Friday, August 20, 2010

Ulafi Wa Ruzuku Wadhihirishwa Na ‘Vyama Vya Mifukoni’


· Vingi havina hata ofisi za taifa, achilia mbali za mikoa
· Badala ya kukimbilia Ikulu, vijipange kusukuma maendeleo

Na Daniel Mbega

KIPENGA cha kampeni za uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani kinapulizwa rasmi Ijumaa hii huku kukiwa na mambo mengi ambayo bado yanaonyesha kambi ya upinzani ina kazi ngumu ya kuingia Ikulu.

Tayari vyama vyote 18 vya siasa vimekwishateua wagombea wao wa nafasi mbalimbali katika kinyang’anyiro hicho cha uchaguzi mkuu wa nne wa vyama vingi tangu mfumo huo ulipoanza mwaka 1992.

Hadi sasa tayari vyama 10 vimekwishatangaza kusimamisha wagombea wa urais huku uwezekano wa vingi kujitokeza kabla ya tarehe ya mwisho ya uchukuaji na urejeshaji wa fomu za wagombea Agosti 19 ukiwa mkubwa.

Hadi kufikia mwishoni mwa wiki, wagombea wa vyama hivyo Jakaya Mrisho Kikwete na Dk. Mohammed Bilal (CCM), Profesa Ibrahim Haruna Nguyuru Lipumba (CUF), Mutamwega Mugahywa (TLP), Dk. Wilbroad Peter Slaa (Chadema), Christopher Mchungaji Mtikila na Kibwana Said (DP), Obeid Mshana (Demokrasia Makini), Humphrey Emmanuel Haule wa Tanzania People's Party (TPP), Peter Mziray (PPT-Maendeleo), Paul Henry Kyara na Hamis Msabaha (SAU), Hashim Rungwe (NCCR-Mageuzi) walikuwa wamechukua fomu za kuwania urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mwenyekiti wa Chama cha NLD Emmanuel Makaidi aliyegombea wadhifa huo mwaka 2005 safari hii amesema chama chake hakisimamishi mgombea kwa sababu hakikujiandaa vya kutosha kufanya hivyo, huku mwenzake wa UDP John Cheyo akisema wamejiandaa kwenye udiwani na ubunge kwa kuwa wanataka kuongeza nafasi za uwakilishi.

Vyama ambavyo hadi sasa havijatangaza kusimamisha wagombea urais ni Alliance for Tanzania Farmers (AFP), CHAUSTA, TADEA, PPT-Maendeleo, NRA, UPDP, UMD na Jahazi Asilia.

Idadi ya wanaowania urais mwaka huu hadi sasa ni sawa na ile ya mwaka 2005 iliyopitishwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na kwa namna moja ama nyingine, karibu ni vyama vile vile vilivyogombea kwenye uchaguzi uliopita, isipokuwa NLD iliyojitoa na TPP ambayo imeingia kwa mara ya kwanza.

Ukiangalia kwa juu juu chaguzi hizi mbili wa mwaka 2005 na 2010 unaweza kusema kwamba demokrasia imepanuka zaidi nchini kwani chaguzi nyingine mbili za mwaka 1995 na 2000 zilishuhudia vyama vitano tu vikishiriki kinyang’anyiro cha urais ambavyo ni CCM, NCCR-Mageuzi, UDP, TLP na CUF.

Hata hivyo, kwa wanaotafakari kwa kina wanaweza kupingana na mawazo ya kukomaa kwa demokrasia, badala yake watakubaliana nami kwamba kinachojitokeza sasa ni wimbi la watu wenye uroho wa madaraka, tamaa ya fedha na uzandiki ambao wanaona hiki ni kipindi chao cha mavuno.

Tulishuhudia waliogombea wa mwaka 2005 Leonard Shayo (sasa marehemu), Suleiman Huss Ally (Demokrasia Makini), Freeman Mbowe (Chadema), Dk. Edmund Aidan Sengondo Mvungi, Naila Jidawi (NCCR-Mageuzi), Anna Senkoro, Yusuf Rashid Nchenga (PPT-Maendeleo), Profesa Ibrahim Lipumba, Juma Duni Haji (CUF), Augustine Mrema, Rukia Kiota (TLP), Paul Henry Kyara, Haji Ramadhan (Sauti ya Umma), Emmanuel Makaidi, Cassim Omary Mohamed (NLD) na Mtikila Mchungaji Christopher, Said Sudi Said (DP) walivyoburuzwa na Jakaya Kikwete, Ally Mohamed Shein wa CCM.

