Friday, August 10, 2007

MIUNGU-WATU

MIUNGU-WATU

DANIEL MBEGA

“UMESEMA umeamua kuja kwangu? Unadhani ni kwa nini umefikiria kwamba kesi hii inahusika ama inahusiana na ofisi yangu?” Inspekta Muhogo Mchungu, mkuu wa Kikosi Maalum cha Usalama alimuuliza Daktari Idrissa Mhando kwa mara nyingine. Inspekta Muhogo Mchungu alikuwa amesahau kabisa kama swali hilo lilikuwa limejibiwa mara mbili, tena kwa kina kabisa.
Kilichomchanganya zaidi afande huyo ni kule kumuona daktari huyo bingwa wa magonjwa ya akili katika Hospitali ya Rufaa ya Taifa ya Muhimbili akiwa kachanganyikiwa. Kwa kumtazama haraka haraka ungeweza kusema kuwa ni yeye daktari ambaye sasa ndiye aliyekuwa na ugonjwa wa akili wala siyo wagonjwa wake aliowaacha wodini.
Muhogo Mchungu alikuwa askari mwenye msimamo, asiyependa kuchukua maamuzi ya haraka bila kutafakari kwa kina, lakini katika suala hili ambalo lilikuwa limeibuliwa na daktari huyu aliyekikataa hata kiti alichokaribishwa, aliona hakuwa na muda wa kufanya maamuzi. Lakini ni maamuzi gani ambayo alipaswa kuyafanya katika kipindi kifupi kama hicho na katika suala tete kama hilo? Ndilo swali kubwa lililokuwa likimtatiza afande huyo kiasi cha kusahau kama alikuwa amepewa maelezo ya jinsi kadhia hiyo ilivyostahili kuripotiwa katika ofisi yake.
Hali ya furaha aliyokuwa nayo muda mfupi uliopita sasa ilikuwa imemezwa na wahaka. Alikuwa na uhakika kwamba kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi na Idara ya Usalama wa Taifa, tayari taifa lilikuwa limefanikiwa kwa kiasi kikubwa kupunguza wimbi la uhalifu, hasa ujambazi wa kutumia silaha. Tayari Jeshi hilo lilikuwa limetoa pikipiki nyingi na kutawanya askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) wenye silaha kila mahali kuhakikisha kwamba wanakabiliana kivitendo na wahalifu wote nchini.
Lakini wakati akisherehekea ushindi huo kimoyomoyo, jambo jingine kubwa na lenye utata linaibuka. Hapana, aliona kama ni masikhara Fulani yaliyofanywa na daktari huyo ili kuja kuichafua siku yake. Alihisi kama kukaa kwake na wagonjwa wa akili muda mwingi kulikuwa kumemfanya naye akili zake zipungue ama zifanane nao. Si kuna vipindi ambavyo madaktari hao bingwa wa akili huwachorea wagonjwa wao picha ya mlango na kuwataka wapitie kwenye mlango huo aliouchora katika hali tu ya kupima kama wamepona ama la?! Lakini mbona Inspekta hakuwa mgonjwa, au ni utani mwingine uliokuwa umeibuka ama ni mbinu ya daktari huyo kutaka kuwachunguza hata maafisa wa jeshi kama walikuwa na matatizo ya akili au la? Akamtazama na kumkazia macho.
Daktari huyo, ambaye alikuwa ametahadharishwa kuhusu Inspekta Muhogo Mchungu jinsi alivyo, alipatwa na hofu kidogo, lakini hakupepesa macho yake. Alikuwa ameambiwa jinsi afande huyo alivyo na msimamo mkali katika utendaji wake wa kazi.
“Ni kweli afande. Kama nilivyoeleza awali, tukio hili linaonekana ni la ajabu na nimeona kwamba ofisi yako ndiyo pekee inayoweza kulitatua,” Dk. Idrissa Mhando akasema huku akingali amesimama.
“Enhe? Hebu rudia tena kunieleza…” Inspekta akarai huku akiketi vyema kwenye kiti chake. Safari hii Dk. Mhando pia aliketi.
“Kama nilivyosema, afande,” Dk. Mhando alisema baada ya kulisafisha koo lake kwa kikohozi chepesi. “Ni matukio ya kushangaza sana, kwamba katika kipindi cha siku tatu tumeshapokea wagonjwa kumi na mbili ambao wote wanaonekana kuwa na ugonjwa unaofanana. Awali tulihisi kwamba wana matatizo ya akili, lakini baadhi yao, kama si wote, tumechukua historia zao na kugundua kwamba hazina matatizo yoyote.”
“Kwa nini unasema hivyo? Historia zao hazina matatizo yoyote, una maana gani?” Inspekta Muhogo Mchungu akauliza sasa akiwa anasikiliza kwa makini.
“Watu hawa, Inspekta, hawajawahi kushikwa na ugonjwa wa akili tangu wazaliwe,” akasema Dk. Mhando.
“Unataka kusema kwamba mtu hawezi kupata wazimu katika utu uzima?”
“Anaweza kupata, Inspekta, lakini katika kesi hizi, tunahisi kwamba kuna zaidi ya wazimu. Kwanza tulidhani wana malaria ambayo yamepanda vichwani. Kweli walikuwa na malaria, lakini siyo makali kiasi cha kusababisha ukichaa. Ndipo tulipofikiria uwezekano mwingine wa hali hii…”
“Enhe? Upi huo?”
“Kwamba yawezekana wameleweshwa dawa za ulevya!”
Sasa Inspekta Muhogo Mchungu akaanza kupata picha. Alikuwa anaelewa kwamba kichaa halisi si yule wa kuzaliwa, bali yule anayetumia dawa za kulevya.
“Dokta, nadhani ninyi nyote ni wataalamu na mnaweza kupima na kujua kama kweli wanatumia dawa za kulevya au vipi. Sasa iweje ukimbilie kwangu? Unadhani ninaweza kuwa na msaada wowote?”
Dk. Mhando aligundua namna alivyokuwa na kazi nzito ya kumweleza Inspekta huyo ingawa kwa hakika mazungumzo hayo yalikuwa yamemvutia sana Inspekta na moja kwa moja lilikuwa ni jukumu lake kuchunguza. Hata hivyo, ilitakiwa kazi ya ziada kwa dokta ili kuifanya safari yake iwe na mafanikio, kwani matokeo yote ya uchunguzi yalikuwa yamefanyika kwa siri sana, yeye mwenyewe akiwa ameufanya uchunguzi huo bila mtu yeyote kujua.
“Tumepima kila kitu. Damu zao zilionyesha kuwa walikuwa wametumia dawa za kulevya, lakini mkanganyo zaidi ukatokea, kwamba watu hao hawajawahi kuvuta sigara katika maisha yao, na wengine hawayajui madawa hayo.”
“”Dokta usiwe na uhakika kiasi hicho, wengine ni waongo, wanaweza kuwa wanatumia lakini baada ya kuona mambo yamewazidi kimo wameamua kuja kwenu. Wengine wanaweza kuwa wametiliwa dawa hizo kwenye chakula, vinywaji na kadhalika. Nadhani unaielewa hiyo,” Inspekta Muhogo Mchungu akasema.
“Kote huko tumechunguza, baadhi ya wagonjwa hawajihusishi na vitendo vyovyote viovu… yupo na Mchungaji mmoja wa Kanisa la Mungu. Lakini kuna kitu kimoja ambacho kinanichanganya…”
“Kitu gani hicho!?” Inspekta akauliza akisikiliza kwa makini zaidi.
“Tuna mashaka na dawa walizotumia.”
“Dawa? Dawa gani hizo?”
“Ni dawa za kutibu malaria. Kwani hawa wote wanaonekana kama walitumia dawa za aina moja ambazo ndizo zilizowaletea matatizo haya. Zinaitwa Paranoxyquine,” akasema Dk. Mhando huku akishusha pumzi kuona ameutua mzigo mzito uliokuwa umemuelemea.
“Paranoxyquine? Ni dawa gani mbona sijawahi kuisikia?”
“Ni dawa mpya. Lakini hapa nchini imeingia yapata mwaka sasa. Ni dawa yenye nguvu ambayo inatibu sana malaria, na hasa malaria sugu.”
“Imekuja muda mrefu, umesema?”
“Ndiyo, ina mwaka mmoja hivi. Matokeo yake yamekuwa mazuri kwa sababu ina nguvu zaidi ya Cotexcine na Alnate na imethibitishwa na Tume ya Udhibiti wa Dawa za Binadamu, Wizara ya Afya, Shirika la Viwango, na zaidi imethibitishwa na Shirika la Afya Duniani kwamba inafaa kutumika katika nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara ambako malaria imeonekana kuwa tatizo sugu na ugonjwa hatari zaidi hasa kwa watoto.”
“Sasa kama unasema dawa hiyo inatibu vizuri, iweje useme kwamba una mashaka nayo?”
“Ninahisi kwamba huenda kuna vitu zaidi ya dawa zenyewe, yaani inawezekana dozi waliyopewa ni ile ile lakini zenyewe ndani zina walakini.”
Inspekta Muhogo Mchungu tayari alikwishahisi kwamba kuna jambo, lakini kama ilivyo kazi ya uchunguzi, usitoe majibu kama chanzo bado kinaendelea kutoa maelezo yanayohusiana na kadhia husika. Hivyo akaendelea kumsaili. Yeye alikuwa amechaipata picha halisi na kuhisi kama kulikuwa na hujuma Fulani nanndiyo maana daktari huyo akaamua kumwendea yeye kwa matumaini kwamba kikosi chake kingeweza kupeleleza na kupata ufumbuzi wa suala hilo.
“Ni mwaka sasa tangu dawa hizi ziingie nchini, je, mmeshawahi kupata kesi kama hizi?” Inspekta akauliza.
“Hapana. Hii ndiyo mara ya kwanza…”
“Sasa dokta hapo ndipo unaponishangaza. Umesema dawa zimethibitishwa na vyombo mbalimbali, tena kwa kipindi chote hamjawahi kupata wagonjwa wa aina hiyo. Huoni kama unazunguka pale pale ulipo?”
“Ndiyo maana nimesema kwamba nahisi kama kuna kitu Fulani, kama hujuma vile. Unajua haya mambo ya utandawazi na soko huria limefanya watu wengi wavamie hata kazi zisizowahusu. Nahisi dawa hizi zina matatizo, au niseme bayana kwamba, yawezekana kuna baadhi ya watu wameamua kuingiza dawa zilezile lakini zikiwa ni hatari.”
“Mmepata baadhi ya dawa walizokuwa wakitumia watu hao? Yaani zilizobakia ambazo pengine mmezifanyia uchunguzi?” akauliza Inspekta.
“Ndiyo, Inspekta. Tumezipata na tumegundua kwamba hizi siyo zile dawa zinazotibu malaria, bali ni dawa za kulevya aina ya heroin ambazo zimetengenezwa katika umbile la vidonge vidogo kama vile vya Paranoxyquine halisi na kuwekwa katika pakti halisi. Kumbuka kwamba dawa hizi ni ghali sana kwani dozi ya vidonge vinne inauzwa kwa shilingi 25,000,” Dk. Mhando akasema huku akitoa sampuli ya dawa hizo, zile halisi na zile zilizosadikiwa kuwa ni za kulevya.
Inspekata Muhogo Mchungu alizitazama na kushindwa kuona tofauti hadi pale alipoelekezwa kwamba ipi ni halisi na ipi si halisi. Akili yake sasa ikaanza kuchemka. Tayari alikwishahisi kwamba nchi imevamiwa na wahujumu uchumi ambao walikuwa hatari zaidi pengine kuliko hata majambazi. Aliamini hivyo kwa sababu kama dawa hizo zingeenea nchini kote, kulikuwa na uwezekano mkubwa kwamba baada ya muda mfupi nchi ingekuwa na wendawazimu. Watu wangetumia dawa za kulevya bila hiyari yao.
“Mmepata mahali walikozinunua dawa hizi?” akauliza,
“Kati ya ndugu wa waathirika hao ni mmoja tu aliyeweza kujua mahali zilikonunuliwa. Wengine wote hawakujua, kwani walisema kwamba ndugu zao walirejea nyumbani wakiwa na dawa hizo na kuanza kuzimeza.”
“Huyo aliyeweza kujua, amesema alizinunua wapi?”
“Kuna duka moja liko Kariakoo hapa hapa Dar es Salaam, linaitwa Quick Pharma. Lakini nilikwenda pale na kununua paketi mbili ambazo baada ya kwenda kuzichunguza zote zimeonekana kuwa hazina kasoro.”
“Unadhani ni kweli? Kwani hizo zilinunuliwa lini?”
“Juzi, na dawa alizonazo huyo mwenye duka zimeingizwa nchini tangu mwezi jana.”
“Sawa sawa, sasa tunaweza kwenda kuwaona wagonjwa wako ili tujue wako katika hali gani?” Inspekta alisema.
“Hakuna shida, itakuwa ni vuziri. Lakini Inspekta…” Dk. Mhando akasema akisita.
“Enhe? Nini tena?”
“Ningeshauri kwamba mimi nitangulie halafu ninyi mje baadaye. Nimekuja kwa siri sana, hakuna anayejua, na ningependa niondoke kwa siri na haya mazungumzo yaendelee kuwa siri vile vile. Nahofia kwamba kama kuna wahujumu, basi wanaweza kuwa na mkono mrefu,” Dk. Mhando akasema kwa mashaka makubwa.
“Sawa sawa, nimekuelewa. Wewe tangulia, lakini wakati wowote ukiwa na shida ya haraka nipige moja kwa moja mimi,” alisema na kumpatia kadi yake maalum. “Hii ni namba yangu ya moja kwa moja na ni wachache sana walionayo.”
Inspekta Muhogo Mchungu alimtazama daktari huyo akiufunga mlango nyuma yake. Hapo hapo akainua mkono wa simu na kumpigia Kachero Ismail Bondo, ambaye alikuwa na utaalamu wa tiba, na kumwambia amsubiri chini kwenye gari lake dogo la kiraia.

