweli sisi wanawake, mtu wakati mwingine unaweza kusema kwamba bora uzae mwanamume hata akiwa jambazi atauawa huko potelea mbali kuliko mtoto wa kike ambaye daima anakupa presha,” akasema yule wa kwanza, ambaye na hisi ndiye mama mzazi wa binti huyo.

Hapo ndipo nilipoelewa kwamba kumbe walikuwa wakimsaka binti yao ambaye alitoweka nyumbani kwao siku kadhaa kwa maelezo kwamba yuko kwa rafiki zake anajisomea, kumbe siyo! Unaona mambo ya dunia haya ndugu zanguni?

Ni kwa mantiki hiyo basi leo nimeamua kuwaletea kibao hiki cha Rosa Nenda Shule, kibao kilichotungwa na Jabali la Muziki Tanzania, Marijani Rajab Marijani ‘Dozzer’, mwaka 1973 wakati huo akiwa na bendi ya Safari Trippers.

Jamani msije mkasema kwamba nampendelea Marijani kwa sababu Jumamosi iliyopita nilikuwa naye hapa akiwa na kibao chake cha Usia wa Baba alichoimba na Dar International, bali nimelazimika kutokana na tukio ambalo limetokea.

Matukio kama haya yametukuta wengi, tukiwa kama wazazi ama wanajamii. Watoto wa kike wanaosoma wanaleta matatizo sana, ingawa siwezi kuwatetea wale wa kiume nao kwani kila mmoja ana matatizo yake.

Na hapa lazima niseme kwamba, simuungi mkono yule mama anayesema bora mtoto wa kiume. Jamani mtoto ni mtoto tu, awe wa kiume au wa kike. Namna tabia yake itakavyokuwa ni malezi ayapatayo, ikiwa ni pamoja na kuepuka makundi na zaidi kumuomba Mungu amtangulie na ampe mwenendo mwema!

Hata hivyo, watoto wa kike wana matatizo makubwa sana kuliko wa kiume, hasa wanapoingia kwenye ule umri wa ujinga, yaani foolish age. Vichuchu vikianza kuchomoza tu na sauti nayo kubadilika, mtoto wa naye huanza kubadili tabia. Atachagua mavazi, vipodozi na hata mwendo ataubadilisha! Ndio umri wa balekhe huo ambao humfanya ajione kama yeye ndiye anayejua kila kitu.

Na hapa ndipo ninaposema kwamba, wengi wetu tumeshuhudia tabia za watoto hawa, wengine wakishindwa kumaliza masomo, na kama wanamaliza, basi huwa ni mbinde kweli kweli.

Tabia zao wengine hata walimu wao huziona jinsi zinavyobadilika na walimu wengine waungwana huwa wanapenda kuwasiliana na wazazi wa binti husika, kama Marijani anavyosema;

“Habari zako nimezipata kutoka kwa walimu wako, Kwamba siku nyingi zimepita na wewe shule mbona huonekani, Unaniaga baba nakwenda shule, Na mapesa mengi kuniomba, Kumbe muongo mkubwa ukitoka kumbe una njia zako...”

Hebu nielezni ndugu zangu, ni nani kati yetu ambaye hajashuhudia mambo haya? Mimi mwenyewe nimeshuhudia watu wengine wakishindwa kumaliza masomo na wale waliomaliza hufanya hivyo ili kutimiza wajibu.

Lakini hakuna mzazi ambaye hamtakii mema mwanawe, na ndiyo maana hivi sasa wazazi wote wako radhi kujinyima na hata kufanya vibarua ili kugharamia elimu ya watoto wao, kwa sababu ndio urithi wao.

Katu wasijidanganye kusema, “Aaah, baba yangu mimi Danny mwandishi wa habari, hata nisiposoma nitaishi tu!” Huu ni ujinga tena upumbavu. Hivi unajua mali aliyonayo babayo aliipata vipi? Unajua jinsi alivyosoma? Si walisema Waswahili kwamba nguo ya kuazima haistili maungo!

Tazama yule binti mwingine ninayemfahamu mimi ambaye baba yake alikuwa tayari kuachilia ujenzi wa nyumba ya familia ili amsomeshe baada ya kufaulu mtihani wa darasa la saba. Lakini alipokwenda shule akaingia kwenye makundi, akaanza kujirusha. Mtihani wa kidato cha pili ulipokuja, akaanguka vibaya sana, lakini nyumbani akadanganya kwamba amepasi. Siri ilipogundulika, akaamua kuachana na shule!

Marijani anasema hivi, hata mimi na mzazi mwingine anayewatakia maendeleo watoto tunasema hivi; “Ooo Rosa wewe nenda shule eeee, Ukimaliza faida utaiona eeee... Wacha tamaa Rosa ee wacha tamaa mama ee, Tamaa yako Rosa ee itakuponyesha… Ipende shule mama ee wacha uhuni mama ee.”

Labda nimalizie kwa kuwaasa hawa binti zetu kwamba, wanaume, yaani sisi wanaume, ashakum si matusi, ni washenzi kweli kweli. Wengi wao wanapenda kuwahadaa mabinti pale wanapoona wameanza kuchipukia. Wakishamaliza haja zao, na pengine tayari watakuwa wamewatwisha mimba, au hata magonjwa ya zinaa, haoo wanakimbia.

Utahangaika na mzigo wako peke yako na ndipo hapo huwa napenda kutumia ule msemo wa wahenga na wahenguzi kwamba, Kijuto msuto kisicho kito! Yaani Majuto ni mjukuu, upo hapo mama.

Hebu wadogo zangu ngoja niwaambie. Hayo mapenzi hayo mnayoyakimbilia yalikuwepo, yapo na yataendelea kuwepo. Walikuwepo akina babu na bibi, wameondoka wameyaacha. Sasa kwa nini msisubiri mkamaliza jambo moja na kasha muende jingine?

Halafu maskini ya Mungu, mara nyingi zaidi ukimfuatilia binti huyu utakuta huyo anayemzuzua ni mwanafunzi mwenzake ama muuza chips au hata kondakta wa daladala. Kama huyu mwanafunzi, ambaye dira yake haijui kabisa kwa sababu bado na yeye anahudumiwa na wazazi, halafu leo hii anakudanganya kwamba lazima akuoe! Hivi kwa nini muwe na akili za kuku kupewa mtama kwenye ungo na kisha kuumwaga na kuuchanganya na mchanga ndipo uudonoe?

Gonganisheni vichwa vyenu, halafu mtapata majibu sahihi, vinginevyo nendeni shule kwa sababu faida ni yenu wenyewe. Mali ya urithi ukiitegemea utakufa kibudu!

Wasalaaam!

Kwa majadiliano, hoja na ushauri gonga 0784 – 939319, au brotherdanny2003@yahoo.com.
Hizi ndizo mechi muhimu ambazo Tanzania ilipoteza

DANIEL MBEGA
Dar es Salaam

JUMAMOSI iliyopita tumeshuhudia timu ya soka ya taifa, Taifa Stars, ikipoteza mechi muhimu sana ambayo wengi walitegemea ingeweza kuiweka Tanzania kwenye nafasi ya kufuzu kwa fainali za Mataifa ya Afrika mwaka 2008 kule Ghana.

Stars ilijikuta ikichapwa bao 1-0 nyumbani na kuzima ndoto hizo huku Watanzania wakiwa hawaamini kilichokuwa kimetokea. Hapa tunawaletea kumbukumbu ya mechi mbalimbali zikiwemo za vilabu vya Tanzania ambazo zilikuwa muhimu sana kwa timu hizo kama zingeweza kushinda:

YANGA VS ASANTE KOTOKO 1969: Baada ya Yanga kufanikiwa kuzinyuka timu za Fitarikandro Soa Fireguina ya Madagascar kwa jumla ya mabao 4-3 katika raundi ya awali ya Klabu Bingwa Afrika, ikajikuta uso kwa uso na St. George ya Ethiopia katika raundi ya pili ambayo waliinyuka kwa mabao 5-0 na ndipo walipofuzu kwa robo fainali dhidi ya Asante Kotoko ya Ghana. Matokeo katika mechi zote yalikuwa 2-2 (yaani 1-1 Kumasi, na 1-1 Dar es Salaam). Yanga wakazubaa na kujikuta wakitolewa kwa shilingi.

YANGA VS ASANTE KOTOKO 1970: Kwa mara nyingine tena Yanga ilifanikiwa kuingia robo fainali ya Klabu Bingwa Afrika mwaka huu baada ya kuzitoa US Fonctionnaires ya Madagascar kwa jumla ya mabao 6-4 katika raundi ya kwanza, na Nakuru All Stars ya Kenya kwa jumla ya mabao 3-2. Ikakumbana na Asante Kotoko ambapo mjini Dar es Salaam matokeo yalikuwa 1-1, na walipokwenda Kumasi mechi ikaisha kabla ya muda wake matokeo yakiwa 1-1. Ikabidi ichezwe kwenye uwanja huru, ambapo wakaenda Addis Ababa na Yanga wakanyukwa mabao 2-0. Wakawa wametolewa kwa mara nyingine.

SIMBA VS MEHALLA AL KUBRA 1974: Simba ndiyo iliyokuwa inashiriki Klabu Bingwa ya Afrika, ambapo ilianza kwa kuitoa Linare ya Lesotho kwa mabao 5-2 katika raundi ya kwanza kabla ya kuizamisha Green Buffaloes ya Zambia kwa jumla ya mabao 3-1 katika raundi ya pili. Kwenye robo fainali walikumbana na Accra Hearts of Oak ya Ghana ambayo nayo waliikandamiza jumla ya mabao 4-1. Ndipo wakatinga nusu fainali na kukabiliana na Mehalla Al Kubra ya Misri. Walishinda bao 1-0 mjini Dar es Salaam, lakini walipokwenda Cairo walifanyiwa visa ikiwa ni pamoja na kuzimiwa taa huku golikipa Athumani Mambosasa akitishiwa kuuawa kama angedaka. Wakafungwa 1-0 katika muda wa kawaida. Lakini wakafungwa kwa mikwaju ya penati 3-0.

YANGA VS ENUGU RANGERS 1975: Yanga ilishiriki Klabu Bingwa Afrika mwaka 1975 na ilipita moja kwa moja hadi raundi ya pili baada ya kukosa mpinzani kwenye raundi ya kwanza. Katika raundi ya pili ikakumbana na Enugu Rangers ya Nigeria ambapo katika mchezo wa kwanza nchini Nigeria timu zilitoka suluhu, lakini zilipocheza Dar es Salaam zikafungana 1-1. Yanga ikatolewa kwa sheria ya bao la ugenini.

SIMBA VS RACCAH ROVERS 1979: Baada ya kuiondosha kiajabu Mufulira Wanderers ya Zambia katika raundi ya kwanza ya Klabu Bingwa Afrika mwaka 1979, ikipata ushindi wa ugenini wa mabao 5-0 mjini Lusaka na kufukia mabao 4-0 waliyofungwa nyumbani, Simba ilijikuta ikikwama mbele ya Raccah Rovers ya Nigeria kwenye raundi ya pili. Katika mchezo wa kwanza mjini Dar es Salaam Simba ilitoka suluhu huku mlinzi wake Hussein Tindwa akifariki baada ya kuanguka uwanjani, lakini walipokwenda Nigeria wakachapwa mabao 2-0.

PAN AFRICAN VS AS VITA CLUB 1979: Pan African ilitolewa katika raundi ya pili ya Kombe la Washindi mwaka huo na AS Vita Club ya Zaire (sasa DRC) kwa sheria ya bao la ugenini. Ilishinda nyumbani 2-1, na ziliporudiana mjini Kinshasa ikafungwa bao 1-0. Katika raundi ya kwanza Pan ilikuwa imeitoa Omedla ya Ethiopia kwa mikwaju ya penati 5-4 baada ya matokeo ya jumla kuwa sare ya bao 1-1. Pan ilifungwa nyumbani 1-0, ikashinda ugenini 1-0.

PAN AFRICAN VS SHOOTING STARS 1980: Pan ilitolewa tena katika raundi ya pili ya Kombe la Washindi, safari hii na Shooting Stars ya Nigeria kwa jumla ya mabao 2-1. Ilifungwa 1-0 nyumbani, na kulazimisha sare ya 1-1 ugenini. Katika raundi ya kwanza Pan iliitoa AC Sotema ya Madagascar kwa jumla ya mabao 5-4.

PAN AFRICAN VS POWER DYNAMOS 1982: Pan tena ilishiriki Kombe la Washindi Afrika na safari hii ikatolewa kwa penati 5-3 na Power Dynamos ya Zambia katika raundi ya pili baada ya kila timu kushinda bao 1-0 nyumbani kwao. Katika raundi ya kwanza Pan ilikuwa imeiadhibu Mukura Victory Sports ya Rwanda kwa jumla ya mabao 8-0.

PAN AFRICAN VS NKANA 1983: Mwaka huu Pan ilishiriki Klabu Bingwa Afrika na kutolewa na Nkana Red Devils ya Zambia kwa mikwaju ya penati 4-2 katika raundi ya pili baada ya mechi zote mbili kushindwa kuwa na magoli. Katika raundi ya kwanza Pan iliitoa Wagad Mogadishu ya Somalia kwa jumla ya mabao 2-1.

SIMBA VS NATIONAL 1985: Simba ilikuwa inashiriki Kombe la Washindi mwaka huu na ikatolewa na National Al Ahly ya Misri kwa jumla ya mabao 3-2. Ilishinda 2-1 mjini Mwanza, lakini ilipokwenda Cairo ikachapwa 2-0. Katika raundi ya kwanza ilikuwa imeitoa Eritrea Shoe Factory ya Asmara, Ethiopia kwa jumla ya mabao 5-1.

PAMBA VS BTM 1990: Pamba ilikosa bao moja ambalo lingeipa ushindi wa bao la ugenini dhidi ya BTM ya Madagascar baada ya kukubali kipigo cha mabao 2-1 ugenini kufuatia sare ya bila kufungana Mwanza katika raundi ya kwanza ya michuano ya Kombe la Washindi Afrika. Katika raundi ya awali Pamba ilikuwa imeweka rekodi ya mabao mengi ya kufunga baada ya kuikandamiza Anse-aux-Pins Boileau ya Shelisheli kwa jumla ya mabao 17-1. Ilishinda 5-0 ugenini ikashinda 12-1 nyumbani.

SIMBA VS STELLA ABIDJAN 1993: Simba ililikosa Kombe la CAF katika mazingira ambayo mpaka leo hii wengi wanayahusisha na rushwa. Ilikuwa imetoka suluhu katika mchezo wa kwanza wa fainali mjini Abdijan na wengi waliamini kwamba kikosi kile, ambacho kilikuwa kimeahidiwa magari aina ya KIA na mfadhili wao Azim Dewji, kingeweza kupata hata mabao mawili nyumbani. Lakini ni wao waliofungwa mabao 2-0 na kulikosa kombe hilo. Simba ilianza kwa kuzitoa Ferroviario de Maputo ya Msumbiji kwa faina ya bao la ugenini baada ya kutoka suluhu mjini Mwanza katika raundi ya kwanza. Kwenye raundi ya pili ikaitoa Manzini Wanderers ya Swaziland kwa jumla ya mabao 2-0, katika robo fainali ikainyuka USM Al-Harrach ya Algeria kwa mabao 3-2, na katika nusu fainali iliiondosha Atletico Sports Aviacao ya Angola kwa jumla ya mabao 3-1.

SIMBA VS ASEC MIMOSAS 1995: Simba ilishindwa kufuzu kwa robo fainali ya Klabu Bingwa Afrika mwaka 1995 baada ya kuchapwa na ASEC Mimosas ya Ivory Coast kwa jumla ya mabao 4-2 ikifungwa 2-1 ugenini na nyumbani. Hii ilikuwa baada ya kufuzu katika raundi ya kwanza ambapo iliitoa Power Dynamos ya Zambia kwa mikwaju ya penati 4-3 baada ya mechi zote mbili kwisha kwa sare ya 1-1.

YANGA VS BLACKPOOL 1995: Yanga nayo mwaka huu ilirudia robo fainali ya Kombe la Washindi baada ya kunyukwa na Blackpool ya Zimbabwe kwa jumla ya mabao 4-2, ilichapwa 2-1 ugenini na nyumbani. Awali ilikuwa imeitoa Vaal Reef Professionals ya Afrika Kusini kwa mabao 4-3 katika raundi ya kwanza, na kasha kuiondoa Tamil Cadets Club ya Mauritius kwa mabao 4-2.