Kikwete alipata kura 9,123,952 (80.28%), Lipumba kura 1,327,125 (11.68%), Mbowe kura 668,756 (5.88%), Mrema kura 84,901 (0.75%), Mvungi kura (55,819 (0.49%), Mtikila kura 31,083 (0.27%), Makaidi kura 21,574 (0.19%), Senkoro kura 18,783 (0.17%), Shayo kura 17,070 (0.15%) na Kyara kura 16,414 (0.14%).

Wanaofuatilia kwa karibu siasa za Tanzania wataelewa dhahiri kwamba mwenendo wa vyama vya siasa nchini umeendelea kushuka kwa kasi ikilinganishwa na mwaka 1995 na 2000 ambapo wapinzani walionyesha ushindani mkubwa.

Mwaka 1995 Augustine Mrema wa NCCR-Mageuzi alipata kura 1,808,616 sawa na 27.77% dhidi ya Benjamin Mkapa wa CCM aliyeshinda kwa kura 4,026,422 (61.82%), huku Ibrahim Lipumba (CUF) akipata kura 418,973 (6.43%) na John Cheyo (UDP) akipata kura 258,734 (3.97%).

Uchaguzi wa mwaka 2000 ulishuhudia Ibrahim Lipumba wa CUF akishika nafasi ya pili kwa kukusanya kura 1,329,077 sawa na 16.26%, dhidi ya Benjamin Mkapa wa CCM aliyeshinda kwa kupata kura 5,863,201 sawa na 71.74%, huku Augustine Mrema (TLP) akipata kura 637,115 (7.80%) na John Cheyo (UDP) kura 342,891 (4.20%).

Jambo ambalo wapinzani wanashindwa kulikubali ni kwamba hawana umoja na wanatumia kisingizio cha uhuru wa kidemokrasia kuingia kwenye uchaguzi kwa maslahi yao binafsi badala ya maslahi ya umma.

Wapinzani wanashindwa kutambua kwamba urais si suala la mchezo wala la kukurupuka na kuliletea mzaha, kwa sababu Ikulu ni mahali nyeti, hivyo anayetaka kuingia ni lazima awe msafi kweli. Lazima mgombea Urais afanye maandalizi madhubuti na ya muda mrefu.

Tatizo kubwa lililopo ni kwamba, wapinzani kama walivyo Watanzania wengi hawapendi kuambiwa ukweli. Hata watakapokuwa wamemaliza kusoma makala haya jibu watakalokuwa nalo mara moja ni kwamba ‘huyo anatumiwa’, ‘kibaraka wa sisiemu’ na kauli nyingi kama hizo.

Ni mara ngapi wameambiwa waunganishe nguvu zao kama kweli wanataka kuing’oa CCM madarakani na wamewapuuza wale wanaotoa ushauri? Ni mara ngapi wamekuwa wakijaribu kuunda umoja wao, lakini umoja huo ukivunjikia njiani kabla ya safari kuanza?

Kwa mazingira ya aina hiyo, unawezaje kusema kwamba wapinzani wana nia thabiti ya kuleta mabadiliko nchini? Leo hii ukiwachunguza wapinzani na mwandishi wa makala haya utaelewa ni nani ‘anayetumiwa’ baina yao!

Kama mwaka 2000 CUF walau ilikuwa imevuka asilimia iliyofikiwa na NCCR-Mageuzi mwaka 1995, basi wangeweza kuleta mapinduzi makubwa ya kidemokrasia endapo wangeungana mwaka 2005 na kusimamisha mgombea mmoja ashindane na Jakaya Kikwete wa CCM.

Lakini kwa tamaa zao na uroho wa madaraka, wakaona lazima wote waingie msambweni, wakajitosa. Hawakujua, na hawajui mpaka sasa, kwamba utitiri wao kwenye kinyang’anyiro hicho cha urais unaipa mwanya CCM ishinde kirahisi kwa sababu wenyewe kwa wenyewe hawana msimamo, ni vipofu ambao wanakonyeza gizani, na viziwi ambao hata uwapigie mavuvuzela hawataweza kusikia!