****

Inspekta Muhogo Mchungu alikuwa amechanganyikiwa asubuhi ya siku iliyofuata baada ya kukuta magazeti yote ya siku hiyo yakiwa na habari za watu kurukwa na akili baada ya kumeza dawa za malaria aina ya Paranoxyquine. Kibaya zaidi ni kwamba, habari hizo zilieleza pia mpaka duka la dawa la Quick Pharma kwamba ndilo lililohusika na uuzaji wa dawa hizo.
Hata hivyo, magazeti yote hayakumnukuu afisa yeyote wa polisi zaidi ya kuzungumza na ndugu wa wagonjwa pamoja na kuhojiana na wenye duka hilo na madaktari. Gazeti moja lilithubutu kuchaisha cheti kilichotumika kutolea dawa hizo kikiwa na nembo ya duka hilo.
“Shit! Ni upuuzi gani tena huu?” Inspekta Muhogo Mchungu alifoka akimuuliza Kachero Ismail Bondo ambaye alikaa kwa unyonge mbele yake.
“Sielewi, Inspekta. Hata sijui watu hawa wamenusaje habari hii, maana kama utakumbuka vizuri tulisema kuwa ifanywe kuwa siri kubwa,” Kachero Bondo alisema.
“Sasa hapa wameharibu kabisa upelelezi. Kama ni wenye duka hili, au wafanyabiashara wanaojihusisha na biashara ya dawa hizi ni wazi kwamba watafanya haraka kuficha maovu yao.”
“Ni kweli, afande, sijui tutafanyaje?” Kachero Bondo alisema akiwa anaonekana kukata tamaa.
“Hilo ndilo swali la kujiuliza, itabid…” kabla hajamaliza sentensi yake, mara simu ya mezani kwake ikalia kwa nguvu. Akainua mkono wake haraka na kukwanyua mkonga wa simu akiwa na matumaini kwamba huenda simu hiyo ilikuwa na ufumbuzi wa utata uliokuwa umejitokeza.
“Haloo! Inspekta Muhogo hapa, nikusaidie nini?” Inspekta aliunguruma kwenye chombo cha kuzungumzia.
“Mimi ndiye wa kukusaidia wewe. Sikiliza, nakuomba usijiingize kwenye upelelezi wa kesi hii. Ni nzito na haibebeki, kama utaendelea utashuhudia nchi nzima ikiwa na mataahira wa akili, wewe ukiwa wa mwisho,” sauti ya upande wa pili ilikuwa nzito na iliyomaanisha nini inachokisema.
“Unasemaje? Wewe ni nani na uko wapi?” Inspekta akauliza kwa hasira iliyochanganyika na fadhaa.
“Hupaswi kujua mimi ni nani na niko wapi. Nadhani umeupata ujumbe wangu, hivi ninavyokwambia kuna watu wasiopungua ishirini wamekimbizwa katika hospitali za Mount Meru Arusha, KCMC Moshi, Teule Muheza, Bombo Tanga, Bugando Mwanza, Rufaa Mbeya, na Mirembe Dodoma, achilia mbali watu wanaomiminika hapo Muhimbili,” sauti ya upande wa pili ilisema na kuangua kicheko cha dharau.
“Hivi una wazimu? Ni nani wewe?” Insepkata walikuwa akitetemeka mwili mzima kwa hasira huku jasho likimtoka. Kachero Bondo alishangaa kumuona bosi wake akiwa katika hali hiyo.
“Nina wazimu, siyo? Basi wewe ndiwe mwenye wazimu. Narudia tena, achana na kesi hii, mambo ya Ngoswe mwachie Ngoswe mwenyewe! Na hii ni amri!” sauti ya upande wa pili ilisema na kabla Inspekta hajasema kitu, simu ikakatika upande wa pili.
“Haloo! Haloo! Amekata?” Inspekta akasema huku akiwa amemsahau kabisa Kachero Bondo.
Akakiacha kiti chake na kuanza kuzunguka zunguka ofisini. Kachero Bondo alimtazama na kumhurumia, kwa sababu aliamini kazi ilikuwa imeanza. Baada ya muda, Inspekta akageuka na kumatazama Bondo kana kwamba ndiyo kwanza anamuona.
“Kuna nini?” Bondo akauliza kwa woga.
“Sikiliza Bondo, nadhani hii ni vita kuba kuliko tulivyokuwa tunafikiria,” akatulia kumwangalia, kisha akaendelea; “Kuna mtu kanipigia simu na kunionya nisiendelee na kesi hii, nadhani ni mwendawazimu. Sasa twende Muhimbili mara moja.”
Bila ubishi, Bondo aliinuka kitini na kuongozana na bosi wake hadi chini ambako waliingia kwenye gari na kuongoza hadi Muhimbili. Inspekta alikuwa amemwamuru dereva wake aendeshe kwa mwendo wa kupaa, hivyo dakika tano tu baadaye tayari walikuwa wamefika.
Walipofika walishangaa kukuta foleni ya wagonjwa huku wengine wakipiga kelele ovyo. Walipouliza wakaambiwa kwamba wamepatwa na wazimu wa ghafla. Hima hima Inspekta Muhogo Mchungu akaongoza hadi ofisini kwa Dk. Idrissa Mhando. Aligonga mara moja nkabla ya kuitikiwa akafungua. Mlango ulikuwa umeegeshwa tu, hivyo wakaingia mpaka ndani. Walimkuta daktari, lakini walikuwa wamechelewa, kwani alikuwa kapoa kitambo, akiwa maiti. Kisu kikubwa chenye mpini mweusi kilikuwa kimezama kifuani upande wa kushoto huku damu nyingi zikiwa zimevuja.
Ilivyoonekana muuaji hakupata kazi sana ya kumuua na yawezekana alikuwa ameketi kwenye kiti cha wagonjwa.
Inspekta akazidi kuchanganyikiwa. Akaanza kupekuapekua kila mahali kuona kama kulikuwa na nyaraka zozote. Kila kitu kilikuwa swa, isipokuwa kitu kimoja. Faili la wagonjwa wale waliotangulia halikuwepo. Faili hilo ndilo lililokuwa na ripoti za vipimo vyote na Dk. Mhando alikuwa ameahidi kuliwasilisha kwa Inspekta baada ya kukamilisha ripoti yake.
Akageuka haraka na kutoka nje, ambapo alimuuliza mgonjwa aliyekuwa kwenye foleni kama mgonjwa aliyemtangulia alitoka na alikuwa amevaaje pamoja na jinsia yake.
“Alikuwa mwanamke, lakini mbona hajatoka? Tulikuwa tunamsubiri atoke ili nasi tuingie na kaingia muda mrefu kweli, kwani hayupo ndani?” ndugu wa mgonjwa huyo akasema na kuzidi kumchanganya Inspekta Muhogo Mchungu. Hakujisumbua hata kujibu, badala yake alirejea ndani ambako alimkuta Kachero Bondo akiendelea kuuchunguza mwili wa marehemu pamoja na sehemu nyingine za chumbani humo.
“Vipi, umegundua nini?” akauliza.
“Hakuna kitu chochote cha ziada, naona kila kitu kipo kawaida tu!”
“Muuaji bado yuko humu ndani, au atakuwa ametokea dirishani!” Inspekta akamweleza msaidizi wake.
Hata hivyo, hakukuwa na dalili zozote za kuwemo kwa mtu humo ndani kwa sababu ofisi yenyewe ilikuwa ndogo isiyoweza kuficha chochote. Zaidi ni muuaji mpumbavu ambaye anaweza kuua na kuendelea kubaki humo ndani kwa zaidi ya nusu saa. Kuhusu kupitia dirishani, uwezekano huo pia haukuwepo, kwani kulikuwa na kadirisha kadogo ambako kalikuwa juu kabisa, tena kasikoweza kupitisha mtu mzima. Chumba chenyewe kilipambwa na hewa ya kiyoyozi.
Hali hii ikaendelea kumchanganya Inspekta, ambaye alikwenda tena nje na kuwauliza wagonjwa kama kuna mtu yeyote ambaye alitoka kabla wao hawajaingia. Ukimya wa ghafla ulitanda, lakini baada ya muda, mama mmoja akasema; “Nesi alitoka akasema daktari alikuwa bado na mgonjwa ndani!”
“Unasema nesi? Alikuwaje?” Inspekta akaona swali hilo ni kama la kipuuzi. Akajisahihisha; “Nina maana umri wake, rangi yake, au analinangana na yule mgonjwa aliyeingia mwanzo?”
“Ni msichana, nadhani kati ya umri wa miaka ishirini na tano hivi, mwembamba, mweusi, ila amevaa miwani ya jua. Mimi nikahisi pengine huu ugonjwa wa macho wa Red Eye ambao umeanguka. Alikuwa na mkoba na faili moja.”
Faili? Yawezekana ndilo hilo hilo lenye ripoti. Na kuhusu mkoba? Inawezekana pia ndio ulikuwa na nguo ambazo alibadilisha alipoingia na baada ya kufanya mauaji akavaa za kiuguzi. Inspekta aliwaza na kuwazua. Tayari alikuwa ametambua kwamba ‘nesi’ huyo ndiye muuaji mwenyewe na kwamba huenda aliingia akiwa na mavazi hayo ya akiba. Bila kufikiria mara mbili, alipiga simu polisi ili waje wauchukue mwili wa marehemu.
Muda si mrefu eneo lote la hospitali likajaa watu baada ya kusikia taarifa kwamba daktari kauawa ofisini kwake. Polisi walifika na kuubeba mwili wa marehemu wakiongozana na daktari ambaye alikwenda kuufanyia uchunguzi kabla ya kuhifadhiwa.
Inspekta Muhogo Mchungu na msaidizi wake walirejea ofisini kwao kila mmoja akiwa ameishiwa nguvu. Hawakujua waanzie wapi kufanya uchunguzi. Hata hivyo, walifarijika baada ya kusikia kwamba daktari mwingine bingwa wa magonjwa ya akili alikuwa ameanza kuwahudumia wagonjwa wote, ambao hali zao zilianza kurejea kawaida.
Alipofika ofisini akaambiwa na katibu Muhtasi wake, Jennifer, kwamba simu kadhaa zilikuwa zimepigwa kumuulizia.
“Zimetoka wapi? Umezijibu?” maswali mfululizo yakamtoka. Haikuwa kawaida yake kuuliza maswali kama hayo. Jennifer alitambua mara moja kwamba bosi wake hakuwa katika hali ya kawaida.
“Hapana, niliwaambia kwamba umetoka kidogo. Pengine watapiga baadaye maana hawakutaka kuacha hata majina yao,” Jennifer akajibu.
Inspketa akaingia ndani huku akifuatiwa na Bondo, ambaye muda wote huo alikuwa ameshikwa na wasiwasi. Kabla hawajaketi simu ya mezani ikapata uhai. Inspekta, akiwa amekasirika, akaukwapua mkonga wa simu na kuupachika sikioni kabla ya kuunguruma; “Unasemaje?”
“Umeamini siyo? Tafadhali…” kabla mtu wa upande wa pili hajamaliza, ambaye alikuwa ni yule yule aliyempigia awali kumuonya, Inspekta akamkatiza.
“Unadhani ni uendawazimu gani unaoufanya? Kwa nini mmemuua Dk. Mhando?”
“Ahaaaa haaaa haaaa! Unanichekesha sana Inspekta. Unaniita mwendawazimu halafu unasema ni kwa nini nimemuua Dk. Mhando! Yule alistahili kufa na wengine ambao watakuwa wakaidi watakufa vile vile. Nakuonya kwa mara nyingine, usijiingize kwenye kesi hii, tena usidhani kwamba mimi ni mwendawazimu, nina akili zangu timamu. Jihadhari sana, kwaheri!” simu ikakatika.
Inspekta aliendelea kuushikilia mkonga kana kwamba kuna miujiza ambayo ingetokea akamkamata mtu huyo aliyekuwa akifanya unyama wa kutisha kama huo halafu kwa dhihaka kubwa. Badala ya kuacha kama alivyoonywa, aliapa kwamba atafanya kila jitihada kuhakikisha kwamba anafuatilia kesi hiyo mpaka mwisho.
“Bondo, kuna mtu nadhani anatuchezea akili. Huyu anafahamu kila kitu kinachoendelea, naagiza kwamba wapange wenzako wote na make katika sehemu zote nyeti zenye huduma za jamii. Maduka yote ya dawa yachunguzwe kwa kina kujua nini kinaendelea, ikiwezekana hata kampuni iliyoingiza dawa hizo nchini ichunguzwe, sawa?” Inspekta alisema huku akiketi chini.
“Sawa afande, tutatekeleza!” alisema huku akisimama kwa ukakamavu. Alitaka kuondoka, lakini akasita kidogo na kugeuka.
“Nini tena?” Inspekta Muhogo Mchungu akauliza.
“Nilikuwa na wazo moja,” akasita kidogo tena kabla ya kuendelea, “Kama tutaigundua kampuni hii, unaonaje kama itafutiwa kibali, maana naona kama tunaweza kuwa tunahatarisha maisha ya watu wengi sana!”
Akiwa amefumba macho, Inspekta Muhogo Mchungu alivuta pumzi ndefu na kuzishusha, akaketi vizuri na kumtazama kwa makini Ismail Bondo, ambaye amekuwa mchapakazi mwadilifu na tegemeo kubwa katika kitengo hiki kwa kipindi kirefu.
“Siyo kazi rahisi kama unavyodhani. Iwe ni kampuni ya nchi za nje ya au kizalendo, kuifutia kibali bila kuwa na ushahidi wa kutosha ni kitu kisichowezekana. Kumbuka kwamba hili ni soko huria na lolote linaweza kutokea. Yawezekana kampuni utakayoipata siyo inayoingiza dawa hizi hatari bali yawezekana ipo kampuni nyingine au kikundi cha watu ambacho kinaihujumu kampuni lengwa. Hata hivyo, wazo lako ni la msingi sana, nenda kapeleleze, tutaangalia uwezekano.”
“Sasa afande, kama inawezekana basi dawa hizi zipigwe marufuku kwa sababu watu wataendelea kuathirika kama zitabaki madukani!”
“Wazo hilo siyo baya pia. Lakini kumbuka kwamba ni gumu kutekelezeka, kwanza kupigwa marufuku kwa dawa kutakwamisha upelelezi wetu, halafu serikali kupiga marufuku dawa hizi kunaweza kuifanya kampuni husika ikaishtaki na kudai fidia ya mamilioni ya fedha. Kimsingi, utatuzi wake unahitaji juhudi zetu binafsi na si vinginevyo,” akafafanua inspekta.
“Sawa sawa afande! Wacha tukajipange vizuri,” alisema na kuondoka kwa ukakamavu.