MALINDI VS ETOILE DU SAHEL 1995: Malindi ilitolewa kwa penati 4-3 katika nusu fainali ya Kombe la CAF na Etoile du Sahel ya Tunisia baada ya kila timu kushinda bao 1-0 nyumbani kwake. Mwaka huo Malindi, ikiwa inafadhiliwa na Noushard Mohammed na kuwaita wachezaji wa kulipwa wa Zambia kama Elijah Tana na wengineo, ilikuwa imeitoa Mbabane Swallows ya Swaziland katika raundi ya kwanza, ikainyuka KCC ya Uganda jumla ya mabao 3-0 kwenye raundi ya pili, kabla ya kuichapa Agaza Lome ya Togo 2-0 ugenini baada ya kutoka suluhu mjini Zanzibar.

SIMBA VS ARAB CONTRACTORS 1996: Simba ilikuwa ikiwania Kombe la Washindi Afrika mwaka huo na baada ya kuvuka raundi ya kwanza kufuatia Chapungu ya Zimbabwe kushindwa kuja kurudiana na Simba baada ya kupoteza mechi yake ya nyumbani 1-0, Simba ikaingia raundi ya pili na kukabiliana na klabu hiyo ya Misri maarufu kama Al Makaoulun ambapo iliifunga 3-1 Dar es Salaam lakini Wamisri hao wakapata faida ya bao la ugenini baada ya kushinda 2-0 Cairo.

YANGA VS MAMELODI SUNDOWNS 2001: Yanga ilishindwa kupata bao moja tu dhidi ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini katika raundi ya pili ya Ligi ya Mabingwa Afrika kufuatia kufungwa 3-2 ugenini. Matokeo yake timu hizo zikafungana 3-3 mjini Mwanza na hiyo Yanga ikatolewa kwa jumla ya mabao 6-5. Awali ilipata mchekea baada ya mechi yao ya marudiano na Highlanders ya Zimbabwe kuvunjika na CAF kuipa ushindi. Mechi ya kwanza mjini Dar es Salaam timu hizo zilifungana 2-2.
YANGA VS ESPERANCE 2007: Yanga ilishindwa kufuzu kwa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kunyukwa na Esperance ya Tunisia katika raundi ya tatu kwa jumla ya mabao 3-0. Awali ilikuwa imezitoa AJSM ya Mutsamudu, Comoro kwa mabao 5-1, na kasha ikaitoa Petro Atletico ya Angola kwa mabao 3-2. Katika mchezo wa kuwania kucheza makundi ya Kombe la Shirikisho ikatolewa na El Merreikh ya Sudan kwa mabao 2-0.

Hizi ndizo baadhi ya mechi za kimataifa kwa upande wa klabu ambazo zilikuwa muhimu lakini timu zetu zikashindwa na kuwaacha midomo wazi mamilioni ya wapenzi wa soka nchini wakiwa hawaamini kilichotokea..

Mwisho.
TUNAZIKUMBUKA
KILIO CHA ASHURA NI CHA WANAWAKE WOTE!

DANIEL MBEGA

AHLANI Wasaalani wapendwa wasomaji wa gazeti hili. Ni matumaini yangu kwamba nyote mu' wazima popote pale mlipo na mnaendelea na majukumu yenu ya kila siku. Karibu kwa mara ya kwanza katika makala yetu hii mpya ambayo itaanza kupatikana katika gazeti hili kila siku kama ya leo.
Hapa tutakuwa tunazungumzia nyimbo mbalimbali za enzi zile, ambazo zinaonekana bado rasilimali kubwa katika sanaa ya muziki ambayo si vibaya hata tukaziita ni miongoni mwa rasilimali-kale.
Kwa kuwa nyimbo hizi zimeanza kusahaulika kwa vijana wa sasa, basi nimeona ni vyema tukumbushane wale vijana wa zamani zile kwa kuzichambua na kuelezea ujumbe maridhawa uliopo na nini tunachotakiwa kujifunza.
Siyo siri, nyimbo zile bado zina mguso wa aina yake na wale vijana wenzangu watakubaliana na mimi kwamba, ujumbe na mpangilio wake ulikuwa mzuri na kila mojawapo ya nyimbo hizo inaposikika redioni huwakumbusha hizo enzi, enzi ambazo si ajabu kumkuta shabiki wa Msondo Ngoma akicheza kifua wazi, shati kalifutika kwenye mfuko wa nyuma wa suruali na chupa kaiweka chini mbele yake. Ole wako kivuli chako kikatize kwenye eneo analochezea!
Hata hivyo, leo naanza na kibao kimoja cha mwanzoni mwa miaka ya 1990 kinachokwenda kwa jina la 'Ashura' ambacho kiliimbwa na Magereza Jazz Band 'Wana Mkote Ngoma'.
Katika kibao hiki, Ashura, au Nana Njige, ambaye ndiye aliyekiimba, anasikika akilalama kwamba mumewe wa sasa anamfanyia visa visivyo kifani. Anasema; "...Visa ninavyofanyiwa na bwana huyu, Nimeamini methali isemwayo, Mkataa pema, pabaya panamwita... nilidanganyika, Kumuacha mume wangu, kumfuata bwana mwingine, Kumbe ni mwizi baba, kumbe ni muongo."
Ashura anazungumza wazi bila kificho, kwamba alidanganyika na kuamua kumwacha mumewe ili aende kwa mwanamume mwingine aliyemhadaa na mambo kadha wa kadha. Lakini matokeo yake mwanamume huyo ameonekana kuwa muongo, na zaidi mwizi.
Waswahili walinena; 'Kijuto msuto kisicho kito', wakiwa na maana kwamba majuto ni mjukuu. Nami nasema swadakta kabisa, kwa sababu huu ndio ujumbe halisi uliomo katika kibao hiki ambacho kilitingisha kweli kweli katika anga la muziki wa dansi nchini Tanzania mwanzoni mwa miaka ya 1990.
Kilichoonekana, na ambacho Ashura mwenyewe anakinadi ni kwamba, amejifunika shuka wakati tayari kumepambazuka! Laiti kama angalifikiria wakati bwana huyo anamrubuni, akatafakari kwamba kuisaliti ndoa yake ni kosa ambalo angekuja lijutia baadaye kama ajutavyo sasa, kamwe asingefikia hatua hiyo.
Lakini niseme wazi tu kwamba, akina Ashura wapo wengi mno katika jamii yetu. Wengi sana na idadi yao haina kipimo. Mambo yaliyompata Ashura yanawapata wanawake hawa kila kukicha na daima wanashindwa kujua wafanye nini ili kuyarejesha mapenzi yaliyopotea.
Niseme wazi tu kwamba, wanaume, ashakum si matusi, ni washenzi, tena washenzi kweli kweli. Wapo wengi wao ambao wanapenda kuwanyatia wake za watu tu, au niseme, wanawake ambao tayari wako kwenye uhusiano.
Wao huwa wanasema kwamba wanawake hao hawana gharama kubwa kwa sababu hawawezi kuwasumbua kwa kodi ya nyumba wala pesa ya chakula. Si wameolewa na waume zao, kodi ya nini tena? Au pesa ya chakula ya nini wakati kila siku bwana wake anamwachia pesa ya matumizi!
Wanafahamu kwamba mwanamke aliyeolewa hataweza kuwadai fedha za nguo kwa sababu si itakuwa balaa kwa waume zao? Unadhani watasemaje pindi watakapokuwa wameonekana na nguo mpya za gharama wakati uwezo wa waume zao ni mdogo?
Hii ndiyo faida ambayo wanaume hawa wakware huwa wanaiona na gharama pekee ambayo wanaweza kuingia kwa hawa wake za watu ni matumizi madogo madogo tu kama chips-kuku, vipodozi na kadhalika, vitu vidogo ambavyo si ajabu mwanamke akamdanganya mumewe kwamba amenunua baada ya kupokea fedha zake za mchezo. Si mnafahamu kwamba michezo ya kupeana imeenea hata maofisini?
Ashura mwenyewe anasema hivi; "...Muheshimu ndoa zenu zisijevunjika, Muachane na mabwana wadanganyifu eeeh, Atakupenda wakati una mumeo ooh, Ukishaachika wala hana habari nawe, Atakudanganya kwa curl na relaxer, ... Na starehe za muda hazina mwisho sikia..."
Lakini pia wapo wanawake ambao baada ya kufuatwa na wanaume hawa, wakigeuka nyuma kuona kwamba wana matatizo katika ndoa zao, hukurupuka na kuwaendea hao wadanganyifu baada ya kuhadaiwa kwa vitu vidogo vidogo ambavyo vimekuwa adimu kwa waume zao.
Ndiyo. Hili si jambo la ajabu. Mnapokuwa kwenye ndoa, mara nyingi kutokana majukumu ya kifamilia ambayo huwa yanazidi hasa pale watoto wanapokuwa wamezaliwa, baadhi ya vionjo vya ndoa kama mabusu, maneno matamu ya 'mpenzi', 'laazizi' na kadhalika huwa yanapungua.
Lakini yanapungua tu si kwamba mwenzako hakupendi, bali kutokana na majukumu na kujisahau, jambo ambalo ni dogo ikiwa tu mtatafuta muda wa kutafakari na kujirekebisha katika jitihada za kuboresha mapenzi yenu badala ya kukimbilia kwa mwanamume mwingine kwa vile tu analitamka neno 'nakupenda' zaidi ya mara elfu moja.
Kumbuka kwamba, kwenda nje ya ndoa siyo suluhu ya matatizo, iwe kwa mwanamke ama mwanamume, bali kutazidisha matatizo ikiwa hata kuachana na mmoja wenu akishakumbuka kwamba pembeni kuna mtu ambaye kila wakati anamsumbua kwa kumwambia anampenda, basi kiburi kitaibuka nyumbani na kuzaa tamaa.
Tunaambiwa kwamba tamaa ikipata mimba huzaa dhambi na hakuna dhambi mbaya zaidi kama zinaa, kwani tunaambiwa haisameheki kwa vile inafanyika kwenye mwili ambalo ni Hekalu la Mungu.
Suluhu la matatizo yoyote ndani ya familia na hasa ndoa, ni majadiliano. Tafuteni muda wa kutosha kuwa pamoja na kuzungumza mambo mbalimbali ili kudumisha ukaribu, kwa sababu kutokufanya hivi hujenga daraja baina yenu na inakuwa rahisi kwa mmoja wenu kushawishika kwenda nje ya ndoa.
Lakini pamoja na hayo, lazima muwe na kumbukumbu kwamba nyote wawili mmekula yamini ya kuishi pamoja milele; kwa shida na raha, hadi kifo kitakapowatenganisha. Iweje leo Brother Danny baada ya kufilisika umuone si lolote si chochote na kuamua kukimbilia kwa Hemed? Au inakuwaje baada ya mkeo Amina, ambaye ulimpenda wakati ule kutokana na umbile lake jembamba, awe hana thamani leo hii baada ya kuzaa watoto na kuwa mnene? Zi wapi basi hizo ahadi zenu? Lazima tubadilike wanajamii kama kweli tunataka kujenga heshima zetu katika ndoa.
Kabla ya kuwaaga, nawaletea mashairi yote ya kibao cha Ashura, lakini msikose kuwa nami katika ukurasa huu kila siku kama ya leo ili tukumbushane mashairi ya vigongo vya zamani. Kwa herini.

Mwenye maoni na ushauri ama ombi, tafadhali asisite kunipigia kupitia 0784 – 939319, au barua-pepe: brotherdanny2003@yahoo.com.

Ashura mimi najuta, Mwenzenu kweli najuta sasa x2

Visa ninavyofanyiwa na bwana huyu [Bwana huyu]
Nimeamini methali isemwayo [isemwayo]
Mkataa pema, Oooh, pabaya panamwita x2

Leo hii mwenzenu, Kusema hivi mimi, Nina maana yangu, nilidanganyika,
Kumuacha mume wangu, kumfuata bwana mwingine,
Kumbe ni mwizi baba, kumbe ni muongo.

Visa ninavyofanyiwa na bwana huyu [Bwana huyu]
Nimeamini methali isemwayo [isemwayo]
Mkataa pema, Oooh, pabaya panamwita x2


Kibwagizo:
Nawausia wanawake wenzangu wote eeh, Muheshimu ndoa zenu zisijevunjika x2

Muachane na mabwana wadanganyifu eeeh, Atakupenda wakati una mumeo ooh,
Ukishaachika wala hana habari nawe [Hana habari nawe]

Atakudanganya kwa curl na relaxer, Atakudanganya kwa khanga za Mombasa,
Atakudanganya kwa vitenge vya Zaire, Atakudanganya kwa chips na mayai,
Na starehe za muda hazina mwisho sikia

Nawausia wanawake wenzangu wote eeh, Muheshimu ndoa zenu zisijevunjika x2


MWISHO.
PROJO ZA MZEE WA SHAMBA

AHADI ZA KILIMO CHA KISASA NA MASHAMBA YA UJAMAA

DANIEL MBEGA

HABARI za leo ndugu zetu wa huko Tanzania. Ni matumaini yangu kwamba nyote hamjambo kabisa wenzetu mkipata upepo mwanana uliojaa marashi. Huku Tanganyika tunaendelea kulikoga vumbi.
Msishangae ninaposema kwamba sisi tuko Tanganyika, tena Tanganyika yenyewe asavali ile ya mkoloni. Nitasemaje tuko Tanzania wakati mambo yetu yako shaghalabaghala na nyie huko mkiendelea kujipendelea, mkitembelea mashangingi sijui na mabaluni huku vimwekamweka vikiuangaza usiku na kuonekana kama mchana?
Nitasemaje hata mimi Mzee wa Shamba nafaudu matunda ya uhuru wakati niko kwenye giza totoro? Au nalingana na ninyi kwa haki na asili ya Utanzania wakati huku asilimia 110 tukiendelea kutumia usafiri wa ‘tizedi ileveni’, usafiri wa ngoko maarufu kama sakalakale. Gharama yetu kubwa ni kumuomba Jalali uzima na kununua viatu vinavyotokana na mabaki ya yaliyokuwa matairi ya gari?
Hebu subirini kwanza, nisije nikawa nabwabwaja tu wakati sina uhakika kwamba hizi porojo zangu zimechapishwa na huyo bwana mkubwa wanayemwita sijui muhariri! Kwanza nimshukuru, hata kama atazisoma mwenyewe tu, kwa kunipa heshima ya kuropoka kwenye gazeti lake.
Mpaka nafanikiwa kuzitumbukiza porojo hizi posta, nilitumia siku mbili. Mvua huku ilikuwa inanyesha kweli kweli na magari yale tunayoyategemea, ambayo ni malori, huu si msimu wake. Mara nyingi yanakujaga wakati ule wa mavuno, yakiwa yamewabeba walanguzi ambao hawajui hata mmea wa karanga au muhindi ukoje zaidi ya kufurahia punje zake tu.
Halafu kibaya zaidi utakuta wanayashikashika mahindi yetu na kuyabeza “Utaniuziaje gunia moja shilingi alfu saba, unadhani pesa zinatingishwa kwenye mti? Kwanza mahindi yenyewe yamekondeana namna hii, nitatoa alfu tano!”
Bladifulu kabisa! Hivi huyu mtu anaongea hivi anajua hata kushika jembe? Anajua… Anajua… aisee hasira zinanipanda mara mbili na ole wake angekuwepo sasa hivi akayarudia maneno haya, angeniambia kama maharage mboga ama kiungo cha kande!
Basi nirejee kwenye mada, kwamba nilitumia usafiri wa bakseli nitakuwa nadanganya, umri wenyewe huu umekwenda ningewezaje kunyonga pedali umbali wa kilometa thalathini kwa kutumia injini-kiuno. Nikaamua bora niukanyage tu maana tumeshazowea sisi kuhesabu ekari ati!
Najua kwa maelezo haya huyo muhariri, anaweza kunihurumia na kuzichapisha porojo zangu.
Basi ndugu zangu wa huko Tanzania, ni kwamba, nilifanikiwa kusikiliza sehemu tu ya hotuba ya huyo waziri wenu wa kilimo ambayo kwa hakika mimi mzee wa shamba iliniacha kinywa wazi.
Kwamba kuna mikopo kwa wakulima na sisi akina Mzee wa Shamba tunaweza kukopeshwa pembejeo ili tujikwamue na jembe hili la mkono katika kuendeleza kilimo ili kuinua pato la taifa ambalo viongozi wa huko Tanzania wanaendelea kutudanganya kwamba kilimo ndio uti wa mgongo. Nikaona hizi ni ahadi za kuku za kunyonya kesho mpaka mtoto anakua.
Jamani niseme ule ukweli tu, sisi wakulima, ambao asilimi 95 tunaishi huku Tanganyika, tumesahaulika mno tangu yale mashamba ya Ujamaa yalivyokufa, yaani miaka ile ya mwanzoni mwa themanini. Hakuna mtu ama kiongozi anayejali kwamba kuna Watanganyika huko ambao wanamenyeka na kilimo cha jembe la mkono, lakini ndio wanaosaidia kulisha nchi hii huku wakidhulumiwa mazao yao.
Asavali kipindi kile cha Vijiji vya Ujamaa na mashamba ya ujamaa mkulima alionekana kuwa na thamani, kwa sababu Mzee Mchonga Meno, alikuwa ameona mbali kwa kutilia mkazo kilimo na ushirika ili kuongeza pato la taifa.
Walikuwepo mabwana na mabibi shamba. Bahati nzuri niliwahi kuwa bwana shamba kipindi cha miaka minne enzi hizo, nilipokuwa shuleni na kujifunza mbinu mbalimbali za kilimo.
Hawa mabwana shamba walisaidia sana kwa sababu watu walijua walime nini mahali walipo kutokana na ardhi yao. Tukaamrishwa kila kaya iwe na walau ekari moja ya muhogo, serena, uwele na mazao yanayostahimili ukame. Tukavuna na kupeleka kwenye ofisi za vijiji, ingawa wenyeviti, ambao waliogopwa enzi hizo kuliko hata Malaika Mtoa Roho, wakajinufaisha na wale waliojiita wajumbe wa halmashauri ya kijiji!
Hatimaye Ujamaa ukafa, ushirika ukazimia, na Azimio la Arusha likazikwa kabisa. Wale wasiokuwa na mtazamo wa mbele wakashangilia kwamba wasingefuatwa na mgambo wa vijiji waliokuwa wakiwakamata na kuwafungulia mashtaka bila sababu.
Baada ya hapo sisi huku Tanganyika tukaanza kushuhudia ahadi kedekede, kila mwaka wa bajeti tukaambiwa kilimo kingeboreshwa, wakulima wangepewa pembejeo, bei za mazao zingekuwa nzuri na kadhalika.
Nikashangaa kuona miaka inapita na watu kama mimi Mzee wa Shamba tukiendelea kukongoroka kwa jembe la mkono. Hakika ukifanikiwa kuja huku Tanganyika usishangae kumkuta Mzee wa Shamba akiwa mwembamba na uso uliosinyaa kama anakula sumendi. Unaweza kudhani ni mtoto kutokana na umbile lake, lakini akikwambia alipigana Vita vya Kagera utakataa. Ndiyo hali halisi hiyo.
Sasa leo bado tu tunaahidiwa mikopo, na pembejeo, wakati hao wanaoahidi hayo mara ya mwisho kuwaona walikuja kipindi kileeeeeeee cha kampuni, aaah siyo, kampeni. Tena walikuwa wanaona kinyaa hata kusimama ardhini. Lakini mbali na kutupumbaza kwa ahadi zisizotekelezeka, wakaondoka na kuku, mbuzi na zawadi kedekede kutoka huku.
Uchaguzi wa mwisho tuliufanya wakati ule BM alipoachia madaraka, lakini mpaka leo, hatujamuona hata mmoja wao aje walau atoe shukrani, leo hii wanakula kuku kwenye lile Jumba la Legico kule Dodoma na kusema, “Tumetenga kiasi fulani katika kijiji cha Mtakuja kwa maendeleo ya kilimo,” wakati si kweli. Hapa ni kijijini kwetu, nashangaa kusikia kila mwaka tumetengewa fedha za mikopo lakini fedha zenyewe hatuzioni wala kivuli cha hao wajumbe wa Legico na mawaziri wao hakionekani.
Zile za mwaka jana zimekwenda wapi? Hivi mtaendelea kutudanganya hadi lini sisi Watanganyika? Au ndiyo mmegeuza msemo na kutuita Wadanganyika! Bwana sisi tulishazowea, mvua na jua ni jadi yetu, mkileta hewala, msipoleta mashaalah.