Inavyoonekana, na huo ndio ukweli wenyewe, wengi kati ya viongozi wa vyama vya siasa vya upinzani huamua kujitosa kwenye uchaguzi kwa sababu tu ya kufuata ruzuku zinazotolewa na serikali na siyo dhamira ya kweli ya kutaka ushindi.

Binafsi ninasema kwa kujiamini kwa sababu vipo vyama ambavyo nasikitika kuviita ni ‘vya mifukoni’ na ‘viko kwa ajili ya uchaguzi tu’ huku viongozi wao wakitawaliwa na ulafi wa ruzuku kila msimu wa uchaguzi unapowadia.

Leo hii tukifanya ziara ya kuzungukia ofisi za vyama hivyo tunaweza kujikuta tunalia badala ya kusikitika, kwa sababu vingi kati ya vyama hivyo havina ofisi, ofisi zao ni za mifukoni kwani ama nyumba zao ndizo ofisi za vyama, ama wanawasiliana na wanachama wao kwa simu. Tushukuru mabadiliko ya sayansi na teknolojia kwa kutuletea simu hizi za mikononi, vinginevyo hali ingekuwa mbaya zaidi.

Sikatai, vipo vyama vichache sana makini na ndivyo tunavyovitegemea vilete mabadiliko, lakini vinavurugiwa na vyama vingine ambavyo havijisumbui hata kidogo kutafuta wanachama ama kujiimarisha na kuwafanya wananchi wawe na imani navyo.

Kutokana na vyama vingi kutokuwa na mifumo mizuri, imekuwa vigumu sana hata kukagua mapato na matumizi yao, yakiwemo ya fedha za ruzuku kwa vile ambavyo vinabahatika kupata.

Hali hii ndiyo inayotufanya tuseme wazi kwamba, ulafi wa ruzuku, uroho wa madaraka na kupenda sifa zaidi kwa baadhi ya viongozi hawa wa upinzani haviwezi kuleta mabadiliko yoyote kwa kujitokeza kwao kuwania urais.

Kuwatumikia wananchi si lazima uingie Ikulu, bali unaweza kuweka mikakati madhubuti na kushirikiana nao katika shughuli mbalimbali za maendeleo badala ya kuendelea kupandikiza chuki kwa wananchi dhidi ya serikali yao, huku wapinzani hao wakiketi kulaumu jambo hili halijatekelezwa wakati wenyewe hawana wanalolifanya la haja.

Urais siyo kazi pekee ya kuwatumikia wananchi, na kwa hakika kama tunataka kuleta mabadiliko, basi tushirikiane na wananchi na kuzinadi sera zetu kwa vitendo badala ya kuota ndoto za Alinacha kwamba tunaweza kuleta mabadiliko kwa kulaumu.

Wapinzani wakumbuke kwamba, wananchi wa leo siyo wa jana, hivyo wanapoendelea kuilaumu serikali na chama tawala CCM huku wenyewe wakikaa chini bila kufanya lolote la maendeleo, wakumbuke kuwa mwisho wa siku wananchi hao hao watawapuuza na kuendelea kuichagua CCM ambayo walau inafanya hata hayo mambo madogo.

Kama hawawezi kusoma alama za nyakati, wapinzani waelewe kuwa wataendelea kupiga kelele na kuimba nyimbo zisizo na viitikio.

SOURCE: DIRA YA MTANZANIA.

No comments:

JUST ANOTHER THOUGHT

JUST ANOTHER THOUGHT

A person asked God, “What surprises you most about mankind?”

And God answered,
“That they loose their Health to make money and they loose their money to restore their Health.

That by thinking anxiously about the future, they forget the present, such that they live neither for the present nor the future.

That they live as if they will never die and they die as if they had never lived.….”

BECAUSE I'M A MAN...

Because I’m a man, when one of our appliances stops working I will insist on taking it apart, despite evidence that this will just cost me twice as much once the repair person gets here and has to put it back together.

Because I’m a man, I don’t think we’re all that lost, and no, I don’t think we should stop and ask someone. Why would you listen to a complete stranger I mean, how the hell could he know where we’re going?

Because I’m a man, there is no need to ask me what I’m thinking about. The answer is always either sex or football, though I have to make up something else when you ask, so don’t.