*****

Siku mbili zilikuwa zimepita tangu kuuawa kwa Dk. Mhando. Tayari Kachero Bondo alikuwa ameipata kampuni iliyoingiza dawa za Paranoxyquine nchini Tanzania. Ilikuwa kampuni ya Kitaliano iliyojulikana kama Materazzi Health Unit ambayo ilikuwa na tawi lake hapa Tanzania. Alikuwa amepata taarifa zote za namna ilivyoingia nchini na kuanza biashara zake pamoja na kuanza nyaraka za uingizaji wa dawa zake. Alipelekwa mpaka kwenye bohari moja iliyokuwa ikituka kuhifadhi dawa hizo, na baada ya kuchukua sampuli akaenda kwenye maabara ya kikosi chao na kufanya uchunguzi.
Mpaka anakamilisha zoezi hilo tayari usiku ulikuwa umeingia, hivyo akachukua faili lake la ripoti, ambayo alipanga kuiwasilisha kwa Inspekta kesho yake asubuhi, na kwenda nayo nyumbani ili akaimalizie.
Wakati anaondoka kuelekea nyumbani kwake Kigogo, huku akiwa anapiga mluzi taratibu, akashtukia kitu cha baridi kikigusa kisogo chake. Nusura asababishe ajali kwa jinsi alivyopata mshtuko.
“Usigeuke, nenda kaegeshe gari pale Msimbazi Centre, kwenye stendi ya mabasi, kasha nitakwambia cha kufanya,” sauti yakike ya mtu aliyekuwa nyuma yake ilimwambia. Ilikuwa ni sauti ya mwanamke, lakini yenye kujiamini mno.
Bondo alifuata maelekezo hayo bila ubishi, na baada ya kuegesha gari, akiwa bado ameambiwa kwamba asigeuke nyuma wala kutazama kwenye kioo cha dereva, alishtukia mikono yenye nguvu ya mwanamke huyo ikimkaba mdomo na kisu kikali kikizama kwenye ubavu wake wa kushoto. Bondo alijaribu kupigana na kifo, lakini mikono ya mwanamke huyo ilikuwa na nguvu za ajabu sana. Bondo alikukuruka kwa dakika mbili hivi, kisha nguvu zikamwishia na pumzi ya uhai ikamtoka.
Kituoni hakukuwa na mtu yeyote wakati huo na kulikuwa na hali ya utulivu mkubwa. Maiti yake iliokotwa na askari wa doria ambao walishangaa kuiona gari hiyo ikiwa imeegeshwa muda mrefu.
Usiku huo huo taarifa zilimfikia Inspekta Muhogo Mchungu, ambaye alizidi kuchanganyikiwa kwani aliona kabisa wahusika hao walikuwa hawatanii. Alizidi kusaga meno kwa hasira, lakini juhudi zake zilionekana kama mtu akonyezae gizani!

*****

“Kesho nataka kwenda Milan, ninaomba nifanyie mpango wa tiketi ya ndege ambayo inaweza kuwa ya kwanza,” Joab Chimaisi alimweleza katibu muhtasi wake na msaidizi wake wa karibu, Rosemary asubuhi moja. Ilikuwa ni baada ya kuripotiwa mauaji ya Kachero Bondo, ambayo yaliambatana na mauaji ya waandishi watano walioripoti tukio la watu kuchanganyikiwa na kutokana na kunywa dawa aina ya Paranoxyquine.
Joab, akiwa anaendesha taasisi yake ya Relationship Consultants and Research Centre akishirikiana na rafikiye Danny Mahaho, mwanahabari aliyeamua kujishughulisha na utafiti na mambo ya uchunguzi baada ya kuhitimu stashahada yake ya Upelelezi wa Kujitegemea, alikuwa amezipitia taarifa zote za matukio hayo na kufanya utafiti wa chini kwa chini mpaka akajua kampuni iliyokuwa ikiingiza dawa hizo nchini na mawakala wao.
Kwa kuwa Danny alikuwa likizo, majukumu yote yalikuwa kwake na alikuwa amedhamiria kuifanya kazi hiyo bega kwa bega mpaka aupate ukweli, aliamini kwamba kulikuwa na namna katika matukio yote hayo na kwamba taifa lilikuwa katika janga kubwa sana endapo hali hiyo ingeendelea hivyo.
Kitaaluma yeye alikuwa mpelelezi wa kujitegemea ambaye alihitimu katika chuo kimoja cha masuala ya kijasusi nchini Marekani baada ya kuachana na jeshi kabla ya kuchukua mafunzo ya kujihami bila kutumia silaha huko Uchina kwa muda wa miaka mitatu. Zaidi ya hayo, yeye alikuwa na taaluma ya uchumi aliyoipata katika Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) na aliikuta taasisi hiyo tayari imeanzishwa na kwa kuwa wote walikuwa na mtazamo sawa wakaamua kuwa shirika.
Joab ndiye kimsingi aliyemfanyia mpango Danny naye akaenda Uchina kuchukua mafunzo ya kung-fu, lakini mwenzake alikwenda mbali zaidi baada ya kufanikiwa kupata ujuzi wa mafunzo ya ninjitsu kwa mwaka mzima. Kiufupi, linapokuja suala la mapigano ya bila kutumia silaha, Danny alikuwa kinara ingawa hakuwahi kujionyesha kutokana na kuhofia kwamba sanaa ya uninja, ambayo ni hatari zaidi katika sanaa za kujihami bila silaha, ilikuwa haijaingia Tanzania.
“Mbona ghafla hivyo? Kuna nini?” Rosemary aliuliza.
“Mambo yanayotokea nchini yamenifanya niende huko, nataka nikaanzie upelelezi wangu huko badala ya kuanzia hapa,” Joab akajibu.
“Unataka kupeleleza mauaji haya? Mbona unatafuta matatizo, Joab, kwa nini usiwaachie polisi na idara zinazohusika? Nadhani wao hawajashindwa bado,” Rosemary alishauri huku akionyesha masikitiko ya dhahiri.
“Hapana, Rosemary, siwezi kuendelea kushuhudia vifo zaidi vikitokea pamoja na watu wengi wakipata wazimu. Huwezi kujua kama kesho mimi nitakuwa mwendawazimu, basi ni bora nife kuliko kushuhudia hali hiyo. Polisi siwadharau, lakini kazi zao zina mlolongo mrefu sana. Wacha niende nikaanzie huko.”
“Sawa, wacha basi niwapigie mawakala wa mashirika ya ndege ya kimataifa nijue kuna ndege gain.”
“Hapana, subiri nikwambie, ulizia ndege inayokwenda Paris, Ufaransa, nitaunganisha huko huko. Sitaki wajue kwamba kuna mtu kaenda moja kwa moja Milan, wanaweza wakanikwamisha,” Joab alishauri.
“Sawa, ni jambo la busara kuchukua tahadhari.”“Nashukuru kusikia hivyo, jitahidi basi, mimi nakwenda nyumbani kujiandaa, lakini ukifanikiwa naomba uniletee tiketi yangu nyumbani.”
“Hakuna tabu!” Rosemary aliitikia kwa shauku. Siku zote alikuwa akionyesha kumzimia Joab, ingawa Joab mwenyewe hakuonyesha dalili zozote zile. Si kwamba Rosemary hakuwa mzuri, la hasha. Alikuwa mzuri tosha, lakini hakuwa aina ile ya wanawake ambao Joab huwapenda. Alikuwa na umbile la kiuanamitindo, wakati yeye Joab alipendelea wanawake wanene na waliojazia. Daima Joab alimuona Rosemary kama chaguo la Danny, ambaye alikuwa akipenda wanawake wembamba.
Wakati akiwa nyumbani Joab alimpigia simu Danny na kumweleza kimafumbo kuhusu azma yake ya kwenda Milan na nini alichokuwa anakwenda kukifanya. Wakati huo Danny alikuwa Nairobi akifanya utafiti Fulani wa masuala ya michezo. Hakuwa tayari kukaa nyumbani tu bila kujishughulisha, japokuwa hiyo ilikuwa ni likizo yake ya kwanza katika kipindi cha miaka mitano!
Danny aliposikia taarifa hizo alishangilia na kusema kwamba angeikatisha likizo yake ili arudi Dar es Salaam kusimamia ofisi na kufanya upelelezi akiwa hapo.