MWISHO.
POROJO ZA MZEE WA SHAMBA
KWETU TANGANYIKA HATUJUI RUSHWA NDOGO NA KUBWA!

DANIEL MBEGA

AHLANI Wasaalani wapendwa ndugu zetu wa huko Tanzania. Sisi huku Tanganyika tunaendelea vyema na majukumu yetu ya shamba. Juzi tu kulikuwa na kikao cha Wazee wa Kimila ambao walikuwa wanajadili kama msimu ujao wa mvua, ambao kwetu hauna majira maalum, utakuwa na neema kama uliopita au la.
Unashangaa vikao vya Wazee wa Kimila? Sisi huku hatuna watabiri, tunaongozwa na wazee hawa na tunawaheshimu sana. Nakumbuka msimu uliopita Mzee Magwina aliipata joto ya jiwe baada ya kuitwa na wazee hao akituhumiwa kuzuia mvua kunyesha!
Mzee yule aliwekwa juani, akakokewa moto, na kuwekewa kigae na mahindi pembeni akiamriwa akaange bisi na kumaliza debe zima. Ndiyo adhabu yake! Baadaye akakiri kwamba alikuwa anazuia mvua kwa sababu eti alikuwa anamkomoa kijana wa Mzee Mgaza aliyepata mavuno mengi mwaka uliotangulia.
Alipoachiwa mvua ilinyesha mara moja tu, halafu hiyooooo ikaondoka. Wazee wale wakatuamuru twende msituni kwenye mti mkubwa kutambika ili mvua inyeshe. Hamjui matambiko eee? Sisi bado tunaendeleza mila na desturi zetu.
Lakini kwanza nachukua fursa hii kumshukuru nanihiino, aaah si yule mkubwa wa gazeti aliyenipa nafasi hii ya kumwaga porojo zangu? Wanamwita nani vile? Editori! Safi kabisa, huyo huyo editori.
Nakushukuru sana, maana huku gazeti lilikuja baada ya siku tatu au nne hivi, tena kuna jamaa kule mjini aliliona likiwa na sura yangu, na kwa kuwa ananifahamu tulikuwa tunawinda wote mijusi enzi zile za utoto, akaamua kunitafuta haraka na kuniletea. Sasa nimemwambia awage ananitumiaga kila wakati.
Halafu huko kwetu shamba, au niseme Tanganyika kwa ujumla, wameanza kufuatilia mambo mbalimbali yanayoendelea huko Tanzania. Kumbe hata yule ‘Mzenge ’Tumbi’ wetu alikuwa hafuatiliagi mambo yanayoendelea. Eti alikuwa anauliza Tanzania ndiyo wapi!
Basi si ndiyo wiki ile nikamwambia kwamba Tanzania ni kule ambako watu wanaishi maisha ya uzunguni, wakitembelea magari makubwa wanayoyaita ‘mashangingi’. Nilicheka aliposema hata mashangingi hajui kama ni aina ya magari, ati yeye anajua shangingi ni janamke limbeya ambalo kwetu tunaliitaga ‘shan’kupe’, tena hasa yale majanamke yanayopenda kusarandia midume ya watu.
Sasa juzi tulikuwa kwenye uwa wa nyumba ya yule kijana tajiri mwenye Land Rover 109 na trekta aina ya Swalaj. Jamaa huwa anatusaidiaga sana hasa tunapopatwa na shida. Basi sote tukakusanyika kwake kutazama siivii ambayo ninyi mnaiitaga luninga sijui ni pelevisheni?! Tukakuta mahali fulani jamaa walikuwa wakizungumza, nadhani ni kwenye Legico, yaani lile jumba tukufu la kutungiaga sheria.
Nikamuona mtu mmoja, sijui kama wenzangu walimuona ama kumsikia, maana wao walikuwa wakilumbana kuhusu namna jumba lile lilivyokuwa linaonekana. Viti vingi vya vono, watu wamependeza katika suti wakati sisi kwetu shamba wanaume tunaendelea kupiga lubega na akina mama wanavaa kaniki kifuani.
Watoto wetu wanaendelea kupekua kwenda shule, maili kumi kutoka hapa kijijini, asavali wameanza kujenga shule moja hapa kijijini, lakini sijui itakamilika lini maana nasikia fedha zilizotolewa kwa ujenzi zililiwa na wasimamizi, akiwemo Mzenge ’Tumbi wetu. Jamani edotori usichapishe haya ninayokwambia, ni siri kubwa maana eti nasikia walikula pamoja na wakubwa kadhaa huko wilayani. Wakijua kwamba mimi nimesema sijui watakachonifanya.
Yule jamaa niliyemuona kwenye jumba lile la Legico alikuwa anamalizia kauli yake kwamba wamefanikiwa kupambana na rushwa ndogo ndogo, lakini watafanya jitihada za kupambana na rushwa kubwa kubwa.
Akili yangu ilizimia kidogo nikahisi moyo wangu uko upande wa kulia badala ya kushoto. Niliporejewa na fahamu, nikaanza kutafakari; rushwa, kama tunavyofahamu sisi huku Tanganyika, ni rushwa tu. Iwe ya chumvi, mbuzi, ng’ombe au pesa. Kwetu sisi hatujui kabisa kama kuna rushwa kubwa na ndogo, kumbe wenzetu huko Tanzania wana rushwa kubwa na ndogo?!
Sikuelewa alikuwa na maana gani kwa sababu huku kwetu mwezi uliopita tu jirani yangu Maliyatabu Kuchumasiwezi alimpoteza mkewe hivi hivi baada ya kukosa shilingi alfu mbili ambazo muuguzi wa ile wodi ya wazazi kwenye wilaya yetu kulazimisha apewe kabla ya kumzalishwa.
Halafu wakati wa masika watoto watatu walifariki dunia baada ya wauguzi wa zahanati yetu kugoma kutoa dawa za malaria mpaka wapewe shilingi alfu moja moja za vocha za simu. Wazazi hawakuwa na pesa, hivyo watoto wakapoteza maisha.
Kwa hiyo, utaona ni jinsi gani kukosa shilingi alfu tatu ama alfu moja kunavyoweza kupoteza uhai wa mtu. Hiyo si rushwa kubwa jamani? Eti Watanganyika wenzangu, nadanganya? Ama rushwa kubwa ni zile za kutaka kuiuza Tanzania kama tunavyosikia huko kwamba Wazungu wanataka kurejea kwa msamiati wa uwekezaji?
Rushwa, kwa uelewa wangu wa darasa la nne la mkoloni, ni kitu chochote ambacho mtu anapewa kinyume cha taratibu na sheria kwa minajiri ya kumshawishi amtimizie mambo fulani.
Mimi nadhani kuna haja ya kuwa wakweli, huko Tanzania, hayo mashangingi na mishahara minono mnayopeana pamoja na rushwa zenu za mikataba, zisiwafanye mkakwepa ukweli wa rushwa ni rushwa.
Hivi hamjui rushwa ‘ndogo’ mnazowagea wananchi, zile za khanga, fulana na kofi, wakati wa kampeni ni kubwa sana? Hamjui kwamba ndizo zinazozaa hizo mnazoziita rushwa kubwa? Utawashaje moto bila kuwa na cheche? Yai na kuku nani kaanza kutokea?
Najua mnaamua kujenga tafsiri za namna hiyo kwa maana wengi wenu, hata nyie mnaotunga sheria, ni watoaji na wapokeaji wakubwa wa rushwa। Bisheni! Kama mnabisha tunawasubiri mwaka 2010, si mtakuja kudanganya tena?! Haki ya mtungi shahidi kata, mtanitambua miye mjukuu wa Mahaho Mbukwa Senyagwa!
NAANZISHA ‘BIG BROTHER’ TANGANYIKA, LAKINI NATAKA WALIOACHIKA!

SANGO nini bandeko na baninga ba Tanzanie? Awa na Tanganyika la vie ezala pasi. Mosala ezali te, mbongo ezali te… tokokufa kaka. Salisa pe mosala wana. Oooh, sore jamani. Sikujua kama nitawaacha mbali ndugu zangu kwa kuzungumza lugha hiyo, lakini nilikuwa namaanisha kuwajulia hali ndugu na marafiki wa Tanzania na kuwaeleza kwamba huku tanganyika maisha ni magumu, hatuna kazi, hatuna pesa na tunasubiri kufa, ikibidi mtutafutie kazi huko. Mpo hapo?

Sisi Waafrika tunapaswa kujifunza lugha mbalimbali bwana, siyo Kitanganyika peke yake. Unaweza kujikuta umezunguka na kutua kwa akina L’Okanga la Ndju Pene Luambo Makiadi pale Bandundu, halafu hata cha kuombea maji hukijui. Utatanga na njia ndugu yangu, shauri yako. Si mnaelewa mokili ekobaluka? Yaani dunia inabadilika!

Basi tuachane na hayo bandugu, tuendelee na mada zetu za kawaida ambapo leo hii nakuja na wazo jipya, wazo ambalo linaweza kuwafanya wale wenye akili na vipaji vya ajabu kutengeneza pesa au mbongo, faranga, mapene, mavumba, njuruku na chochote utakachopenda kukiita ambacho kinamaanisha pale pale kwenye pesa, upo hapo mwanangu?!

Wazo hili, ambalo kama nilivyosema wenye akili na vipaji vya ajabu watalifurahia, linaweza kutengeneza pesa sana kwa sababu nawajua ninyi Watanganyika akili zenu zilivyo, jinsi mnavyopenda kushabiki mambo makubwa na ya ajabu ambayo bila kuwa na akili za ajabu huwezi kuwa mfuasi.

Kwa sababu nazijua akili zenu Watanganyika zilivyo mbovu, nimeamua kuanzisha shindano la Big Brother Tanganyika, litakalokuwa likirushwa hewani kupitia kituo kimoja cha luninga ambacho nakamilisha taratibu za mwisho kuingia nacho mkataba.

Tayari nimeshapata wadhamini wengi walioahidi kutoa jumla ya shilingi milioni 20 kwa mshindi wa kwanza, milioni 15 kwa mshindi wa pili na milioni 10 kwa mshindi wa tatu. Kwa hiyo hapo jumla zitatolewa shilingi milioni 45 za zawadi, pamoja na huduma kibao ambazo zitatolewa kwa washiriki wote 20 wanaotakiwa.

Kampuni hizi zitatoa fedha hizo kwa masharti ya kutangaza bidhaa zao ; kuna kampuni ya wazawa ya kutengeneza vitanda, ambayo imetoa vitanda 10 kwa ajili ya washiriki hao. Sasa mnashangaa nini? Ndiyo washiriki wako 20, lakini vitanda viko 10, si vinatosha? Hapo maana yake watalala watu wawili wawili wakijifunika shuka moja, kama wataamua kulala ‘mzungu wa nne’ ni juu yao.

Kampuni nyingine ni ile maarufu kwa vinywaji vikali, nyingine inatengeneza pombe za kawaida na nyingine inatengeneza pombe za asili za makabila mbalimbali ya Tanganyika. Lakini kampuni ambayo imetoa fedha nyingi zaidi ni ile inayotengeneza kondomu. Naona wengi mmeanza kukenua mimeno yenu mliposikia kondomu, maana nawajua wengi wenu hakuna mnachokifurahia kama ‘ugoni’. Ndiyo. Kama si hivyo ni nini basi?

Ndiyo maana nikasema shindano hili litakuwa la aina yake kuliko yote yaliyopata kutokea duniani. Sijasikia katika mashindano yaliyopita wala kuona kama walikuwa wanatangaza kondomu, ingawa ninyi wenyewe mlikuwa mkishabikia vitendo vilivyokuwa vikifanyika ndani yake. Bado mnaendelea kuombea mashindano hayo yaendelee, na ndiyo sababu hasa nikaamua kuanzisha shindano hili ambalo litadumu kwa kipindi cha miezi sita mfululizo!

Shindano litashirikisha wanaume 10 na wanawake 10, lakini sifa yao ya kwanza ikiwa ile ya kuachika katika ndoa. Ndiyo. Tunataka washiriki waliozowea kuacha na kuachika ili yasiwepo manung’uniko huku uraiani kama tunayoyasikia na kuyashuhudia. Tena kwa sababu humo ndani watakuwa wawili wawili, tunataka tujue tabia za watu hao zilizofanya mpaka wakaachwa ama kuwaacha wenzi wao uraiani, kwa sababu hawataweza kukaa miezi yote sita bila kuachana.

Shindano hili litakuwa likionyeshwa laivu kuanzia saa sita usiku. Sasa mnamaka nini? Kama mnaweza kukesha usiku kucha kutazama Big Brother Africa, mnashindwa nini kukesha kutazama Big Brother Tanganyika? Au kwa vile lile limeanzishwa na wazungu na hili linaanzishwa na Mtanganyika mwenzenu? Hebu niambieni; ni kitu gani kilichokuwa kikiwavutia katika Big Brother kama si kushabikia ugoni?

Hivi hamjui kwamba wazungu ni washenzi na bado wanaendelea na ushenzi wao wa kutuona Waafrika kama wanyama fulani ambapo wanaweza kutufuga kama mbwa na kutazama tunavyofanya mambo ya ajabu? Kufungiwa kwenye lile jumba na kuweka mikamera ambayo inawafanya warekodi matukio yote yanayofanyika, mpaka chooni, ni kuwadhalilisha Waafrika.