Because I’m a man, I do not want to visit your mother, come visit us, or talk to her when she calls, or think about her any more than I have to. Whatever you got her for mother’s day is okay, I don’t need to see it. And don’t forget to pick up something for my mommy, too!

Because I’m a man, I am capable of announcing, “one more beer and I really have to go”, and mean it every single time I say it, even when it gets to the point that the one bar closes and my buddies and I have to go hunt down another. I will find it increasingly hilarious to have my pals call you to tell you I’ll be home soon, and no, I don’t understand why you threw all my clothes into the front yard. Like, what’s the connection?

Because I’m a man, you don’t have to ask me if I liked the movie. Chances are, if you’re crying at the end of it, I didn’t.

Because I’m a man, yes, I have to turn up the radio when Bruce Springsteen or The Doors comes on, and then, yes, I have to tell you every single time about how Bruce had his picture on the cover of Time and Newsweek the same day, or how Jim Morrison is buried in Paris and everyone visits his grave. Please do not behave as if you do not find this fascinating.

Because I’m a man, I think what you’re wearing is fine. I thought what you were wearing five minutes ago was fine, too. Either pair of shoes is fine. With the belt or without it looks fine. Your hair is fine. You look fine. Can we just go now?

Because I’m a man and this is, after all, the 90’s, I will share equally in the housework. You just do the laundry, the cooking, the gardening, the cleaning, and the dishes. I’ll do the rest.

A SIMPLE GUIDE TO LIFE

1. Follow your dream! Unless it’s the one where you’re at work in your underwear during a fire drill.

2. Always take time to stop and smell the roses and sooner or later, you’ll inhale a bee.

3. Do not walk behind me, for I may not lead. Do not walk ahead of me, for I may not follow. Do not walk beside me, either. Just leave me alone.

4. If you don’t like my driving, don’t call anyone. Just take another road. That’s why the highway department made so many of them.

5. If a motorist cuts you off, just turn the other cheek. Nothing gets the message across like a good mooning.

6. When I’m feeling down, I like to whistle. It makes the neighbor’s dog run to the end of his chain and gag himself.

7. It’s always darkest before dawn. So if you’re going to steal the neighbor’s newspaper, that’s the time to do it.

8. A handy telephone tip: Keep a small chalkboard near the phone. That way, when a salesman calls, you can hold the receiver up to it and run your fingernails across it until he hangs up.

9. Each day I try to enjoy something from each of the four groups: the bonbon group, that salty-snack group, the caffeine group and the “What ever-it-is-the-tinfoil-in-the-back-of-the-fridge”.

10. Into every life some rain must fall. Unusually when your car windows are down.

11. Just remember: You gotta break some eggs to make a real mess on the neighbor’s car!

12. When you find yourself getting irritated with someone, try to remember that all men are brothers and just give them a noogie.

13. This morning I woke up to the unmistakable scent of pigs in a blanket. That’s the price you pay for letting the relatives stay over.

14. It’s a small world. So you gotta use your elbows a lot.

15. Keep your nose to the grindstone and your shoulder to the wheel. It’s a lot cheaper than plastic surgery.

16. This land is your land. This land is my land. So stay in your land.

17. Love is like a roller coaster: When it’s good you don’t want to get off, and when it isn’t, you can’t wait to throw up.

DEDICATION TO YOUNG PEOPLE

Youth is a time of hope. Also of uncertainty. But for a person who is young and healthy, uncertainty just means a challenge. It is important to be positive. First of all about yourself. But also about your family and your people. As a unique person and each human being are unique, you have enormous potential. Because you have so much potential, people may sometimes feel negatively challenged by that potential and try to undermine it.

You have to fight for your right to make your place in society. To do that you have to use all the chances given you now to be a positive element in whatever situation you find yourself in, in future. So, it may be necessary to be a ‘rebel in reverse’ as it were. That takes real courage, to set your goal and stick to it. You choose your crowd. You exercise your right to choose.
Don’t lose your freedom for the sake of anyone. Real freedom, freedom to choose the right thing, the best for you.

Always bear a few things in mind while exercising your right to choose.

* Never take a decision when you are in a fit of anger or depression.
* Never take a decision when you are emotionally high.
* Why should fads or the decision of the group tie you down?
* What are you?
* What do you want tomorrow to be for you?