*****

Joab aliingia mjini Milan yapata saa sita mchana siku ya pili yake. Alikuwa ameunganisha ndege mara mbili, kwani baada ya kufika Paris, alipanda ndege iliyoelekea Uswisi. Huko akaunganisha ndege nyingine mpaka Milan.
Hakuwa mgeni wa jiji la Milan, kwani alikwishawahi kufika mara tatu kwa matembezi. Alikuwa na rafiki yake mmoja aitwaye Francesco Schilacci, ambaye baba yake alikuwa Profesa katika Hospitali Kuu ya Milan.
Tangu anaondoka nchini Tanzania, alikuwa amepanga kuanza kupata mwanga kutoka kwa baba wa rafikiye huyo, Profesa Beluscan Schilacci. Aliamini kwamba huyo angemsaidia kupata mwanga kabla ya kuanza safari yake ndefu.
Walikutana na Francesco katika chuo cha ujasusi huko Marekani na tangu hapo wamekuwa wakiwasiliana vizuri tu. Francesco mwenyewe alikwishawahi kutembelea Tanzania na kuzuru katika mbuga za wanyama pamoja na vivutio vingine vya kihistoria.
Kwa kawaida Joab hakuwa mpenda makuu, hivyo baada ya kuingia kwenye taxi hapo uwanja wa ndege alimwelekeza dereva ampeleke katika hoteli ya kati iitwayo Imprezzo di Milano. Ilikuwa ni hoteli nzuri ambayo aliwahi kufikia katika safari zake mbili za mwisho.
Baada ya kuoga na kupata chakula cha mchana, alimpigia simu kumtaarifu Francesco kwamba tayari alikuwa amewasili nchini mwake, tena kimya kimya.
“Mbona ghafla, halafu hata taarifa hakuna? Tungekuandalia msafara na vimulimuli kibao?!” Francesco akasema kwa utani. Alitambua jinsi gain Joab alivyochukia misafara mirefu ya viongozi ambayo kama kule Tanzania, ilichukua muda mwingi wa wananchi kutokana na kusimamisha magari ili kuwapisha. Wakati mwingine Joab aliwahi kudhihaki kwamba, magari husimamishwa wakati kiongozi husika hajaingia hata bafuni kuoga, achilia mbali kupata chai! Lakini hiyo ilikuwa kawaida kwa nchi nyingi za Kiafrika kwa kisingizio cha usalama na mambo ya protokali, ambayo yeye binafsi aliyapinga kwa kusema ni mipango mibovu tu ya wasaidizi wa chini.
“Nani anataka msafara wa kafara?! Jana tu niliota niko huku, leo asubuhi nikaamua kupaa, nimefika. Kuna ubaya gani kuingia kimya kimya?” Joab naye akajibu kwa utani.
“Nakufahamu wewe, katika hali kama hii hukosi una jambo. Mama anaumwa?” Francesco akauliza kwa mafumbo.
“Yuko chumba cha wagonjwa mahututi, dripu zimesimama anapumulia mashine maalumu. Nimefuata daktari bingwa pamoja na dawa. Niko pale pale ninapofikia.”
“Najua hawezi kufa, nakuja baada ya saa moja hapo.”
Saa moja baadaye walikuwa wameketi chumbani kwa Joab, ambapo Joab alimsimulia azma yake ya kuja hapo. Akamweleza kwamba amefanikiwa kuingia na sampuli ya dawa hizo, zote mbili, ili kuweza kufanya uchunguzi. Akamwambia kwamba alikuwa na haja ya kuomba msaada wa Profesa Beluscan Schilacci ili aweze kujua vidonge hivyo vimetengenezwa kwa kutumia utaalamu gani.
“Unazo hizo sampuli?” Francesco akauliwa kwa shauku.
“Ninazo,” Joab akasema huku akizitoa na kumwonyesha. “Zimeshawafanya watu kadhaa kuwa wendawazimu wa muda na kusababisha mauaji ya watu wasiopungua saba, sijui nyuma yangu. Kifupi hali ni mbaya sana.”
Francesco alizitazama kwa makini, kisha akanusa harufu yake. Baada ya muda alionekana kubadilika usoni kabla ya kuziweka mezani huku akitingisha kichwa.
“Vipi Franc?” Joab akamuuliza baada ya kuona akitingisha kichwa kwa huzuni na mashaka.
“Joab, una uhakika hivi vitu umevitoa Tanzania?” akauliza kwa mshangao.
Swali hilo lilimshangaza sana Joab ambaye alitaka kukasirika, kwani alikuwa amemweleza kila kitu kwa kirefu. Hata hivyo, alizizuia hasira zake na kumjibu.
“Franc, nimekwambia kwamba nimekuja nazo kutoka Tanzania, na hizo ndizo kiini cha safari yangu hapa,” akamfafanulia.
“Umewezaje kupita sehemu zote, pamoja na ulinzi ulivyo mkali katika viwanja vya ndege, bila kugundulika?” akauliza tena Francesco.
“”Nimepita tu, tena sikuwa nimechukua tahadhari yoyote ile. Kwani zina nini?”
Francesco alitulia kwa muda akitafakari, kasha akasema; “Ni dawa hatari sana hizi ambazo zinapigwa marufuku ulimwenguni kote. Hata hivyo, twende nyumbani kwenye maabara, nadhani mzee anaweza kutoa ufafanuzi wa kutosha kuhusu suala hili.”
Nusu saa baadaye walikuwa nyumbani kwa akina Francesco wakimsimulia Profesa Beluscan Schilacci mkasa mzima. Mzee huyo, ambaye alikuwa katika umri wa miaka 75, alionekana mkimya akisikiliza kwa makini. Mtu mwingine angeweza kudhani kwamba hasikilizi ama anadharau yale yanayosemwa, lakini hii ndiyo ilikuwa staili yake ya usikilizaji.
Baada ya Joab kumaliza kutoa maelezo, Profesa Schilacci aliomba apewe hizo sampuli, ambazo alizitazama kwa makini na baada ya muda akawaomba waongozane kwenda maabara.
Akiwa huko alikivunja kimojawapo cha vidonge hivyo na kuchukua unga wake, ambao aliuweka kwenye mashine maalum iliyokuwa inaendeshwa kwa kompyuta. Akachukua kidaftari kidogo na kalamu na kuanza kunakili baadhi ya mambo aliyokuwa akiyasoma kwenye kompyuta hiyo huku akiendelea kupima.
Zoezi hilo lilidumu kwa takribani saa moja, na baada ya kukamilika, mzee huyo alinyanyuka na kuwaashiria waende kwenye chumba cha kujisomea, ambako kulikuwa na ufaragha mkubwa na alikuwa akikitumia kwa ajili ya mazungumzo nyeti kama hayo. Francesco aligundua kwamba baba yake alikuwa amebaini mambo makubwa, ndiyo maana hakutumia sebule kwa mazungumzo.
“Kijana wangu, kwanza nasikitika kukwambia kwamba ulikuwa umeinadi roho yako kwa kubeba vitu vya hatari kama hivi,” alianza kuzungumza Profesa Schilacci bila kuonyesha badiliko lolote usoni mwake. “Vitu hivi ni hatari kuliko hatari yenyewe, na inaonyesha wazi kwamba vimetengenezwa na watu wanaoijua kazi yao barabara. Ni magalacha hasa wa biashara kama hizi.”
Alitulia kidogo na kumeza funda la maji huku akiwatazama Joab na Francesco kwa zamu ambao walikuwa wametulia kama waliomwagiwa maji, halafu akaendelea; “Hizi si dawa za Paranoxyquine kama walivyoandika. Hizi ni dawa za kulevya zenye mchanganyiko wa Mandrax na Heroin. Ni sumu kali sana kwa mwanadamu, kwani akimeza tu anaweza kulewa baada ya muda mfupi sana, hasa kwa wale ambao si watumiaji. Wale watumiaji wakimeza tembe moja wanaweza wasitamani tena madawa haya hata kwa siku mbili au tatu.”
“Unaweza kusema zinaweza kumtia uchizi mtu yeyote?” Joab akauliza.
“Kabisa. Lakini uchizi huu huwa ni wa muda tu, hasa kwa wale ambao si watumaiji wa dawa za kulevya. Kama nilivyosema, kwa watumiaji wa dawa hizo za kulevya wanaweza kuziona kama mkombozi wao mkubwa. Hata hivyo, lazima zitakuwa zinauzwa aghali sana kwa tembe moja. Nashangaa unaposema kwamba zinauzwa kwenye maduka ya dawa za binadamu huko Tanzania,” Profesa alijaribu kufafanua.
“Ni kweli mzee, dozi moja yenye vidonge vine inauzwa kwa shilingi 25,000, ambayo ni sawa na dola 24 hivi za Kimarekani,” Joab alieleza.
“Basi inaweza kuwa ina faida kubwa zaidi kwao kiuchumi au wana malengo mengine wanayokusudia,” Francesco akachangia.
“Na mzee, nini madhara yake kwa wale wasiotumia dawa za kulevya ikiwa watatumia dawa hizi kwa bahati mbaya au hata kwa kukusudia?” Joab akauliza.
“Madhara yake ni makubwa. Kwanza tembe hii moja inamezwa na mtumiaji mzoefu ambaye anaweza asitamani tena ulevi huu kwa siku mbili au hata tatu. Sasa zinapomezwa tembe mbili kwa mpigo, tena na mtu ambaye si mtumiaji wa dawa hizi, madhara yake yanakuwa makubwa sana. Pili, baada ya ulevi huu kutoka, baada ya siku mbili au tatu, mtu huyu ambaye hakuwahi kutumia, anapatwa na hamu Fulani ya kutamani kumeza tena dawa hizi. Zinakuwa tayari zimeingia kwenye damu na nguvu inapopungua anaona kama anakosa kitu Fulani, ni kama mvutaji wa sigara anavyokuwa na hamu ya sigara kutokana na sumu ya Nicotine ambayo inakuwa kwenye damu yake,” Profesa Schilacci akaeleza.
“Kwa hiyo unataka kusema kwamba mtu huyu anakuwa ameraibiwa au kwa lugha ya moja kwa moja, anakuwa mtumwa wa dawa hizi kama walivyo wale ‘mateja’ wa dawa za kulevya?” Joab akauliza kwa wasiwasi.
“Haswa! Na hii ni mbaya sana, kwa sababu kama atakosa kupata dozi hii anaweza kuumwa zaidi. Tiba yake baadaye itakuwa kupatiwa kidonge kimoja na mara baada ya kumeza anapona, lakini si kupona hasa, bali anakuwa amechanganyikiwa kama kichaa kabisa mpaka nguvu ile ya dawa ipungue.”
Taarifa hizi zilimchanganya sana Joab ambaye alianza kuyafikiria matukio ya wale wagonjwa wa kule Tanzania walivyokuwa. Akafikiria hatari ambayo ilikuwa ikilikabili taifa kwa wale ambao wangetumia dawa hizo na kugeuka kuwa waathirika wa dawa za kulevya. Hasira zilimkaba na akamchukia mtu yeyote aliyebuni mbinu hiyo chafu.
“Ninaamini kwamba huu utakuwa mpango wa kimataifa basi, au unasemaje mzee?” Joab akauliza kama kujifariji huku akipambana na hasira zake.
“Kabisa. Tena mpango huu ni hatari zaidi kwa sababu una lengo la kuwafanya wananchi wote kuwa watumwa wa dawa hizi. Hii inaweza isikwepeke kwa sababu dawa za Paranoxyquine zinatibu malaria, na malaria huko Tanzania na Kusini mwa Jangwa la Sahara ni ugonjwa hatari sana, hivyo kila mmoja anaweza kujikuta akitumia tu dawa hizo bila kupenda akidhani anatibu malaria kumbe anameza dawa zisizostahili.
“Huu ni mpango wa kimataifa na inawezekana kabisa watu hawa wanaweza kufanya njama za kuondoa dawa zote halisi na kuweka dawa zao kwa sababu biashara ya dawa za kulevya imesambaa kila pembe. Huenda wamebuni njia hii baada ya kuona wanabanwa na serikali nyingi ulimwenguni. Nisubirini nije niwape historia kidogo ya dawa hizi la kulevya,” Profesa Schilacci alinyanyuka na kutoka nje, baada ya muda akarejea akiwa na kitabu kimoja kikubwa sana cheusi ambacho kilonekana kilikuwa na vumbi. Akakifuta na kukiweka mbele ya meza yake ndogo.
Francesco alinyanyuka na kwenda kutengeneza kahawa, baada ya kumaliza akaleta vikombe vitatu mezani pamoja na chupa. Wakaendelea kunywa kahawa huku wakisubiri mzee huyo aanze kuwasimulia historia ya dawa za kulevya.
Profesa Schilacci alikunywa kahawa yake chungu huku akiwa amefumba macho, baada ya kukiweka kikombe chini aliwatazama vijana wake na kuanza kueleza.
“Leo vijana wangu mna bahati sana, maana nataka niwaeleze mambo mazito ambayo hamkuwahi kuyasikia kuhusu dawa za kulevya. Mnakiona hiki,” alisema huku akiwaonyesha kitabu hicho cheusi kikuukuu. “Basi hiki kina mambo mengi sana nyeti!”
Alikunywa kahawa yake, halafu akaendelea; “Dawa za kulevya ziko za aina nyingi. Kuna heroin ama opium, kuna cocaine, kuna mandrax, kuna bangi ambayo ina majina mengi kama hashishi, majani na kadhalika.”
Alitulia kidogo na kuwatazama, halafu akaendelea; “Nitaanza kuwaeleza dawa moja baada ya nyingine nikianzia na heroin. Heroin ama opium inaweza kuwa dawa ya kutibu na pia sumu. Inatumika zaidi mahospitalini kwa kazi maalum na kwa vibali maalum, kwani huondoa maumivu, lakini watu wengi wanaitumia ndivyo sivyo, kwa sababu huwafanya watumaiji wakubwa kuwa watumwa na kuwadhoofisha.”
“Asili yam mea wa opium poppy, ambao kitaalamu unaitwa Papaver somniferum L., hapana shaka yoyote kwamba ni Mashariki ya Mbali. Inafikiriwa kwamba, mmea huu mara ya kwanza ulionekana kati ya eneo la Mediteranian na Asia. Usiri wa asili yam mea huo unalinganishwa na kanda mbili zinazozalisha kwa wingi heroin hivi sasa – the Golden Triangle, katika eneo la nchi kavu za Kusini-Mashariki mwa Asia, na eneo la Golden Crescent, Kusini-Magharibi mwa Asia,” aliendelea kueleza Profesa Schilacci huku akina Joab na Francesco wakiwa makini kusikiliza.
“Kiasi kikubwa zaidi cha heroin, au Diacetyl morphine, kinazalishwa katika maeneo ya milima katika umbali wa kilometa 7,500 kutoka Uturuki mpaka Vietnam na kuendelea, zaidi kupitia Afghanistan. Nchi zinazozalisha kwa wingi dawa hizi ni Afghanistan, Pakistan, Laos, Uturuki, na maeneo ya Amerika hasa Colombia.”
“Unataka kusema mimea hiyo inapandwa kama mazao mengine ya kawaida? Na baada ya muda gani yanakuwa tayari kwa kuvunwa?” Joab akauliza.
“Ndiyo. Yanapandwa kama mimea mingine ya kawaida kwa sababu yana mbegu zake. Baada ya kupandwa, mimea ya opium poppy humea kwa miezi mitatu. Maua huanguka baada ya muda huo, tunda lenye umbo kama la yai hubakia. Opium ghafi hutengenezwa kwenye tunda hilo ikiwa katika hali ya ujiuji wenye rangi ya maziwa. Wakulima hutumia visu maalum kukata tunda hilo wanapochuma. Katika mtambo, ambao mara nyingi huwa ni mapipa kadhaa yanayofichwa msituni, opium ghafi hii huchanganywa na kemikali, kuchemshwa, na kupitia mabadiliko kadhaa ya kimemia. Matokeo yake huwa unga mweupe ambao hujulikana kitaalamu kama trade number four heroin,” Profesa Schilacci alisema na kuwatazama vijana wake kwa zami, kisha akaendelea.
“Heroin inaweza kuvutwa au kunuswa kama ugoro, au kwa njia ya sindano ambayo huchomwa kwenye moto mpaka katika hatua ya kutaka kuyeyuka. Madhara yake hutokea kati ya dakika 5 hadi 8 baada ya kujidunga kwa sindano,” akameza funda la kahawa kabla ya kuendelea; “Hata hivyo, heroin kwa muonekano tu inaweza kuchanganywa kwa kuifananisha na vitu kama maziwa ya unga (Procaine), sukari (Ajax Cleaner), unga wa sembe, Baking Soda, sumu ya panya (Strychnine) na kadhalika.”
Profesa Schilacci alitulia akiwatazama Joab na Francesco kama yale aliyokuwa akiyaongea yaliwaingia vizuri. Alipoona wanamsikiliza kwa makini, akaendelea;
“Madhara ya heroin ni makubwa sana kwa sababu inaharibu kitu kinachoitwa kitaalamu kama ‘Blood Brain Barrier’, mfumo thabiti kabisa au utando unaouzunguka ubongo ambao huulinda dhidi ya vitu vya hatari vinavyokuja kwa njia ya damu ambavyo haviyeyuki haraka (low lipids). Pia unaukinga ubongo dhidi ya homoni na vihamasishi hatari vinavyoweza kusambaa mwilini, hudumisha mazingira bora kwa ajili ya ubongo na molekyuli za mafuta huwa haziwezi kupenya kwenye ubongo.
“Kwa hiyo inaweza kuonekana kana kwamba heroin inaweza isipenye kwenye ubongo. Lakini hata hivyo, ubongo kwa kawaida huunda vihamasishi vyake ambavyo huitwa kitaalamu kama endorphin ambavyo husaidia kupunguza uchovu na maumivu. Kwa maana hiyo, ubongo unaweza kuruhusu vihamasishi kama vya opium. Hivyo basi, heroin hukatisha katika ukingo huu wa damu wa ubongo kwa kasi ya mara 100 kuliko morphine kwa kuwa ni kitu ambacho kinayeyuka haraka sana.”
“Kwa hiyo madhara yake hasa ni nini,” Francesco akauliza.
“Madhara ya heroin, kama nilivyosema, ni makubwa sana. Dawa hizi ambazo kitaalamu ziko katika kundi la Diacetyl morphine husababisha Mfumo wa Kati wa Neva kudumaa na hii husababisha matatizo kama usingizi wa kupindukia, kupunguza uwezo wa kupumua, kushindwa kukohoa vizuri, kichefuchefu, kuharibika kwa mishipa ya vena, kuharibika kwa mapafu na matatizo mengine mengi,” akasema Profesa Schilacci.
“matatizo mengine,” akaendelea, “Kuchangia sindano mara nyingi kunasababisha maambukizi ya virusi vya HIV na UKIMWI. Pia magonjwa mengine ya ngozi hutokea wakati watumiaji wa dawa hizi wanapojidunga kwa sindano. Kuna uwezekano mkubwa wa sumu kuingia mwilini kwa watumiaji. Uwezekano wa kushikwa na ugonjwa wa kiharusi pia ni mkubwa. Watoto wanaozaliwa na wazazi walioathirika na heroin wanaweza kufa wangali wachanga, na zaidi watumiaji wanakuwa tegemezi kifikra na kimwili.”
“Kwani mtu anayetumia dawa hizi anaweza kupatwa na madhara gani akiacha?” Joab akauliza.
“Anaweza kuumwa na kichwa, kuharisha sana, kuvimba kwa misuli, kichefuchefu, fadhaa, kukosa usingizi, hofu na kadhalika. Hali hii huzidi katika siku ya pili au ya tatu tangu kuacha kutumia heroin lakini hushuka kuanzia siku ya 7 hadi ya 10,” akafafanua Profesa Schilacci.
“Lakini naamini kwamba mpaka dawa hizo zimekuja kutumika sasa, lazima kuna asili yake ya watu waliokuwa wakitumia. Unaweza ukawa unajua hilo pia, mzee?” Francesco akauliza.
“Franc unanichekesha sana. Nimewaambia kwamba hili buku jeusi lina kila kitu,” akasema huku akikigusa kitabu hicho kikuukuu. “Heroin ilianza kutumika katika mwaka 4000 Kabla ya Kuzaliwa Yesu Kristo. Ilikuwa ikitumiwa na Wagiriki wa Kale, Warumi, na Wamisri. Uvutaji wa heroin ulisambaa Uchina katika miaka ya 1600 Baada ya Kuzaliwa Yesu Kristo.”
Profesa Schilacci aliinua kikombe chake na kukuta kahawa imepoa kitambo. Francesco akamjazia nyingine ya moto. Baada ya kupiga funda mbili, akaendelea; “Mnamo mwaka 1680 opium ikaingizwa kwenye tiba na Thomas Synderham, nadhani mmenielewa nilipozungumzia tiba yenyewe. Mwaka 1729 opium ikapigwa marufuku nchini China, nah ii ikawaudhi sana Waingereza ambao walikuwa wanasimamia biashara ya opium. Mwaka 1803 Morphine ikatenganishwa kutoka kwenye opium na Frederick Serturner. Mwaka 1832 dawa ya Codeine ikatengenezwa kutoka kwenye opium.”
Profesa Schilacci akafungua ukurasa mmoja na kuupitia kwa muda, kisha akasema; “Kuanzia mwaka 1839 hadi 1860 kulikuwa na vita baina ya Uingereza na Uchina kuhusu opium. Mwaka 1853 matumizi ya sindano ya Hypodermic yalianza. Kati ya mwaka 1861-1865 opium ilitumika kuwatibu wanajeshi katika Vita vya Wenyewe kwa Wenyewe nchini Marekani. Mwaka 1874 heroin ikatengenezwa kwa mara ya kwanza kutoka kwenye morphine. Nadhani mpaka hapo mnaweza kuwa mmeielewa historia ya heroin kwa ufupi,” akasema.
“Tumeshaelewa sana mzee, lakini vipi kuhusu dawa nyingine za kulevya kama cocaine na bangi?” Joab akauliza akiwa na shauku kubwa ya kujua mambo mengi kabla ya kuanza kazi yake. Alijiona kana kwamba yuko kwenye darasa akisoma historia ya kufurahisha mno.
“Usiwe na haraka kijana wangu, nimewaambia kwamba leo nataka niwaeleze historia ya mambo ambayo hamkuwahi kuota kuyajua,” akameza funda la kahawa chungu, halafu akatulia kidogo na kuwatazama kwa makini vijana wake.
“Sasa nakuja kwenye dawa aina ya Cocaine. Japokuwa tarehe halisi ya matumizi ya majani ya coca haijulikani, lakini ushahidi unaonyesha kwamba utafunaji wa majani ya m-coca ulikuwa unafanyika kabla ya kustawi kwa Dola ya Inca, yawezekana katika miaka ya 3000 Kabla ya Kuzaliwa Yesu Kristo. Wainca, ambao wanaishi Amerika ya Kusini, ambayo kwa sasa ni nchi za Peru, Bolivia, Ecuador, na sehemu za Chile na Colombia, waliithamini sana tabia ya kutafuna majani ya m-coca kama zoezi lao la kila siku, huku wakiacha midomo yao ikiwa na majani hayo muda mwingi, kama vile Wasomali wanavyopenda kutafuna milungi. Majani hayo yaliwasaidia Wainca kufanya kazi katika mazingira magumu, kwani yaliondoa kabisa njaa na hamu ya kula, yaliwapa nguvu na kuwasaidia kufanya kazi hata katika nyanda za juu,” akatulia kidogo.
“Majani ya m-coca pia yalikuwa yakitumika wakati wa sherehe za kidini na kafara, kutabiri matukio yajayo, kutibu ulozi, kuwasiliana na mungu wao aliyeitwa Andean Pantheon kwa kutoa kafara (ilifanyika zaidi wakati wa majanga makubwa). Kwa ujumla, Wainca waliamini kwamba mmea wa m-coca ni mtakatifu ukiwa na nguvu za miujiza, na Wainca waliamini kwamba roho zao zitakwenda paradise ikiwa watatafuna majani hayo hata wanapokuwa wanakaribia kufa. Nadhani mnawaona hata vijana wa leo wakishapata cocaine huwa wanaota utajiri ama uungu,” wote wakaitikia.