Sidhani kama walikuwa na madhumuni mema. Msikubali kuuza utu wenu kwa sababu ya fedha ambazo zinakwisha. Utu haununuliwi jamani. Sitaki kusikia wazungu wanaendelea kutuchezea wanavyotaka. Kama vipi wajidhalilishe wenyewe huko Ulaya, au vipi bwana!? Kama mbwai mbwai tu, mimi siogopi ngondo bwana!

Mwisho.
IF YOU WANNA KILL YOUR MARRIAGE, JUST DO THIS TO YOUR HUBBY

BROTHER डैनी

If some of you ladies want to know how you can suck the life out of your marriage and drive your husband to insanity … or to the bar … or into the arms of another woman … or to a divorce attorney … or just shrivel him up into a conquered quail who inwardly loathes you as he dies a slow, emotionally tortuous death, well then … this is your lucky day.

Here are 10 surefire principles that’ll make your husband more miserable:

NAG YOUR HUSBAND
Nagging is an awesome instrument in the Torture Your Hubby Toolbox. For a wife to be effective at draining a husband’s love for her and, for life itself, she must not buy into this “loving, sweet, polite and patient” goofiness towards him. On the contrary, she must be a nerve grating, contentious, non-stop dripping faucet of fault-finding and finger pointing. Ladies, if you run out of things to nag your husband about, turn your spurn towards politics, church, culture, friends, neighbours, weather, work, or your children. It doesn’t matter what you blather about—just blather. The point is to become a persistent source of audio pain in your husband’s brain.

CRITICIZE YOUR HUSBAND IN PUBLIC
Waling on your husband in private is good, but it is incomplete. What you’ve got to do, devil woman, is go the next step and publicly shame him. Melt him down when you’re out on the town. Is he going bald, talk about it and how you don’t like it. Does he have a little beer belly? Call him a pig and compare him to The Beast. Did he have a financial set back? Tell your friends! Become a big mouth at indiscriminately unveiling anything about your spouse that’ll cause him to want to jump in front of a speeding bus.

KEEP HIM ON A SHORT LEASH
Better yet - a choke chain. Your goal is three-fold: make your man to feel, fear and heel to your wrath. You’ve got to verbally shackle him to your commands. Make him believe like he can’t sit, stand, play, think, speak or spend money unless you, the queen condor, allow him to. By short leashing your husband with an exacting set of laws, you will, in short order, morph in his head from being his lover to being his mother. This masochistic machination of insane restrictions will make your man feel like a stupid son, controlled by you, his new petulant mummy. Forever gone will be the friend, fan, soul mate and confidant stuff that initially drew the two of you together. Forever gone will be the friend, fan, soul mate and confidant stuff that initially drew the two of you together.

BECOME A DRAMA QUEEN
Another thing that’ll make your husband long to be stranded at the Msimbazi Round About with no where to look at, and no one to keep him company is, become a drama mama. Yes, your goal, ghoulfriend, is to ratchet up every situation so that you emotionally drain your man. Make the atmosphere of your home tense. Make everything, especially the small things, turn into a five alarm fire. The thing drama queens do so effectively is jack up the stress levels in the relationship. This, naturally, robs the relationship of the fertile presence of peace. This redlining, high RPM spirit will stretch his nerves more out of shape.

HATE HIS FRIENDS
Separate your husband from his comrades quickly. You mustn’t allow your husband to hang out with anyone but you. Sever those relational ties your companion has with those who have walked to hell and back with him because now, yes now . . . it’s all about you. You especially want to steer him clear of friends who feel the liberty and responsibility to shed light on you, the whacked wife. In addition, get your guy away from those buddies who have amazing and gracious wives or girlfriends. “Why?” you ask. Well, a loving, caring and an affirming couple will expose your broom riding proclivities and put needed pressure on you to dial freaking down. Remember and beware: trusted and wise friends are able to bring perspective to marital mayhem.

HATE HIS HOBBY
Keeping the husband from his friends is not enough because your husband still has an out in his hobby. Your goal is to joy steal anywhere pleasure can be had, and it is here that hobbies figure in greatly. Therefore, set your cross hairs immediately upon that which flicks his diversionary switch. You don’t want him to enjoy anything that you don’t like. Your duty: remove any recourse he has to find solace in something. Additionally, hobbies create relationships built around shared likes, and remember, your goal is to keep him on a choke chain, with no comrades, sequestered in the house to listen to you moo. Never, under any circumstance, take an interest in his interests, encourage him in his pursuits and just simply let the boy play, as this understanding spirit could actually make him take a shining’ to you and you wouldn’t want that to happen.

CUT HIM OFF SEXUALLY
Another great way to make your man hit a depressed state is to cut him off from hot relations. I mean, give him nada. Guys will stomach some nagging, getting short leashed, multitudinous Naomi Campbellesque dramatic outbursts and your general disinterest of his interests—as long as you rock his world in the bedroom. Yes, most men are that easy. Under no circumstances should you show appreciation, be tender, fun, amorous and adventurous or do any other thing that’ll keep the love flame lit. TLC, if injected into the marriage mix, will cause the two of you to have a healthy sexual relationship, which obviously helps a marriage (plus burns calories)—and that would completely derail your desires for marital misery.

GET YOUR SIBLINGS INVOLVED IN YOUR MARRIAGE
Forget this leave and cleave stuff the Bible dictates. If you want your union to unravel then you’ve got to gang tackle your husband with la familia. For example: if you, as a couple, have a major decision to make, seek counsel and opinions only from your mom and dad, rather than your husband. This will give him that stooge/stepchild feeling of useless stupidity that is, a great alienating agent.

NEVER APOLOGIZE
If, in the odd event you do something that hurts your husband, or … say the unlikely occasion arises where you were woefully and ridiculously wrong on an issue, never, I mean never, under any circumstance, apologize for anything. Why should you say you’re sorry? You … apologize? Please. Whether it’s low blood sugar or the vast ring wing conspiracy, you, the marital femme fatale, are fortunate to live in the 21st century. In this therapeutic age you are afforded excuses aplenty that will help you destroy your marriage by never owning or asking for forgiveness for your hellish behavior.

LOOK UGLY
Women come in all shapes and sizes. The majority of men that I know (who love the testosterone, heterosexual, God-blessed fog in which they dwell) really like women. That is, as long as the ladies take care of what the good Lord has given them. The successful marriages I’ve seen know and abide by this golden nugget: always look your best … to constantly attract and show respect for your mate. It also aids in not terrifying dogs and small children.

“The wise woman builds her house, but the foolish tears it down with her own hands.” - King Solomon, Proverbs 14.1. And do you mind if I say this; "Well-behaved women rarely make history."

Ends.
NIMEAMINI, KWELI DUNIA MSONGAMANO!

DJ DANNY

HABARI za leo wanabaraza wenzangu popote pale mlipo. Natumaini kila mmoja wetu yu bukheri wa afya kwa uwezo wa Jehova. Awali ya yote naomba niwatakeni radhi kutokana na kutobarizi nanyi kwa wiki kadhaa sasa. Hata hivyo, hiyo yote haikuwa kwa mapenzi yangu, kwani hili ‘hekalu langu’ lilipatwa na dhoruba kidogo.

Si mnafahamu ndugu zangu kwamba hata miti hupukutika nyakati za kiangazi na kumea nyakati za masika? Miili yetu pia nayo imeumbwa vivyo hivyo, shurti ipatwe na dhoruba kidogo katika harakati za kubadilika.

Kusema ukweli sababu za kukosekana kwangu ndizo zimenifanya leo hii nikirudie tena kibao hiki, ambacho kama mtakumbuka vizuri niliwahi kukisawiri siku za nyuma.

Maradhi humpata mtu yeyote yule, na kwa hakika kuugua siyo kufa! Lakini inashangaza baadhi ya walimwengu, tena wakati mwingine wale ambao ni wat wa karibu yetu kabisa, hutokea kuombea kwamba fulani afe. Wengi hugeuka watabiri kila wanaposikia fulani anaumwa, na moja kwa moja mawazo yao huwapelekea kuamini kwamba watu hao hawatapona bali watakufa!

Kama hili hujalisikia ama halijakupata, basi mwanabaraza mwenzenu limenipata katika kipindi hiki ambacho sikuwepo barazani baada ya kushauriwa niupumzishe mwili.

Walimwengu ni watu wa ajabu kabisa ndugu zangu. Pindi wanapomuona fulani anasumbuliwa na maradhi, wao tayari huanza kupiga hesabu ya lini atakufa na wapi atazikwa! Binafsi nilipigiwa hesabu hizo na watu ambao niliamini kwamba wangeweza kuwa wafariji wangu.

Fikiria mtu anasikia kwamba unaumwa, lakini bila kujua kinachokusibu, anapokuja kukujulia hali badala ya kukufariji anakwambia; “Mimi na mke wangu tumekubaliana kuzikwa hapa hapa Dar, wewe umepanga kuzikwa wapi?!”

Hizi jamani siyo hekaya zangu, bali ninachokisema kimenitokea mwenyewe. Labda pengine mnaweza kunisaidia leo hii, kama ni ninyi mngemjibu vipi mtu huyu, ambaye kwa vyovyote vile mnamtegemea kama mmoja wa wazazi ama ndugu wa karibu anayeweza kuwa wa msaada kwako.

Lakini watu wa aina hii ni wengi sana ndani ya jamii yetu na inaonekana wamepitiwa hata na maneno ya wimbo wa Salamu kwa wagonjwa ulioimbwa na Omar Kungubaya miaka ile ya 1970 yasemayo; “…Ajuaye Bwana Mungu kwa mzima kuwa mfu, mgonjwa kuwa salama…”

Binafsi naamini kwamba kila nafsi itaonja mauti itaonja mauti, kwa sababu sisi sote ni mavumbi na mavumbini hatuna budi kurejea. Hivyo, suala la kufa huwa silihofii kabisa, ninachokihofia ni kwamba nitakuwa katika kundi gani baada ya kufa. Daima wenye hekima humuomba Mungu awaongoze katika haki na kuwaombea wengine washike mwenendo mwema, si ndivyo jamani?

Hii ndiyo sababu iliyonifanya nikikumbuke kibao cha al-marhum Freddie Ndala Kasheba ‘Supreme’ alichokiimba mwaka 1982 akiwa na Orchestra Safari Sound ‘wana-Dukuduku’ kisemacho Dunia Msongamano; “…Mawazo yamenijia leo, Ya Mzee wangu alokuwa akisema, Dunia ni msongamano wa watu wenye akili tofauti, Ukitaka kuishi vema lazima uwe na utulivu, Ukitaka kuishi vema fikiri kabla ya kujibu, Jifunze kwa walimwengu, na walimwengu wajifunze kwako, Dunia ni kuona mambo, Na halafu kuyasahau…”

Ni kweli kabisa, dunia ni msongamano kwa sababu imejaa watu wengi wenye mawazo tofauti kama hawa waheshimiwa, ambao wanadhani kwamba mtu akiugua basi atakufa tu, tena yawezekana kabisa wakawa wamempangia siku, saa na namna kifo chake kitakavyokuwa.

Watu wa aina hii tunawashuhudia jamani, hawaendi kuwaona wagonjwa mpaka kwanza waulizie; “Anaumwa nini?” “Vipi amekonda?” “Sijui kama atapona, hivi umeomuona Danny alivyo? Na ule wembamba wake kabaki kama chelewa?” Basi hukumu hizi na nyingine nyingi ndizo hutawala mawazo ya watu hawa, na hata pale wanapokuwa wanakwenda kuwatazama wagonjwa huwa ni kama maigizo fulani tu kwao, yaani kana kwamba wamekwenda kuthibitisha hisia zao kwamba watu hao hawatapona! Utadhani wao ni maswahiba wa Mungu na wanajua mipango yake!

Kweli naamini maneno ya Kasheba; “…Dunia msongamano, Kasema baba, Nimeyaona leo nakubali mie, Wengine hupendelea kufurahia, Wanaposiikia fulani kafa, Kufa kwa binadamu hupangwa na Mungu, Namuomba Mwenye Enzi anipe maisha eeh.”

Ndiyo, si mnaniona leo hii tupo pamoja kwenye baraza tukisawiri, nikiwa bukheri wa afya, kwa sababu naamini ugonjwa wangu si wa mauti, bali ulitokea ili Mungu aweze kutukuzwa kwa huo. Pengine nisingeugua kamwe nisingeweza kuitambua tabia ya upande wa pili ya ndugu yangu huyu mpendwa.

Ninachoweza kusema ni kwamba, namuomba Mungu amsamehe na awasamehe wale wote wenye tabia ya kupenda kuwatabiria wenzi wao kwamba watakufa. Wale wenye tabia ya kujifanya madaktari bingwa wa kupima watu kwa macho! Wale wenye kawaida ya kujifanya miungu wa dunia kwa kuweza kutoa hukumu wakati wakijua kwamba hakimu pekee ni Mungu!

Hebu burudikeni na kibao hiki, lakini kusema kweli nahitaji sana mchango wenu katika mada hii. Mnaweza kunitumia mchango wenu kwa sms ama kunipigia kupitia kilongalonga – 0784 – 939 319, au barua-pepe: brotherdanny2003@yahoo.com.

AAhhhh DUNIA MSONGAMANO
Mawazo yamenijia leo,
Ya Mzee wangu alokuwa akisema,
Dunia ni msongamano wa watu wenye akili tofauti,
Ukitaka kuishi vema lazima uwe na utulivu,

Ukitaka kuishi vema fikiri kabla ya kujibu,
Jifunze kwa walimwengu, na walimwengu wajifunze kwako,
Dunia ni kuona mambo,
Na halafu kuyasahau

Kibwagizo:
Dunia msongamano,
Kasema baba,
Nimeyaona leo nakubali mie,

Wengine hupendelea kufurahia,
Wanaposiikia fulani kafa,
Kufa kwa binadamu hupangwa na Mungu,
Namuomba Mwenye Enzi anipe maisha eeh


Mwisho.
BUNGE HILI LA TANZANIA … HERI LA CHAMA KIMOJA!

HABARI za leo ndugu zangu wapendwa sana wa Tanganyika. Natumaini kwamba bado mnaendelea na machungu ya siku zote yanayozidi kutupata tangu tulipopata uhuru. Maisha yanazidi kubana kwetu sisi wakati wenzetu huko Tanzania mambo yao yanazidi kuneemeka.

Kama mtakumbuka wiki mbili zilizopita nilikuwa kule kwenye lile jumba la Legico, la waheshimiwa sana ambao ndio wanaotunga sheria zinazotuongoza hata sisi huku Tanganyika. Sheria ambazo zinaonekana si kutubana akina yakhe, bali kuwaneemesha zaidi wao Watanzania.

Nilichangia hoja kadhaa kwa kuzipinga kwa nguvu zote, kama walivyofanya wenzangu, lakini baadaye nikajikuta nikifinywa mguu na kuambiwa niunge mkono hoja zote.

Niliwaambia wananchi wenzangu wa Tanganyika, kwamba nililazimika kufanya hivyo kutokana na sababu ambazo nilizitaja, nadhani mlinielewa vyema, au siyo ndugu zangu?

Lakini ngojeni leo niseme ukweli wa yale yanayoendelea ndani ya Legico, hasa katika mfumo huu wa vyama vingi. Kwanza naamini kwamba mmepata taarifa kwamba yule mwakilishi kijana mwenye makeke kutoka kambi ya upinzani amesimamishwa.

Kusimamishwa kwake kunafuatia kutoa hoja binafsi ya kutaka tume iundwe kumchunguza waziri wa vito vya thamani ajieleze ni kwa nini aliamua kwenda kusaini mkataba na wale jamaa wenye pua ndefu kule ughaibuni. Eti ikawa nongwa na jamaa wakasimama kidete kwamba asimamishwe. Akasimamishwa!

Lakini kuna mwakilishi mwingine ambaye alinusurika, kwa sababu yeye alikuwa anataka kutoa shilingi katika hoja ya waziri mmoja anayesimamia mambo nyeti ya nchi, wakamwambia ukirudia utaishia kunawa, kula huli.

Nashangaa kwa nini hakusimamishwa, lakini nafikiri ni kwa sababu yeye anatoka katika kile chama kidumu kilichoshika hatamu za uongozi wa Tanzania tangu enzi zile. Yeye walimwita kwenye vikao vya chama kidumu, nasikia walimsimanga na kumkebehi, kisha wakasema kama angeendelea tu angekwenda kwao kuchunga mbuzi na ng’ombe. Jamaa akanywea kweli kweli na mpaka sasa hajasikika tena.

Mimi binafsi nilikuwa nataka kuwasilisha hoja binafsi kumchunguza waziri wa nanihino ambaye wizara yake imekumbwa na kashfa nyingi sana katika kipindi cha miaka miwili tu, ikiwa ni pamoja na kujaza watu wa kabila lake kuanzia mfagiaji mpaka dereva.