No matter how strong the group decision may be, you must think and make your decision. Many times it is necessary to consult before taking a decision. Go to someone whose life you admire, not necessarily the person you like most, but the person who is whole, who is one person, wherever she or he is and whatever she or he does.

* Remember that there is always tomorrow, and tomorrow is hope. Very few things are ‘written in stone’. Most of the mistakes we make can be rectified. They can be corrected. Problems have a solution, and each new day is a new start, a new chance, a New Hope. Indeed the youth are our hope you are our future.

Also remember that your parents love you unconditionally, you have their support and want the best in life for you ¨

COSTA VICTOR NAMPOKA

Mguu ulivyokatisha ndoto za kucheza soka Ulaya

DANIEL MBEGA
Dar es Salaam

NI majira ya saa 5.20 hivi asubuhi, niko hapa Ukonga-Banana nikiwania kupanda daladala la kwenda kwenye kitongoji cha Kitunda-Kibeberu, moja ya vitongoji vinavyokua kwa kasi hapa jijini Dar es Salaam.
Sijui ni umbali gani kutoka hapa, hivyo namuuliza dereva ambaye nimeketi naye pembeni yake. Ananiambia ni mwendo kama wa dakika 15 tu hivi. Nashusha pumzi kwa kujua kwamba kumbe si mbali sana kama nilivyofikiria.
Nawasili kwenye kitongoji cha Kibeberu, ambako ndiko magari yanakogeuzia, na bila kupoteza muda nampigia simu mwenyeji wangu kwamba tayari nimeshafika. Namhurumia huko aliko kama ataamua kuja kunipokea, lakini nafarijika anaponiambia kwamba nimuulize mtu yeyote hapo kituoni atanileta.
Watoto wawili wanajitolea kunipeleka nyumbani kwa mwenyeji wangu, ambaye namkuta akiwa kajilaza kwenye kochi akizungumza na rafiki zake wawili waliomtembelea. Anapenda kuketi vizuri, lakini hali haimruhusu.
“Poleni jamani kwa safari ndefu!” ndivyo anavyoanza kusema huyu mwenyeji wangu, ambaye si mwingine zaidi ya mlinzi mahiri wa timu ya soka ya Taifa, Taifa Stars, pamoja na klabu ya Simba, Costa Victor Nampoka ‘Nyumba’. Anajaribu kuuweka vyema mguu wake wa kulia ambao bado umefungwa bandeji gumu (POP) baada ya kuvunjia mazoezini takribani mwezi mmoja na nusu uliopita.
“Hakuna shaka, Dar es Salaam ni moja na hakuna sehemu unayoweza kusema ni mbali,” namjibu kumpa matumaini.
“Hapana! Pamoja na ukweli kwamba mkoa kazini, lakini naamini uamua kufunga safari mpaka kuja kuniona ni jambo kubwa sana. Mngeweza hata kuniuliza maendeleo yangu kwa njia ya simu. Sina budi kushukuru kwa kuja kunijulia hali,” anasema.
Mara anaingia dada mmoja mweupe hivi ambaye anaketi pamoja na Costa kwenye kochi moja. Costa mwenyewe anamtambulisha kwamba ndiye mkewe, Dina, ambaye wamebahatika kuzaa naye watoto wawili; Victor Costa mwenye miaka miwili na Rio Costa mwenye mwaka 1.5. Anatukaribisha.
Anapoondoka namwambia ni jambo la kawaida kuwatembelea wagonjwa, na katika suala lake yeye ni mmoja wa watu waliotoa mchango mkubwa katika timu ya taifa ya soka ambayo sasa iko katika nafasi nzuri ya kufuzu kwa fainali za Mataifa ya Afrika mwakani ikiwa tu itashinda mechi yake ya mwisho.
“Nashukuru kusikia hivyo, lakini sura zinazokuja hapa daima ni zile nilizozizowea, yaani marafiki zangu na wachezaji wenzangu wa klabu ya Simba, labda na viongozi wa Simba,” anasema kwa huzuni.
“Una maana kwamba viongozi wa timu ya taifa na hata TFF huwa hawakutembelei?” nauliza.
Anasema tangu alipoumia siku tatu kabla ya Taifa Stars kupambana na Zambia katika mechi ya kirafiki na kupelekwa Muhimbili na daktari wa timu Shecky Mngazija, hajatembelewa wala kujuliwa hali hata kwa simu na kiongozi yeyote yule wa chombo hicho cha juu cha soka nchini.
Anaongeza kwamba, ni wachezaji wenzake wa Simba ndio baadhi yao huwa wanawasiliana naye pamoja na viongozi na marafiki wa klabu ambao wameonekana kumjali vya kutosha kiasi cha kutuma gari kila siku katika mechi zote ambazo Simba ilicheza kwenye hatua ya Sita Bora ya Ligi ya Mpito hadi fainali.
“Kwa kweli viongozi wa klabu yangu wananijali sana na sina budi kuwashukuru,” anasema. Kama vile amekumbuka kitu, anasema anamshukuru pia mtu mmoja wa Benki ya NMB anayeitwa Kajura (Imani Kajura ambaye ni Meneja Masoko).
“Huyu jamaa baada ya kutoa zawadi za shilingi 500,000 kwa kila mchezaji kutokana na timu ya Taifa kushinda kule Burkina Faso, alinipigia simu kuniambia nilitakiwa kwenda kusaini fomu za akaunti. Nikamwambia sina hata pesa ya nauli na kwa jinsi ninavyoumwa nisingeweza kupanda daladala, lakini akaniambia nichukue teksi nay eye angelipa. Namshukuru sana,” anasema.
Hata hivyo, amewaasa wachezaji wengine; wa klabu na hata timu ya taifa, kwamba pindi watakapoumia na kushindwa kujuliwa hali na viongozi wao wasife moyo bali hiyo iwe changamoto kwao kufanya vizuri watakaporejea uwanjani.
“Binafsi sina kinyongo na yeyote. Naomba Mungu nipone nirejee uwanjani, ikibidi niliwakilishe taifa langu, kwa sababu natambua kwamba timu ya Taifa ni ya Watanzania wote wala si ya mtu mmoja. Naamini Watanzania milioni kadhaa wako pamoja na mimi na hata walipojua kwamba nimeumia walinitumia meseji za pole zaidi ya 3,000, hata sijui walikoipata namba yangu,” anasema.