Akionekana kubadilika kidogo usoni, Profesa Schilacci akaeleza; “Mwanzoni mwa karne ya 16, Wahispania wakaivamia Dola ya Inca. Japokuwa waliwafanya Wainca kuwa watumwa wao, Wahispania waliwaruhusu Wainca waendelee kutafuna majani ya m-coca, kwani kazi zilionekana kuwa zikienda kwa kasi zaidi na kwa ufanisi wanapokuwa wanatafuna majani hayo. Japokuwa majani ya m-coca yalisafirishwa kupelekwa Ulaya katika kipindi hiki, hayakuwa maarufu zaidi huko mpaka baada ya karne chache baadaye.”
Profesa Schilacci alitulia kidogo kabla ya kuendelea. Lilikuwa darasa zuri la historia ambalo hata yeye mwenyewe alijisikia furaha kujiona ndiye mwalimu wa historia hiyo.
“Mnamo mwaka 1862, mkemia Albert Niemann akayatwanga majani ya m-coca na kutoa cocaine. Katika miaka ya 1880, mtaalamu mmoja wa mambo ya misuli Sigmund Freud akaanza kuichunguza cocaine na kuamini kwamba inaweza kuongeza nguvu za kimwili, kurejesha uwezo wa akili, kutibu matatizo ya mmeng’enyo wa chakula, ikiwa ni pamoja na kutibu ulevi wa pombe na morphine wa kupindukia. Baada ya hapo cocaine ikawa maarufu sana, na ilikuwa ikitumiwa hata na mapapa, watawala, na marais wakati inapowekwa kwenye kinywaji maarufu kilichoitwa Vin Mariani. Kinywaji kingine kilicho na cocaine ambacho ni maarufu mpaka sasa ni Coca Cola,” akasema Profesa Schilacci na kumfanya Joab atoe macho ya mshangao.
“Ina maana soda ya Coca Cola ina kilevi cha cocaine?” akauliza.
“Maana ya coca ni mmea wa coca, hivyo si ajabu kukuta kwamba Coca Cola ina kemikali nyingi za cocaine. Hata hivyo, zimewekwa katika kiwango cha kuhamasisha hisia tu na siyo kulevya. Hata Pepsi Cola nayo ina kiasi kidogo cha coca,” akafafanua Profesa.
“Duh! Nilishaanza kushangaa kwamba soda ya Coca Cola ina kilevi cha cocaine na kupiga picha ya watu watakaokuwa wameathirika,” Joab akasema akishusha pumzi.
“Hapana, haiwezi kuwa hivyo. Kama ingalikuwa hivyo basi watumiaji wote wa soda hiyo wangekuwa waathirika,” alifafanua Profesa Schilacci kabla ya kuendelea; “Hata hivyo, hadi kufikia miaka ya 1900, matatizo yatokanayo na dawa hizo yakaanza kujitokeza, ikiwa ni pamoja na kuzuka kwa matumizi yaliyokithiri ya dawa hizo. Mwaka 1914, Sheria ya kukataza dawa hizo, Narcotics Act, nchini Marekani ilipitishwa kuzuia matumizi ya cocaine. Katika miaka yote ya 1930, matumizi yaliyokithiri ya cocaine hayakuwa makubwa sana. Mwaka 1970 dawa mpya ya amphetamine ikaingizwa sokoni, ambayo ilikuwa na madhara kama yale ya cocaine. Wakati matangazo mabaya na madhara yalipotolewa kuhusiana na amphetamine, watu wengi wakaamua kutumia cocaine ili kupata madhara yale yale ya ulevi, wakiamini kwamba kumbe cocaine ilikuwa ‘dawa salama’, na uwiano wa watumiaji waliokithiri ukaongezeka maradufu. Hadi hii leo watu wengi wanaendelea kuamini kwamba cocaine ni salama.”
“Mzee, tunashukuru kwa ufafanuzi huo, lakini m-coca unalimwaje na unalimwa wapi?” Francesco, ambaye muda wote alikuwa kimya, akauliza.
“Mmea wa m-coca, ambao leo hii unajulikana kitaalamu kama Erythroxylon coca, una jamii mbili ambazo zina dawa ya drug cocaine; Huanuco coca (coca ya Bolivia) na Colombian coca. M-coca wa Bolivia una rangi ya kijani iliyochanganyika na rangi ya udongo, unaong’ara, una shina nene, huku majani yake yakiwa na upana wa inchi moja mpaka tatu. Coca ya Bolivia inauzwa katika soko la kimataifa kama hydrochloride powder, na ina asilimia 85 ya cocaine. M-coca wa Colombia una rangi ya kijani iliyopauka na majani madogo. Coca ya Colombia ina asilimia 60 ya cocaine. Mimea yote inakua kati ya futi tatu hadi 12,” alieleza Profesa Schilacci.
“Nini madhara ya cocaine?” Joab akauliza baadaye.
“Madhara yake ni mengi, yapo ya muda mfupi na ya muda mrefu,” akatulia kidogo kabla ya kuendelea; “Madhara ya muda mfupi ni kama kuongezeka kwa joto la mwili, hitilafu ya macho, kuongezeka kwa shinikizo la damu, kuongezeka kwa nguvu za mwili, kupungua kwa hamu ya kula, kuongezeka kwa mapigo ya moyo na kadhalika.”
Sasa kila mtu alikuwa makini akionyesha kuvutiwa mno na historia hiyo. Joab na Francesco walikuwa wanafunzi, na walilifurahia somo hilo, wakati Profesa Schilacci, aliyekuwa mwalimu, naye aliifurahia hadhi hiyo ya ualimu kwa wakati huo. Profesa alipoona hali imetulia, akaendelea;
“Matatizo ya muda mrefu ni utumwa uliokithiri, kuchanganyikiwa, kushindwa kutulia, magonjwa ya moyo, kushindwa kupumua, kiharusi, matatizo ya utumbo, na mengineyo,” akamalizia.
“Aisee! Kumbe ni hatari kiasi hicho?” Joab akauliza.
“Naam, tena hatari sana,” Profesa akaitikia.
“Na vipi kuhusu bangi?” Joab akauliza tena.
Kabla ya kujibu, Profesa Schilacci alitulia kwa muda akisoma kitabu hicho, ndipo alipouinua uso wake na kuwageukia. Akatabasamu na kisha kuyashusha tena macho yake kwenye kitabu kabla ya kuanza kueleza.
“Bangi, unaweza ukaiita Marijuana, Hashish, Cannabis, Mche na kadhalika. Ina majina mengi sana. Lakini historia inaanzia nyuma kabisa katika miaka ya 2700 Kabla ya Kuzaliwa kwa Yesu Kristo. Kwa wakati huo haikuwa ikitumika kama kilevi, ilikuwa ikitumika kama tiba za Kichina. Mara ya kwanza kutumika kama kilevi ilikuwa nchini India karibu mwaka 1000 Kabla ya Kuzaliwa kwa Yesu Kristo. Jina la Marijuana linaweza kuwa limetokana na maneno ya Kimexico ya Mary-Jane au neno la Kireno marigu-ano ambalo linamaanisha kilevi. Dawa yenyewe inatokana na mmea wa jamii ya hemp uitwao kwa kitaalamu kama Cannabis sativa. Marijuana siyo dawa pekee inayotokana na mche huo. Mchanganyiko mkubwa unaoitwa hashish na mafuta yanayonata ya hash yanatokana na Cannabis sativa. Hata hivyo, kiwango kikubwa cha kemikali kilichomo kwenye marijuana ni THC au kwa kirefu delta-tetrahydrocannabinol. Kemikali hizi zinaweza kuonekana kwenye sampuli ya mkojo hata kama mtumiaji amevuta bangi kwa siku kadhaa ama wiki kadhaa zilizopita.”
Aliwatazama ‘wanafunzi wake’ kwa makini kabla ya kuendelea; “Marijuana ni miche na majani ya Cannabis sativa yaliyokaushwa. Inaweza kuingia mwilini kwa njia mbalimbali, kuvuta ndiyo njia inayotumika zaidi. Pia inaweza kuongezwa kwenye chakula ama kinywaji au kuvutwa kwenye mtemba. Madhara ya bangi kwa watumiaji yanategemeana na ubora wa bangi yenyewe, kiasi kinachovutwa, mazingira ambayo mtumiaji yumo (kama mtumiaji alikuwa peke yake ama kwenye kundi la watu) na uzoefu wa mtumiaji. Madhara ya kimwili yanaweza kuwa pamoja na: macho kuwa mekundu, mdomo kukauka pamoja na koo, kuongezeka kwa mapigo ya moyo na misuli kushindwa kuwasiliana vyema. Matatizo ya kisaikolojia ni pamoja na: kuchanganyikiwa, kushindwa kuona vizuri, fadhaa, hasira, ghadhabu, kubadilika kwa tabia na matatizo mengine ya kisaikolojia yanayoweza kudumu kwa saa 4-6 pia yanaweza kujitokeza,” akamalizia.
“Mzee, kwa kweli binafsi nakushukuru sana kwa historia hii ndefu ambayo sikuwa naifahamu. Sina budi kusema kwamba safari yangu imekuwa na mafanikio makubwa ingawa bado sijapata jibu la kile kilichonileta. Hata hivyo, kuna kitu kimoja ambacho kinanitatiza,” akasema Joab.
“Enhe? Kitu gain hicho?” Profesa Schilacci akauliza.
“Ni kwa muda gain dawa hizi, ikiwa ni pamoja na vileo, vinaweza kukaa kwenye mfumo wa mwili wa binadamu?” akauliza Joab.
“Muda wa dawa yoyote kukaa kwenye mfumo (iwe dawa ya kulevya ama dawa ya kawaida ya tiba) unategemeana. Kwa sehemu kubwa, unategemeana na ulivyo kisaikolojia; kwa mfano urefu wako, uzito, kiwango cha mafuta mwilini mwako, umri wako, hali ya afya, na kadhalika. Bado wengine wanatathmini pia hata utumiaji wako wa mara kwa mara; iwe mara moja kwa siku au zaidi ya mara tano, kiasi cha dawa unachotumia kila wakati, muda unaotumia kuvuta ama kunywa dawa hizo, ubora wa dawa zenyewe,” akasema Profesa kabla hajaendelea; “Kwanza lazima ieleweke kwamba matumizi ya dawa haramu ni kubomoa maisha yako… unapotumia dawa haramu unakuwa mtumwa… Dawa hizi zinabomoa ndoto zako na kuzaa ndoto za ajabu. Unashindwa kutekeleza wajibu wako katika familia na katika jamii. Malengo yako yote yanafutika. Utaota unajenga ghorofa wakati hata pesa ya kula huna, na si ajabu ukaanza kuota siku moja kwamba wewe ni mungu!”
Alitulia kidogo, kabla ya kuendelea; “Vileo kama vile bia, mvinyo na vinywaji vikali, ulevi wake unaweza kukaa kwenye damu kwa saa moja mpaka 12. ndiyo, Franc anataka kuuliza, vileo ni kama dawa za kulevya pia! Kunywa pombe kupita kiasi kunakufanya uwe mwathirika kama mtumiaji wa dawa za kulevya. Dawa za jamii ya Amphetamine ambazo ni Biphetamine, Black Beauties, Crosses, Dexedrine, Hearts, zinaweza kubaki mwilini kwa siku 1-2, dawa za jamii ya Anabolic steroids kama Amytal, Nembutal, Seconal, Phenobarbital; Barbs, zinaweza kubaki mwilini kwa siku 2-3, wakati dawa za jamii ya Benzodiazepine ambazo ni Ativan, Halcion, Librium, Rohypnol, Valium; Roofies, Tranks, Xanax, zinaweza pia kubaki mwilini kwa siku 2-3.
Alitulia kidogo kabla ya kuendelea tena; “Cocaine jamii zake ni kama Candy, Coke, Crack, Flake, Rocks, Snow, Whitecoat na zinaweza kubaia mwilini kwa siku 1-2; dawa za jamii ya Codeine kama vile Fiorinal w/codeine, Robitussin A-C, Empirin w/codeine, Tylenol w/codeine, zinaweza kubaki mwilini kwa siku 1-2; Heroin na jamii zake kama Horse na Smack znaweza kubakia mwilini pia kwa siku 1-2; dawa za jamii ya Ketamine kama K, Kit Kat, Special K, Vitamin K zinaweza kubakia mwilini kwa siku 2-4; Marijuana ambayo ia inaitwa kama Bud, Blunt,Majani, Herb, Pot, Reefer, Sinsemilla, Smoke, Weed, inaweza kubakia mwilini kwa siku 2-5 na hata zaidi ya mwezi kwamtumiaji wa kila siku. Dawa za jamii ya Nicotine kama sigara, sigara kubwa yaani Cigar, tumbaku isiyo na mosi na ugoro, hubakia mwilini kwa siku 1-2,” alimalizia.
“Kweli hili lilikuwa darasa tosa, hata mimi mwenyewe kuna mambo nilikuwa siyafahamu kuhusiana na dawa hizi za kulevya. Hata hivyo, baba, turudi kwenye suala ailokuja nalo Joab, nadhani ndilo lililozaa yote haya,” akasema Francesco.
“Suala la Joab ni gumu, na ndiyo maana tangu mapema kabisa nikasema kwamba waliofanya kazi hii ni watu majahili wa kimataifa. Kazi kama hizi zinafanywa na watu kama Mafia, nadhani mnawaelewa?” akauliza.
Francesco akasema anawaelewa vizuri ingawa hajui asili yao. Joab yeye alisema alikuwa akifahamu kwamba una kundi linaloitwa Mafia, lakini akadhani zilikuwa historia tu au kwamba watu hao hawapo tena.
“Wapo watu hawa, na wanaendelea kufanya mambo yao mpaka sasa. Vijana wangu, mnataka kunipa kazi kubwa ya kuwafunulia mambo ambayo yako nje ya taaluma yangu ya udaktari. Franc wewe ni Mtaliano kama mimi, ulipaswa uwe unawafahamu watu hawa, kwa sababu chimbuko lao ni hapa hapa Italia!” akasema akimgeukia mwanawe.
“Kweli mzee, nadhani sijaingia kiundani kuchunguza asili ya kundi hili, japo nipo kwenye mambo ya upelelezi kitambo sasa. Niliwahi kusikia kwamba sijui asili yake ni Sicily, huko Perlamo au siyo?” akauliza Francesco.
Badala ya kujibu, Profesa Schilacci akainuka taratibu na kwenda dirishani, ambako alifunua pazia na kuchungulia nje kwa makini. Giza lilikuwa limeingia ingawa mwanga wa taa ulikuwa ukiangaza vizuri. Kilichompeleka hapo hakikuwa kuangalia hali ya hewa ya nje, bali alitaka kuhakikisha usalama wao. Pamoja na ukweli kwamba nyumba yake ilikuwa katika uzio imara wa ukuta mrefu, lakini mzee huyu hakuonekana kama kuuamini. Baada ya kutafakari kwa muda na kuridhika, hatimaye alirejea mezani na kuketi akiwa makini zaidi. Akawatazama Joab na Francesco kwa zamu kasha akarejea kwenye kitabu chake cheusi kikuukuu alichokuwa nacho.
“Mmeniuliza swali ambalo ni gumu sana na la hatari kuliko hatari yenyewe,” alitulia na kuwatazama kabla ya kuendelea. “Hawa jamaa ni watu hatari sana na wanaweza kufanya jambo lolote, mahali popote, na wakati wowote bila kuhofia kitu.”
Akapekuapekua kitabu hicho na baadaye akakifunga. Akaiteremsha sauti yake na kuwa ya chini mno.
“Ninayowapa ni historia ambayo wengi hawaifahamu kuhusu kundi hili la Mafia. Wengi hudhani kwamba kundi hili linazungumzwa tu kama hadithi za kufikirika ama kusadikika na kwamba halijawahi kuwepo. Hii inatokana na vitendo viovu wanavyovifanya wanachama wa kundi hili,” alimeza funda la maji kabla ya kuendelea.
“Wengi wanatafsiri neno Mafia kwa Kitaliano kama Morte alla Francia Italia anela, yaani ‘Kifo kwa Mfaransa ni kilio kwa Mtaliano’. Wengine wanaitafsiri Mafia kama ‘Mazzini autorizza furti, incendi, avvelenament’, wakimaanisha kwamba ‘Mazzini (bosi maarufu wa kundi hili Guiseppe Mazzini) amehalalisha wizi, unyang’anyi, na mauaji ya sumu.”