Bado najishauri kama niiwasilishe au la, lakini hakyanani vile, nikipandisha mori wangu wa Kimasai, nitakwenda kuropoka halafu nije nipumzike huku na Watanganyika wenzangu.

Lakini kitu pekee ambacho kinaendelea kunisikitisha mimi na Watanganyika wenzangu ni kwamba, Legico la sasa hivi limevurugika kuliko kawaida na naungana na yule mhishimiwa wa kule wapi sijui, kule pembezoni mwa Tanzania, ambaye aliomba Legico isigeuzwe kijiwe cha kutetea maslahi ya chama Fulani badala ya kutetea maslahi ya taifa.

Mimi naunga mkono kabisa hoja yake hiyo, kwa sababu Legico ya sasa ni afadhali ile ya chama kimoja. Wawakilishi wetu wanakwenda kutetea maslahi yao binafsi na yale ya maswahiba wao. Wanajali zaidi kutetea chama chao na kusahau kwamba wamekwenda kule kutetea maslahi ya taifa.

Hata wale wawakilishi kutoka chama kidumu, wale wenye msimamo, wamebadilika kabisa. Demokrasia ya kweli haipo kwenye Legico na badala yake Watanganyika tunashuhudia mijadala ya kufurahisha nafsi za wachache tu na kuacha mambo ama kero za wananchi.

Unajua naongea ndugu zangu mpaka hasira zinajiaa! Naogopa tu editori asije akaninyooshea kidole, maana hakika inakera sana.

Huyu bwana mdogo waliyemsimamisha sijui hata walitumia vigezo gani. Tangu lini kesi ikahukumiwa kwa kura? Hivi nyie waungwana hamjishangai wenyewe? Ninyi si ndio mnaotunga sheria za nchi? Inakuwaje mnakuwa wa kwanza kuzivunja?

Kwa nini hamkukubali hoja za yule mwakilishi wa wapi vile, aah kule kwa ndugu zangu, ambaye alisema mhishimiwa waziri wa vito alete mikataba na aliyosaini huko ‘Kwa Mama’ na huyu bwana mdogo alete ushahidi wake? It is unbearable, kwa kweli!

Jamani kumbukeni kuwa; Unaweza kumdanganya mtu Fulani wakati wote, unaweza kuwadanganya watu wote wakati Fulani, lakini katu huwezi kuwadanganya watu wote wakati wote! Usemi huu uzame kwenye vichwa vyenu wahishimiwa huko Legico, maana itakuja siku inayotisha, siku ambayo mtakuja kushindwa kuomba maji!

Kama mnabisha, subirini na sisi tunawasubiri mkija kwetu mwaka huo, hakyanani nitawambia morani wote wasimame attention kuwasubiri. Nyie subirini, hakika nimekasirika kiasi kwamba naona hakuna demokrasia. Au mnataka nizungumze kwa lugha ya mama? MBIFILE SANA!!

Mwisho.
NATAKA KUWA BALOZI WA HESHIMA PAKISTAN!

MZEE WA SHAMBA

HABARI zenu ndugu zangu huko Tanganyika. Nina hakika kwamba wenzetu huko Tanzania mambo yenu yanakwenda vizuri, tofauti kabisa na sisi huku Tanganyika ambako tunaendelea kuchanja mbuga huku soli za viatu zikiendelea kumong’onyoka.

Nimerejea juzi huku Tanganyika kutoka kwenye lile Jumba la Legico, jumba takatifu la kutunga sheria, ambako nami nilipata bahati ya kutoa mchango wangu katika hoja za wizara kadhaa.

Mpaka sasa nasikitika kwamba yale niliyoyapigia kelele hayajarekebishwa kwenye bajeti za mwaziri hao, hasa baada ya kuungana na wabunge wenzangu kuunga mkono hoja hizo ingawa zilikuwa na mapungufu kibao.

Lakini wananchi wenzangu, ninyi mlionichagua niende kuwawakilisha, si mliniona kwenye video nilivyokuwa nazungumza kwa jazba huku mishipa ya shingo ikiwa imenitoka? Si mliniona jamani nilivyombana waziri yule wa mambo ya nanihiino?

Sasa mnanilaumu nini kuunga mkono ile hoja wakati wabunge wote wa chama chetu kitukufu waliiunga mkono? Nyie mlitaka mimi niitwe kwenye kikao cha faragha? Hivi mnajua mambo ambayo wale wabunge wenzetu huwa wanaambiwaga wanapoitwa kwenye vikao vya aina hiyo? Mnajua yanayotokea lakini au kazi ni kunilaumu tu?

Nani anayeweza kunionyesha mbunge Fulani ambaye alikuwa akipinga hoja ama kuonekana akizungumza sana, ambaye baada ya vikao vyetu vya faragha akaendelea na msimamo wake ule ule? Kama yupo na asimame nimuone.

Wananchi wenzangu wa Tanganyika na Tanzania, naomba mnielewe, napalilia unga jamani. Wakinimwaga mimi kwenye chama huku wapinzani watakuja kutawala, halafu hata uwakilishi wa huku Tanganyika utakuwa mashakani.

Hata hivyo, nimekuja kwenu wazee wenzangu wa Tanganyika nikiwa na ombi moja. Nahitaji baraka zenu kwamba nataka niende nikaishi Pakistan halafu nifungue Ubalozi wa Tanganyika katika mji mmojawapo.

Najua mnanicheka, msicheke jamani. Si mlimsikia waziri akisema siku ile kwamba mtu yeyote mwenye uwezo anaweza kutuma maombi serekalini na kuruhusiwa kufungua Ubalozi wa Heshima? Sasa tatizo liko wapi hapa?

Mimi naamini nina uwezo, kwa sababu ni mkulima na nikienda kule nakwenda kuendeleza kilimo maarufu cha mazao ya kule. Mnayajua mazao ya huko jamani, au hamyajui? Heroin, hashish, milungi na kadhalika, ndiyo mazao yanayoweza kunitoa haraka nikapata pesa na utajiri utakaonifanya nifungue ubalozi wa heshima.

Sasa mnashangaa nini jamani? Kitu gani hakiwezekani hapa? Serekali imeshasema kwamba watu wanaostahili kufungua balozi kama hizi ni wenye fweza, wafanyabiashara na siyo watu kapuku kama sisi Watanganyika tunaotegemea kilimo cha jembe la mkono.

Ndiyo maana nasema hivi, nikienda huko nitapata fweza haraka sana kwa kilimo hicho, kwa sababu nitatumia zana za kisasa za kilimo na kwa kuwa soko la mazao hayo ni kubwa, hakika ninaweza kufanikiwa haraka sana.

Msishangae jamani. Hivi ni nani anayefahamu kwamba Watanzania walioko Ulaya na Marekani wanajishughulisha na biashara gani? Ni nani mwenye rekodi sahihi za Watanzania hawa, tangu kuondoka kwao mpaka sasa?

Naamini kabisa kwamba, ikiwa mtindo wa kufungua Balozi za Heshima utakuwa hivi, mwisho wa siku tutakuwa na Mabalozi wa Heshima wauza unga, wafanyabiashara haramu, wacheza kamari na mafisadi wa kutupwa, ambao watakuwa wamepata hadhi hiyo kutokana na fweza walizozichuma kwa njia haramu lakini kwa mwavuli wa ufanyabiashara.

Kama mnabisha, subirini, maana hata serekali ikijitetea kwamba itafanya uchunguzi wa kina, kwa mtandao wa Kimafia naamini tunaweza tukawa tumewapata mabalozi wasiofaa hata kulumagia.

Unajua wakati mwingine huwa mnanilaumu bure Mzee wa Shamba kwamba mropokaji, lakini hili la ubalozi wa heshima, naamini serekali yetu itakuwa imepotoka, kwa mtazamo wangu. Kusema akina sisi wenye uwezo tunaweza kufungua balozi hizi ni sawa na kurusha mifupa kwenye kundi la fisi wenye uchu.

Si ajabu mwakani kwenye Bunge la Bajeti tukaambiwa kwamba watu alfu moja tayari wameomba kuwa mabalozi wa heshima. Na kweli wanaweza kuupata ubalozi huo, ambao utakuwa sit u umewapa heshima, bali utatumika kama kivuli cha kuficha maovu yao.

Kama vipi, subirini. Na mimi naapa hakyanani vile, mtakuja kuniambia.
SASA NAITAKA TUZO YA CHISSANO!

POROJO ZA MZEE WA SHAMBA

AHLAN wasaalani ndugu zangu wote Watanganyika. Natumaini mnaendelea vizuri na majukumu yenu ya kila siku, kadiri Mungu anavyotujalia. Si mnaelewa ndugu zangu hali halisi inayotukabili sisi akina yakhe?

Maisha kwetu bado ni magumu hayana unafuu wowote. Barabara hazipitiki huku na kuna makondorasi waliopewa tenda ya zabuni ya ujenzi wa barabara ya huku wanalipua ujenzi wao kama yale mabomu ya Angola. Si mnayajua yale mabomu yaliyotegwa na Mreno kwa hasira baada ya kung’olewa mwaka 1975 ambayo yamewaacha ndugu zetu wengine wakiwa walemavu wa maisha?!

Basi ujenzi wa makondorasi wa barabara hii ndivyo ulivyo. Umelipuliwa badala ya kulipuka, na kama viongozi wa Tanzania hawaamini, waje waone ama washuhudie jinsi uji mwepesi wa lami ulivyonyunyiziwa kwenye kokoto halafu wahusika wakasema tayari wameshajenga barabara ya lami.

Lakini sishangai, haya yote ndiyo matunda ya teni pasendi ambazo wakubwa wamekuwa wakizigombea kila leo kila wanapoitisha tenda za zabuni mbalimbali. Ukiona mkataba umesainiwa, ujue kuna watu wamekula teni pasendi!

Sasa mnabisha nini? Si mnakumbuka ule mkataba wa kumuuzia yule Mwarabu mbuga ya uwindaji kule Loliondo? Mnaukumbuka lakini ulivyozua kashfa maarufu ya Loliondo Gate? Halafu basi ulisainiwa Siku ya Wajinga Duniani! Mnaijua? Aprili Mosi.

Ndiyo. Viongozi wa Tanzania wametulazimisha Watanzania katika mambo mengi tu. Mnakumbuka suala la kukabiliana na pancha za magari wakubwa wale walivyotulazimisha tufunge Oko kwenye magurudumu ya matairi ya magari eti kwamba pancha ikitokea tu, basi ile dawa itakwenda haraka kuziba. Matokeo yake yalikuwaje? Matairi yote yakaoza! Lakini wakati huo waheshimiwa wakiwa tayari wametengeneza fedha za kutosha.

Likaja suala la kudhibiti ajali. Mkubwa mmoja wa Sirikali ya Tanzania ambaye inasemekana alikuwa na hisa kwenye kampuni mmoja, akatakangaza agizo la Sirikali kwamba magari yote yafunge sijui Spidi Limited ili kuyazuia yasiende kasi na hivyo kupunguza ajali. Ajali hazikukoma, zikaendelea na zinaendelea mpaka leo, wakati tayari wao walikuwa wamejitengenezea mabilioni kwa mabilioni ya pesa.

Jamani msinione hivi Mzee wa Shamba, nina kumbukumbu nyingi kiasi kwamba wakati mwingine huwa zinanifanya niwe nalia machozi tu nikizikumbuka.

Nakumbuka Sirikali iliposema kwamba inaondoa kodi ya kichwa kwa sisi Watanganyika wengi tulifurahia. Lakini hatukujua, kwa sababu sasa hivi tunalipa kodi kubwa asavali ile ya kichwa. Ukienda dukani utaambiwa bei ya mkate shilingi 50, lakini itabidi ulipie shilingi 60 ikiwemo kodi ya asilimia 20, yaani kodi ya FAT.

Mikataba ya ulaghai kama ile ya akina Carl Peters imezidi kwenye sekta mbalimbali kama hizo zinazotajwa za majini sijui. Watu wanatafuna fedha kama hawana akili nzuri wakati sisi Watanganyika tunakondeana. Hakika inakera mno.

Hali hii ndiyo inayonifanya leo hii nianze kuingia kwenye mchakato wa kuwania uongozi mwaka 2010. Nataka nipate uongozi wa Watanganyika kwa sababu ninaamini naweza kuwaondolea kero zote hizi ambazo mwenyewe nazishuhudia.

Kilichonihamasisha, hata hivyo, ni ile tuzo aliyoitwaa Joakimu Alberto Chissano kule Uingereza, tuzo ya utawala bora na demokrasia, ambayo imeambatana na kitita kikubwa cha mihela.

Kwa hakika, nikiingia madarakani nitahakikisha naleta mabadiliko makubwa sirikalini na kuboresha maisha ya Watanganyika walau yafikie ama yakaribiane na yale ya Watanzania. Nitahakikisha kero za Watanganyika zinasikilizwa na kutekelezwa, badala ya kupuuzwa kama ilivyo sasa.

Sitakuwa mnafiki kama walivyo viongozi wengi wa Tanzania, ambao siku zote wanapiga porojo mdomoni wakati mioyoni wanafahamu wazi kwamba hawawezi kutekeleza lolote kati ya waliyoyaahidi. Sitajipendelea kama wanavyofanya wale wanaoingia mikataba na makondorasi wanaonyunyiza lami kwenye barabara za Tanganyika na kuchukua mabilioni ya pesa sirikalini.

Zaidi, nitahakikisha kwamba, nakaa na wapinzania na kusikiliza hoja zao na ushauri wao, kwa maana naamini hata wapinzani wanapenda kuona nchi yetu inapiga hatua mbele kimaendeleo. Nitapitia mikataba yote ya ndani na ya nje na kuangalia kama kuna mazingira yoyote ya rushwa na ufisadi, na kama kuna kiongozi yeyote atakayehusika nitahakikisha namwadhibu kulingana na sheria.

Haya yote hayatatekelezwa kabla ya kuirekebisha katiba ya Tanganyika na hakika nitaweka kipengele kwenye katiba ambacho kitaruhusu mtawala yeyote wa serikali, aliyeko madarakani na aliyestaafu, ikiwa amejihusisha na ufisadi, lazima apandishwe kizimbani kujibu tuhuma. Ikionekana ana hatia afungwe na hata kunyongwa!

Kwa mtaji huu, naamini kabisa nitakuwa nimefikia vigezo vya kuinyakua tuzo ile aliyoitwaa Chissano. Au mnasemaje Watanganyika wenzangu?

Mwisho.
TUSISUBIRI RAIS ATUANDIKIE BARUA ZA KUTUFUKUZA KAZI TUZISAINI!
*Wazembe wengi serikalini wanakingiwa vifua na vigogo
*Ni tatizo sugu kwa nchi za Dunia ya Tatu

DANIEL MBEGA
Dar es Salaam

MKURUGENZI Mtendaji wa TANESCO kajiuzulu! Hii ni taarifa ambayo bado ya moto kabisa miongoni mwa Watanzania baada ya mtendaji mkuu wa Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania, Dk. Idris Rashid, kuamua kuachia ngazi baada ya kutofautiana na wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa shirika hilo kuhusu uamuzi wake wa kutaka kuongeza tarifu za umeme kwa asilimia 40.

Uamuzi huo umepingwa kwa muda mrefu na wanaharakati wengi hasa ikizingatiwa kwamba gharama za sasa tu bado zinawapiga chenga wananchi wa kawaida wanaotumia nishati hiyo, ambao ni asilimia 10 tu kati ya Watanzania wote milioni 37, huku asilimia 8 kati yao ni wa mijini na asilimia 2 ni vijijini.

Wengi wamepinga uamuzi huo kwa sababu badala ya kuweka mikakati ya kuhakikisha kila Mtanzania anapata nishati hiyo hasa katika kipindi hiki cha sayansi na teknolojia, Tanesco inataka kuwanyang’anya hata wale wachache wanaoitumia kwa sasa. Kwa maana hiyo wataendelea kujenga ukuta mrefu zaidi wa kuzuia wale wasio nayo kuendelea kuikosa milele.

Inawezekana Dk. Idris Rashid akawa amejiuzulu kutokana na kusakamwa kwa uamua wake huo, lakini wachunguzi wa mambo wanajaribu kutafakari kwamba, kujiuzulu kwake kumekuja wakati ‘mbaya’ hasa baada ya Kamati Teule ya Kuchunguza Mikataba ya Madini kuanza kuchunguza kashfa ya Richmond.

Baadhi ya watu wanahisi kwamba, kwa kuwa tayari kamati hiyo, chini ya Jaji Mark Bomani, imeshaanza kuchunguza mkataba wa Richmond na Tanesco unaodaiwa kuzingirwa na ufisadi mkubwa, huenda mtendaji huyo wa Tanesco akawa ameamua kutafuta mahali alipoangukia ili ang’atuke, kupanda kwa tarifu za umeme kukawa ni mahali muafaka kwake.