Kuvunjika mguu
Costa anasema kwamba walikuwa kwenye mazoezi kama kawaida kwenye uwanja wa Karume, akauzuia mpira bila kumkwatua ama kukwatuliwa, kisha akaserereka.
“Ghafla nikasikia maumivu makali sana, ikabidi wajaribu kuniganga pale, lakini yalipozidi wakanikimbiza Muhimbili. Huko nikaambiwa kwamba nimevunjika mfupa mdogo wa mguu wa kulia. Sikuwa na jinsi, wakanifunga hogo (bandeji gumu – POP) na kusema kwamba nirudi baada ya wiki sita,” anasema kwa majonzi.
Anasema kwamba, baada ya kutolewa kwa bandeji hilo ndipo atakapojua kama atakuwa nje ya uwanja kwa muda gani, kwani mpaka sasa hajaanza hata kuukanyangia mguu huo.
Akasema kuvunjika mguu kumemnyima nafasi ya kuliwakilisha taifa, na zaidi kumechelewesha kutimia kwa ndoto zake kwani pengine hivi sasa angeweza kuwa Afrika Kusini kujaribu kucheza soka ya kulipwa akiwa njiani kwenda cheza Ulaya.
“Kuna wakala mmoja ambaye kwa muda mrefu sasa amekuwa akinufuatilia, yuko Afrika Kusini, na alikwenda Burkina Faso kunitazama, lakini mimi sikuwepo. Ilikuwa niende Afrika Kusini kufanya majaribio na naamini ningewea kufanikiwa,” anasema mchezaji huyo.
Anasema kwamba, alikuwa na matumaini ya kufuzu kwa sababu soka ya Afrika Kusini haina tofauti na ya huku, tena hakuwa mgeni baada ya kucheza kwa muda nchini humo miaka mitatu iliyopita.
“Wanachotuzidi kule ni promosheni, televisheni zinajitahidi sana kuonyesha mpira hata wa daraja la tatu, na hiyo inamsaidia mchezaji kutazama na kuona wapi alipokosea ili kujirekebisha, ama afanye nini kuongeza jitihada,” anasema.
Anaongeza kwamba alishindwa kuendelea kucheza huko kwa sababu klabu aliyokuwa akiichezea wakati ule ya Marlasburg (Tembas) iliyokuwa daraja la kwanza mwaka 2005 ikiwa chini ya kocha wa zamani wa Simba Trott Moloto, iliinunua klabu moja iliyokuwa ligi kuu. Ikabidi wachezaji wa timu hizo wachekechwe, na majungu ndipo yakaibuka ambapo Moloto, ambaye ndiye aliyemfanyia mpango wa kwenda huko, akamgeuka. Ikabidi afungashe virago kurejea.
Hata hivyo, anasema kwamba ndoto zake bado hazijafutika, kwani anaamini anaweza kucheza Ulaya bila matatizo yoyote, na zaidi anasema angependa siku moja avae ‘uzi’ wa Manchester United akicheza pembeni ya Rio Ferdnand ambaye uchezaji wake unamvutia kiasi cha kumwitia mwanawe mdogo jina hilo kutokana na kumhusudu.