Neno Mafia ni nomino ya neno la ki-Sicily ‘mafioso’, ambalo lina mizizi yake katika lugha ya Kiarabu. Kama litatafsiriwa kwa haraka maana yake ni ‘Mkuu wa Jamii’, na kwa jinsi wanavyofanya mambo yao gizani bila kugunduliwa, sina shaka kwamba wanastahili kujiita ‘wakubwa wa jamii’.
“Hata hivyo, neno hili la Mafia Kitaliano linaitwa Cosa Nostra, yaani ‘Kitu Chetu’, likiwa ni kundi la siri mno ambalo lilianzishwa katikati ya karne ya 19 huko Sicily, jimboni Palermo kama ulivyosema Franc. Kikundi kingine kikazaliwa kwenye Pwani ya Mashariki ya Marekani mwishoni mwa karne ya 19 kutokana na wahamiaji wengi wa Kitaliano waliokuwa wanakwenda nchini humo. Nguvu za Mafia nchini Marekani zilishika kasi katikati ya karne ya 20, mpaka upelelezi wa kina wa FBI ulipofanyika katika miaka ya 1970 na 1980 kuweza kulibaini. Pamoja na kudhibitiwa, lakini jamii ya hawa Mafia bado inaendelea huko Marekani na kwingineko duniani, na inatajwa zaidi kwa mabaya kwenye filamu na vitabu mbalimbali vya hadithi.”
“Unataka kusema kwa sasa kundi hili limetoweka?” Joab akauliza kwa shauku.
“Hapana. Bado lipo, tena lipo hai. Mbaya zaidi limepenya mpaka kwenye idara mbalimbali za serikali na za jamii. Linahujumu uchumi wan chi, linafisidi viongozi wa serikali, linapanga njama za mauaji na hata mapinduzi ya serikali, linaweza kutoa fedha kununulia silaha na kuwashawishi watu wakapigana kuipindua serikali, linaweza kuhujumu uchaguzi kwa kumweka mtu wao, linasafirisha dawa za kulevya, kushiriki biashara haramu, linashiriki hata kupanga bei za baadhi ya bidhaa, na mambo mengine kadha wa kadha,” Profesa Schilacci akasema.
“Duh! Kumbe kundi hili ni hatari kiasi hicho?” Joab akasema kwa mshangao.
“Ndiyo maana nikasema awali kwamba ni hatari kuliko hata hatari yenyewe.”
“Lakini kila kitu lazima kiwe na asili yake. Asili ya Mafia ni Sicily, sawa, lakini nini hasa chanzo chake mpaka kuja kutumika kwa neno hilo?” Francesco akauliza baada ya ukimya mrefu.
“Kundi hili wakati linaanzishwa katikati ya karne ya 19 huko Sicily lilikuwa kama kundi la kuwatetea wananchi wa huko, likilinda mashamba makubwa ya machungwa na limau katika maeneo yaliyouzunguka mji wa Palermo. Kuanzia hapo Mafia wakaanza kusambaza mizizi yao mpaka kwa wamiliki wa ardhi na wanasiasa wa Sicily. Kwa kupata mtandao mpana na mkubwa wenye nguvu katika serikali (ilikuwa wazi kwamba wanasiasa qwengi walikuwa wanachama na washirika wakubwa) Mafia likapata nguvu sana.”
Profesa Schilacci alimeza mafunda mawili ya maji na kuendelea; “Wakati wa utawala wa Kifashisti wa Bennedicto Mussolini nchini Italia, Cesare Mori, kiranja wa Palermo, alitumia nguvu maalum alizopewa kulisambaratisha kundi la Mafia, akiwalazimisha wanachama wa kundi hilo kukimbia kwenda ng’ambo vinginevyo wangefungwa. Wengi waliokimbia walikwenda Marekani, akiwemo Guiseppe ‘Joseph’ Bonanno, maarufu kama Joe Bananas, ambaye alikuja kuwa kiranja mkuu wa tawi la Mafia nchini Marekani…”
“Mzee, haya yote unayazungumza kwa ufasaha kabisa, wewe umeyajuaje au umeyatoa wapi?” Joab akamkatisha Profesa Schilacci.
“Mimi ni Mtaliano, nimesoma sana historia ya Mafia na nimesomea udaktari wangu New York, Marekani. Kwa maana hiyo nayafahamu sana mambo ya huko kwani hata mimi wakati nakwenda walinihisi huenda nitakuwa mmoja wa Mafia,” alisema Profesa.
“Sasa ikawaje baada ya wale kukimbia?” Francesco akauliza.
“Wakati Cesare Mori alipoanza kuwafungulia mashtaka wanachama wa kundi hilo waliojihusisha na utawala wa Kifashisti, aliondolewa madarakani, na utawala wa Kifashisti ukadai kwamba Mafia walikuwa wametokomezwa. Pamoja na kauli hiyo, Mussolini alikuwa na washirika wake katika kundi la Mafia la New York, hususan Vito Genovese.
“Marekani nayo ilitumia mtandao wa Mafia wa Marekani katika kuivamia Italia na Sicily mwaka 1943. Lucky Luciano na wanachama wengine wa Mafia, ambao walikuwa wamefungwa wakati huo nchini Marekani, walitoa taarifa za kijasusi kwa jeshi la Marekani, ambalo lilitumia maelekezo ya Luciano kusonga mbele vitani. Kwa bahati nzuri, wengi wa wanachama wa Mafia walikuwa si mashabiki wa ujamaa, hivyo ikawa faida kwa Marekani. Baadhi ya wachunguzi wanasema kwamba Luciano aliruhusiwa kufanya biashara yake ya dawa za kulevya akiwa gerezani kama malipo kutokana na msaada aliokuwa amelipatia jeshi la Marekani, na baada ya vita akarejeshwa Italia ambako aliendelea na vitendo vyake vya kihalifu bila kuzuiwa. Inasemekana ndiye aliyeongoza kuenea kwa mtandao wa biashara ya heroin kutoka Uturuki hadi Marseille katika mtandao ambao uliitwa ‘French Connection’. Baadaye wakati Uturuki ilipoanza kukomesha biashara hiyo, alitumia mtandao wa Corsican kusambaza biashara hizo haramu huko Vietnam wakati nchi hiyo ilipokuwa ikipigana na Marekani. Huu ndio mtandao ambao uliitwa ‘Golden Triangle’ ambao ulihusisha Marekani, Asia na nchi nyingine kupitia kwa wanajeshi wa Marekani.”
Alitulia kidogo na kisha kuendelea; “Baada ya Ufashisti kuondka, kundi la Mafia halikuwa na nguvu sana nchini Italia mpaka nchi hiyo iliposalimu amri katika Vita Kuu ya Pili ya Dunia, na Marekani kuitawala. Katika miaka ya 1980 na 1990 mlolongo wa magenge mengi ya mauaji ulishuhudia mauaji ya wanachama wengi maarufu wa Mafia, na kikundi kipya kikaibuka ambacho kimekuwa kikifanya uhalifu kwa umakini zaidi kuliko wale wa zamani.
“Mgawanyiko mkubwa zaidi kwa Mafia wa Sicily kwa sasa ni kati ya mabosi ambao wameshtakiwa na wako jela, Salvatore ‘Toto’ Riina na Leoluca Bagarella, na wale ambao wamekimbia aiwamo Bernerdo Provenzano. Wanachama maarufu na viongozi wa Mafia ni pamoja na Calogero Vizzini, bosi wa Villalba, ambaye alichukuliwa kama mmoja wa mabosi mashuhuri wa Mafia huko Sicily baada ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia hadi alipokufa mwaka 1954; Guiseppe genco Russo, bosi wa Mussomeli, alichukuliwa kama mrithi wa Calogero Vizzini; Salvatore ‘Ciaschiteddu’ Greco bosi wa familia ya Mafia huko Ciaculli, alikuwa ‘katibu’ wa kwanza wa Kamisheni ya kwanza ya Mafia huko Sicily iliyoundwa wakati Fulani mwaka 1958; Tommaso Buscetta, mwanachama wa kwanza wa Mafia wa Sicily kuwa ‘informa’ mwaka 1984, mrithi wa Leonardo Vitale, ambaye alijipeleka mwenyewe polisi mwaka 1973; Salvatore Riina, maarufu kama Toto Riina ni miongoni mwa viongozi hatari wa Mafia huko Sicily. Alijulikana kwa majina mengi ya utani kama ‘Mnyama’ au ‘Kijeba’ na alotawala Sicily kwa mkono wa chuma kuanzia miaka ya 1980 hadi mwaka 1993 alipokamatwa; Bernerdo Provenzano, mrithi wa Riina na alichukuliwa kama kiongozi mwenye nguvu zaidi kama Mafia wa Sicily; Giovanni ‘lo sannacristiani’ Brusca, ambaye alihusishwa na mauaji ya Giovanni Falcone; Matteo Messina Denaro, aichukuliwa kama mrithi wa Provenzano; na Salvatore Lo Piccolo.”
“Unataka kusema kwamba hawa Mafia walikuwa na uongozi wao kamili?” Joab akauliza haraka haraka.
“Bila kuwa na utawala huwezi kuendesha kitu. Hawa watu ni hatari sana ambao tunaweza kuwaita leo kwamba ni Miungu-Watu. Wamesambaa kila kona ya dunia kwa sasa na wanakwenda kwa uongozi ulio thabiti. Muundo wa zamani wa uongozi wa Mafia ulikuwa hivi; Mkubwa wa Mabosi wote aliitwa Capo di Tutti Capi yaani Bosi wa Mabosi; mwanachama mkongwe ama yule aliyestaafu aliitwa Capo dui Capi Re; Bosi Mkuu ambaye ndiye mtendaji mkuu anaitwa Don au Godfather kwa Kiingereza, na nyie Waswahili mnamwita ‘Mungu-Mtu’ – huyu anajulikana Kitaliano kama Capo Crimini ambaye anaongoza uhalifu; msaidizi wake anaitwa Capo Bastone; Mshauri anaitwa Consigliere; kiongozi wa kikundi cha watu kumi hivi anaitwa Caporegime; askari wao wanaitwa Sgarrista au Soldati na kadhalika,” akafafanua.
“Viongozi hawa walikuwa wanapatikana namna gani?” Joab akauliza tena akiwa amevutiwa na simulizi hii.
“Bosi au Don – mkuu wa familia, mara nyingi huongoza kama dikteta. Yeye hupata mgao wake kutoka katika kila operesheni inayofanyika. Ndiye hutoa maamuzi yote ya nini kifanyike. Yeye anachaguliwa na makapteni wa familia. Yeye ndiye humteua mshauri na huteua msaidizi wake ambaye anakuwa mkuu wa makapteni wote wa famili,” akafafanua Profesa Beluscan Schilacci.
“Umesema kwamba Mafia wameenea kila sehemu duniani, sidhani kama wanatumia jina hilo hilo moja kila sehemu, maana wangekuwa wanafahamika basi?!” Francesco akauliza.
“Ni kweli, hawatumii jina hilo hilo. Kila nchi kuna jina lake lakini shughuli wanazozifanya karibu zinafanana na wengi wao wana uhusiano na Mafia wa huku Italia. Nchini Albania kuna makundi mawili, moja linaitwa Albania Mafia na jingine Rudaj Organization; huko Colombia kuna makundi ya Cali Cartel na Medellin Cartel; Canada kuna makundi ya Bandidos, Hells Angels, C-Lo Krak Krew na Mafia wenyewe; China kuna kundi la Triads; Italia mbali ya kuwepo kwa Mafia, pia kuna makundi ya ‘Ndrangheta, Camorra, Sacra Corona Unita na Stidda; Ireland kuna Irish Mob; Japan kuna akuza; Russia kuna Russian Mafia; Marekani kuna Cosa Nostra, Latin Kings na Aryan Brotherhood; Mexico kuna Cartel de Juarez na Cartel del Golfo; Korea Kusini kuna Golden Fist; na Scotland kuna Camorra na Tartan Mafia.”
“Duh! Kweli hii ni kiboko. Unajua nilikuwa makini sana kwa kudhani kwamba hata nchini kwetu Tanzania kuna kundi la uhalifu linaloshabihiana na Mafia…” Joab alisema akishusha pumzi.
“Ingawa sijalitaja kwa kuwa silijui, lakini amini nakwambia kwamba litakuwepo tu, tena linahusisha watu wengi wenye mamlaka kiutawala na hata kifedha. Naamini kwamba vitendo vya ujambazi vipo, tena majambazi wengi wenye rekodi chafu wanakamatwa na kuwekwa ndani na kasha kuachiwa! Biashara ya fedha bandia naamini ipo, hata biashara ya dawa za kulevya, si ushahidi unao kuhusu dawa hizi? Unadhani zingewezaje kuingia kama si kwa njama za kundi hatari kama hili?” Profesa Schilacci akasema na kumtia hofu Joab.
“Unataka kusema kwamba hawa wanaweza kuwa Mafia?” Joab akauliza kwa hofu kidogo.
“Haswa! Nilisema tangu awali kwamba, kazi hii haiwezi kufanywa na watu wengine ispokuwa majahili wakubwa kama Mafia. Nani anayeweza kutengeneza dawa kama hizi zinazofanana na Paranoxyquine halisi ambayo imethibitishwa na Shirika la Afya Dunia kwamba ndiyo tiba mbadala ya malaria kutokana na malaria kuwa sugu katika ukanda wa Kusini mwa Jangwa la Sahara? Nani anayeweza kufanikisha kuingizwa kwa bidhaa kama hii kama si kuwepo kwa ushirikiano wa kutosha kutoka kwa wakubwa wa serikali? Nimesema kwamba hawa jamaa wanaweza kuipindua serikali na kuweka mtawala wanayemtaka, na kama unawanufaisha kwa namna moja ama nyingine, wanaweza kukulinda hata kama wananchi na wapinzani hawakutaki, mpaka mwenyewe uamue kuachia madaraka lakini si kwa shinikizo la watu baki. Kumbuka kwamba, umesema mwenyewe kuwa watu kadhaa wamekufa kwa dawa hizi, wengine wameuawa na watu wasiojulikana, wakiwemo maafisa wa upelelezi. Ni nani anayejua nini kinaendelea katika ofisi nyeti za serikali kama hizo kama si kuwepo kwa watu wenye madaraka? Mimi si mpelelezi, lakini jaribuni kusugua vichwa vyenu muone,” profesa akasema.
Ndiyo kwanza Joab akagundua kwamba kumbe kadhia ya sasa ilikuwa ngumu kuliko zote alizowahi kuzifanya kama ile ya ‘Pigo la Kifo’. Safari hii alikuwa akipambana na watu ambao wanamfahamu vizuri adui yao kuliko adui mwenyewe anavyojifahamu mwenyewe. Walikuwa ‘Miungu-Watu’ ambao daima walitaka kunyenyekewa na kuabudiwa. Kamwe hawakuwa tayari kuona mipango yao inakwamishwa kwa namna moja ama nyingine.
“Nashukuru sana mzee kwa ufafanuzi wako wote. Sasa nadhani umefanya uchunguzi wa kina kuhusu dawa hizi za Paranoxyquine, unadhani zinaweza kuwa zimechanganywa na nini na zinatengenezwa wapi?” akauliza.
“Dawa za Paranoxyquine zinatengenezwa Ufaransa, lakini Italia inazitengeneza kwa kibali maalum. Kuhusu suala lako hili, hizi dawa zinazowachanganya watu huko Tanzania zimechanganywa na heroin na cocaine kama nilivyoanza kueleza, na kwa uzoefu wangu hii ni kazi nyingine pevu ya Mafia. Kama ambavyo wanaweza kutengeneza noti za nchi yoyote ile wakafanya hila mpaka zikaingia kwenye mzunguko wa benki kubwa duniani, wamefanikiwa tena kuingilia katika biashara ya dawa hizi za malaria. Wasiwasi mkubwa nilio nao ni kwamba, isije ikawa dawa hizi zimesambaa katika nchi nyingi za Afrika ambazo zina matatizo makubwa ya ugonjwa wa malaria,” Profesa akasema kwa masikitiko.
“Madhara yake ni nini hasa?” Joab akauliza.
“Nimekwishasema mapema, kwamba dawa zote zinaingia kwenye mfumo wadamu na kwa kesi ya dawa za kulevya, mtu anapatwa na madhara makubwa ambayo pia nimeyaeleza.”