Japokuwa hakuwepo wakati mkataba huo ukisainiwa, ambao pia unasemekana ulikuwa na shinikizo kutoka kwa vigogo wa juu serikalini waliokiuka taratibu za zabuni za serikali, lakini ameona bora aondoke katika kipindi hiki cha kashfa ya kupanda kwa umeme, tatizo ambalo kwa hakika linaweza kuathiri hata uzalishaji na shughuli zote za maendeleo na uchumi.

Vyovyote iwavyo, kujiuzulu tayari amejiuzulu, na niseme tu ukweli kwamba, hata kabla ya kujiuzulu tayari nilikuwa nimepanga kuandika makala haya ili kuhoji uhalali wa viongozi wetu wa Tanzania, Kiafrika na hata wa nchi zinazoendelea, kuwa na tabia ya kung’ang’ania madaraka hata pale wanapokuwa wamekumbwa na kashfa nzito zinazohusu maslahi ya jamii na taifa kwa ujumla.

Tangu serikali ya Awamu ya Nne chini ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete iingie madarakani siku 701 zilizopita (Desemba 21, 2005), watendaji wake wengi, wakiwemo mawaziri na wakurugenzi, wamekumbwa na kashfa nyingi zisizo na idadi na daima wameendelea kuwa makaidi hata pale wanapoelezwa ukweli.

Zipo tuhuma ambazo wamezifanya wakati wa utawala uliopita, wakishirikiana kwa namna moja ama nyingine na watawala waliopita, lakini pia zipo ambazo zimefanyika katika kipindi cha awamu hii nab ado wahusika wameendelea kuziba masikio, huku wakubwa wao nao wakiwafumbia macho na kuleta tafsiri ya kulindana.

Inaelezwa kwamba kashfa ya Benki Kuu kuhusiana na malipo ya akaunti ya madeni ya nje (EPA) yanayowahusisha watu wengi kuchota mamilioni ya fedha ilikuwa inajulikana muda mrefu eti hata kabla ya vyombo vya habari na Wabunge kulivalia njuga. Kwamba madai hayo yalikwishatolewa ufafanuzi na eti kulikuwa na watu waliokuwa wakiyakuza.

Gavana wa BoT, Daudi Balali akagoma kujiuzulu japo ukweli unaonekana dhahiri kwamba kuna ufisadi na mazingira ya rushwa yaliyotanda kwenye chombo hicho kuhusiana pia na mikataba mbalimbali, ukiwemo wa ujenzi wa minara miwili ya makao makuu ya Benki Kuu.

Watu waliohusika na ununuzi wa ndege ya rais, ununuzi wa rada ya bei mbaya, ununuzi wa helikopta za kijeshi na magari ya jeshi, uuzaji wa viwanja vya serikali na rasilimali za umma kwa bei ya kutupa, wote wapo na wanafahamika, lakini pamoja na ufisadi wao kufichuliwa, bado wameendelea kukalia viti vya enzi wakisema hawaondoki hata iweje.

Suala la mikataba feki na ile iliyozingirwa na rushwa liko wazi. Watendaji wengi wa serikali katika awamu iliyopita wanajulikana kwa sababu walifanya hivyo huku wakiwa katika madaraka yao, lakini pamoja na kufahamika kwa tuhuma zao hakuna hatua ambayo mpaka sasa imechukuliwa.

Ukiwaachilia hao waliofanya ufisadi kipindi hicho, wapo wale ambao bado wangali madarakani, wakiwemo gavana wa Benki Kuu Daudi Balali, na waziri wa nishati na madini Nazir Karamagi, ambaye tuhuma za mikataba ‘mibovu’ ya madini ndizo zilizoleteleza kuundwa kwa kamati teule yenye wajumbe wengi akiwemo Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe (CHADEMA) ambaye alitoa hoja binafsi kuhusiana na mkataba wa uchimbaji wa madini katika mgodi wa Buzwagi.

Inavyoonekana ni kwamba, viongozi wengi wa nchi zinazoendelea, ikiwemo Tanzania, hawana desturi ya kung’atuka pindi mambo yanapokuwa yamekwenda kombo, hata pale ukweli unapowekwa bayana, kama ilivyo sasa kwa kashfa zinazowakabili Karamagi na Balali pamoja na watendaji wengi wa serikali.

Taratibu za ‘kulindana’ baina ya viongozi wa juu serikali, wa kati na wale wa chini, ndizo zilizoshika hatamu nchini Tanzania kiasi kwamba mtu anaona hawezi kuguswa hata kama ufisadi uliofanyika umeigharimu serikali na jamii kwa ujumla kiasi kikubwa sana cha fedha.

Nakumbuka mwaka 2001 wakati treni ilipoanguka nchini India waziri aliyekuwa akihusika na usafirishaji alilazimika kujiuzulu. Treni tu! Kwani yeye ndiye aliyelipindua? Lakini hiyo ndiyo gharama ya siasa, kwa sababu alijua kwamba tukio hilo limetokea chini ya uongozi wake na kama kulikuwa na uzembe wowote ungeweza kujulikana baadaye yeye akiwa pembeni kutoa nafasi ya uchunguzi.

Leo hii viongozi wengi wa Tanzania hawataki kuwajibika wakati hata nafsi zao zinawasuta bayana kwamba wamefanya uzembe. Lakini kutokana na kiburi walicho nacho, kilichopandikizwa kutoka juu mpaka chini kwa kutumia kanuni isiyojulikana ya ‘Wakubwa kulindana’, waheshimiwa hawa wamekuwa kama miungu-watu ambao daima wanaona hawawezi kunyooshewa hata kidole na awaye yote.

Ni jambo lililo dhahiri kwamba kuna matatizo katika nchi zetu, na viongozi wanapaswa kuwajibika mara matatizo yanapotokea. Tusisubiri ifikie mahali Rais akaandika barua ya kukufukuza kazi na kukuletea uisaini! Nadhani hiyo itakuwa aibu kubwa na fedheha isiyostahimilika.

Katika kipindi cha awamu ya tatu tulishuhudia mawaziri wanne na manaibu wao wawili wakijiuzulu kutokana na kashfa mbalimbali. Kwanza mwaka 1996 Waziri wa Fedha Profesa Simon Mbilinyi na naibu wake Kilontsi Mpologomyi walilazimika kujiuzulu baada ya kuibuka kwa kashfa ya misamaha ya kodi ya minofu ya samaki na mafuta kwa makampuni kadhaa.

Hoja iliyosababisha kung’atuka kwa mawaziri hao ilitolewa binafsi na Mbunge wa Ilala wa wakati ule, Idd Mohammed Simba, ambaye baadaye aliteuliwa kuwa mwenyekiti wa kamati teule iliyoundwa kuchunguza kashfa hiyo.

Baadaye aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Juma Ngasongwa, naye alilazimika kujiuzulu kutoa nafasi ya uchunguzi baada ya kutajwa katika ripoti ya Tume ya Kero ya Rushwa ya Jaji Joseph Warioba kwamba alikuwa amehusika kwa namna moja ama nyingine na suala la minofu ya samaki.

Miaka miwili baadaye aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utawala Bora), Dk. Hassy Kitine, naye alilazimika kujiuzulu. Mkurugenzi huyo wa zamani wa Idara ya Usalama wa Taifa alijiuzulu baada ya kuibuka kwa kashfa ya kumtibu mkewe nje ya nchi kwa kutumia mamilioni ya fedha za serikali kinyume cha taratibu. Hapo ndipo unapoweza kujiuliza, msimamizi wa utawala bora anavunja kanuni kinyemela kama hivyo.

Oktoba 7, 1998 aliyekuwa naibu waziri wa fedha Bi Monica Mbega, naye akaandika barua kuomba kujiuzulu kwa maelezo kwamba anakwenda kusoma. Rais Benjamin Mkapa alimkubalia, ingawa wachunguzi wa masuala ya kisiasa walihusisha kujiuzulu kwake na kashfa ya kuwapeleka ‘ndugu zake’ Ureno (ambao walizamia huko huko) katika mkutano wa dunia wa vijana, wakati huo akiwa naibu waziri wa kazi na maendeleo ya vijana.

Ndipo hatimaye Novemba 4, 2001 Idd Simba akatangaza kujiuzulu uwaziri wa viwanda na biashara kufuatia kashfa ya sukari, baada ya tume ya Jaji Bernard Michael Luanda kubainisha kwamba kulikuwa na ukiukwaji wa taratibu katika utoaji wa vibali kwa makampuni yaliyokuwa yanaagiza sukari nje ya nchi baada ya nchi kukumbwa na hali mbaya ya uhaba wa sukari.

Hoja iliyoleteleza Simba kujiuzulu ilitolewa na Mbunge wa Kwela, Chrisant Majiyatanga Mzindakaya ‘Mzee wa Mabomu’, lakini pamoja na serikali ‘kuiteka’ hoja hiyo na kuunda tume yake badala ya Tume ya Bunge, ukweli ulianikwa hadharani kwamba makampuni mengi kati ya yale yaliyokuwa yameruhusiwa yalikuwa yameingizwa kinyume cha taratibu.

Lakini nakumbuka siku ambayo Mzindakaya alitoa hoja binafsi Agosti 10, 2001 pale Dodoma, almanusura Idd Simba atangaze kujiuzulu siku hiyo hiyo kwa sauti ya upole, yenye mashaka pale aliposema; “…Kupitia Bunge lako tukufu,” akasita kwa sekunde chache “…napenda kuwasalimu wananchi wa Ilala na wananchi wote kwa ujumla na niseme sijalidanganya Bunge na sijihusishi na vitendo vyovyote vya rushwa.”

Licha ya tuhuma za sukari, pia Idd Simba alikuwa anakabiliwa na tuhuma za kukiuka maagizo ya Baraza la Mawaziri na Ikulu katika kubinafsisha Kampuni ya Taifa ya Wakala wa Meli (NASACO) ambayo ilikuwa inajiendesha kwa faida.

Haya ni baadhi tu ya mambo yaliyokuwa yamejitokeza katika awamu ya tatu, ingawa yalikuwepo mengi yaliyofichika ambayo sasa yamefichuliwa na wahusika wapo, lakini kwa vile wengine walishirikiana na viongozi wa juu serikalini, wanaona kwamba hawawezi kufanywa kitu chochote kwa kuwa walioshirikiana nao hawaguswi na sheria kikatiba!

Yawezekana hizi zikawa ni ndoto za wengi wanaoingia madarakani, madaraka ambayo walio wengi wanayanunua kwa bei kubwa sana na wanapopewa nyadhifa wanataka kwanza kuziba mapengo ya gharama walizotumia wakati huo.

Hata hivyo, hatudhani kama huu ni ustaarabu kwa mtu kuharibu mali ya umma kwa kisingizio kwamba unakula na wakubwa. Umechaguliwa kwa ajili ya kuwatumikia wananchi ambao hasa ndio waajiri wako na unapokiuka maadili ya uongozi unakuwa umewatendea dhambi kubwa wale waliokupa dhamana ya kuwaongoza.

Hivi kweli waheshimiwa hawa wanataka turejee enzi zile za awamu ya kwanza ambapo tulishuhudia mawaziri na viongozi kadhaa wa serikali wakitangazwa kustaafishwa kwa manufaa ya umma? Ni kwa nini wasiwe waungwana kwa kuamua kuwajibika, wakajiuzulu na kukaa kando kama alivyofanya Alhaj Ali Hassan Mwinyi enzi zile alipokuwa Waziri wa Mambo ya Ndani kabla hajawa Rais wa Jamhuri ya Muungano?

Tunaamini kwamba kwa mtu muungwana, kujiuzulu ni uamuzi wa busara mara linapotokea tatizo zito kama haya tunayoyaona, wala si dhambi au aibu. Tumeshuhudia hata katika mataifa yaliyoendelea jinsi mawaziri na viongozi mbalimbali wanapoamua kujiuzulu wanapokabiliwa na kashfa, kwa nini sisi tnaoendelea tunakuwa wagumu?

Utawala bora unahitaji busara na hekima ya kutosha, kinyume chake tunakuwa na serikali iliyojaa miungu-watu wanaopenda kujiamulia mambo yao wenyewe, ambao hawako tayari kukosolewa. Tunahitaji kubadilika kama kweli tunataka kujenga taifa lenye nidhamu. Ada ya mja kunena, muungwana ni vitendo!

Mwisho.
BIASHARA ILIVYOFUTA UTAKATIFU WA IKULU!
*Nyerere hakujua kama aliowatetea ni wajasiriamali wa kubwa

DANIEL MBEGA
Dar es Salaam

WAKATI wa mchakato wa kumtafuta mgombea wa urais kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi mkuu wa kwanza wa vyama vingi Tanzania mwaka 1995 tulishuhudia wanaccm wengi wakijitokeza kuwania nafasi hiyo adhimu kwa tiketi ya chama hicho.

Miongoni mwao, ambao nilihudhuria hata mikutano yao ya kutangaza azma zao za kuwania nafasi hiyo walikuwemo mawaziri wakuu watatu wastaafu; Jaji Joseph Sinde Warioba, John Samuel Melecela na Cleopa David Msuya.

Wanaccm wengine walikuwa Katibu Mkuu wa chama hicho wakati huo Horace Kolimba, Jaji Mark Bomani, Jakaya Mrisho Kikwete, Edward Ngoyayi Lowassa na mgombea ‘asiyefahamika’ wakati huo Benjamin William Mkapa.

Kuibuka kwa wagombea wengi kiasi hicho ndani ya CCM kuliwafanya Watanzania waamini kwamba ile demokrasia iliyokuwa imefichwa kwa miaka mingi na utawala wa chama kimoja ilikuwa imeibuka na kukomaa. Wananchi sasa waliamini walikuwa na nafasi ya kumchagua mgombea yeyote waliyedhani anafaa badala ya kupewa karatasi ya kura yenye picha ya mtu mmoja na kivuli huku wakilazimika kupiga kura za ‘NDIYO’ au ‘HAPANA’.

Lakini pia kuibuka kwa wanaccm wengi kiasi hicho kulimpagawisha sana mtu mmoja; Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, ambaye aliamini kwamba hiyo haikuwa demokrasia tena bali chama kilikuwa kimevamiwa na kwamba kilikuwa na viongozi ‘wabaya’, ambao dhahiri aliwaona walikuwa na nguvu na wangeweza kupitishwa na chama kushika madaraka ya nchi.

Pengine kilichomshtua zaidi ni kule kuona Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, John Malecela, ambaye hakuwa amejitokeza mapema kama wenzake, akiibuka ghafla na kupata wadhamini 250,000 waliotakiwa huku akiungwa mkono na kundi kubwa la vijana na baadhi ya wazee.

Akiwa tayari ametajwa mapema kwamba alikuwa anakusudia kumpigia debe mgombea wa upinzani, Mwalimu Nyerere akawaonya wale wabaya ndani ya chama waliokuwa na nguvu kwamba; “Wasipotupatia mgombea mzuri, hawatutawali… Kama hawatuwekei mgombea mzuri, kwa nini watutawale?”

Nyerere aliona kabisa kwamba chama kilikuwa kimevamiwa na watu wenye fedha, ambao walikuwa tayari kumsimika ‘mtu wao’ kwa kutumia fedha hizo ambazo Mwalimu Nyerere aliwahi kuziita ‘fedha za bangi’, akimaanisha kwamba zilikuwa fedha chafu ambazo hata upatikanaji wake ulikuwa wa njia zisizo halali ndiyo maana walikuwa tayari kuzitumiza watakavyo ili kulinda ‘maslahi’ yao.

Lakini pia inaonekana Nyerere alishtushwa zaidi na kuibuka na vijana wawili ambao baadaye walikuja kupachikwa jina la ‘Boys II Men’; Jakaya Kikwete na Edward Lowassa, ambao wakati wa kurejesha fomu za kuwania kuteuliwa kugomea urais kule Dodoma walikodi ndege ya binafsi. Ni huko ambako tunaambiwa Mwalimu aliwahi kuwauliza wagombea, akiwemo Lowassa, ni wapi walikozipata fedha walizokuwa nazo.

Lakini majina yale yalipochujwa na Kamati Kuu ya CCM katika mchakato wa kwanza na kubaki matatu – Msuya, Mkapa na Kikwete – Nyerere alisikika akisema kwamba; “Rais bora angetoka CCM,” na akamtaja Ben Mkapa kwamba ndiye aliyekuwa bora zaidi kati ya wale watatu. Huyu mwingine wa mwisho, Kikwete, aliambiwa kwamba kura zake hazikutosha na kwamba asubiri mpaka kipindi kingine.

Mwalimu akamnadi Ben kila pembe ya nchi huku akisema “Mgombea wa CCM anauzika.” Aliweka matumaini makubwa kwamba mgombea huyo mara atakaposhinda na kutwaa madaraka angeweza kufuata falsafa zake na kujenga taifa lililo imara katika misingi ya haki, usawa, uadilifu na uwajibikaji.