Akizungumzia nafasi ya Taifa Stars kufuzu kwa fainali za Mataifa ya Afrika mwakani, Costa (25) ambaye ni mtoto wa nne katika familia ya watoto watano wa mzee Victor Nampoka – wawili wanawake na watatu wanaume, anasema kwamba nafasi ipo, lakini mechi ya mwisho dhidi ya Msumbiji ni ngumu sana.
“Ile mechi ni kama fainali na inabidi maandalizi ya nguvu yafanyike pengine kuliko mechi zote zilizotangulia. Msumbiji ni wazuri sana kuliko hata Burkina Faso, na ina nafasi ya kufuzu ikiwa itashinda na Senegal wakafungwa, hivyo Watanzania tusibweteke bali tujiandae vizuri,” anasema huku akisikitika kwamba anaweza kuikosa mechi hiyo pia ikiwa ataambiwa apumzike.
Akizungumzia kuhusu maendeleo ya soka, mlinzi huyo anasema kwamba hakuna kitakachoinua zaidi ya soka la vijana, na kuongeza kwamba mashindano ya Copa Coca Cola yawe chachu wa klabu na wadau mbalimbali kuanza kuibua vipaji.
“Kule Brazil tulikokwenda kuna taasisi ya soka ya watoto wadogo. Watoto wanatoka nchi mbalimbali kwenda kufundishwa mpira, na wazazi wao wanalipia wastani wa dola 1,500 kwa mwezi ili watoto wao wajue mpira. Tusione wenzetu wamepiga hatua tukadhani kwamba ni miujiza, wamewekeza.
“Watanzania wanapaswa kuunga mkono juhudi za maendeleo ya soka ya vijana, kuanzia kwa wazazi, ambao wanapaswa kuwapa ‘sapoti’ watoto wao ikiwa ni pamoja na kuwapatia vifaa vya michezo na nauli ya kwenda mazoezini,” anaongeza.
Costa aliyemaliza elimu ya msingi mwaka 1994 Kinondoni Hananasif, jijini Dar es Salaam na kuungana na maelfu ya watoto ambao hawakufanikiwa kuchaguliwa kujiunga na sekondari, amewashauri wachezaji kuachana na anasa na kwamba wawe na malengo kama kweli wanataka kupiga hatua katika mchezo huo.
“Sijafanikiwa sana, lakini niseme ukweli kwamba nimejiepusha na mambo mengi. Sivuti sigara wala bangi, halafu niliacha kitambo kunywa pombe, tena basi nilikuwa nikinywa bia mbili ama tatu tu, lakini sasa sitaki kabisa nahitaji kukazana kwenye mpira ambao pekee ndio mwokozi wangu katika maisha,” anamalizia.

Wasifu:
Jina: Costa Victor Nampoka
Kuzaliwa: Oktoba 11, 1982, Dar es Salaam.
Umri: 25

Klabu za awali:
Five Star Kinondoni, Mkunguni FC Ilala, Eleven FC Buguruni, Saddam FC na International FC za Kinondoni.
Taifa Jang’ombe – Zanzibar (1998 – 1999)
Forodha Zanzibar (2000 – 2001)
Mtibwa Sugar (2002)
Simba (2003 – 2004)
Marlsburg – Afrika Kusini (2005)
Simba (2006 – mpaka sasa).