No comments:

JUST ANOTHER THOUGHT

JUST ANOTHER THOUGHT

A person asked God, “What surprises you most about mankind?”

And God answered,
“That they loose their Health to make money and they loose their money to restore their Health.

That by thinking anxiously about the future, they forget the present, such that they live neither for the present nor the future.

That they live as if they will never die and they die as if they had never lived.….”

BECAUSE I'M A MAN...

Because I’m a man, when one of our appliances stops working I will insist on taking it apart, despite evidence that this will just cost me twice as much once the repair person gets here and has to put it back together.

Because I’m a man, I don’t think we’re all that lost, and no, I don’t think we should stop and ask someone. Why would you listen to a complete stranger I mean, how the hell could he know where we’re going?

Because I’m a man, there is no need to ask me what I’m thinking about. The answer is always either sex or football, though I have to make up something else when you ask, so don’t.

Because I’m a man, I do not want to visit your mother, come visit us, or talk to her when she calls, or think about her any more than I have to. Whatever you got her for mother’s day is okay, I don’t need to see it. And don’t forget to pick up something for my mommy, too!

Because I’m a man, I am capable of announcing, “one more beer and I really have to go”, and mean it every single time I say it, even when it gets to the point that the one bar closes and my buddies and I have to go hunt down another. I will find it increasingly hilarious to have my pals call you to tell you I’ll be home soon, and no, I don’t understand why you threw all my clothes into the front yard. Like, what’s the connection?

Because I’m a man, you don’t have to ask me if I liked the movie. Chances are, if you’re crying at the end of it, I didn’t.

Because I’m a man, yes, I have to turn up the radio when Bruce Springsteen or The Doors comes on, and then, yes, I have to tell you every single time about how Bruce had his picture on the cover of Time and Newsweek the same day, or how Jim Morrison is buried in Paris and everyone visits his grave. Please do not behave as if you do not find this fascinating.

Because I’m a man, I think what you’re wearing is fine. I thought what you were wearing five minutes ago was fine, too. Either pair of shoes is fine. With the belt or without it looks fine. Your hair is fine. You look fine. Can we just go now?

Because I’m a man and this is, after all, the 90’s, I will share equally in the housework. You just do the laundry, the cooking, the gardening, the cleaning, and the dishes. I’ll do the rest.

A SIMPLE GUIDE TO LIFE

1. Follow your dream! Unless it’s the one where you’re at work in your underwear during a fire drill.

2. Always take time to stop and smell the roses and sooner or later, you’ll inhale a bee.

3. Do not walk behind me, for I may not lead. Do not walk ahead of me, for I may not follow. Do not walk beside me, either. Just leave me alone.

4. If you don’t like my driving, don’t call anyone. Just take another road. That’s why the highway department made so many of them.

5. If a motorist cuts you off, just turn the other cheek. Nothing gets the message across like a good mooning.

6. When I’m feeling down, I like to whistle. It makes the neighbor’s dog run to the end of his chain and gag himself.

7. It’s always darkest before dawn. So if you’re going to steal the neighbor’s newspaper, that’s the time to do it.

8. A handy telephone tip: Keep a small chalkboard near the phone. That way, when a salesman calls, you can hold the receiver up to it and run your fingernails across it until he hangs up.

9. Each day I try to enjoy something from each of the four groups: the bonbon group, that salty-snack group, the caffeine group and the “What ever-it-is-the-tinfoil-in-the-back-of-the-fridge”.

10. Into every life some rain must fall. Unusually when your car windows are down.

11. Just remember: You gotta break some eggs to make a real mess on the neighbor’s car!

12. When you find yourself getting irritated with someone, try to remember that all men are brothers and just give them a noogie.