Lakini kabla kampeni rasmi za kitaifa hazijaanza, wanaccm wengi wakatoka na kujiunga na vyama vya upinzani huku baadhi yao, akiwemo Augustine Lyatonga Mrema, wakionekana kuwa na mvuto mkubwa sana kwa wananchi.

Mwalimu akasimama kidete kuwaponda wagombea hao huku akitamka bayana; “I cant let this country to the dogs (Siwezi kuwaachia mbwa nchi hii),” kauli ambayo wapinzani waliifananisha na kashfa kwao kufananishwa na mbwa ingawa kihalisia Nyerere hakuwa amemaanisha hivyo.

Nyerere akashika hatamu za kampeni kwa nguvu zote akimpamba na kumsifu ‘mteule’ wake – Mkapa. Kwa kuwa tayari alikuwa amewaponda viongozi wengine wa serikali na chama kama Malecela na kolimba kwenye kitabu chake cha ‘Uongozi wetu na hatma ya Tanzania’, aliweza kuzibadili fikra za wananchi wengi ili wamshabikie mgombea wake.

Akawaponda wagombea wengine wa vyama vya upinzani waliokuwa kwenye mchakato huo akisema; “Mnakimbilia Ikulu, Ikulu kuna biashara gani pale? Mnataka kwenda kufanya nini Ikulu? Ikulu ni mahali patakatifu, si mahali pa mchezo mchezo pale. Ni mahali pa kuheshimika!”

Ndiyo. Kauli hizi na nyinginezo alizozitoa Mwalimu ziliwagusa wengi na wakaamini kwamba chaguo lake – Mkapa – lilikuwa sahihi mno. Mkapa, ambaye awali wengi walimkejeli kwamba hajulikani kimataifa tofauti na akina Warioba, Malecela na Msuya, sasa akawa maarufu hata kabla ya kuingia Ikulu.

Hizi ndizo falsafa za Mwalimu Nyerere ambazo zilisaidia Tanganyika ikapata uhuru wake kwa kutumia nguvu ya hoja. Alimudu kuiongoza Tanzania kwa miaka 24 si kwa sababu ya usomi wake na kuzungumza kwake, bali karama ya uongozi ilikuwa ndani yake.

Hata hivyo, kitu pekee ambacho hakukijua ni kwamba, miaka michache baadaye wale aliodhani wangefuata falsafa yake wakawa wamekengeuka na kuamua kuitia najisi Ikulu, sehemu takatifu ambayo Nyerere alipigania kuhakikisha hakiingii kilicho ‘kichafu’.

Yaliyofanyika pale Ikulu, ambayo kama leo hii Nyerere angekuwa hai, hakika angeweza kulia machozi, tena ya damu, kwa kuona kwamba kumbe juhudi zake za kuwapiga vijembe wengine waliotaka kupaendea mahali pale pa juu palipoinuka zikuwa bure kabisa hasa baada ya wale alioamini kwamba wangepaenzi kuamua kuyafanya yale yale aliyokuwa akiyakataza!

Leo hii Watanzania wengi walikuwa wanaombea walau Mwenyezi Mungu angempa uhai zaidi Mwalimu Nyerere wa kuweza “kumuona rais wa awamu ya nne” kama alivyokuwa amesema mwenyewe siku ile ya ‘birthday’ yake ya miaka 75 mwaka 1997, hakika angeweza kushuhudia ufisadi mkubwa ambao ulikuwa unafanywa na wale ambao aliamini wangeyafanya ‘mapenzi ya baba’.

Kilichotokea ni kama ule mfano wa wana wawili, ambapo mkubwa alitumwa na babaye aende shambani, lakini akakataa kwamba hatakwenda, lakini baadaye akabadili mawazo na kwenda. Mdogo akatumwa aende, akasema atakwenda, lakini baadaye hakwenda! Ni nani aliyeyafanya mapenzi ya baba kama si yule wa kwanza?

Mwalimu alikuwa amefanya kazi na wakongwe wengi ambao walijitokeza katika mchakato ule wa mwaka 1995, lakini kwa kuwa huko nyuma walikuwa wamekosea na kuona kwamba hawafai, akaamua kumpigia chapuo ‘mdogo wao’ Mkapa, ambaye ‘alimuahidi’ kwamba angekwenda kutekeleza yale aliyotumwa. Lakini kwa bahati mbaya zaidi, wale wakongwe ambao walikuwa wamekosea huko nyuma walikuwa wamejirekebisha na kuwajibika iwapasavyo, na yule ambaye aliaminiwa kwamba ndiye angeweza kutekeleza mapenzi ya Mwalimu, akafanya ndivyo sivyo.

Mwalimu Nyerere alifariki Oktoba 14, 1999, lakini kwa kudhihirisha kwamba mwanafunzi wake Mkapa alikuwa amemsaliti, tayari alikuwa ameanzisha kampuni ya kibiashara akiwa Ikulu, miezi mitatu na siku 22 kabla Mwalimu hajaaga dunia, yaani Juni 22, 1999 wakati Mkapa na mkewe mama Anna, wakati huo wakiwa madarakani, walipoanzisha kampuni ya ANBEM Limited. Kampuni hiyo ni kifupishi cha majina yao, yaani Anna na Ben Mkapa.

Wakati hayo yakitokea, tayari serikali ilikuwa imeshachafuliwa na kashfa kadhaa za mawaziri wa serikali ya awamu ya tatu, ambapo kwanza Waziri wa Fedha Profesa Simon Mbilinyi na naibu wake Kilontsi Mpologomyi walikuwa wamejiuzulu kutokana na kashfa ya misamaha ya kodi kwa mafuta na minofu ya samaki, Waziri wa Maliasili na Utalii Dk. Juma Ngasongwa alikuwa amejiuzulu baada ya kutajwa katika Tume ya Kero ya Rushwa ya Jaji Joseph Warioba kuhusiana na minofu ya samaki, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utawala Bora) Dk. Hassy Kitine alikuwa amejiuzulu kwa kashfa ya kumtibia mkewe nje ya nchi kwa mamilioni ya fedha za serikali kinyume cha utaratibu, na naibu waziri wizara ya fedha Monica Mbega alijiuzulu kwa madai ya kwenda kusoma, ingawa wachunguzi wa masuala ya siasa walikuwa wamehusisha kujiuzulu kwake na kashfa ya kuwapeleka ndugu zake kwenye mkutano wa dunia wa vijana jijini Lisbon, Ureno, ambako inasemekana walizamia moja kwa moja.

Tangu hapo viongozi waliokuwa Ikulu ya Tanzania wkaendelea kufanya biashara, tena wakitumia ofisi za serikali, ambapo tunaambiwa kwamba Julai 2002 kampuni ya ANBEM ilichukua mkopo wa Dola za Marekani 500,000 (takribani milioni 620/-) kutoka benki ya NBC, ambayo ilibinafsishwa kwa kuingia ubia na Benki ya ABSA ya Afrika Kusini pamoja na Mwalimu Nyerere, enzi ya uhai wake, kupinga kwa nguvu zote kwamba chombo hicho kisibinafsishwe. Mwezi Desemba ANBEM ikachukua mkopo mwingine wa milioni 250/- kutoka benki ya CRDB.

Miaka miwili baadaye tukashuhudia kuanzishwa ka kampuni nyingine ya Tanpower Resources (ilisajiliwa Desemba 29, 2004), ambayo taarifa za wachunguzi zinabainisha kwamba inamilikiwa na Rais mstaafu Benjamin Mkapa (wakati huo akiwa bado madarakani) na mkewe kupitia kampuni yao ya ANBEM Limited, motto wao Nicholas kupitia kampuni yao na mkewe Foster Mbuna iliyoanzishwa mwaka huo huo iitwayo Fosnik Enterprises Limited.

Wengine wanaotajwa kumiliki hisa za Tanpower Resources Company Limited ni pamoja na Waziri wa Nishati na Madini (wakati huo) Daniel Ndhira Yona na mwanawe Danny kupitia kampuni yao ya DEVCONSULT Limited (Yona ana hisa 90% kwenye kampuni hiyo na mwanawe ana 10%), baba mkwe wa Nicholas Mkapa, Joseph Mbuna, kupitia kampuni yake ya Choice Industries Limited, na kampuni ya Universal Technologies Limited inayomilikiwa kwa pamoja na Evans Mapundi na Wilfred Malekia.

Kampuni ya Tanpower Resources ambayo Machi 2006 iliingia mkataba na Tanesco wa kuzalisha umeme wa Megawatts 200 katika mgodi wa makaa yam awe wa Kiwira, mkoani Mbeya wenye thamani ya Dola za Marekani milioni 271.8 (takribani bilioni 340/-) mbali ya kuanzishwa na viongozi ambao walikuwa bado wako Ikulu, lakini pia inamilikiwa na familia, au kwa kifupi ni ya ukoo!

Lakini si hao tu, ziko kashfa nyingi zinazoendelea ndani ya serikali yetu ya sasa na ile iliyopita. Kwa mfano; inakumbukwa jinsi jinsi Benki Kuu ilivyoingia mkenge kwa kulipa mabilioni ya fedha kufidia deni la kampuni iliyoibuka ghafla na kufa ya Meremeta Gold Mine, ambayo ilirithiwa na kampuni ya Tangold.

Tunaambiwa kwamba kampuni ya Tangold, ambayo ilisajiliwa Aprili 2005 mjini Port Louis, Mauritius, ilikuwa inamilikiwa na viongozi wakubwa serikalini wakiwemo Gavana wa Benki Kuu Daudi Ballali, Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Gray Mgonja, Mwanasheria Mkuu wa wa Serikali (wakati huo enzi ya Mkapa) Andrew John Chenge, Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Patrick Rutabanzibwa na Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Mifugo Vincent Mrisho.

Ballali na Mgonja bado wanaendelea kuzishikilia nyadhifa zao mpaka sasa, wakati Rutabanzibwa ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Mrisho ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu.

Hakika haya ni matumizi mabaya ya madaraka kwa sababu ni kinyume kabisa na kanuni za maadili ya utawala bora na utumishi wa umma ibara ya 12 hadi ya 14, na kama Nyerere angalikuwa hai leo akaona namna wapendwa wake, wale aliowateua ‘wanywee kikombe cha bwana wao’, wanavyoyatumia vibaya madaraka yao, kwa kuwapora wananchi mkate wao.

Tuwafananishe na nani viongozi wa zama hizi basi? Tuwafananishe na Mfalme Daudi aliyemtwaa Baarsheba kuwa mkewe kutoka kwa Uria, ambaye aliamua kumuua ili amtwae moja kwa moja? Au tuwafananishe na Mfalme Nebukadneza wa Babeli aliyejitukuza na kujiona kama yuko karibu na Mungu kabla ya kufukuziwa porini kula umande kwa miaka mitatu na nusu kabla ya kutambua kwamba utawala wa wanadamu unawekwa na Mungu?!

Watawala hawa wameonyesha kumkosoa Mwalimu Nyerere kwa vitendo, kwamba kama alidhani Ikulu hakuna biashara, basi wao wameweza kuifanya, tena wakiwa hawana hofu wala woga wa aina yoyote, huku wakisimama majukwaani kusisitiza utawala bora.

Tunataka tuwe na watawala bora, lakini viongozi wa aina hii ambao wanaonekana kuinajisi Ikulu na ofisi za umma hakika wanapandikiza mbegu mbaya kwa vijana wetu, ambao nao wanaendelea kuiga mle mle walimopitia wazee wao na kuzidi kulifanya taifa hili kuwa la watu wasiokuwa makini, ambao ufisadi kwao ni kama kitu kilichohalalishwa.

Laiti kama Nyerere angefufuka leo na kuona jinsi alivyosalitiwa, hakika angeifuta kauli yake kwamba wale aliodhani ‘mbwa’ walikuwa bora zaidi kuliko hawa!

Mwisho.
THIS IS WHAT MEN DO WANT!

BROTHER DANNY

Women often say that men confuse them and that they are unsure what a man is really looking for. They have tried to please them in the past and it hasn't worked so now, the man can concentrate on pleasing them or leave. If the media is to be believed, many women don't care what a man is looking for anymore because they have been empowered by their own sexuality and are comfortable in their new role as sexually liberated career woman in charge of their own destiny. In which case, as long as the man wants them, that is fine.

It doesn't matter whether that view is actually true or not. What is true is that the modern man is increasingly struggling to find his place in the world. The old male bastions are crumbling and with them their innate self respect as well as their understanding of how they should act and what they desire.

Any woman reading this may say well it's a problem for men and they should deal with it. Absolutely I can reply, but you cannot expect miracles instantly. Generations of history dictating a man's role and function cannot be decided and altered in the space of 20 years without some fallout. Few can argue against the excitement felt by women as their empowerment continues but at the same time, one must expect issues to coincide with this. And one of those as I said is the question of understanding what the modern man is looking for.

Men have started to evolve and are starting to grasp the fact that their role may not be as it once was. 'Starting' is the operative word because this does not mean that there aren't large swathes of the world where men insist on being the breadwinner and women should still remain at home rearing children. It is going to take a long time to change the world.

Okay so what does a man want? First of all a man is seeking a love-interest. This may surprise many women but men like to love and they like being loved in return. The problem is that many women come across as impassioned and cold. It is not easy to find a loving woman and it is very noticeable how many men try and hang on when they think they have found their Miss Right.

Men are seeking a woman who is attractive to them. Women may despair that men can be so shallow and that looks could matter so much but be careful. Men aren't necessarily looking for a catwalk model and many men don't like women who weigh 60kgs. But men do want a woman who takes pride in their appearance (though not excessively). Men are proud of having a girlfriend who looks good and I don't believe any man who says otherwise.

Men are looking for a trustworthy girl, someone they can have faith in and someone who will be there for them. This may sound like an odd thing to say, but the fact is, some women are not trustworthy and many are not faithful either. So many in fact that men are increasingly wary. A man can never forgive a woman being unfaithful and so he is looking for someone who he really does trust.

Men want to make a home eventually and are looking for a woman who will be a willing sharer in home life. Women with a sociable lifestyle are attractive because they can be relied upon to keep the social diary running in a long term relationship.

Men are seeking women who are feminine gentle and kind because deep down the qualities that make a woman a great mother are an attraction in themselves. I am not suggesting that the man himself needs mothering, though some do, it is more the point that men seek the attributes in women that point to someone who would make a great mother to future offspring.

Men want women with a great sense of humour. Women often come across as uptight or too bothered by too many small details. You will sometimes hear mention of a girl who is 'one of the boys'. What this means is that she is able to fit in with their humour and is sociable and fun to be with. Such women are extremely attractive to many men. Men want to have a good time and relax when not working and so their ideal partners are women who are able to do the same.

Men are looking for women who retain their femininity and are caring and kind. In recent years, aping men may be a female fashion statement, but it doesn't make them attractive. Whilst every woman in the world burps and farts and has the right to drink pints of beer, it doesn't necessarily attract them to the opposite sex. Women can get angry and say well men will just have to get used to it, but the issue is that they don't. They can just choose not to go for women who act in the same way as their drinking buddies.

Men want someone who is supportive. Many women are quick to criticize men in their behaviour, career and set about trying to alter them and mould them. This is a crucial mistake. Men can be manipulated yes, but they see their partnerships as support systems. The best relationships work both ways in terms of support. Where a woman is not able or willing to give that support and is too quick to criticize then she may lose her man.

Men love a challenging woman, someone who keeps them on their toes. Men are generally lazy in relationships once they feel they're in secure territory. When a man is challenged so he does something about it. If you want to keep your man interested, keep him challenged.

Men are generally more reserved about sex than women. Men know what they like in bed and tend to stick to it. The adventurous sexual appetite in most men isn't there even if they are convinced it is. Men in reality are quite conservative. Sexually adventurous has nothing to do with having lots of partners and more to do with the things they will try with the same partner.

Men want a woman who will commit to them. Though increasingly this is hard to find, it doesn't take away the wish. Men want a girlfriend who they can share with and trust and be open with. Commitment is not a one way street and therefore men are struggling to find the levels of commitment they found previously. But the need is still there. Men don't want to be alone.

I think, for today, let me end here until next weekend. Let me wish you good weekend with your loved ones.

ENDS

JUST ANOTHER THOUGHT

JUST ANOTHER THOUGHT

A person asked God, “What surprises you most about mankind?”

And God answered,
“That they loose their Health to make money and they loose their money to restore their Health.

That by thinking anxiously about the future, they forget the present, such that they live neither for the present nor the future.

That they live as if they will never die and they die as if they had never lived.….”

BECAUSE I'M A MAN...

Because I’m a man, when one of our appliances stops working I will insist on taking it apart, despite evidence that this will just cost me twice as much once the repair person gets here and has to put it back together.

Because I’m a man, I don’t think we’re all that lost, and no, I don’t think we should stop and ask someone. Why would you listen to a complete stranger I mean, how the hell could he know where we’re going?