13. This morning I woke up to the unmistakable scent of pigs in a blanket. That’s the price you pay for letting the relatives stay over.

14. It’s a small world. So you gotta use your elbows a lot.

15. Keep your nose to the grindstone and your shoulder to the wheel. It’s a lot cheaper than plastic surgery.

16. This land is your land. This land is my land. So stay in your land.

17. Love is like a roller coaster: When it’s good you don’t want to get off, and when it isn’t, you can’t wait to throw up.

DEDICATION TO YOUNG PEOPLE

Youth is a time of hope. Also of uncertainty. But for a person who is young and healthy, uncertainty just means a challenge. It is important to be positive. First of all about yourself. But also about your family and your people. As a unique person and each human being are unique, you have enormous potential. Because you have so much potential, people may sometimes feel negatively challenged by that potential and try to undermine it.

You have to fight for your right to make your place in society. To do that you have to use all the chances given you now to be a positive element in whatever situation you find yourself in, in future. So, it may be necessary to be a ‘rebel in reverse’ as it were. That takes real courage, to set your goal and stick to it. You choose your crowd. You exercise your right to choose.
Don’t lose your freedom for the sake of anyone. Real freedom, freedom to choose the right thing, the best for you.

Always bear a few things in mind while exercising your right to choose.

* Never take a decision when you are in a fit of anger or depression.
* Never take a decision when you are emotionally high.
* Why should fads or the decision of the group tie you down?
* What are you?
* What do you want tomorrow to be for you?

No matter how strong the group decision may be, you must think and make your decision. Many times it is necessary to consult before taking a decision. Go to someone whose life you admire, not necessarily the person you like most, but the person who is whole, who is one person, wherever she or he is and whatever she or he does.

* Remember that there is always tomorrow, and tomorrow is hope. Very few things are ‘written in stone’. Most of the mistakes we make can be rectified. They can be corrected. Problems have a solution, and each new day is a new start, a new chance, a New Hope. Indeed the youth are our hope you are our future.

Also remember that your parents love you unconditionally, you have their support and want the best in life for you ¨

COSTA VICTOR NAMPOKA

Mguu ulivyokatisha ndoto za kucheza soka Ulaya

DANIEL MBEGA
Dar es Salaam

NI majira ya saa 5.20 hivi asubuhi, niko hapa Ukonga-Banana nikiwania kupanda daladala la kwenda kwenye kitongoji cha Kitunda-Kibeberu, moja ya vitongoji vinavyokua kwa kasi hapa jijini Dar es Salaam.
Sijui ni umbali gani kutoka hapa, hivyo namuuliza dereva ambaye nimeketi naye pembeni yake. Ananiambia ni mwendo kama wa dakika 15 tu hivi. Nashusha pumzi kwa kujua kwamba kumbe si mbali sana kama nilivyofikiria.
Nawasili kwenye kitongoji cha Kibeberu, ambako ndiko magari yanakogeuzia, na bila kupoteza muda nampigia simu mwenyeji wangu kwamba tayari nimeshafika. Namhurumia huko aliko kama ataamua kuja kunipokea, lakini nafarijika anaponiambia kwamba nimuulize mtu yeyote hapo kituoni atanileta.
Watoto wawili wanajitolea kunipeleka nyumbani kwa mwenyeji wangu, ambaye namkuta akiwa kajilaza kwenye kochi akizungumza na rafiki zake wawili waliomtembelea. Anapenda kuketi vizuri, lakini hali haimruhusu.
“Poleni jamani kwa safari ndefu!” ndivyo anavyoanza kusema huyu mwenyeji wangu, ambaye si mwingine zaidi ya mlinzi mahiri wa timu ya soka ya Taifa, Taifa Stars, pamoja na klabu ya Simba, Costa Victor Nampoka ‘Nyumba’. Anajaribu kuuweka vyema mguu wake wa kulia ambao bado umefungwa bandeji gumu (POP) baada ya kuvunjia mazoezini takribani mwezi mmoja na nusu uliopita.
“Hakuna shaka, Dar es Salaam ni moja na hakuna sehemu unayoweza kusema ni mbali,” namjibu kumpa matumaini.
“Hapana! Pamoja na ukweli kwamba mkoa kazini, lakini naamini uamua kufunga safari mpaka kuja kuniona ni jambo kubwa sana. Mngeweza hata kuniuliza maendeleo yangu kwa njia ya simu. Sina budi kushukuru kwa kuja kunijulia hali,” anasema.
Mara anaingia dada mmoja mweupe hivi ambaye anaketi pamoja na Costa kwenye kochi moja. Costa mwenyewe anamtambulisha kwamba ndiye mkewe, Dina, ambaye wamebahatika kuzaa naye watoto wawili; Victor Costa mwenye miaka miwili na Rio Costa mwenye mwaka 1.5. Anatukaribisha.
Anapoondoka namwambia ni jambo la kawaida kuwatembelea wagonjwa, na katika suala lake yeye ni mmoja wa watu waliotoa mchango mkubwa katika timu ya taifa ya soka ambayo sasa iko katika nafasi nzuri ya kufuzu kwa fainali za Mataifa ya Afrika mwakani ikiwa tu itashinda mechi yake ya mwisho.
“Nashukuru kusikia hivyo, lakini sura zinazokuja hapa daima ni zile nilizozizowea, yaani marafiki zangu na wachezaji wenzangu wa klabu ya Simba, labda na viongozi wa Simba,” anasema kwa huzuni.
“Una maana kwamba viongozi wa timu ya taifa na hata TFF huwa hawakutembelei?” nauliza.
Anasema tangu alipoumia siku tatu kabla ya Taifa Stars kupambana na Zambia katika mechi ya kirafiki na kupelekwa Muhimbili na daktari wa timu Shecky Mngazija, hajatembelewa wala kujuliwa hali hata kwa simu na kiongozi yeyote yule wa chombo hicho cha juu cha soka nchini.
Anaongeza kwamba, ni wachezaji wenzake wa Simba ndio baadhi yao huwa wanawasiliana naye pamoja na viongozi na marafiki wa klabu ambao wameonekana kumjali vya kutosha kiasi cha kutuma gari kila siku katika mechi zote ambazo Simba ilicheza kwenye hatua ya Sita Bora ya Ligi ya Mpito hadi fainali.
“Kwa kweli viongozi wa klabu yangu wananijali sana na sina budi kuwashukuru,” anasema. Kama vile amekumbuka kitu, anasema anamshukuru pia mtu mmoja wa Benki ya NMB anayeitwa Kajura (Imani Kajura ambaye ni Meneja Masoko).
“Huyu jamaa baada ya kutoa zawadi za shilingi 500,000 kwa kila mchezaji kutokana na timu ya Taifa kushinda kule Burkina Faso, alinipigia simu kuniambia nilitakiwa kwenda kusaini fomu za akaunti. Nikamwambia sina hata pesa ya nauli na kwa jinsi ninavyoumwa nisingeweza kupanda daladala, lakini akaniambia nichukue teksi nay eye angelipa. Namshukuru sana,” anasema.
Hata hivyo, amewaasa wachezaji wengine; wa klabu na hata timu ya taifa, kwamba pindi watakapoumia na kushindwa kujuliwa hali na viongozi wao wasife moyo bali hiyo iwe changamoto kwao kufanya vizuri watakaporejea uwanjani.
“Binafsi sina kinyongo na yeyote. Naomba Mungu nipone nirejee uwanjani, ikibidi niliwakilishe taifa langu, kwa sababu natambua kwamba timu ya Taifa ni ya Watanzania wote wala si ya mtu mmoja. Naamini Watanzania milioni kadhaa wako pamoja na mimi na hata walipojua kwamba nimeumia walinitumia meseji za pole zaidi ya 3,000, hata sijui walikoipata namba yangu,” anasema.

Kuvunjika mguu
Costa anasema kwamba walikuwa kwenye mazoezi kama kawaida kwenye uwanja wa Karume, akauzuia mpira bila kumkwatua ama kukwatuliwa, kisha akaserereka.
“Ghafla nikasikia maumivu makali sana, ikabidi wajaribu kuniganga pale, lakini yalipozidi wakanikimbiza Muhimbili. Huko nikaambiwa kwamba nimevunjika mfupa mdogo wa mguu wa kulia. Sikuwa na jinsi, wakanifunga hogo (bandeji gumu – POP) na kusema kwamba nirudi baada ya wiki sita,” anasema kwa majonzi.
Anasema kwamba, baada ya kutolewa kwa bandeji hilo ndipo atakapojua kama atakuwa nje ya uwanja kwa muda gani, kwani mpaka sasa hajaanza hata kuukanyangia mguu huo.
Akasema kuvunjika mguu kumemnyima nafasi ya kuliwakilisha taifa, na zaidi kumechelewesha kutimia kwa ndoto zake kwani pengine hivi sasa angeweza kuwa Afrika Kusini kujaribu kucheza soka ya kulipwa akiwa njiani kwenda cheza Ulaya.
“Kuna wakala mmoja ambaye kwa muda mrefu sasa amekuwa akinufuatilia, yuko Afrika Kusini, na alikwenda Burkina Faso kunitazama, lakini mimi sikuwepo. Ilikuwa niende Afrika Kusini kufanya majaribio na naamini ningewea kufanikiwa,” anasema mchezaji huyo.
Anasema kwamba, alikuwa na matumaini ya kufuzu kwa sababu soka ya Afrika Kusini haina tofauti na ya huku, tena hakuwa mgeni baada ya kucheza kwa muda nchini humo miaka mitatu iliyopita.
“Wanachotuzidi kule ni promosheni, televisheni zinajitahidi sana kuonyesha mpira hata wa daraja la tatu, na hiyo inamsaidia mchezaji kutazama na kuona wapi alipokosea ili kujirekebisha, ama afanye nini kuongeza jitihada,” anasema.
Anaongeza kwamba alishindwa kuendelea kucheza huko kwa sababu klabu aliyokuwa akiichezea wakati ule ya Marlasburg (Tembas) iliyokuwa daraja la kwanza mwaka 2005 ikiwa chini ya kocha wa zamani wa Simba Trott Moloto, iliinunua klabu moja iliyokuwa ligi kuu. Ikabidi wachezaji wa timu hizo wachekechwe, na majungu ndipo yakaibuka ambapo Moloto, ambaye ndiye aliyemfanyia mpango wa kwenda huko, akamgeuka. Ikabidi afungashe virago kurejea.
Hata hivyo, anasema kwamba ndoto zake bado hazijafutika, kwani anaamini anaweza kucheza Ulaya bila matatizo yoyote, na zaidi anasema angependa siku moja avae ‘uzi’ wa Manchester United akicheza pembeni ya Rio Ferdnand ambaye uchezaji wake unamvutia kiasi cha kumwitia mwanawe mdogo jina hilo kutokana na kumhusudu.
Akizungumzia nafasi ya Taifa Stars kufuzu kwa fainali za Mataifa ya Afrika mwakani, Costa (25) ambaye ni mtoto wa nne katika familia ya watoto watano wa mzee Victor Nampoka – wawili wanawake na watatu wanaume, anasema kwamba nafasi ipo, lakini mechi ya mwisho dhidi ya Msumbiji ni ngumu sana.
“Ile mechi ni kama fainali na inabidi maandalizi ya nguvu yafanyike pengine kuliko mechi zote zilizotangulia. Msumbiji ni wazuri sana kuliko hata Burkina Faso, na ina nafasi ya kufuzu ikiwa itashinda na Senegal wakafungwa, hivyo Watanzania tusibweteke bali tujiandae vizuri,” anasema huku akisikitika kwamba anaweza kuikosa mechi hiyo pia ikiwa ataambiwa apumzike.
Akizungumzia kuhusu maendeleo ya soka, mlinzi huyo anasema kwamba hakuna kitakachoinua zaidi ya soka la vijana, na kuongeza kwamba mashindano ya Copa Coca Cola yawe chachu wa klabu na wadau mbalimbali kuanza kuibua vipaji.
“Kule Brazil tulikokwenda kuna taasisi ya soka ya watoto wadogo. Watoto wanatoka nchi mbalimbali kwenda kufundishwa mpira, na wazazi wao wanalipia wastani wa dola 1,500 kwa mwezi ili watoto wao wajue mpira. Tusione wenzetu wamepiga hatua tukadhani kwamba ni miujiza, wamewekeza.
“Watanzania wanapaswa kuunga mkono juhudi za maendeleo ya soka ya vijana, kuanzia kwa wazazi, ambao wanapaswa kuwapa ‘sapoti’ watoto wao ikiwa ni pamoja na kuwapatia vifaa vya michezo na nauli ya kwenda mazoezini,” anaongeza.
Costa aliyemaliza elimu ya msingi mwaka 1994 Kinondoni Hananasif, jijini Dar es Salaam na kuungana na maelfu ya watoto ambao hawakufanikiwa kuchaguliwa kujiunga na sekondari, amewashauri wachezaji kuachana na anasa na kwamba wawe na malengo kama kweli wanataka kupiga hatua katika mchezo huo.
“Sijafanikiwa sana, lakini niseme ukweli kwamba nimejiepusha na mambo mengi. Sivuti sigara wala bangi, halafu niliacha kitambo kunywa pombe, tena basi nilikuwa nikinywa bia mbili ama tatu tu, lakini sasa sitaki kabisa nahitaji kukazana kwenye mpira ambao pekee ndio mwokozi wangu katika maisha,” anamalizia.

Wasifu:
Jina: Costa Victor Nampoka
Kuzaliwa: Oktoba 11, 1982, Dar es Salaam.
Umri: 25

Klabu za awali:
Five Star Kinondoni, Mkunguni FC Ilala, Eleven FC Buguruni, Saddam FC na International FC za Kinondoni.
Taifa Jang’ombe – Zanzibar (1998 – 1999)
Forodha Zanzibar (2000 – 2001)
Mtibwa Sugar (2002)
Simba (2003 – 2004)
Marlsburg – Afrika Kusini (2005)
Simba (2006 – mpaka sasa).