Because I’m a man, there is no need to ask me what I’m thinking about. The answer is always either sex or football, though I have to make up something else when you ask, so don’t.

Because I’m a man, I do not want to visit your mother, come visit us, or talk to her when she calls, or think about her any more than I have to. Whatever you got her for mother’s day is okay, I don’t need to see it. And don’t forget to pick up something for my mommy, too!

Because I’m a man, I am capable of announcing, “one more beer and I really have to go”, and mean it every single time I say it, even when it gets to the point that the one bar closes and my buddies and I have to go hunt down another. I will find it increasingly hilarious to have my pals call you to tell you I’ll be home soon, and no, I don’t understand why you threw all my clothes into the front yard. Like, what’s the connection?

Because I’m a man, you don’t have to ask me if I liked the movie. Chances are, if you’re crying at the end of it, I didn’t.

Because I’m a man, yes, I have to turn up the radio when Bruce Springsteen or The Doors comes on, and then, yes, I have to tell you every single time about how Bruce had his picture on the cover of Time and Newsweek the same day, or how Jim Morrison is buried in Paris and everyone visits his grave. Please do not behave as if you do not find this fascinating.

Because I’m a man, I think what you’re wearing is fine. I thought what you were wearing five minutes ago was fine, too. Either pair of shoes is fine. With the belt or without it looks fine. Your hair is fine. You look fine. Can we just go now?

Because I’m a man and this is, after all, the 90’s, I will share equally in the housework. You just do the laundry, the cooking, the gardening, the cleaning, and the dishes. I’ll do the rest.

A SIMPLE GUIDE TO LIFE

1. Follow your dream! Unless it’s the one where you’re at work in your underwear during a fire drill.

2. Always take time to stop and smell the roses and sooner or later, you’ll inhale a bee.

3. Do not walk behind me, for I may not lead. Do not walk ahead of me, for I may not follow. Do not walk beside me, either. Just leave me alone.

4. If you don’t like my driving, don’t call anyone. Just take another road. That’s why the highway department made so many of them.

5. If a motorist cuts you off, just turn the other cheek. Nothing gets the message across like a good mooning.

6. When I’m feeling down, I like to whistle. It makes the neighbor’s dog run to the end of his chain and gag himself.

7. It’s always darkest before dawn. So if you’re going to steal the neighbor’s newspaper, that’s the time to do it.

8. A handy telephone tip: Keep a small chalkboard near the phone. That way, when a salesman calls, you can hold the receiver up to it and run your fingernails across it until he hangs up.

9. Each day I try to enjoy something from each of the four groups: the bonbon group, that salty-snack group, the caffeine group and the “What ever-it-is-the-tinfoil-in-the-back-of-the-fridge”.

10. Into every life some rain must fall. Unusually when your car windows are down.

11. Just remember: You gotta break some eggs to make a real mess on the neighbor’s car!

12. When you find yourself getting irritated with someone, try to remember that all men are brothers and just give them a noogie.

13. This morning I woke up to the unmistakable scent of pigs in a blanket. That’s the price you pay for letting the relatives stay over.

14. It’s a small world. So you gotta use your elbows a lot.

15. Keep your nose to the grindstone and your shoulder to the wheel. It’s a lot cheaper than plastic surgery.

16. This land is your land. This land is my land. So stay in your land.

17. Love is like a roller coaster: When it’s good you don’t want to get off, and when it isn’t, you can’t wait to throw up.

DEDICATION TO YOUNG PEOPLE

Youth is a time of hope. Also of uncertainty. But for a person who is young and healthy, uncertainty just means a challenge. It is important to be positive. First of all about yourself. But also about your family and your people. As a unique person and each human being are unique, you have enormous potential. Because you have so much potential, people may sometimes feel negatively challenged by that potential and try to undermine it.

You have to fight for your right to make your place in society. To do that you have to use all the chances given you now to be a positive element in whatever situation you find yourself in, in future. So, it may be necessary to be a ‘rebel in reverse’ as it were. That takes real courage, to set your goal and stick to it. You choose your crowd. You exercise your right to choose.
Don’t lose your freedom for the sake of anyone. Real freedom, freedom to choose the right thing, the best for you.

Always bear a few things in mind while exercising your right to choose.

* Never take a decision when you are in a fit of anger or depression.
* Never take a decision when you are emotionally high.
* Why should fads or the decision of the group tie you down?
* What are you?
* What do you want tomorrow to be for you?

No matter how strong the group decision may be, you must think and make your decision. Many times it is necessary to consult before taking a decision. Go to someone whose life you admire, not necessarily the person you like most, but the person who is whole, who is one person, wherever she or he is and whatever she or he does.

* Remember that there is always tomorrow, and tomorrow is hope. Very few things are ‘written in stone’. Most of the mistakes we make can be rectified. They can be corrected. Problems have a solution, and each new day is a new start, a new chance, a New Hope. Indeed the youth are our hope you are our future.

Also remember that your parents love you unconditionally, you have their support and want the best in life for you ¨

COSTA VICTOR NAMPOKA

Mguu ulivyokatisha ndoto za kucheza soka Ulaya

DANIEL MBEGA
Dar es Salaam

NI majira ya saa 5.20 hivi asubuhi, niko hapa Ukonga-Banana nikiwania kupanda daladala la kwenda kwenye kitongoji cha Kitunda-Kibeberu, moja ya vitongoji vinavyokua kwa kasi hapa jijini Dar es Salaam.
Sijui ni umbali gani kutoka hapa, hivyo namuuliza dereva ambaye nimeketi naye pembeni yake. Ananiambia ni mwendo kama wa dakika 15 tu hivi. Nashusha pumzi kwa kujua kwamba kumbe si mbali sana kama nilivyofikiria.
Nawasili kwenye kitongoji cha Kibeberu, ambako ndiko magari yanakogeuzia, na bila kupoteza muda nampigia simu mwenyeji wangu kwamba tayari nimeshafika. Namhurumia huko aliko kama ataamua kuja kunipokea, lakini nafarijika anaponiambia kwamba nimuulize mtu yeyote hapo kituoni atanileta.
Watoto wawili wanajitolea kunipeleka nyumbani kwa mwenyeji wangu, ambaye namkuta akiwa kajilaza kwenye kochi akizungumza na rafiki zake wawili waliomtembelea. Anapenda kuketi vizuri, lakini hali haimruhusu.
“Poleni jamani kwa safari ndefu!” ndivyo anavyoanza kusema huyu mwenyeji wangu, ambaye si mwingine zaidi ya mlinzi mahiri wa timu ya soka ya Taifa, Taifa Stars, pamoja na klabu ya Simba, Costa Victor Nampoka ‘Nyumba’. Anajaribu kuuweka vyema mguu wake wa kulia ambao bado umefungwa bandeji gumu (POP) baada ya kuvunjia mazoezini takribani mwezi mmoja na nusu uliopita.
“Hakuna shaka, Dar es Salaam ni moja na hakuna sehemu unayoweza kusema ni mbali,” namjibu kumpa matumaini.
“Hapana! Pamoja na ukweli kwamba mkoa kazini, lakini naamini uamua kufunga safari mpaka kuja kuniona ni jambo kubwa sana. Mngeweza hata kuniuliza maendeleo yangu kwa njia ya simu. Sina budi kushukuru kwa kuja kunijulia hali,” anasema.
Mara anaingia dada mmoja mweupe hivi ambaye anaketi pamoja na Costa kwenye kochi moja. Costa mwenyewe anamtambulisha kwamba ndiye mkewe, Dina, ambaye wamebahatika kuzaa naye watoto wawili; Victor Costa mwenye miaka miwili na Rio Costa mwenye mwaka 1.5. Anatukaribisha.
Anapoondoka namwambia ni jambo la kawaida kuwatembelea wagonjwa, na katika suala lake yeye ni mmoja wa watu waliotoa mchango mkubwa katika timu ya taifa ya soka ambayo sasa iko katika nafasi nzuri ya kufuzu kwa fainali za Mataifa ya Afrika mwakani ikiwa tu itashinda mechi yake ya mwisho.
“Nashukuru kusikia hivyo, lakini sura zinazokuja hapa daima ni zile nilizozizowea, yaani marafiki zangu na wachezaji wenzangu wa klabu ya Simba, labda na viongozi wa Simba,” anasema kwa huzuni.
“Una maana kwamba viongozi wa timu ya taifa na hata TFF huwa hawakutembelei?” nauliza.
Anasema tangu alipoumia siku tatu kabla ya Taifa Stars kupambana na Zambia katika mechi ya kirafiki na kupelekwa Muhimbili na daktari wa timu Shecky Mngazija, hajatembelewa wala kujuliwa hali hata kwa simu na kiongozi yeyote yule wa chombo hicho cha juu cha soka nchini.
Anaongeza kwamba, ni wachezaji wenzake wa Simba ndio baadhi yao huwa wanawasiliana naye pamoja na viongozi na marafiki wa klabu ambao wameonekana kumjali vya kutosha kiasi cha kutuma gari kila siku katika mechi zote ambazo Simba ilicheza kwenye hatua ya Sita Bora ya Ligi ya Mpito hadi fainali.
“Kwa kweli viongozi wa klabu yangu wananijali sana na sina budi kuwashukuru,” anasema. Kama vile amekumbuka kitu, anasema anamshukuru pia mtu mmoja wa Benki ya NMB anayeitwa Kajura (Imani Kajura ambaye ni Meneja Masoko).
“Huyu jamaa baada ya kutoa zawadi za shilingi 500,000 kwa kila mchezaji kutokana na timu ya Taifa kushinda kule Burkina Faso, alinipigia simu kuniambia nilitakiwa kwenda kusaini fomu za akaunti. Nikamwambia sina hata pesa ya nauli na kwa jinsi ninavyoumwa nisingeweza kupanda daladala, lakini akaniambia nichukue teksi nay eye angelipa. Namshukuru sana,” anasema.
Hata hivyo, amewaasa wachezaji wengine; wa klabu na hata timu ya taifa, kwamba pindi watakapoumia na kushindwa kujuliwa hali na viongozi wao wasife moyo bali hiyo iwe changamoto kwao kufanya vizuri watakaporejea uwanjani.
“Binafsi sina kinyongo na yeyote. Naomba Mungu nipone nirejee uwanjani, ikibidi niliwakilishe taifa langu, kwa sababu natambua kwamba timu ya Taifa ni ya Watanzania wote wala si ya mtu mmoja. Naamini Watanzania milioni kadhaa wako pamoja na mimi na hata walipojua kwamba nimeumia walinitumia meseji za pole zaidi ya 3,000, hata sijui walikoipata namba yangu,” anasema.

Kuvunjika mguu
Costa anasema kwamba walikuwa kwenye mazoezi kama kawaida kwenye uwanja wa Karume, akauzuia mpira bila kumkwatua ama kukwatuliwa, kisha akaserereka.
“Ghafla nikasikia maumivu makali sana, ikabidi wajaribu kuniganga pale, lakini yalipozidi wakanikimbiza Muhimbili. Huko nikaambiwa kwamba nimevunjika mfupa mdogo wa mguu wa kulia. Sikuwa na jinsi, wakanifunga hogo (bandeji gumu – POP) na kusema kwamba nirudi baada ya wiki sita,” anasema kwa majonzi.
Anasema kwamba, baada ya kutolewa kwa bandeji hilo ndipo atakapojua kama atakuwa nje ya uwanja kwa muda gani, kwani mpaka sasa hajaanza hata kuukanyangia mguu huo.
Akasema kuvunjika mguu kumemnyima nafasi ya kuliwakilisha taifa, na zaidi kumechelewesha kutimia kwa ndoto zake kwani pengine hivi sasa angeweza kuwa Afrika Kusini kujaribu kucheza soka ya kulipwa akiwa njiani kwenda cheza Ulaya.
“Kuna wakala mmoja ambaye kwa muda mrefu sasa amekuwa akinufuatilia, yuko Afrika Kusini, na alikwenda Burkina Faso kunitazama, lakini mimi sikuwepo. Ilikuwa niende Afrika Kusini kufanya majaribio na naamini ningewea kufanikiwa,” anasema mchezaji huyo.
Anasema kwamba, alikuwa na matumaini ya kufuzu kwa sababu soka ya Afrika Kusini haina tofauti na ya huku, tena hakuwa mgeni baada ya kucheza kwa muda nchini humo miaka mitatu iliyopita.
“Wanachotuzidi kule ni promosheni, televisheni zinajitahidi sana kuonyesha mpira hata wa daraja la tatu, na hiyo inamsaidia mchezaji kutazama na kuona wapi alipokosea ili kujirekebisha, ama afanye nini kuongeza jitihada,” anasema.
Anaongeza kwamba alishindwa kuendelea kucheza huko kwa sababu klabu aliyokuwa akiichezea wakati ule ya Marlasburg (Tembas) iliyokuwa daraja la kwanza mwaka 2005 ikiwa chini ya kocha wa zamani wa Simba Trott Moloto, iliinunua klabu moja iliyokuwa ligi kuu. Ikabidi wachezaji wa timu hizo wachekechwe, na majungu ndipo yakaibuka ambapo Moloto, ambaye ndiye aliyemfanyia mpango wa kwenda huko, akamgeuka. Ikabidi afungashe virago kurejea.
Hata hivyo, anasema kwamba ndoto zake bado hazijafutika, kwani anaamini anaweza kucheza Ulaya bila matatizo yoyote, na zaidi anasema angependa siku moja avae ‘uzi’ wa Manchester United akicheza pembeni ya Rio Ferdnand ambaye uchezaji wake unamvutia kiasi cha kumwitia mwanawe mdogo jina hilo kutokana na kumhusudu.
Akizungumzia nafasi ya Taifa Stars kufuzu kwa fainali za Mataifa ya Afrika mwakani, Costa (25) ambaye ni mtoto wa nne katika familia ya watoto watano wa mzee Victor Nampoka – wawili wanawake na watatu wanaume, anasema kwamba nafasi ipo, lakini mechi ya mwisho dhidi ya Msumbiji ni ngumu sana.
“Ile mechi ni kama fainali na inabidi maandalizi ya nguvu yafanyike pengine kuliko mechi zote zilizotangulia. Msumbiji ni wazuri sana kuliko hata Burkina Faso, na ina nafasi ya kufuzu ikiwa itashinda na Senegal wakafungwa, hivyo Watanzania tusibweteke bali tujiandae vizuri,” anasema huku akisikitika kwamba anaweza kuikosa mechi hiyo pia ikiwa ataambiwa apumzike.
Akizungumzia kuhusu maendeleo ya soka, mlinzi huyo anasema kwamba hakuna kitakachoinua zaidi ya soka la vijana, na kuongeza kwamba mashindano ya Copa Coca Cola yawe chachu wa klabu na wadau mbalimbali kuanza kuibua vipaji.
“Kule Brazil tulikokwenda kuna taasisi ya soka ya watoto wadogo. Watoto wanatoka nchi mbalimbali kwenda kufundishwa mpira, na wazazi wao wanalipia wastani wa dola 1,500 kwa mwezi ili watoto wao wajue mpira. Tusione wenzetu wamepiga hatua tukadhani kwamba ni miujiza, wamewekeza.
“Watanzania wanapaswa kuunga mkono juhudi za maendeleo ya soka ya vijana, kuanzia kwa wazazi, ambao wanapaswa kuwapa ‘sapoti’ watoto wao ikiwa ni pamoja na kuwapatia vifaa vya michezo na nauli ya kwenda mazoezini,” anaongeza.
Costa aliyemaliza elimu ya msingi mwaka 1994 Kinondoni Hananasif, jijini Dar es Salaam na kuungana na maelfu ya watoto ambao hawakufanikiwa kuchaguliwa kujiunga na sekondari, amewashauri wachezaji kuachana na anasa na kwamba wawe na malengo kama kweli wanataka kupiga hatua katika mchezo huo.
“Sijafanikiwa sana, lakini niseme ukweli kwamba nimejiepusha na mambo mengi. Sivuti sigara wala bangi, halafu niliacha kitambo kunywa pombe, tena basi nilikuwa nikinywa bia mbili ama tatu tu, lakini sasa sitaki kabisa nahitaji kukazana kwenye mpira ambao pekee ndio mwokozi wangu katika maisha,” anamalizia.

Wasifu:
Jina: Costa Victor Nampoka
Kuzaliwa: Oktoba 11, 1982, Dar es Salaam.
Umri: 25

Klabu za awali:
Five Star Kinondoni, Mkunguni FC Ilala, Eleven FC Buguruni, Saddam FC na International FC za Kinondoni.
Taifa Jang’ombe – Zanzibar (1998 – 1999)
Forodha Zanzibar (2000 – 2001)
Mtibwa Sugar (2002)
Simba (2003 – 2004)
Marlsburg – Afrika Kusini (2005)
Simba (2006 – mpaka sasa).